Madiwani wa CCM Moshi watishiana kutoana roho, tamaa ya mali yatajwa

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
3,510
7,755
MWENENDO wa mambo ndani ya Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Mjini si shwari.

Taarifa zilizoifikia Tanzania PANORAMA Blog kutoka vyanzo vyake vya habari vilivyoko ndani ya manispaa hiyo, zinadai Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Mjini limegawanyika katika makundi mawili hasimu na kwamba madiwani wawili walio katika makundi tofauti yanayohasimiana wamekuwa wakitukanana hadharani matusi mazito ya nguoni.

Taarifa hizo zinakwenda mbali zaidi zikidai madiwani hao, wanaotajwa kuwa ni Diwani wa Kata ya Miembeni, Mohamedi Mushi na Diwani wa Kata ya Bomambuzi ambaye pia alipata kuwa meya wa manispaa hiyo, Juma Raibu hivi karibuni walishambuliana kwa maneno makali wakiwa katika kikao cha Kamati ya Mipangp Miji na kwamba Raibu alitishia kumuangamiza Mushi.

Inadaiwa, Diwani Raibu alitishia kumuangamiza Mushi wakati wa kikao cha Kamati ya Mipango Miji ya Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, kilichoketi Januari 20, mwaka huu, kwenye ukumbi wa Manispaa ya Moshi.

Vyanzo vya habari vinadai kuwa katika kikao hicho, Mushi alihoji kuhusu maeneo ya wazi ambayo Raibu anadaiwa kujimilikisha baada ya kutengeneza hati yeye mwenyewe jambo ambalo lilimkasirisha Raibu na kuanza kumshambulia Mushi kwa maneno makali kabla ya kutishia kumwangamiza.

Inadaiwa zaidi kuwa baada ya tukio hilo, Mushi aliandika barua ya malalamiko kwenda Kamati ya Maadili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Moshi lakini alipoulizwa jana na Tanzania PANORAMA kuhusu hilo alikataa kulizungumzia kwa madai kuwa anayemuuliza (mwandishi wa PANORAMA) anaweza kuwa ametumwa na mbaya wake, Raibu.

Alipoulizwa leo Raibu kuhusu hilo, huku akitumia baadhi ya maneno makali ambayo PANORAMA haitayaandika kwa sababu za kimaadili, alisema hilo jambo siyo la kweli na kwamba Mushi asitafute ‘kiki’ dhidi yake kwa sababu jambo la kutokea mtafaruku kwenye kikao ni jambo la kimaadili hivyo vipo vyombo vinavyoshughulikia mambo hayo alivyovitaja kuwa ni kamati ya maadili ya chama, maadili ya halmashauri lakini pia Jeshi la Polisi.
 
Mwamba wa Chato alijaza madalanzi sehem moja kwa tamaa ya kutawala milele..
Hayo ndio matokeo
 
Kawaida palipo mafisi,hakuna ustaarabu,zaidi ni kung'ata na na kuraruana(omba usiitwe "you Animal")Hilo ni zaidi ya tusi ukiweza pambana hadi mwisho ukishindwa kimbia hadi ipoteze mguu😂😂
 
Kama ni kweli hicho kinachotokea Moshi ndo kinatokea kote ndani ya ccm, jumuiya zake na Kwa watu wao waliowapa vyeo serikali!
Ni scramble for national resources!
Kwenye siasa wapo kijasiriamali zaidi!
Mali kwanza!!
 
Na wote wawili hakuna atakaye rudi kwenye kata yake uchaguzi mkuu ujao 2025,
Manispaa yote tunairudisha CDM kama ilivyokuwa enzi za marehemu Ndesamburo.
 
MWENENDO wa mambo ndani ya Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Mjini si shwari.

Taarifa zilizoifikia Tanzania PANORAMA Blog kutoka vyanzo vyake vya habari vilivyoko ndani ya manispaa hiyo, zinadai Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Mjini limegawanyika katika makundi mawili hasimu na kwamba madiwani wawili walio katika makundi tofauti yanayohasimiana wamekuwa wakitukanana hadharani matusi mazito ya nguoni.

Taarifa hizo zinakwenda mbali zaidi zikidai madiwani hao, wanaotajwa kuwa ni Diwani wa Kata ya Miembeni, Mohamedi Mushi na Diwani wa Kata ya Bomambuzi ambaye pia alipata kuwa meya wa manispaa hiyo, Juma Raibu hivi karibuni walishambuliana kwa maneno makali wakiwa katika kikao cha Kamati ya Mipangp Miji na kwamba Raibu alitishia kumuangamiza Mushi.

Inadaiwa, Diwani Raibu alitishia kumuangamiza Mushi wakati wa kikao cha Kamati ya Mipango Miji ya Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, kilichoketi Januari 20, mwaka huu, kwenye ukumbi wa Manispaa ya Moshi.

Vyanzo vya habari vinadai kuwa katika kikao hicho, Mushi alihoji kuhusu maeneo ya wazi ambayo Raibu anadaiwa kujimilikisha baada ya kutengeneza hati yeye mwenyewe jambo ambalo lilimkasirisha Raibu na kuanza kumshambulia Mushi kwa maneno makali kabla ya kutishia kumwangamiza.

Inadaiwa zaidi kuwa baada ya tukio hilo, Mushi aliandika barua ya malalamiko kwenda Kamati ya Maadili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Moshi lakini alipoulizwa jana na Tanzania PANORAMA kuhusu hilo alikataa kulizungumzia kwa madai kuwa anayemuuliza (mwandishi wa PANORAMA) anaweza kuwa ametumwa na mbaya wake, Raibu.

Alipoulizwa leo Raibu kuhusu hilo, huku akitumia baadhi ya maneno makali ambayo PANORAMA haitayaandika kwa sababu za kimaadili, alisema hilo jambo siyo la kweli na kwamba Mushi asitafute ‘kiki’ dhidi yake kwa sababu jambo la kutokea mtafaruku kwenye kikao ni jambo la kimaadili hivyo vipo vyombo vinavyoshughulikia mambo hayo alivyovitaja kuwa ni kamati ya maadili ya chama, maadili ya halmashauri lakini pia Jeshi la Polisi.
Huyo Mohamed Mushi na Juma Raibu si wapo katika mfungo wa Ramadhani?
 
Na wote wawili hakuna atakaye rudi kwenye kata yake uchaguzi mkuu ujao 2025,
Manispaa yote tunairudisha CDM kama ilivyokuwa enzi za marehemu Ndesamburo.
Kwa sera za kutukana bodaboda, mama ntilie ,kutetea ushoga hamna atakayechagua chadema
 
Back
Top Bottom