Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,214
- 3,587
Elimu ni mojawapo ya wizara zilizoleta taharuki ya kuondolewa mawaziri wao kufuatia ladha za utendaji wao zilivyokuwa tamu kwa taifa (wananchi).
Wizara zingine ni Ardhi na Sheria & Katiba. Malalamiko ya ardhi yaliyokuwa yamepunguzwa sana na Mhe. Lukuvi sasa yameanza kurudi kwa kasi.
Prof. Kabudi aliboresha sekta ya Sheria na Idara ya Mahakama. Lakini pia alipokuwa Mambo ya Nje kwa kutumia uzalendo wake alitetea rasilimali za nchi zilizokamatwa ikiwa ni pamoja na kurejesha nyumbani wanafunzi wa Kitanzania walionasa nje ya JMT kwa lockdown ya Uviko-19 hasa China na India (wale wa vita ya Ukraine sijui wako wapi?).
Kiini cha wasilisho (post) hili ni elimu. Inawezekanaje mwanafunzi aliyehitimu kidato cha nne kwa ufaulu wa daraja la kwanza alama 8 (tena shule ya Junior Seminary) anapangiwa kwenda kusoma ualimu.
Binafsi sijasikia kama kuna mabadiliko ya sera wizara ya elimu yaliyoleta utaratibu huu mpya ambao hapo awali haukuwepo asilani.
Kama kuna mdau Mwalimu humu naomba taarifa ya kitaalam toka kwake kama mtaalam wa fani ya ualimu; ili nijuwe kama kuna mabadiliko ya sera chini ya Prof. Mkenda.
Watendaji wasio mahiri ndiyo walimponza Prof. Muhongo ambaye anajulikana kimataifa kwa umahiri wake, Dr. Kalemani alipopokea kijiti cha Prof. Muhongo ilibidi awe makini na watendaji na akawa na kasi kubwa ya kazi.
Mwl. Nyerere akihutubia katika hafla ya kubadili Chuo cha Itikadi Kivukoni kuwa taasisi ya kiserikali ya taaluma za jamii alisema kama atathibitika kufeli kwenye utawala wake basi wahusika ni watendaji aliowaweka na kama angeweza kurudi kutawala basi angepambana na watendaji zaidi kuliko watumishi wengine.