Madhara ya Kufutwa kwa CHADEMA!

Chadema ni chama ni chama cha Wakatoliki, na Padre Slaa ndiye Padre Mkuu wa chama hicho. Mbinu za Padre Slaa ni kuleta Ukatoliki wake zaidi ndani ya Serikali. Chadema bora kifutwe kabla Counter-Attack kutoka haijaanza kazi yake.

Angalia Somalia, Pakistan, au Iraq. Kama Chadema kitaendelea kuwepo basi ujue kabisa nchi itaingia ktk vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kwa sababu, Waislamu hakubali Padre Slaa awe Rais.

mmhhh,kazi ipo watanzania wenzangu!! hata wakati wa mapinduzi ya zanzibar, kulikuwa na watu/vikundi vya watu na hata vyama vya siasa vilivyopigania sultani abaki simply because walikuwa wananufaika na tende na halua za mwarabu likewise huyu jamaa yetu!!
so, kama CDM wakimtoa Slaa (PhD) asigombee urais wala asiwe na cheo chochote na badala yake wamsimamishe muislam na hata running mate awe muislam, mtakubali??? i thought you go for material and delivery, kumbe udini???!!! kazi ipo kweli kweli!! katika mapambano, wapo watakaobaki nyuma kwa u-slow wao au kwa kupinga kwao ila vita ikishinda WOOOTE wana-join furaha!! so ngoja sisi tumtoe mkoloni mweusi then tutakula wote matunda ya ushindi.
 
Chadema si Chama cha kushika dola. Wako kibiashara zaidi, na kikanda zaidi. Kunamsemo toka siku nyingi nchi haiwezi kuongozwa na kabila lenye influency ya kipesa au lugha ni hatari. Hamu yao kubwa ni kushika dola si kuwakomboa wananchi. Kuwatumia wananchi ni mtego wa kutaka wapewe nchi. In fact they will never get it. And we pray. Wana pepo la damu.

Kwanza kabisa Tanzania hakuna ukabila (Nyerere took care of that loooong time ago) hivyo futa usemi wa Tanzania kuongozwa na kabila fulani.na hamu kubwa ya CCM ni nini hasa maana wameshika dola for so many years na hawajamkomboa mwananchi.Think about it!
 
Nimekuwa nikitafakari sana jinsi kejeli toka katika Serikali ya JK na chama chake cha CCM wakati wa uchaguzi kwamba Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), pamoja na vyama vingine vya upinzani ni "vyama vya msimu-uchaguzi!" Pamoja na kejeli hizo CHADEMA kilitoa upinzani mkali sana kwa CCM na kuna uwezekano mkubwa wa uchakachuaji wa kura za urais na hatimaye kimekuwa ni Chama Kikuu cha Upinzani!

CCM kwa kujua umahiri wa Wabunge wa CHADEMA hasa wawapo Bungeni (2005 - 2010) walijiandaa sana na hata kubadili Kanuni za Kudumu za Bunge, 2007 ili kukidhoofisha Bungeni ambako umaarufu wake ulianzia.

Kubaini hivyo CHADEMA kilifuata utaratibu wa "kuishtaki CCM/Serikali kwa wananchi" kama walivyofanya wakati wa kusoma "List of Shame" wakati walipobaini kuwa ufisadi wote ulioibuliwa (Meremeta, Tangold, Mwananchi Gold, EPA, Richmond, Deep Green Finance, etc) haukufuatiliwa kwa undani unaostahili na Serikali.

CCM/Serikali wameshabaini kwamba CHADEMA si "chama cha msimu" kama walivyokuwa wamefikiria, lakini badala ya kujibu mapigo wamekimbilia msaada wa dola ili angalau kiendelee kulinda ka-umaarufu kaliobakia ili kasimalizwe kabisa na CHADEMA.

Bila shaka hoja iliyoko mezani kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Mh John Tendwa, ni kukifuta CHADEMA au la kwa madai eti kwamba wametoa kauli ambazo zinahatarisha amani na utulivu wa nchi, na wameenda mbali kwa kudai kwamba kauli hizo zinaashiria uhaini!

