Madhara ya kuchelewesha sana Baraza la Mawaziri

Pamoja na madudu yote...Saada na Mwingulu wanafaa kweli kuwa mawaziri....??????.kama Kitilya anayo kashfa..naamini kabisa wizara ya fedha hiyo kashfa ipo pia.
 
Inashangaza kuona unajiita mchambuzi na kutoa hoja potofu ya aina hii. Mapema mwaka huu nchi ya Nigeria yenye watu zaidi ya 150million ilimteua Buhari kuwa Rais badala ya Jonathan. Ameongoza nchi hii kubwa kwa zaidi ya miezi minne bila baraza la mawaziri. Utakumbuka Nigeria imo vitani Boko Haram. Sembuse Tanazania ambapo tuna amani? Anachofanya jpm ni kufumua mfumo mbovu wa ufujaji wa serikali za ccm, kupambana na ufisadi na kuweka benchmark ya uchapaji kazi chini ya utawala wake. Yeyote atakayechaguliwa kuwa waziri sasa anajua kiwango anachotaka jpm na siyo lelemama. ni vema aendelee hivi walau kwa miezi miwili zaidi. hapa kazi tu. mawaziri baadaye.
 
Nchi imemaliza mwezi bila kuwa na baraza dogo lakini mambo yanaenda.... hakuna haja ya kuwa na baraza coz wanakula hela za walipa kodi bila huruma
 
Mawaziri ni ceremonial figures tu, uwepo au kutokuwepo kwao hakuna tofauti katika utendaji wa siku kwa siku wa shughuli za serikali. Zaidi sana ni mzigo kwa wananchi katika uhalisia!
Hata hivyo, kwa kuwa wapo kikatiba, wanateuliwa tu kama formality! Rais aweza kuteua idadi anayotaka!
 
Kama Baraza la Mawaziri ndio dira na mwelekeo wa serikali basi serikali ya Kikwete ingekua mbali sana.

Hao Mawaziri unaowalilia ndio Hao hao wametuletea mabehewa mabovu, nikikumbuka hasara zilizosababishwa na mawaziri najiridhisha kuwa Magufuli yuko sahihi!

kwa hiyo unadhani kuwa kwa kuchelewa kutangaza baraza la mawaziri ndio itafanya mawaziri wawajibike zaidi?
 
huyu atakuwa ni miongoni mwa wanaoutaka uminister; sasa kila siku ikipita haoni dalili kwahiyo ameamua kuwatikisa wanajf kwakuwa anaamini kuwa sometimes watu wa system ni wanajf ili eti wakamshauri Tingatinga afanye haraka: mie naona kwanza mawaziri sometimes hawana hata msaada wowote; pamoja na uwepo wao si umeona bandarini? sasa walikuwa wapi kugundua hadi JPM ametufunua macho?

Tena ikiwezekena avute subira kidogo ili awapate wale waliotayari kutumikia watz na kama awapata wapya wote hapo ndo patakuwa patamu kuliko kuchukua mizigo ya serikali iliyopita.
 
Ni karibia mwezi mmoja sasa Rais mteule John Magufuli anaongoza nchi bila ya Baraza la Mawaziri. Wapo watu ambao wanachukulia jambo hili kwa wepesi, na pengine wanasukumwa zaidi na ushabiki wa kisiasa kuliko mantiki ya kawaida kabisa.

Kuna pande mbili za hoja:

Upande wa kwanza ni hoja kwamba Rais mteule anabana matumizi yasiyokuwa ya lazima. Na upande wa pili wa hoja ni kwamba Rais mteule anataka kuhakikisha kwamba anateua watu sahihi na anaunda serikali ndogo.

Kutoteua mawaziri kwa wakati hakuokoi Gharama. Kuendesha serikali kwa kutumia watendaji ni Gharama. Utendaji serikalini unaongozwa na sera. Nchi ina Serikali mpya isiyokuwa na Mawaziri (policy makers). Waliopo ni Watendaji/civil servants (makatibu wakuu n.k). Watendaji hawa huwa hawatungi Sera (they are not Policy Makers). Civil servants do not define policy. Kazi ya bunge ni kusimamia serikali. Bunge lijalo halipo mbali sana. Mawaziri watakuwa na majukumu mengi na pengine muda hautawatosha kukamilisha sera mbalimbali kwa ajili ya utawala wa awamu mpya ya Tano.

Watumishi wa serikali (Makatibu wakuu n.k) wanategemea political leaders (Mawaziri) to define policy. Ni Mawaziri ndio wenye jukumu hilo, huku watumishi wa serikali wakiongozwa na makatibu wakuu, wakiwa ni watekelezaji tu wa sera husika. Ingawa Makatibu Wakuu huwa wanahusishwa katika kuandaa sera mbali mbali (hasa kama washauri), but at the end of the day, they never make policy choices. Hilo sio jukumu lao. Jukumu hilo lipo mikononi mwa Political leaders (Mawaziri).

Kazi ya Watumishi wa serikali huwa ni kusubiri mawaziri wawaambie nini cha kufanya. Wasipopewa mwongozo huo, watachofanya ni kuweka mfumo uliopo on autopilot, na kujikita zaidi on operational issues, malipo ya mishahara, na kusimamia regulatory functions.

Hauwezi kupunguza gharama kwa kuamua tu kutoteua mawaziri. Unaweza rationalise idadi ya mawaziri utakaoteua, unaweza kuhakikisha kwamba unateua watu sahuhi, unaweza kuamua kuhusu mishahara na posho zao, yote haya yanaweza kufanyika lakini hauwezi kuokoa fedha kwa kutoteua mawaziri.

Hauwezi kuendesha nchi bila ya Waziri wa Fedha, Waziri wa Mambo ya nje, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Waziri wa Kilimo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Waziri wa TAMISEMI.

Hauwezi kuendesha na kuongoza uchumi kupitia Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na wasemaji wawili wa Ikulu (Katibu Kiongozi na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano).

Kiuchumi it's a much bigger problem. Chini ya serikali mpya, ni mwezi sasa, bado hakuna kauli rasmi ya serikali kuhusu sera, mwelekeo wa uchumi na usimamizi wa uchumi. Katika hali ya kawaida, huwa kuna madhara kwenye capital markets, currency markets, inflow of foreign capital n.k. Inaweza kuwa a good indicator of political risk, swali kuu likiwa ni - what would happen? Wawekezaji na wadau kwenye soko la mitaji, fedha za kigeni n.k, wote hawa wanahitaji matamko yanayo onyesha serikali inaelekea wapi kisera (hasa kiuchumi).

Bila ya uangalifu, muda sio mrefu, markets, investors, economic activities, vyote hivi vitaanza kuchukua a pessimistic view kwa sababu hakuna baraza la mawaziri, hakuna policy makers. Kwa mfano, leo hii, Wawekezaji hawajui waende wapi au wamwone nani. Fursa nyingi zinaweza kupotea.

From a global perspective, hali iliyo haikubaliki. Its unacceptable kwamba mtu anaweza kuendesha nchi bila ya Mawaziri wa sekta muhimu tulizojadili. Haiwezekani. Ni Kujidanganya. Kwa mfano, Waziri wa Fedha ni Chief Economic Advisor wa Rais. Leo hii nani anamshauri Rais kuhusu masuala ya uchumi wa nchi?

In a global sense, chini ya presidential system of government (vis a vis parliamentary system), hauwezi kushawishi watu kwamba unafanya kazi nzuri bila ya mawaziri katika serikali kwa muda mrefu kiasi hiki.

With all due respect, ni muhimu tukubali kwamba tunaanza kujenga utamaduni utakaotuletea matatizo makubwa katika governance machinery.

Tusiache kusifia mazuri lakini pia Tusiache kukosoa mapungufu.

Huyo cyo raisi mteule bhanaaa
 
A policy is a deliberate system of principles to guide decisions and achieve rational outcomes. A policy is a statement of intent, and is implemented as a procedure or protocol. (Energy policy)

Act is A bill which has passed through the various legislative steps required for it and which has become law (Rural Energy Act)

Strategy is A method or plan chosen to bring about a desired future, such as achievement of a goal or solution to a problem (Biomass Energy Strategy-Tanzania)
Programme is a planned series of future events, items, or performances (Tanzania Domestic Biogas Programme).

Manifesto is a public declaration of policy and aims, especially one issued before an election by a political party or candidate. (CCM/Magufuli Manifesto, Chadema Manifesto etc)
======================
Sera/Policy na Act/ sheria hazibadiriki imediately rais anapoapa kuwa rais. Tunazo sera tayari na sheria pia na watekelezaji wapo...baraza la mawaziri kama ulivyosema ni kwa ajili ya kumshauri rais na kuwa wasemaji wakuu namna sera na sheria zinavyotekelezwa kupitia mikakati na mipango iliyowekwa; vile vile wanahusika wakati mwingine kutia saini mikataba kwa niaba ya serikali. Sasa kama sasa hivi hata kibali cha kusafiri nje tunakipata Ikulu...waziri wa haraka gani...!? Kwa ujumla ukiangalia kwa undani hakuna ulazima wa kuharakisha uteuzi wa baraza la mawaziri.
 
Ni karibia mwezi mmoja sasa Rais mteule John Magufuli anaongoza nchi bila ya Baraza la Mawaziri. Wapo watu ambao wanachukulia jambo hili kwa wepesi, na pengine wanasukumwa zaidi na ushabiki wa kisiasa kuliko mantiki ya kawaida kabisa.

Kuna pande mbili za hoja:

Upande wa kwanza ni hoja kwamba Rais mteule anabana matumizi yasiyokuwa ya lazima. Na upande wa pili wa hoja ni kwamba Rais mteule anataka kuhakikisha kwamba anateua watu sahihi na anaunda serikali ndogo.

Kutoteua mawaziri kwa wakati hakuokoi Gharama. Kuendesha serikali kwa kutumia watendaji ni Gharama. Utendaji serikalini unaongozwa na sera. Nchi ina Serikali mpya isiyokuwa na Mawaziri (policy makers). Waliopo ni Watendaji/civil servants (makatibu wakuu n.k). Watendaji hawa huwa hawatungi Sera (they are not Policy Makers). Civil servants do not define policy. Kazi ya bunge ni kusimamia serikali. Bunge lijalo halipo mbali sana. Mawaziri watakuwa na majukumu mengi na pengine muda hautawatosha kukamilisha sera mbalimbali kwa ajili ya utawala wa awamu mpya ya Tano.

Watumishi wa serikali (Makatibu wakuu n.k) wanategemea political leaders (Mawaziri) to define policy. Ni Mawaziri ndio wenye jukumu hilo, huku watumishi wa serikali wakiongozwa na makatibu wakuu, wakiwa ni watekelezaji tu wa sera husika. Ingawa Makatibu Wakuu huwa wanahusishwa katika kuandaa sera mbali mbali (hasa kama washauri), but at the end of the day, they never make policy choices. Hilo sio jukumu lao. Jukumu hilo lipo mikononi mwa Political leaders (Mawaziri).

Kazi ya Watumishi wa serikali huwa ni kusubiri mawaziri wawaambie nini cha kufanya. Wasipopewa mwongozo huo, watachofanya ni kuweka mfumo uliopo on autopilot, na kujikita zaidi on operational issues, malipo ya mishahara, na kusimamia regulatory functions.

Hauwezi kupunguza gharama kwa kuamua tu kutoteua mawaziri. Unaweza rationalise idadi ya mawaziri utakaoteua, unaweza kuhakikisha kwamba unateua watu sahuhi, unaweza kuamua kuhusu mishahara na posho zao, yote haya yanaweza kufanyika lakini hauwezi kuokoa fedha kwa kutoteua mawaziri.

Hauwezi kuendesha nchi bila ya Waziri wa Fedha, Waziri wa Mambo ya nje, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Waziri wa Kilimo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Waziri wa TAMISEMI.

Hauwezi kuendesha na kuongoza uchumi kupitia Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na wasemaji wawili wa Ikulu (Katibu Kiongozi na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano).

Kiuchumi it's a much bigger problem. Chini ya serikali mpya, ni mwezi sasa, bado hakuna kauli rasmi ya serikali kuhusu sera, mwelekeo wa uchumi na usimamizi wa uchumi. Katika hali ya kawaida, huwa kuna madhara kwenye capital markets, currency markets, inflow of foreign capital n.k. Inaweza kuwa a good indicator of political risk, swali kuu likiwa ni - what would happen? Wawekezaji na wadau kwenye soko la mitaji, fedha za kigeni n.k, wote hawa wanahitaji matamko yanayo onyesha serikali inaelekea wapi kisera (hasa kiuchumi).

Bila ya uangalifu, muda sio mrefu, markets, investors, economic activities, vyote hivi vitaanza kuchukua a pessimistic view kwa sababu hakuna baraza la mawaziri, hakuna policy makers. Kwa mfano, leo hii, Wawekezaji hawajui waende wapi au wamwone nani. Fursa nyingi zinaweza kupotea.

From a global perspective, hali iliyo haikubaliki. Its unacceptable kwamba mtu anaweza kuendesha nchi bila ya Mawaziri wa sekta muhimu tulizojadili. Haiwezekani. Ni Kujidanganya. Kwa mfano, Waziri wa Fedha ni Chief Economic Advisor wa Rais. Leo hii nani anamshauri Rais kuhusu masuala ya uchumi wa nchi?

In a global sense, chini ya presidential system of government (vis a vis parliamentary system), hauwezi kushawishi watu kwamba unafanya kazi nzuri bila ya mawaziri katika serikali kwa muda mrefu kiasi hiki.

With all due respect, ni muhimu tukubali kwamba tunaanza kujenga utamaduni utakaotuletea matatizo makubwa katika governance machinery.

Tusiache kusifia mazuri lakini pia Tusiache kukosoa mapungufu.

Hoja yako ni nzito tatizo watu wengi wamejikita katika kupiga makofi kumshangilia Magufuli. Ni kweli bunge linakuja mwezi February, inatakiwa by that time Mawaziri wawe wameshakaa kwenye wizara zao wamekuwa familiar na policy na strategic plans ili wakija kuhojiwa bungeni wawe na majibu. Nchi iendeshwe kwa mfumo sio one man Army style.
 
muache awaonyeshe jinsi ya kufanya KKS na KDS ili wakipewa zoezi na kukosa wachapwe.
 
Kwanza umeandika kwa dharau halafu eti unatoa ushauri.

Ni dharau kesema Rais Magufuli ni Rais Mteule wakati unafahamu ameapishwa kikatiba.

Nani amekuambia sababu ya kuchelewesha kuteuwa bataza la mawaziri ni kubana matumizi.

Nani amekuambia nchi haiendi kwa sababu hakuna mawaziri
 
hivi jaman tuna sera ngapi tulizo implement na zikaleta positive impacts bila ufisadi?? hebu tuangalie suala la escrow ni nani alitia saini kuidhinisha zile pesa?? iptl, mikataba ya madini...... etc yote hayo yalifanywa na mawaziri, bado mnasema kuna faida ya kuwa na mawaziri??? bunge ni february, nahisi kanuni za bunge zinaruhusu kuahirishwa kwa bunge...... jpm sio chizi mpaka achelewe kutangaza baraza la mawaziri, je una uhakika hao mawaziri wakipewa wizara na majipu yake, wataweza kuijua wizara ipasavyo??? wataweza kujua na kutumbua hayo majipu?? mwacheni jpm asafishe wizara zote ili akitangaza baraza la mawaziri wakute kila kitu kisafi na wakizingua watawajibika vizuri........ mkuu nisamehe sijaona point kwenye post yako....
 
KWa Hali ya Nchi ilipokuwa imefikia, kila kitu kuwa politicised, viongozi kukosa uzalendo na competence ya kufanya kazi ya utumishi wa umma, Civil servants kugeuka kuwa Civil Bosses, mifumo ya kiutawala kuzidiwa na rushwa, ubinafsi, kiburi na kutazama maslahi binafsi kwanza kabla ya makusudio ya vyeo vyao, gharama kubwa za uendeshaji serikali, viongozi kuteuliwa kwa kujuana badala ya merits, Hakika Madhara ya kucheleweza kulitangaza Baraza la Mawaziri na kuwaapisha, in the real and true sense ya kuapa Mawaziri watakao teuliwa ni madogo kuliko hasara ya kulitangaza kwa haraka.

Hekima kwa sasa, wacha Rais atumie muda wakutosha kabisa, kurekebisha makosa makubwa ya kimfumo ikiwa ni pamoja na uteuaji wa Mawaziri na viongozi mbalimbali. We need no excuses once the Government in in full force.

No more Nyoka-nyokas. We are tired, very much tired and now that we see there is true and honest determination of shading off all the vices we have had over decades, its worth a wait for the rightful Governance not just a government.
 
Hoja yako ni nzito tatizo watu wengi wamejikita katika kupiga makofi kumshangilia Magufuli. Ni kweli bunge linakuja mwezi February, inatakiwa by that time Mawaziri wawe wameshakaa kwenye wizara zao wamekuwa familiar na policy na strategic plans ili wakija kuhojiwa bungeni wawe na majibu. Nchi iendeshwe kwa mfumo sio one man Army style.
Aliahidi kuteua mawaziri kulingana na taaluma zao walizosomea....hatutengemei mwanataaluma wa masuala ya Nishati atakapo teuliwa atakuwa hajui policy na strategic plan za nchi na mnana zinavyotekelezwa kwa sasa katika wizara husika...! Hiyo ya February bunge kukaa tunaweza kulisogeza mbele ili maziri wapewe muda wa kutosha kwenye wizara...! Cha msingi kwa sasa wabunge wote watumie muda huu kupitia sera na mikakati iliyopo na wajiandae kutoa hoja za kuboresha sera na mikakati hiyona utekelezaji wake watakapo kutana bungeni.
 
Hapa kinachotakiwa ni je system nzima ya serikali inafanya kazi? maana Mawaziri ni political figure na kila kitu uwa kinafanywa na watalaam ndani ya wizara na kumkabidhi waziri kupresent tu. System chini ya watalaam ikiwa sawa hakuna haja ya hawa political figures. Serikali ya Uholanzi iliwahi kukaa miaka mitatu bila Waziri mkuu kwa maana pamoja na baraza lake la mawaziri. hakuna kilichoharibika. Uchumi ulizidi kukua na watu wake wakastawi. Nadhani wewe unaongelea mazoea bila kujua serikali inafanyaje kazi
Mtoa mada naona umeleta hoja nzuri lakini pia haina mashiko. Unasahau kwamba mawaziri ni political figures na kuwa sera, mikakati na mwelekeo wa nchi kwa ujumla unatokana na hao watendaji wataalam. Kwa taarifa yako hao mawaziri wanaandaliwa kila kitu na kupitishwa kwenye kila kipengele ili aelewe na aseme kile anachotakiwa kusema.

Hoja unayoleta kuwa serikali sasa inaoperate kwenye outpilot sio kweli nadhani hujawahi kufanya kazi serikalini na kuona jinsi serikali inavyofanya kazi. Utakumbuka Rais wa Nigeria amefanya kazi kwa zaidi ya Miezi sita bila kuwa na baraza la Mawazir na nchi imeenda baraza la Mawaziri limeapishwa Juzi tu na hatujasikia wawekezaji wameondoka na Naijeria inasonga.

Tatizo mazoea yanatulemaza. Kama ingekuwa ni muhimu kuwa na baraza la mawaziri mapema kiasi hicho basi kungekuwa na provision ya muda maalum wa kuwa na baraza la mawaziri kwenye Katibu. Mwache JPM aandae mambo yake na naamini hata hao watakaoteuliwa wanajifunza kuwa Rais wa sasa anataka kufanya kazi namna gani.
 
Mimi ni mwana CCM damu damu. Nina marafiki zangu bungeni na ningependa kuona wanatumikia taifa katika nafasi kubwa zaidi za uwaziri. kama ulidhani sitaki mawaziri basi umepotea njia. Actually nilipendekeza vijana wangu wanne inabidi wawepo kwenye baraza la mawaziri katika awamu hii ya tano nao ni: January Makamba, Mwigulu Nchemba, Simbachawene na Ridhiwani Kikwete.

wote hao "mizigo" wote wapenda sifa tu
 
Back
Top Bottom