Madereva Wa STK, STL. Speed zao ni 120km/Ph na Kuendelea

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,544
Wiki jana nime drive kwenda na kurudi Tabora, kama kawaida ya hizi gari za serikali huwa mara zote huwa na haraka kuliko watumiaji wengine wa Bara Bara
Wakati Sie wanyonge Tutasafiri kwa woga wa kupigwa tochi za mbele na nyuma Hawa ndugu huwa hawajali Hilo badala yake ukiwa ktk speed 80 au 100 utapitwa kama vile umesimama! Hawa ndugu zetu hawajali usalama wao, hawana tahadhari na wala hawaogopi tochi kama sie kitu kinachowapata kujiamini kulikopitiliza, madereva wenzangu wa njia kuu watakua mashahidi kwa hili, hizi gari zipigwe jicho la ziada vinginevyo madhara hasa vifo hivi vya barabarani vitaendelea kututafuna
Serikali ilimulike hili na kulifanyia kazi vinginevyo nguvu Mali ya taifa itazidi teketea kwa ajali hizi
Wapumzike kwa amani marehemu 7wa ajali ya Dodoma pia wiki mbili zilizopita manyoni.
 
Speed limits zote kama zilizowekwa na mkandarasi au Tanroads zapaswa kuzingatiwa na magari yote na hata boda boda. Huo ndio utaratibu utumiwao katika nchi zingine.

Palipo 80, 60, 65, 80 au 100km/h zawahusu wote wenye vyombo vya moto. Huu upuuzi tunaoaminishwa kuwa magari binafsi na sasa ya serikali ati yao wazingatie 50km/h kwingine kote wajiendee wapendavyo huu ni utaratibu wa Muslim uko fyongo na ndiyo sababu ya ajali zote hizi.

Hakuna ajali kwenye 50km/h ila huko kweingine.
 
Exactly...!
 
Wiki jana nime drive kwenda na kurudi Tabora, kama kawaida ya hizi gari za serikali huwa mara zote huwa na haraka kuliko watumiaji wengine wa Bara Bara
Wakati Sie wanyonge Tutasafiri kwa woga wa kupigwa tochi za mbele na nyuma Hawa ndugu huwa hawajali Hilo badala yake ukiwa ktk speed 80 au 100 utapitwa kama vile umesimama! Hawa ndugu zetu hawajali usalama wao, hawana tahadhari na wala hawaogopi tochi kama sie kitu kinachowapata kujiamini kulikopitiliza, madereva wenzangu wa njia kuu watakua mashahidi kwa hili, hizi gari zipigwe jicho la ziada vinginevyo madhara hasa vifo hivi vya barabarani vitaendelea kututafuna
Serikali ilimulike hili na kulifanyia kazi vinginevyo nguvu Mali ya taifa itazidi teketea kwa ajali hizi
Wapumzike kwa amani marehemu 7wa ajali ya Dodoma pia wiki mbili zilizopita manyoni.
Unamchukua dereva wa teksi,au daladala,una mpa VX aendeshe,bila mafunzo yoyote diplomatic driving,unategemea nini,wengi wao wana viburi,akiwa ndani ya Vx,anajiona na yeye ni Mbunge au waziri,
 
Buraza lile gari lako lipo wapi??
Nimilipaki hapo nje, nipo kanisani
tapatalk_1521144929388.jpeg
 
Wiki jana nime drive kwenda na kurudi Tabora, kama kawaida ya hizi gari za serikali huwa mara zote huwa na haraka kuliko watumiaji wengine wa Bara Bara
Wakati Sie wanyonge Tutasafiri kwa woga wa kupigwa tochi za mbele na nyuma Hawa ndugu huwa hawajali Hilo badala yake ukiwa ktk speed 80 au 100 utapitwa kama vile umesimama! Hawa ndugu zetu hawajali usalama wao, hawana tahadhari na wala hawaogopi tochi kama sie kitu kinachowapata kujiamini kulikopitiliza, madereva wenzangu wa njia kuu watakua mashahidi kwa hili, hizi gari zipigwe jicho la ziada vinginevyo madhara hasa vifo hivi vya barabarani vitaendelea kututafuna
Serikali ilimulike hili na kulifanyia kazi vinginevyo nguvu Mali ya taifa itazidi teketea kwa ajali hizi
Wapumzike kwa amani marehemu 7wa ajali ya Dodoma pia wiki mbili zilizopita manyoni.
Naunga mkono hoja...
 
Ilikua nifungue uzi kwa ajili ya jambo hili, kwangu Mimi ajali za magari Haya zinachangiwa na sababu mojawapo Kati ya hizi

Mosi, Uharaka wa Mabosi wao, kila siku wao wana haraka, Wanataka kuwahi. Ukiwauliza walikua wapi hupewi jibu. Kwahio Dereva anajikuta Anaendesha under influence yako mtu.

Pili, Madereva wengi hawaheshimu taaluma zao kwakua wengi wamepata nafasi hizo either kwa Upendeleo au Kwa bahati tu. Matokeo yake unaamini kuwa Boss wako pia nae ni Dereva Kwahio akikuambia kimbia unakimbia, overtake una overtake, unaogopa kumpinga. Ujinga huu huukuti kwenye international NGOs, Dereva anaheshimu na anaheshimiwa pia, Dereva sio Msaidizi wa Boss.

Tatu, Uchovu utokanao na tamaa. Mtu Ametoka safari ndefu, hajapumzika, kesho anaanza safari nyingine, anajikuta Anaendesha Amechoka Kwahio level ya decision making kwa road inakua ndogo Sana

Nne, Barabara ni mbaya saana Zinahitajika kuwa mwangalifu na mtulivu Wakati wote uwapo barabarani

Tano, very poor servicing and maintenance ya magari Haya. Mengi yanapelekwa kwenye gereji za uchochoroni au zenye mafundi ambao sio waaminifu kabisa, hivyo kufanya Hali ya gari kutokua kwenye ubora wake.

Sita, baadhi ya madereva ni Watoaji wazuri wa Rushwa huko walikotoka, hili halina ubishi maana wao ni mashahidi jinsi walivyopass Road Test (naongea kwa experience). Rushwa inaharibu Taifa.

Saba, Double standards za Matrafic huko barabarani, ukipita wewe umepitisha speed hata tano tu watakushikilia Weee lakini muda ule ule mahali pale pale wanakuja STK, STJ, SU na nduguze wanavunja sheria Ile Ile. Unajiuliza, hawa wanatumia sheria Ipi na Mimi Natumia Ipi. Maskini, Kumbe wanawaharakishia Vifo wenzao wakidhani wamewasaidia.

Baada ya mambo Haya tujiandae kusikia ajali za Magari ya Jeshi, wao siku zote wana haraka, wana njia zao, wana dharura Siku zote. Watatumaliza siku moja.... Hasa huko Dar, ndio maana Nimehama.

Alamsiki

Greetings from Mambwemkoswe - Rukwa
 
Una dharau na kuhukumu mtu kwa elimu yake huo ni ushamba ndio yawezekana ni Form four ila ana mafunzo mengi toka nje na ndani ya nchi, usihukumu industry hiyohiyo wakati kuna watu wako vzur kutembea na hiyo speed bila madhara
 
Back
Top Bottom