Madikteta wote duniani hufanana

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Madikteta wote wanafanana; wawe ni wale ambao ni mtu mmoja mmoja au wawe wa chama kimoja; kufanana kwao kunatabiri vitendo vyao. Hufanana katika mambo makubwa matano:

a. Huamini kuwa wao ndio pekee wenye uwezo wa kutawala (Katika fikra zao hawaamini kama kuna mtu au chama kingine kinachoweza kutawala vizuri kuliko wao). Baadhi yao (kama ni mtu mmoja au chama) hujiaminisha kabisa kuwa ni wateule wa Mungu kutawala nchi zao.

b. Huamini kuwa wanapendwa sana kupita kiasi (hili kuelezea kwanini picha, sanamu, n.k zao huenezwa kila kona ya nchi) Hupenda kuimbiwa nyimbo za kusifiwa na kupeperushiwa maua kila wapitapo kama ishara ya "upendo" huu.

c. Hawako tayari kuamini wanaweza kukataliwa; Mara zote inapotokea mtu anawapinga au kuwakataa hutafutiwa sababu ya kuoneshwa kuwa haiwezekani awakate wao kwani (b) wao wanapendwa sana!

d. Hata siku moja hawajawahi kutengeneza mifumo itakayowaondoa wao wenyewe madarakani. Hivyo, hutumia mbinu zote kufanya mabadiliko ya kimapambo tu ambayo kwa watu wasiofuatilia huweza kuvutiwa kuwa ni mabadiliko. HIvyo aidha hujikuta wanaondoka kwa kukimbia au kwa kukimbizwa na wananchi wao au mataifa ya nje!

e. Wako tayari kufanya jambo lolote kubakia madarakani - msisitizo hapa uko kwenye neno "LOLOTE".

Kutokana na hayo matatu tabia za madikteta wote huweza kutabirika (wawe ni mtu mmoja au chama kimoja). Na ili kuhakikisha hayo matatu madikteta wote duniani (wanaovaa nguo za kiraia na wale wanaovaa nguo za kijeshi).

1. Hutumia vitisho kulazimisha kupendwa na kukubalika - silaha ya dikteta ni vitisho (terror). Wakikukamata watakasumbua sana hadi uogope. Lengo ni kukushawishi uone ni kwanini wao wanastahli kupendwa! Hupenda kujiona kama wazazi wa wananchi - nani atamchukia mzazi wake?

2. Hutengeneza masimulizi ya sifa na kuyalazimisha yaaminiwe hata kama msingi wake ni uongo. Madikteta ni mabingwa wa kuunda (manufacture) uongo. Uwezo wao mkubwa wa kufanya hivi hutokana na ukweli kuwa wao humiliki vyombo vya habari vyenye kufikia watu wengi zaidi (radio, TVs n.k)

3. Inapofikia mahali kuwa upendo wa wananchi unapungua au wanaanza kuwa na mashaka nao madikteta huanza kupoteza watu. Yaani, pole pole watu huanza kukamatwa na kuwekwa "vizuizini" ili wasimpinge sana dikteta.

4. Kisingizio pekee cha madikteta wote (wawe wa mtu mmoja au chama kimoja) kuhalalisha kuwanyanyasa, kuwanyima wananchi uhuru na hata kuwatia watu nguvuni ni "kwa ajili ya nchi". Yaani, hutumia "taifa" kama kisingizio cha wao kuendelea kutawala.

Kwanini?

Kwa sababu madikteta wote wanataka kupendwa na kukubaliwa!

Ole wao wananchi wanaposema "hapana"!!!

Na. M. M. Mwanakijiji (BGM)
 
Hakuna nguvu ya mamlaka iliyowahi kushinda nguvu ya umma duniani.

Hakuna Dikteta aliyewahi kustaafu. Siku zote anguko lao ni aibu, na sifa kuu ya dikteta ni kutokuwa na uwezo wa kujifunza kutokana na matukio au mifano.
 
Vyema, na Kweli kabisa. Sasa tuanze kuwaorodhesha madikteta wa dunia hii hapa. Mimi naanza na wachache ninaowafahamu. Wadau tusaidiane kutaja hadi wakamilike:

1) Gbagbo wa Ivory Coast ni Dikteta
2) Hosni Mubarak wa Egypt ni Dikteta
3) Yoweri Museveni wa Uganda ni Dikteta
4) Chama cha Mapinduzi cha Tanzania ni cha Kidikteta

5) ...
 