Maswali ya kujiuliza ni kwamba: Hivi kwa nini wananchi wanaitikia maandamano yanayoitishwa na CHADEMA kwa wingi kiasi hicho? Ina maana wananchi hawawezi kufikiria kwamba CHADEMA ni chama cha namna gani mpaka CCM iwaambie? Hivi kauli za kukataa malipo haramu ya DOWANS na kupinga kupanda kwa bidhaa za vitu kwa mfumuko wa ajabu kunahatarisha amani na utulivu? Mbona wananchi wenyewe wameandamana kwa amnani na hakuna aliyesababisha vurugu yoyote? Hivi CCM inaogopa nini hasa mpaka Mwenyekiti wake Mh JK aliongea kwa unyonge wa ajabu wakati wa Hotuba yake ya mwisho wa mwezi Februari, 2011. Kumbuka kwamba JK kwenye Hotuba yake alidai eti kwamba "hivi karibuni wananchi wameingiwa na hofu!" Hivi ni wananchi wa mkoa upi walioingiwa na hofu? Na kama wangeingiwa na hofu kwa nini wajitokeze kwenye maandamano? Hivi ni wananchi walioingiwa na hofu au ni CCM ndiyo iliyoingiwa na hofu kwa kuogopa kivuli cha CHADEMA?

Sasa nije kwenye title ya thread hii. Je, Msajili wa Vyama vya Siasa, Mh John Tendwa, akiamua kucheza shilingi chooni akakifuta CHADEMA kutoka kwenye daftari lake, nini kitatokea?
1. Demokrasia ya nchi itakuwa imebakwa sana kwa kuwa nchi itaongozwa na Chama kimoja kikiwa katika matawi mbalimbali: CCM-A (CCM), CCM-B (CUF), CCM-C (TLP), CCM-D (UDP), CCM-E (NCCR-MAGEUZI), etc.
2. Nchi itaingia tena kwenye chaguzi nyingine ndogo za wabunge na madiwani ambazo zitasababisha gharama kubwa zisizo za lazima. Kwa sasa nasikia nchi haina fedha za kutosha kwa sababu wafadhili waligoma kugharamia uchaguzi mkuu, 2010, kwa hiyo tulitumia fedha zetu wenyewe! Sasa kwa nini tuingie kwenye gharama za namna hiyo? Si afadhali tuilipe DOWANS kama hatuna uchungu na fedha kiasi hicho?
3. Mafisadi watapumua kwa kiasi kikubwa sana kwa sababu hakutakuwa na wa kuwabughudhi kwenye ufisadi wao watakaokuwa wanaufanya!
4. Kuna uwezekano wa kutokea vurugu, maana wananchi wenye kuipenda nchi yetu hawatapendezwa na hatua ya kukifuta CHADEMA! Mungu apishe mbali kwenye hili!
5. EX-CHADEMA members wataenda Mahakamani kupinga kufutwa kwa CHADEMA na kwa kuwa haki huwa haiwezi kuzuiwa, huwa inacheleweshwa tu, watashinda kesi na watakuwa na nguvu ya ajabu kuliko ilivyokuwa mwanzo.
6............
7...........
Mh John Tendwa tafadhali usilewe madaraka, Maisha ni zaidi ya huo usajili wa vyama, zawadi ambayo umeikabidhiwa kwa muda na JK! Itakie mema nchi yetu ambayo demokrasia yake ndio kwanza imeanza kuchipua! Serikali inapokosolewa hailali usingizi, inafanya juu chini itekeleze ahadi zake kwa wananchi! Badala ya kutekeleza ahadi zenu mmekuwa busy kuangalia CHADEMA inafanya nini na kupoteza muda na resources za nchi kwa kuwafuatilia, shame on you! Historia itawahukumu kwa hili!


Tujadili!

....hata wakikifuta kamwe hawatafuta harakati za ukombozi na hisia tulizonazo wananchi!!!!
 
Chadema ni chama ni chama cha Wakatoliki, na Padre Slaa ndiye Padre Mkuu wa chama hicho. Mbinu za Padre Slaa ni kuleta Ukatoliki wake zaidi ndani ya Serikali. Chadema bora kifutwe kabla Counter-Attack kutoka haijaanza kazi yake.

Angalia Somalia, Pakistan, au Iraq. Kama Chadema kitaendelea kuwepo basi ujue kabisa nchi itaingia ktk vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kwa sababu, Waislamu hakubali Padre Slaa awe Rais.

Ila wakristo wamekubali sheikhe Kikwete awe rais?wewe ni mpuuzi tena sana, jiondoe kwenye Jf maana unawaza pumba kwenye kichwa chako. What is Catholic ktk nchi hii?tuna madhehebu mangapi ya kikristo?unadhani wakristo waote ni wakatolic?nani anakwambia all christians wanasupport RC?acha upuuzi na ujenge hoja, hii nchi ina watu wenye akiri timamu na wanaishi kwa amani wakristo, waislamu na wasabato, hakuna anayeuliza dini ya mwenzake isipokuwa wapuuzi wachache km nyie na propaganda za CCM kuwadanganya kuwa CDM ni chama cha catholic?Lutheran,Anglican,Menonite,AIC,Winners,TAG,EAGT,Morovian,etc, watakuwa na vyama vyao pia au?Acha bangi, km siasa huwezi njoo tukupe kazi.
 
Chadema si Chama cha kushika dola. Wako kibiashara zaidi, na kikanda zaidi. Kunamsemo toka siku nyingi nchi haiwezi kuongozwa na kabila lenye influency ya kipesa au lugha ni hatari. Hamu yao kubwa ni kushika dola si kuwakomboa wananchi. Kuwatumia wananchi ni mtego wa kutaka wapewe nchi. In fact they will never get it. And we pray. Wana pepo la damu.
Aliyewaambia mababu zako wasisome na kuwa kabila kubwa ni nani?Ukubwa wa kabila unakuja kwa wingi wa watu au vitu mnavyoweza kufanya?Huo usemi aliutoa nani?Acha propaganda za kipuuzi, anyway, elimu yako ni level gani maana huenda tunajadili mambo na darasa la nne au saba.Shame on you!!!
 
Ushahidi? angalia Uongozi wa Chadema, na Wabunge wa Chadema, majority ni kutoka Dini moja na Kabila moja. Naona huo ni ushahidi tosha.


Duh! Mkuu kwakweli reasoning yako ni very poor and low! Umeambiwa utoe ushahidi wa vifungu kutoka kwenye katiba ya CHADEMA au quotes toka kwenye mikutano yao,wewe unasema viongozi na wabunge wa CHADEMA ni wa dini na kabila moja.

Kamanda Mbowe ni mchaga na mkristu. Dr Slaa ni muiraqw na mkristu. Kamanda Arif ni muislamu pamoja na kamanda Zitto muha toka Kigoma. Sasa hapo udini na ukabila unatoka wapi?

Ukija kwa wabunge. Wabunge wa CHADEMA wametoka majimbo mbalimbali TZ na wengi wao wana makabila ya hizo sehemu. Kamanda Mbilinyi,kamanda Wenje,kamanda Nyerere,kamanda Silinde,prof. Kahigi,kamanda Mnyika,kamanda Mdee,Mtema,kamanda Akonaay n.k.

Kwaiyo mkuu toa arguments zenye mashiko si unakurupuka tu.
 
Jamani mimi japo ni mgeni hapa naomba niulize jambo hili hapa;

HIVI CHADEMA WAMESHABATIZA WATANZANIA WANGAPI NA KUWAINGIZA KATIKA UKATOLIKI????.

HEBU ANGALIA SERIKALI YA SASA ILIVYO;
RAIS- MH.JAKAYA KIKWETE - MUISLAM
M/RAIS- DR. MOHAMED GHARIB BILALI- MUISLAM
RAIS ZANZIBAR - DR. ALI MOHAMED SHEIN - MUISLAM
M 1/ RAIS WA ZANZIBAR - MALIM SEIF SHARIFU HAMAD -MUISLAM
M 2/ RAIS WA ZANZIBAR - BALOZI SEIF ALI IDD - MUISLAM
WAZIRI MKUU - MIZENGO KAYANZA PETER PINDA - MKRISTO
JAJI MKUU - MH. JAJI OTHMAN- MUISLAM
SPIKA WA BUNGE MUUNGANO - MH.ANNA SEMAMBA MAKINDA- MKRISTO.

SAMAHANI KIDOGO WADAU KWA KUWACHOSHA NA LISTI YANGU HAPO JUU, ILA NILITAKA NIWAONYESHE TU JINSI MIHIMILI MIKUU MITATU YA NCHI YETU ILIVYO KWA SASA. VIONGOZI WA JUU WENYE KUTOA MAAMUZI 8, KATI YAO WAISLAM 6 NA WAKRISTO 2!!!!!.

JE CCM NI CHAMA CHA KIISLAM????. NA JE VIONGOZI HAWA WOTE WA KUCHAGULIWA WALICHAGULIWA NA WAISLAM PEKEEE????.

KAMA JIBU NI HAPANA, BASI NAOMBA WATANZANIA TUSIDANGANYWE NA WANASIASA KUTUINGIZA KATIKA KUTUGAWA KWA UDINI KWA KUWA WATANZANIA WANA DINI ZAO LAKINI TANZANIA HAINA DINI. HIZI NI PROPAGANDA ZA KIJINGA NA HAZINA TIJA YOYOTE.

CCM, CHADEMA, CUF, NCCR MAGEUZI, UDP, UPDP, JAHAZI ASILIA, PPT MAENDELEO NA VINGINE VINGI TU NI VYAMA VYA KISIASA NA SI VYAMA VYA KIDINI HIVYO BASI WATANZANIA TUWE MACHO NA WANASIASA WANAFIKI NA WASIOPENDA MAENDELEO YA WANANCHI BALI NI KUKUZA MITAJI YAO NA FAMILIA ZAO TU BASI. TUKATAE KUWA MITAJI YAO ILA TUDAI HAKI YETU KWA NGUVU ZOTE BILA KUJALI ITIKADI ZA DINI ZETU WALA KABILA ZETU.

TANZANIA ITAJENGWA NA WENYE MOYO.
 
Minashangaa mada imetolewa yakujadili lakini watu wanaleta chuki za kisiasa, kidini, kabila ambazo kimsingi hazina faida kwa nchi hii yenye changamoto lukuki.

Kwanza ukweli ni kwamba udini upo hata mkatae vipi ushahidi unaonekana katika mada hii. Udini umeingizwa na wanasiasa wote bila kujali chama. Ukabila haujashika kasi kama udini hivyo siuongelei sana. soma kitabu cha Religion Justice and Freedom kilichohaririwa na Prof. Saida Yahya Othman aka Mke wa Prof. Haroub Othman.

Kuna mtu anasema CC1 CCM 2 nk akimaanisha vyama vingine vyote vya upinzani tofauti na chadema vimeungana na ccm. Mimi nasema tuache fikra potofu, tuache uchochezi, tuache ubinafsi wa kichama kuona chadema ndiyo chama pekee kinachotetea wananchi kwa dhati, chama cha upinzani ni kupingana na kila kitu, nk. Kwa mtazamo wangu hata kama hakuna vyama vya siasa katika nchi kukawa na udhibiti wa mali ya nchi na watu wake wakawa katika maendeleo ni saw. Swala la vyama vya siasa ni western democracy amabyo kwa namna moja ama nyingine ni namna ya kutumia haki za binadamu na democrasia kuwa tenga watu wakati watawala wanakula vyao wengine mnagombana. Kwani hizo haki za binadamu zimeshuka toka mbinguni au zimeandikwa nao mabepari (ref; topic ya new imperialism aliyoitoa Prof. Wole Soyinca pale UDSM kama hauna copy mfuate Shivji akupatie)? Cha msingi hapa ni maendeleo ya nchi, na kiuhalisia hayaletwi na wanasiasa wala chama cha siasa bali wananchi wote kwa kufanya kazi kwa bidii, kuheshimiana, kuwa na utu, ukuwa na uzalendo na kujijali, kutokwa na ubinafsi na kushirikiana kupambana na maadui wa ndani na wa nje bila kujali chama, dini, kabila nk. na hivi vyote ndivyo malimu Nyerere alivipromote lakini kwa ubinafsi wetu havipo tena. Libya ndiyo hayohayo lakini kwa ubinafsi wa wanasiasa vijana hwavitaki kumbukeni Gadafi hakua Rais bali kiongozi wa mapinduzi ya Libya na aliyotatenda kwa nchi yake hayahitaji kuadithiwa labda kwa propaganda za walafi wa mafuta na madhalimu.

Kuna mtu kasema kuwa nchi za kiislamu hazionewi hiyo si kweli, wenzetu hawakutaka kutawaliwa ndiyo maana hakuna cha koloni la mwingereza, mjerumani, etc wao walikuwa wazalendo wakiongozwa na umoja waiunganishwa na dini ya kiislamu, hata Ethiopia waliunganishwa na dini Orthodox ndiyo maana hawakutawaliwa hakukuwa na divide and rule. Sasa mabepari lazima yawatenganishe ili kupata kile wanachokitaka yaani super profit kwa vizazi vya sasa na vijavyo. unataka kuniambia Palestina hawaonewi, kinachoendelea Afghanistan, Iraq na Lebanon ni nini? au ndiyo kujazwa propaganda za madhalimu? Madhalimu hayana dini ndugu wana umoja!!!

Kuhusu kupindua nchi: Hakuna chama chochote cha kisiasa kinachoweza kupindua nchi alafu hiyo nchi ikatawalika. Jeshi sawa au chama chenyewe kiungane na jeshi kufanya mapinduzi kama Madagascar hata hivyo bado kutakuwa na mgawanyiko mkubwa. Kumbuka mapinduzi makubwa yaliyosababisha umwagikaji wa damu mkubwa tena ya wanafunzi wakiongozwa na walimu na wacheza kungfu na michezo mingine ya asili chini ya Mao Tse Tung yalikua ya China. Mapinduzi haya haya hayakua ya vyama vya kisiasa bali wananchi na mafanikio yake mpaka sasa yanaonekana. Kumbuka china ni nchi ya chama kimoja, inashutumiwa sana na nchi za magharibi kuwa inavunja haki za binadamu, haina demokrasia na malalamiko mengine mengi.

Ushauri tujadili mada kwa mtazamo wa kujenga nchi na si kwa mtazamo wa kujenga chama.
 
Chadema ni chama ni chama cha Wakatoliki, na Padre Slaa ndiye Padre Mkuu wa chama hicho. Mbinu za Padre Slaa ni kuleta Ukatoliki wake zaidi ndani ya Serikali. Chadema bora kifutwe kabla Counter-Attack kutoka haijaanza kazi yake.

Angalia Somalia, Pakistan, au Iraq. Kama Chadema kitaendelea kuwepo basi ujue kabisa nchi itaingia ktk vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kwa sababu, Waislamu hakubali Padre Slaa awe Rais.

Acheni unafiki nyie, hivi wote walioandamana kanda ya ziwa ni wakatoriki au wakristo? usifikiri watanzania ni wajinga na hoja zenu za udini? hakuna asiyejua CCM imeishiwa sasa inaunda hoja zisizo na kichwa waa miguu.

Kuna watu Tanzania hii wanaulizana udini? huko loliondo kuna maelfu ya watu wanaenda kunywa dawa kwa mchungaji kuna mtu anauliza udini? mmetuchosha na uvuvu wenu wa kufikiri.

Kama CCM itakuja na hoja za msingi za kutatua matatizo ya wananchi unafikiri CHADEMA itaendelea kupata wafuasi lukuki mikoani? inapata sababu hoja za CCM ni weak na hakuna mtanzania wa sasa asiyelijua hilo mbaya zaidi hadi vijijini watu wameshaanza kujua haki zao na hapo panaashiria mwisho wa utawala wa kinyonyaji.

Jibuni hoja kwa hoja msikimbiklie hoja ya udini ambao haupo Tanzania. msituletee mabalaa mengine bila sababu za msingi.
 
Back
Top Bottom