Madikteta wote duniani hufanana

Kuna wachangiaji wengi wanamshangaa Mzee Mwanakijiji (MM) kwa kubadilisha msimamo wake wa kisiasa. Hii ni kwa sababu labda hawafahamu kuwa kwa MM kushiriki katika uandishi wa kiuharakati katika siasa sio suala la kutoa maoni yake bali ni kazi. (Bila shaka maana ya "kazi" inaeleweka!). Wakati wa uchaguzi wa mwaka 2010 MM alikuwa katika timu ya wanamkakati (strategists) wa uchaguzi wa Chadema na mwaka jana akahamia CCM kwa kazi hiyo hiyo! Katika siasa kuhama chama kimoja na kwenda kingine (crossing the floor) ni jambo la kawaida lakini la kutilia shaka (bizarre) kwa sababu huchagizwa zaidi na maslahi binafsi badala ya masuala ya kiitikadi au kisera. Rais Ronald Reagan wa Marekani (1981-89) alisema haya kuhusiana na kazi ya siasa: "Politics is supposed to be the second oldest profession. I have come to realise that it bears a very close resemblance to the first".
 
Hakuna nguvu ya mamlaka iliyowahi kushinda nguvu ya umma duniani.
Hakuna Dikteta aliyewahi kustaafu.Siku zote anguko lao ni aibu, na sifa kuu ya dikteta ni kutokuwa na uwezo wa kujifunza kutokana na matukio au mifano.
na dunia imewashuhudia wengi....
 
Madikteta wote wanafanana; wawe ni wale ambao ni mtu mmoja mmoja au wawe wa chama kimoja; kufanana kwao kunatabiri vitendo vyao. Hufanana katika mambo makubwa matano:

a. Huamini kuwa wao ndio pekee wenye uwezo wa kutawala (Katika fikra zao hawaamini kama kuna mtu au chama kingine kinachoweza kutawala vizuri kuliko wao). Baadhi yao (kama ni mtu mmoja au chama) hujiaminisha kabisa kuwa ni wateule wa Mungu kutawala nchi zao.
b. Huamini kuwa wanapendwa sana kupita kiasi (hili kuelezea kwanini picha, sanamu, n.k zao huenezwa kila kona ya nchi) Hupenda kuimbiwa nyimbo za kusifiwa na kupeperushiwa maua kila wapitapo kama ishara ya "upendo" huu.
c. Hawako tayari kuamini wanaweza kukataliwa; Mara zote inapotokea mtu anawapinga au kuwakataa hutafutiwa sababu ya kuoneshwa kuwa haiwezekani awakate wao kwani (b) wao wanapendwa sana!
d. Hata siku moja hawajawahi kutengeneza mifumo itakayowaondoa wao wenyewe madarakani. Hivyo, hutumia mbinu zote kufanya mabadiliko ya kimapambo tu ambayo kwa watu wasiofuatilia huweza kuvutiwa kuwa ni mabadiliko. HIvyo aidha hujikuta wanaondoka kwa kukimbia au kwa kukimbizwa na wananchi wao au mataifa ya nje!
e. Wako tayari kufanya jambo lolote kubakia madarakani - msisitizo hapa uko kwenye neno "LOLOTE".

Kutokana na hayo matatu tabia za madikteta wote huweza kutabirika (wawe ni mtu mmoja au chama kimoja). Na ili kuhakikisha hayo matatu madikteta wote duniani (wanaovaa nguo za kiraia na wale wanaovaa nguo za kijeshi)

1. Hutumia vitisho kulazimisha kupendwa na kukubalika - silaha ya dikteta ni vitisho (terror). Wakikukamata watakasumbua sana hadi uogope. Lengo ni kukushawishi uone ni kwanini wao wanastahli kupendwa! Hupenda kujiona kama wazazi wa wananchi - nani atamchukia mzazi wake?
2. Hutengeneza masimulizi ya sifa na kuyalazimisha yaaminiwe hata kama msingi wake ni uongo. Madikteta ni mabingwa wa kuunda (manufacture) uongo. Uwezo wao mkubwa wa kufanya hivi hutokana na ukweli kuwa wao humiliki vyombo vya habari vyenye kufikia watu wengi zaidi (radio, TVs n.k)
3. Inapofikia mahali kuwa upendo wa wananchi unapungua au wanaanza kuwa na mashaka nao madikteta huanza kupoteza watu. Yaani, pole pole watu huanza kukamatwa na kuwekwa "vizuizini" ili wasimpinge sana dikteta.
4. Kisingizio pekee cha madikteta wote (wawe wa mtu mmoja au chama kimoja) kuhalalisha kuwanyanyasa, kuwanyima wananchi uhuru na hata kuwatia watu nguvuni ni "kwa ajili ya nchi". Yaani, hutumia "taifa" kama kisingizio cha wao kuendelea kutawala.

Kwanini?

Kwa sababu madikteta wote wanataka kupendwa na kukubaliwa!

Ole wao wananchi wanaposema "hapana"!!!

Na. M. M. Mwanakijiji (BGM)

Haya mawazo ya kipindi kile bado yanafanya kazi?
 
Hili ndiyo swali kubwa ambalo wengi tunajiuliza na mpaka leo hatujapata jibu la kutufungua akili, KULIKONI!?