Wanatumia sana Jeshi na Usalama wa Taifa wakijua ndo ngao yao ya kuendelea kuongoza, wakijisahau kwamba kumbe wanaouawa ni ndugu wa hao Usalama wa Taifa na Jeshi. Mwisho wa siku usalama wa taifa, jeshi ni sehemu ya nguvu ya UMMA...................
 
Kitila U have nailed..Ndiyo maana nchi imejaa viongozi wa ovyo ovyo ambao hawana sifa,wezi na vilaza..
 
Chama Cha Misosi (CCM) Ni cha Dikteta
Kikwete ni Dikteta anapenda kusifiwa wakati hana Akili za kufikiria kila siku anaimba uchumi unakuwa wakati ajira, umeme, maji hakuna
 
hujaza ndugu zao wa damu katika nafasi nyeti kama SHEMEJI kuwa IGP,watoto wao huogopwa sana na wakuu wa idara za serikali na chama mfano ni bora umpe mkulu neno live kuliko mtoto wake maana ataenda kuongeza chumvi na utaambiwa wewe sio raia,wake zao hutumia pesa za umma bila ukaguzi na hutoa ushauri wa kisayansi hata kama si Mwalimu wa sekondari.
Hutumia dini ili kuficha udhaifu wao kiutendaji, hawapendi vijana wawe na elimu sahihi, huteua mvivu atakayejifanya anashida kama za kwenu kuwa mkuu wa utendaji au waziri mkuu kuwazuga wanaichi.
 
1. Madikteta upenda sana kuishi extravagance life: upenda kwenda nchi za nje bila sababu za msingi kimaslahi kwa taifa na kukaa kwenye mahotel makubwa makubwa kupumzika na kuagalia michezo (mpira wa miguu, vikapu nk)

2. Hupenda sana starehe za wanawake na kwa kigezo cha kusema wanawapromote wanawake hutoa nafasi za uongozi kwa wanawake ilikuendelea kustarehe nao!!

3. Dikteta hana mikakati madhubuti ya kuinua uchumi na kubadili maisha ya raia wake, muda mwingi anawaza atumie mbinu gani za kumuwezesha kukaa madarakani, muda mwingi anatumia kupambana na kuziba mianya ya wanaoonekana kumpinga

4. Madikteta always wanabadili sheria na taratibu ilikuwawezesha kutawala vizuri

5. Uteuzi wa Dikteta katika nyadhifa mbalimbali za serikali, hauzingatii uwezo wa mtu katika kuleta mabadiliko tarajiwa, bali kigezo kikubwa ni kwa kiasi gani mtu huyu atakuwa kibaraka wake na kuchangia yeye kukaa madarakani salama
 
Dikteta hujifanya anaumwa sana na shida za wananchi wake na anauchungu sana na Taifa hilo kuliko maskini wa mwisho wa Taifa hilo.
 
Vyema, na Kweli kabisa. Sasa tuanze kuwaorodhesha madikteta wa dunia hii hapa. Mimi naanza na wachache ninaowafahamu. Wadau tusaidiane kutaja hadi wakamilike:

1) Gbagbo wa Ivory Coast ni Dikteta
2) Hosni Mubarak wa Egypt ni Dikteta
3) Yoweri Museveni wa Uganda ni Dikteta
4) Chama cha Mapinduzi cha Tanzania ni cha Kidikteta

5) ...

Bila kumsahau MUGABE wa zimbabwe!
 
Inaonekana watu hawashindwi kuwatambua madikteta; Kitila umesema point moja muhimu sana. Madikteta wanahofia sana intellectuals vile vile. Lakini upande mwingine kundi la wasomi hujitengeneza kama watetezi wa madikteta hao.

Kwakweli you said it all...Na ma dictatorhujua kuwatumia vizuri wasomi walioshindwa kujitambua kutimiza matakwa yao....Kinachonishangaza ni jinsi gani msomi anaweza kuazima akili ya ujinga ili atimize matakwa ya madictator!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom