Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

Ukifanya uchunguzi utagundua pia kwamba Madereva wenyewe hawali kwenye hotel hizo huwa wanalipwa hela tu , wao wanakula sehemu maalum , wana wapishi maalum humo njiani huwaletea msosi kwenye maeneo wanayoahidiana
Madereva wana posho zao kupeleka wasafiri eneo hilo la chakula na chakula cha pale wanakula wapendacho bureeee
 
Sahani moja ya chakula pamoja na 10000 - 20000/-, Inaumiza abiria karibia 45-50
 
Okay sawa mkuu, Mwaka sasa umepita mkuu, Tupe Sifa zake,hiyo hotel kuna Afadhali yeyote ile ?

Ni bei gani hizo mkuu?
Afadhali itoke wapi?...mwendo ni ule ule wa bei za kuruka na vyakula kiduchu kama chakula anachopewa form one shule za boarding kwa wale tuliosoma zamani!
 
Umeshawahi fikiria gharama za uendeshaji wa hizo hoteli? Pale wanakula abiria tu. Hakuna mwananchi wa maeneo yake atathubutu kwenda kula pale. Vinginevyo stendi za mabasi ziwe na migahawa inayoweza kutoa huduma bora. Stendi zikiweza kuwa na hoteli kama 3 zitafanya kuwe na ushindani na walaji kunufaika. Kinyume na hapo kilio kitaendelea.
Huu ni utetezi wa hovyo kabisa...kwamba stend kama Nane nane Dodoma, Msamvu. Hakuna maeneo yaliyotengwa ndani ya stedi kwa ajili ya kutoa huduma ya chakula?

Maeneo yapo, lakini kwa kuwa hakuna usimamizi na nia thabiti ya kusimamia zitoe huduma, ndio maana madereva na wamiliki wa mabasi wanawapeleka abiria kula katika maeneo binafsi yenye bei za kuruka.

Angalia pale Singida, chakula 7000 hadi kumi ila kihalisia ni cha bei ya 2500 hadi 4000. Lakini ni nani asimame awasemee abiria?

Kwa wenye uchumi wa kati sawa lakini kwa mtu wa kuunga Unga aliyeunga kupata nauli ya 100000 kwenda Bukoba atamudu chakula kwa bei hiyo?
 
Afadhali itoke wapi?...mwendo ni ule ule wa bei za kuruka na vyakula kiduchu kama chakula anachopewa form one shule za boarding kwa wale tuliosoma zamani!
😟😟, hatari sana, Na kwa uongozi wa sasa, kila mtu anafanya analotaka,, Maskini wa hali ya chini wamegeuzwa kuwa fursa ya vigogo hapa Tz.
 
Mimi ni dereva ngoja niitetee hii hoja kwa niaba ya wenzangu, zipo sababu kadhaa;

1. Kuzuia abiria kuharisha hovyo, ukiruhusu kusimama maeneo yenye bei nafuu watu watakula hovyohovyo na kuanza kutapita kuharisha hii itapelekea safari kuwa goigoi
2. Tukiwapeleka pale mjue sisi madere tunakula buuure hivyo hii ni fursa kwetu.
3. Huwa tuna pisi kali yale maeneo
4. Wakati mwingine ni maelekezo ya matajir wetu saa tufenyeje
 
1.Kuzuia abiria kuharisha hovyo, ukiruhusu kusimama maeneo yenye bei nafuu watu watakula hovyohovyo na kuanza kutapita kuharisha hii itapelekea safari kuwa goigoi
•Hii hoja haina mashiko. [ kwani zamani abiria walikuwa wana kula wapi?]

2.Tukiwapeleka pale mjue sisi madere tunakula buuure hivyo hii ni fursa kwetu
•Sina uhakika hata ukipeleka Abiria sehemu nyingine alafu ukose posho, mimi niliye wahi fanya kazi ya udalali najua hilo.

3.Huwa tuna pisi kali yale maeneo
Zile dakika 10 - 20 mnazotoa kwa Abiria, zinawatosha kweli kutoa donse kwa pisi?, kufanya ngono pindi unaendesha chombo cha moto huleta mikosi, hii inaweza kupelekea hata ajari barabarani.

4.Wakati mwingine ni maelekezo ya matajir wetu saa tufenyeje
Kidogo hapa naweza nikakuelewa.
 
Tatizo la wabongo ni unafiki tu
hivi abiria kwa umoja wenu mkiamua kukaidi kuburuzwa kwenye mgahawa usio rafiki kwa mifuko yenu dereva na konda watawalazimisha? lakini shida ni Maneno mengi bila vitendo na akitokea abiria mmoja mwenye msimamo hapati support ya wenzake Bali atajikuta peke yake na Maneno kibao ya kejeli kama ungepanda ndege au nunua gari yako binafsi n.k
Tatizo la wabongo ni moja tu, Unafiki hapa utaona kila mmoja hakubaliani na utaratibu Ila kwenye field hali inakuwa ni tofauti kabisa!
 
Huu ni utetezi wa hovyo kabisa...kwamba stend kama Nane nane Dodoma, Msamvu. Hakuna maeneo yaliyotengwa ndani ya stedi kwa ajili ya kutoa huduma ya chakula?

Maeneo yapo, lakini kwa kuwa hakuna usimamizi na nia thabiti ya kusimamia zitoe huduma, ndio maana madereva na wamiliki wa mabasi wanawapeleka abiria kula katika maeneo binafsi yenye bei za kuruka.

Angalia pale Singida, chakula 7000 hadi kumi ila kihalisia ni cha bei ya 2500 hadi 4000. Lakini ni nani asimame awasemee abiria?

Kwa wenye uchumi wa kati sawa lakini kwa mtu wa kuunga Unga aliyeunga kupata nauli ya 100000 kwenda Bukoba atamudu chakula kwa bei hiyo?
mbona kama unanililia utadhani nimekuwa baba yako?
 
Tatizo la wabongo ni unafiki tu
hivi abiria kwa umoja wenu mkiamua kukaidi kuburuzwa kwenye mgahawa usio rafiki kwa mifuko yenu dereva na konda watawalazimisha? lakini shida ni Maneno mengi bila vitendo na akitokea abiria mmoja mwenye msimamo hapati support ya wenzake Bali atajikuta peke yake na Maneno kibao ya kejeli kama ungepanda ndege au nunua gari yako binafsi n.k
Tatizo la wabongo ni moja tu, Unafiki hapa utaona kila mmoja hakubaliani na utaratibu Ila kwenye field hali inakuwa ni tofauti kabisa!

lakini shida ni Maneno mengi bila vitendo na akitokea abiria mmoja mwenye msimamo hapati support ya wenzake Bali atajikuta peke yake na Maneno kibao ya kejeli kama ungepanda ndege au nunua gari yako binafsi n.k
😟😟, Umetoa mfano mzuri sana, kuazia mfumo wa siasa, mpaka kwenye maisha ya kawaida, Utasikia aliyataka mwenyewe alidhani akiwa pekeake ataweza kupingana na mamlaka fulani. Badala ya kumpa Support mtetezi inakuwa tofauti, raia wale wale wanasimama upande wa mnyonyaji
 
Mimi ni dereva ngoja niitetee hii hoja kwa niaba ya wenzangu, zipo sababu kadhaa;

1. Kuzuia abiria kuharisha hovyo, ukiruhusu kusimama maeneo yenye bei nafuu watu watakula hovyohovyo na kuanza kutapita kuharisha hii itapelekea safari kuwa goigoi
2. Tukiwapeleka pale mjue sisi madere tunakula buuure hivyo hii ni fursa kwetu.
3. Huwa tuna pisi kali yale maeneo
4. Wakati mwingine ni maelekezo ya matajir wetu saa tufenyeje
Point namba 3 ni ya kupuuzwa kwenye jamii ya watu wastaarabu wa JF.
 
Ni ujinga tu! Kwani umelazimishwa kula hapo?andaa chakula chako nyumban gari ikisimama kwenye hivo vituo toa chako kula shida ipo wap?

Alafu kitu kingine upo safari safarini unakula kula ili iweje? Si unywe hata soda na biskuti ukifika unapokwenda utakula vizuri. Watu mnajiendekeza kula mataka taka ya njiani .

Binafsi ninapo safiri huwa nanua tende,maji na soda Basi mpka nafika silagi kitu kingine.

Nanunua tende kavu robo nakula mdogo mdogo na huwa sihisi njaa nikila tende nashushia soda tu na maji mpaka nafika.
 
Back
Top Bottom