Hahaha...
Hizi sifa zote John Pombe Joseph Magufuli anazo. Sijui inakuwaje mmkkj amegeuka mtetezi wake mkubwa
 
Madikteta wote wanafanana; wawe ni wale ambao ni mtu mmoja mmoja au wawe wa chama kimoja; kufanana kwao kunatabiri vitendo vyao. Hufanana katika mambo makubwa matano:

a. Huamini kuwa wao ndio pekee wenye uwezo wa kutawala (Katika fikra zao hawaamini kama kuna mtu au chama kingine kinachoweza kutawala vizuri kuliko wao). Baadhi yao (kama ni mtu mmoja au chama) hujiaminisha kabisa kuwa ni wateule wa Mungu kutawala nchi zao.

b. Huamini kuwa wanapendwa sana kupita kiasi (hili kuelezea kwanini picha, sanamu, n.k zao huenezwa kila kona ya nchi) Hupenda kuimbiwa nyimbo za kusifiwa na kupeperushiwa maua kila wapitapo kama ishara ya "upendo" huu.

c. Hawako tayari kuamini wanaweza kukataliwa; Mara zote inapotokea mtu anawapinga au kuwakataa hutafutiwa sababu ya kuoneshwa kuwa haiwezekani awakate wao kwani (b) wao wanapendwa sana!

d. Hata siku moja hawajawahi kutengeneza mifumo itakayowaondoa wao wenyewe madarakani. Hivyo, hutumia mbinu zote kufanya mabadiliko ya kimapambo tu ambayo kwa watu wasiofuatilia huweza kuvutiwa kuwa ni mabadiliko. HIvyo aidha hujikuta wanaondoka kwa kukimbia au kwa kukimbizwa na wananchi wao au mataifa ya nje!

e. Wako tayari kufanya jambo lolote kubakia madarakani - msisitizo hapa uko kwenye neno "LOLOTE".

Kutokana na hayo matatu tabia za madikteta wote huweza kutabirika (wawe ni mtu mmoja au chama kimoja). Na ili kuhakikisha hayo matatu madikteta wote duniani (wanaovaa nguo za kiraia na wale wanaovaa nguo za kijeshi).

1. Hutumia vitisho kulazimisha kupendwa na kukubalika - silaha ya dikteta ni vitisho (terror). Wakikukamata watakasumbua sana hadi uogope. Lengo ni kukushawishi uone ni kwanini wao wanastahli kupendwa! Hupenda kujiona kama wazazi wa wananchi - nani atamchukia mzazi wake?

2. Hutengeneza masimulizi ya sifa na kuyalazimisha yaaminiwe hata kama msingi wake ni uongo. Madikteta ni mabingwa wa kuunda (manufacture) uongo. Uwezo wao mkubwa wa kufanya hivi hutokana na ukweli kuwa wao humiliki vyombo vya habari vyenye kufikia watu wengi zaidi (radio, TVs n.k)

3. Inapofikia mahali kuwa upendo wa wananchi unapungua au wanaanza kuwa na mashaka nao madikteta huanza kupoteza watu. Yaani, pole pole watu huanza kukamatwa na kuwekwa "vizuizini" ili wasimpinge sana dikteta.

4. Kisingizio pekee cha madikteta wote (wawe wa mtu mmoja au chama kimoja) kuhalalisha kuwanyanyasa, kuwanyima wananchi uhuru na hata kuwatia watu nguvuni ni "kwa ajili ya nchi". Yaani, hutumia "taifa" kama kisingizio cha wao kuendelea kutawala.

Kwanini?

Kwa sababu madikteta wote wanataka kupendwa na kukubaliwa!

Ole wao wananchi wanaposema "hapana"!!!

Na. M. M. Mwanakijiji (BGM)
Hili bandiko ni muhimu!
 
Madikteta wote duniani wana tabia za kufanana.
•Wana ndoto za alinacha kuwa vyama wanavyoviongoza vitawale milele.

•Mashabiki wao wengi huwa ni mambumbumbu Sana, ni watu wasiojua ya kwamba, Dikteta ni Kama mnyama mwitu, na hivyo wana roho za kikatili Sana, na maamuzi mabovu ya Madikteta huwaathiri watu wengi sana ikiwemo na washabiki wao.

•Wanapoingia madarakani huhakikisha wanatumia kila mbinu kuzima upinzani, iwe hata Kwa kuua au kuweka wapinzani vizuizini.

•Wakishahakikisha ya kwamba wamezima upinzani, sasa huhamia kwenye vyombo vyote vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii na kuvizima vyote, na yeyote atakayejifanya fyofyoko huuawa au kupotezwa kabisa.

•Huvigeuza vyombo vyote vya habari Kwa nguvu ili viwe vinaandika habari za serikali hata Kama ni za hovyo.

•Hawana mikakati ya kuongoza taifa ni wakurupukaji tu, hata ilani ya vyama vyao huwa hawaifuati.

•Hawapendi kukosolewa, ukijaribu unafukuzwa kazi.

•Wanapenda kusifiwa hata Kama wanaboronga.
Ndo ilivyo kuwa Kwa Saddam Hussein, Samweli Doe, Hitler, Bokasa, Nicolai Secescua,Sani Abacha, Hosni Mubarak.... na wengineo.

Bahati mbaya Sana Kwa Madikteta ni kuwa, hawajawahi kufanikiwa popote pale na historia ni shahidi wa hili kabisa.
Madikteta huishia pabaya Sana, aidha hupinduliwa au huuawa wakiwa madarakani.
Tumeona hayo yakitokea sehemu mbali mbali duniani.
 
Ukweli hujieleza wenyewe. Asiyependa ukweli usimlazimishe. Mwandishi umesema ukweli ambao wengi miongoni mwa wajinga watakupinga.
 
Mbona Kadhafi alikuwa na mafanikio ambayo walibya wanayamisi? Kwabahati mbaya sana utawala wa kidemocrasia ndio hupata viongozi wabovu watokanao na rushwa ushawishi usio na tija ubabe wa wachache na uonevu kwa wanyonge. Utawala wa kimungu ni huo wa kidikteta
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom