Madee: Ni ushamba kupiga mwizi

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Kupitia ukurasa wake wa "X" msanii Madee ameibuka na kutoa mtazamo wake kuhusu hukumu wanayoipata wezi wanapokamatwa na wananchi.

“Sijawahi kumpiga mwizi na sitakuja kumpiga mwizi. Enhee unampiga huyo mwizi then mnamchoma moto baada ya hapo unakua umefaidika na nini”.

“Wote wanaompiga mwizi nakufikia hatua yakumvalisha tairi nakumchoma moto niwashamba tu” ameandika Madee

Screenshot_20240213-162155.jpg

Nini maoni yako?
 
Hivi wale wanaoiba mabilion kwa matrilion wananchi wanaweza kuwafata

Ova
Wanaanzaje? Yaani tena akikusikia umeropoka utakoma.. Madee ana hoja ila tatizo ni mfumo wa haki uliooza. Hata polisi wenyewe wakikuta hamjamuua mwizi wanaishia kuwadharau nyie wananchi. Enzi za Magu wezi wa Kigogo, Mburahati, na Manzese walifungwa na kuuwawa sana. Pia wengi walikimbilia Sauzi.
 
Kupitia ukurasa wake wa "X" msanii Madee ameibuka na kutoa mtazamo wake kuhusu hukumu wanayoipata wezi wanapokamatwa na wananchi.

“Sijawahi kumpiga mwizi na sitakuja kumpiga mwizi. Enhee unampiga huyo mwizi then mnamchoma moto baada ya hapo unakua umefaidika na nini”.

“Wote wanaompiga mwizi nakufikia hatua yakumvalisha tairi nakumchoma moto niwashamba tu” ameandika Madee

View attachment 2902867

Nini maoni yako?
Hajakatazwa kuwa mwizi, ikiwa sumu huonjwa basi naye akaze fuvu kuwa mwizi ili tumtendee haki kisawasawa.

Ubinadamu ni kazi/Humanity is a work.
 
Kwa sababu circle yake ni ya wezi hana hofu na sidhani kama alishawahi kuibiwa, isitoshe inawezekana biashara yake ya sembe ina mlink na wezi wakatili kuliko tulionao hapa mtaani. Mwizi anastahili mob justice popote upatapo mwizi muadhibu kulingana na wizi alioufanya, kama ni mwizi sugu piga moto, ukisubiri apelekwe polisi wazazi wake wanakuja kumtoa anaendelea kudunda mtaani na kuleta ghasia
 
Kupitia ukurasa wake wa "X" msanii Madee ameibuka na kutoa mtazamo wake kuhusu hukumu wanayoipata wezi wanapokamatwa na wananchi.

“Sijawahi kumpiga mwizi na sitakuja kumpiga mwizi. Enhee unampiga huyo mwizi then mnamchoma moto baada ya hapo unakua umefaidika na nini”.

“Wote wanaompiga mwizi nakufikia hatua yakumvalisha tairi nakumchoma moto niwashamba tu” ameandika Madee

View attachment 2902867

Nini maoni yako?

Vibaka, wezi, panya road wanazidi kuadimika mitaani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom