Madanguro yashamiri Dar, sheria iko kimya

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,899
nje+asubuhi.JPG

Biashara ya madanguro katika baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam imeshamiri na kuhatarisha kuporomoka kwa maadili kwa watu wanaoishi jirani na madanguro hayo.

Hata hivyo, watu wanaofanya biashara ya kuuza miili yao wanashindwa kuchukuliwa hatua kutokana na kukosekana kwa sheria ya kuwabana. Hatua hiyo imesababisha kampeni za kuwaondoa wamiliki wa madanguro na wanawake wanaofanya biashara hiyo kushindikana kutokana na watu hao kupanga nyumba kama wapangaji wengine.

Jiji la Dar es Salaam limekuwa na ongezeko kubwa la madanguro na baadhi ya hosteli za wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kudaiwa kutumika kwa biashara hiyo huku mamlaka zinazohusika kushindwa kudhibiti vitendo hivyo.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Makumbusho, Husna Nondo, ambako biashara hiyo imeshamiri, akizungumzia kadhia hiyo katika eneo lake, alisema hakuna sheria inayoruhusu biashara hiyo kuwapo, lakini pia hakuna sheria ya kuwatia hatiani.
“Tumefanya `ambush' mara kwa mara kwa kushirikiana na polisi jamii, lakini mwisho wa siku unajikuta hakuna sheria ya kuwashitaki…” alisema. Aliishauri serikali kutunga sheria kali dhidi ya vitendo hivyo, vinginevyo maadili yataendelea kumomonyoka kutokana na biashara hiyo kufanywa katikati ya makazi ya watu na wakati mwingine jirani na shule za msingi.

Gazeti hili lilifanikiwa kutembelea eneo la biashara hiyo katika dangulo la Mwananyamala mtaa wa Minazini.
Wanawake wanaofanya biashara hiyo wamekuwa waangalifu wanapopata mwanaume mgeni kwani muda wa maongezi wanachukua tahadhari kubwa kutokana na kuvamiwa mara kwa mara na polisi.

Unapofika nje ya vibanda hivyo, utakutana na wakinadada hao wakiwa wamekaa nje ya vizingiti vya vyumba vyao wakiwa wamevaa kanga moja ama gauni jepesi, unachotakiwa ni kumsabahi na kuingia kwenye chumba alipokaa uliyemkusudia.
Vyumba vyao ni vidogo vyenye kitanda kimoja na baadhi vina televisheni ndogo ambayo hutumika kuweka picha za ngono kwa wateja ambao hisia zao ziko mbali.

Unapoingia ndani ya chumba hicho unakumbana na harufu kali ya manukato ambayo ni zaidi ya udi.
“Gharama zetu ni mazungumzo, lakini kama wewe unataka kulala utalazimika kuniachia Sh. 10,000 na uje kuanzia saa nne usiku kwa vile huu muda wa katikati bado tunahudumia wateja wengine,” alisema dada huyo.

Dada huyo mwenye umri wa kati ya miaka 20 na 30, aliyekataa kutaja jina lake, muda wote wa maongezi alionekana mwenye uzoefu na anachozungumza.
Alisema chumba kimoja kinaweza kutumiwa na zaidi ya wasichana watatu na huwa wanaingia kwa zamu kwa kuwa wana makazi yao nje ya maeneo hayo ya biashara na wanafamilia zao. Msichana huyo baada ya kukubaliana na mwandishi wakutane usiku, hakutaka tena mazungumzo kwani muda wote alikuwa akifunua pazia la chumba chake ili asipitwe na mteja na kumtaka mwandishi aondoke.

Akizungumzia mazingira ya biashara hiyo, Ofisa Mtendaji huyo alisema harufu kali iliyomo ndani ya vyumba hivyo ni kwa ajili ya kusafisha uvundo unaotokana na wasichana hao kuhudumia wanaume zaidi ya mmoja kwa muda mfupi.
Alisema katika kata yake vipo vyumba zaidi ya 80 vinavyotumiwa na wafanyabiashara hiyo haramu. “Unajua ukizungumza nao, hii biashara inawalipa sana, wengine wanasomesha watoto wao na wanaweza kulipa kodi ya Sh. 150,000 kwa mwezi na wakati mwingine kwa siku wanaweza kukusanya mpaka Sh. 70,000,” alisema.

Nondo alisema biashara hiyo haramu ambayo ilikuwapo tangu miaka ya 1980, inahitajika jitihada za busara na si nguvu katika kuitokomeza.
“Kuna haya mashirika ya kijamii hasa yanayoshughulika na masuala ya uzazi na ukimwi, wanatakiwa kujikita kwa kundi hilo kutoa elimu ya athari za biashara hiyo, vinginevyo jitihada za serikali za kutokomeza magonjwa ya zinaa na ukimwi hazina maana,” alisema.

Baadhi ya wakazi wa maeneo hayo walionyesha kushangilia kuwapo kwa biashara hiyo kwa kile walichodai kuwa matukio ya ubakaji yamepungua.
Hata hivyo baadhi walilaani kwa maelezo kuwa maadili yanatoweka kwa kuwa biashara hiyo inafanywa waziwazi katikati ya makazi.

Source: Nipashe Jumapili
 
[h=3]Madanguro yachachamaa jijini Dar,vyangudoa vyauza ngono wazi wazi[/h]Danguro jingine ambalo Dar Leo imeligundua ni lile lililoko Posta karibu na baa moja maarufu (jina tunalo) ambapo kuna jengo moja ambalo bado ujenzi wake unaendelea na limezungushiwa mabati, hivyo mabinti wanaofanya biashara hiyo ambao wengi wao ni wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu katikati ya jiji wamedai kuwa hulitumia eneo hilo kwa makubaliano na walinzi wa jengo hilo.

Msichana mmoja aliyejitaja kwa jina moja la Faidha mwenye asili ya Kiarabu ambaye ni mwafunzi wa mwaka wa pili katika chuo kimoja hapa jijni (jina tunalo) amesema anafanya kazi hiyo kutokana na kipato kidogo alichonacho wakati matumizi ya chuoni ni makubwa.

Amesema anapopata mteja huenda naye katika jengo hilo na kumpa mlinzi kati ya sh. 500 na sh. 1,000 kisha yeye humalizana na mteja wake.

Pia gazeti hili lilitembelea danguro jingine lililopo Mwananyamala karibu na klabu ya Masai ambako pia kundi la mabinti lilikutwa likiendelea na biashara hiyo kuanzia saa 6 usiku.

Danguro jingine ni lile la Temeke Sokota ambalo wanaotafuta wanawake kwa ajili ya ngono hawahitaji kuumiza vichwa kutokana na kuwapo kwa kundi kubwa la mabinti ambao huvalia mavazi ambayo ni ya aibu kwa jamii.

Dar Leo limegundua kuwa danguro jingine ni lile la makaka poa (bwabwa) lililoko Magomeni. Tofauti na yale mengine, danguro hili linawahusisha wanaume (mashoga).

Madanguro mengine ni lile la Kigamboni lililopewa jina la Uwanja wa Mpira wa huko Italia unaojulikana kama Sanciro ambalo nalo lina mabinti wa aina mbalimbali wenye umri mdogo.

Ingawa wakati wa mchana ni vigumu kugundua kinachoendelea katika danguro hilo, kwa wateja waliolizoea huingia humo mara kwa mara kufanya shughuli zao hizo.

Hata hivyo, kuanzia saa tano usiku wao hubandika bango lao linalosomeka "Karibu Sanciro, Kiingilio 5,000/-".

Biashara ya hapo ni tofauti na madanguro mengine ambayo msichana hukubaliana na mteja na kisha kwenda kufanya naye ngono na baada ya hapo msichana humlipa msimamizi wa danguro kiasi walichokubaliana.

Katika danguro hilo la Sanciro Kigamboni mteja anapofika huchagua binti anayemtaka na baada ya hapo humlipa msimamizi wao na kisha humchagulia chumba cha kukutana naye.

Msichana aliyejitambulisha kwa jina la Justine lakini akakataa kutaja ubini wake, ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari iliyopo Kigamboni (hakuitaja jina kwa kuogopa kufukuzwa), aliliambia gazeti hili kuwa anaifanya kazi hiyo kutokana na maisha ya nyumbani kwao kuwa magumu.

"Marafiki zangu wamekuwa wakinisema shuleni kuwa mimi ni mzuri lakini sina pamba (nguo). Wanasema kama nitapata nguo nzuri nitakuwa mzuri zaidi na wanaume watanipenda zaidi, hivyo kwa kuwa natamani kuolewa ili niondokane na umasikini wa nyumbani na njia nyepesi nikaona ni hiyo kwani napata pesa na raha naipata pia," alisema Justine.

Hata hivyo, baadhi ya wengine wamesema wanafanya kazi hiyo kwa sababu walipata ujauzito, wakazaa, lakini wakakimbiwa na wanaume waliowapa mamba.

Pia katika danguro hilo kuna baadhi ya mabinti wamedai kuwa wametolewa mikoani kwa kuambiwa wanakuja kufanya kazi za ndani lakini wanapofika mjini wanajikuta wameingizwa katika kazi hiyo.

Danguro lingine liko Buguruni (jina tunalihifadhi) ambalo muda wowote ukitaka huduma utaipata. Katika danguro hilo, siyo mabinti peke yao wanaotoa huduma hiyo, bali hata wanawake ‘ngunguri' wa mjini.

Nyumba nyingi zenye madanguro huwa ni zile zilizokodishwa kwa ajili ya biashara ya baa, lakini huzikarabati na kuweka vyumba ambako baadhi kuna vyumba viwili kwa ajili ya biashara hiyo kutokana na wateja wengine wanaokunywa pombe na kulewa huhitaji kumaliza shida zao papo hapo.

Nyumba nyingine ni nyumba za makazi ya watu ambazo wamiliki wake huamua kuwapangisha wanawake wengi ambao huduma kama chakula, maji, madawa na vitu vingine vyote vinakuwa juu yake lakini fedha zinatokana na kazi hiyo.

Gazeti hili lilipowasiliana na Kamanda wa polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, kuhusu suala hilo, aliwaomba wananchi waliozungukwa na madanguro hayo watoe taarifa ili wamiliki wake wachukuliwe hatua.

Kamanda Kova alisema ni vigumu kuyasaka madanguro hayo, lakini kwa kushirikiana na wananchi kutakuwa na mafanikio.

By Dar Leo
 
Sifael Paul na Vyanzo mbalimbali
Biashara haramu ya ngono ikihusisha watoto wadogo na wanafunzi imeshamiri nchini na inalijengea taifa picha ya aibu mbele ya jamii pana ya kimataifa, Risasi Jumamosi lina ripoti kamili ya madanguro, gesti na hoteli maarufu zinazoendesha ‘unyambilisi’ huo jijini Dar es Salaam.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa, nyuma ya biashara hiyo kuna vigogo ambao wanajitajirisha kwa kuwauza watoto wa kike wa kati ya miaka 11 hadi 14 ambao wanaelezwa kuwa na soko zaidi ukilinganisha na wale wenye umri ulioyoyoma.
Kwa wiki kadhaa chumba chetu cha habari kimekuwa kikipokea ujumbe mfupi kutoka kwa watu walioomba hifadhi ya namba zao kuwa kuna wafadhili wa biashara hiyo ambao huwachukua wasichana wadogo vijijini kisha kuwamwaga jijini Dar kwa ahadi ya kuwatoa kimaisha, lakini huishia kuwafanyisha biashara hiyo haramu inayostahili kupingwa kwa nguvu zote.
Ilifahamika pia kuwa, kuna baadhi ya watu huwashawishi wanafunzi wa kike jijini Dar ambao huaga kwao kuwa wanakwenda shuleni, lakini huishia kwenye madanguro, gesti na hoteli maarufu kwa ajili ya kuuza miili, hivyo kuwafanya wazazi kuwa na matumbo joto wanapowabaini.

Risasi Jumamosi lilifanya mahojiano na wasichana hao wadogo wanaojiuza sehemu mbalimbali jijini Dar ambapo walikuwa na haya ya kusema:

  • WA KWAZA (SINZA): “Huwa natoroka shule na kwenda kujiuza kwa wanaume ili kujikimu kimaisha. Fedha ninayopewa ya matumizi huwa haitoshi.”
  • WA PILI (BUGURUNI): “Kawaida nafanya mapenzi na wanaume 5 hadi 6 kwa usiku mmoja.
  • WA TATU (KINONDONI): “Malipo kwa tendo moja ni 10,000. Saba za tajiri, tatu za kwangu.
  • WA NNE (TEMEKE): “Kazi ni ngumu lakini kwa sababu ni shida, nafanya.”

RIPOTI YA BBC
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC iliyoibua mjadala hivi karibuni na kuwaweka watu presha juu, watoto wanaojihusisha na biashara hiyo walieleza jinsi walivyodanganywa kuzamia jijini Dar kufanya kazi nzuri za kuwapatia mkate wao wa siku, lakini wakaishia kwenye biashara ya ukahaba. Watoto hao walieleza kuwa, kutokana na ugumu wa maisha vijijini walipata matumaini kuwa jijini kuna matunda, lakini walipofika wakawa wakifugwa kama watumwa kwa kazi moja tu, kuuzwa kwa wanaume wapenda ngono za rejareja.

Katika mjadala huo ulioendeshwa kwa siku tatu, vitoto hivyo vibichi viliweka wazi kuwa wanapochukuliwa na wanaume hulipwa Sh. 50,000 lakini huambulia Sh. 10,000 kwani fedha nyingine huchukuliwa na tajiri.

MMILIKI WA DANGURO ALIRITHI KWA BIBI YAKE
Kwa mujibu wa mmoja wa wamiliki wa madanguro hayo machafu (jina tunalo), biashara hiyo alirithishwa na bibi yake kwa hiyo haoni hatari kwa sababu hakusoma hivyo kazi hiyo anaiona ni halali.
Bila aibu, mwanamke huyo mchafuzi aliendelea kubwabwaja kuwa ana ‘kocha’ maalumu wa kuwafunza watoto hao namna ya kujituma wanapokuwa ‘kazini’ na wanaume.

GESTI, HOTELI NA MADANGURO HATARI NI HAYA
Uchunguzi uliofanywa na mtandao wa Jamii Forums ulibaini kuwepo kwa gesti, hoteli na madanguro hatari sehemu tofauti jijini Dar.
Ilibainika kuwa sehemu hizo ni pamoja na hoteli maarufu zilizopo Sinza Madukani, Sinza-Mori, Sinza Afrikasana, Ubungo External, Makuburi, Mbezi, Majumba Sita-Ukonga, Uwanja wa Taifa, Saba Saba, Kawe, Kunduchi, Buguruni na Magomeni.
Pia, kuna hoteli maarufu za nyota tatu katikati ya jiji maeneo ya Posta na Kariakoo katika viunga vya Mnazi Mmoja zinazofanya biashara hiyo hasa kwa wanandoa wanaofanya kazi maeneo hayo ‘wanaocheza nje kapu’ kwenye ndoa zao.

WAZIRI SOFIA SIMBA ANASEMAJE?
Akizungumzia ishu hiyo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sofia Simba (pichani), mbali na kukiri kuwepo kwa hatari hiyo, alidai kuwa wizara yake inajitahidi kutekeleza na kulinda maslahi ya watoto ingawa hakueleza jinsi wanavyokabiliana nayo.

KUTOKA RISASI JUMAMOSI
Ukweli ni kwamba hali ni mbaya kupita maelezo.
Tunatoa wito kwa idara zote zinazohusika kunusuru kizazi cha kesho kwa kuwaepusha na mateso wanayoyapata huku janga la ukimwi likichukua kasi. Pia, tunaiomba jamii kupinga kwa nguvu zote kwa kuripoti kwenye vyombo husika uwepo wa biashara hiyo haramu.

Chanzo: Global Publishers
 
Makamba alishawahi kupambana sana na hii kitu akashindwa sijui nani ataweza??

Tatizo kupambana na biashara hii kwa kuwashika wasichana pekee haiwezi kufa. Nimeona taifa fulani wamefanikiwa kwa kiwangoa fulani kwa kuwashika wanaume wanaowatafuta wasichana hao. Uwepo wa wanaume wanaowataka ndio kuendelea kwa biashara hiyo, vinginevyo biashara itakufa tu, biashara hushamiri kukiwa na wateja.
 
nyakati za mwisho hizi....tumrudie Mungu......mana kila idara hali ni mbaya.....
 
nyakati za mwisho hizi....tumrudie Mungu......mana kila idara hali ni mbaya.....

Kuna yanayoweza kuzuilika ukiwekwa utaratibu wa kweli, lakini hii ya kuwabana akina mama pekee si sahihi, bidhaa humtafuta mteja na mteja sipopatikana basi hakuna bishara itakayoendeshwa. Washikwe wanaume wanaoenda huko hii biashara itapungua au kukoma.
 
Mbona umeweka picha ya maeneo ya Bagamoyo wakati habari nzima hausiani na maeneo hayo ya Bagamoyo?. Ulikosa picha ya Mwananyamala, Buguruni, Kino n.k?. Acha kutubeep wakazi wa Bagamoyo bwana
 
kazi rahisi STONNING !! je tutawezaaaa? la ajabu Tanzania tuna wizara kamili mbona halifuatilii sakata hilo?
 
hatutaweza ku'solve hili tatizo by tough laws..u can't solve such an endemic social problem like this by only attacking the effects of it..only by dealing with the root causes of the problem kama reducing levels of poverty, providing more family and reproductive health education, doing more extensive research work on why prostitution flourish and implementing it's findings ndo unaeza ukaleta unafuu wa kukabiliana na hii hali
 
Sidhani kama hiyo ndiyo itafanikiwa maana hata nchi zilizopaa kimaendeleo na huduma za kijamii biashara hiyo imeshamiri na wamebidi kuhalalisha kwa kuanzisha makampuni yanayoendesha biashara hiyo ambayo wanaita kwa lugha laini sana party escort.

Nchi hizo anayehitaji kuanya bishara hiyo anatakiwa asajiliwe kwenye kampuni na kulipia kodi. Wanaozagaa na kujianika mitaani ni kushikwa pamoja na wanaume wanaowahonga hao wote ndani. Njia hiyo imesaidia kukomesha biashara hiyo haramu.
 
Sifael Paul na Vyanzo mbalimbali
Biashara haramu ya ngono ikihusisha watoto wadogo na wanafunzi imeshamiri nchini na inalijengea taifa picha ya aibu mbele ya jamii pana ya kimataifa, Risasi Jumamosi lina ripoti kamili ya madanguro, gesti na hoteli maarufu zinazoendesha ‘unyambilisi’ huo jijini Dar es Salaam.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa, nyuma ya biashara hiyo kuna vigogo ambao wanajitajirisha kwa kuwauza watoto wa kike wa kati ya miaka 11 hadi 14 ambao wanaelezwa kuwa na soko zaidi ukilinganisha na wale wenye umri ulioyoyoma.
Kwa wiki kadhaa chumba chetu cha habari kimekuwa kikipokea ujumbe mfupi kutoka kwa watu walioomba hifadhi ya namba zao kuwa kuna wafadhili wa biashara hiyo ambao huwachukua wasichana wadogo vijijini kisha kuwamwaga jijini Dar kwa ahadi ya kuwatoa kimaisha, lakini huishia kuwafanyisha biashara hiyo haramu inayostahili kupingwa kwa nguvu zote.
Ilifahamika pia kuwa, kuna baadhi ya watu huwashawishi wanafunzi wa kike jijini Dar ambao huaga kwao kuwa wanakwenda shuleni, lakini huishia kwenye madanguro, gesti na hoteli maarufu kwa ajili ya kuuza miili, hivyo kuwafanya wazazi kuwa na matumbo joto wanapowabaini.

Risasi Jumamosi lilifanya mahojiano na wasichana hao wadogo wanaojiuza sehemu mbalimbali jijini Dar ambapo walikuwa na haya ya kusema:

  • WA KWAZA (SINZA): “Huwa natoroka shule na kwenda kujiuza kwa wanaume ili kujikimu kimaisha. Fedha ninayopewa ya matumizi huwa haitoshi.”
  • WA PILI (BUGURUNI): “Kawaida nafanya mapenzi na wanaume 5 hadi 6 kwa usiku mmoja.
  • WA TATU (KINONDONI): “Malipo kwa tendo moja ni 10,000. Saba za tajiri, tatu za kwangu.
  • WA NNE (TEMEKE): “Kazi ni ngumu lakini kwa sababu ni shida, nafanya.”

RIPOTI YA BBC
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC iliyoibua mjadala hivi karibuni na kuwaweka watu presha juu, watoto wanaojihusisha na biashara hiyo walieleza jinsi walivyodanganywa kuzamia jijini Dar kufanya kazi nzuri za kuwapatia mkate wao wa siku, lakini wakaishia kwenye biashara ya ukahaba. Watoto hao walieleza kuwa, kutokana na ugumu wa maisha vijijini walipata matumaini kuwa jijini kuna matunda, lakini walipofika wakawa wakifugwa kama watumwa kwa kazi moja tu, kuuzwa kwa wanaume wapenda ngono za rejareja.

Katika mjadala huo ulioendeshwa kwa siku tatu, vitoto hivyo vibichi viliweka wazi kuwa wanapochukuliwa na wanaume hulipwa Sh. 50,000 lakini huambulia Sh. 10,000 kwani fedha nyingine huchukuliwa na tajiri.

MMILIKI WA DANGURO ALIRITHI KWA BIBI YAKE
Kwa mujibu wa mmoja wa wamiliki wa madanguro hayo machafu (jina tunalo), biashara hiyo alirithishwa na bibi yake kwa hiyo haoni hatari kwa sababu hakusoma hivyo kazi hiyo anaiona ni halali.
Bila aibu, mwanamke huyo mchafuzi aliendelea kubwabwaja kuwa ana ‘kocha’ maalumu wa kuwafunza watoto hao namna ya kujituma wanapokuwa ‘kazini’ na wanaume.

GESTI, HOTELI NA MADANGURO HATARI NI HAYA
Uchunguzi uliofanywa na mtandao wa Jamii Forums ulibaini kuwepo kwa gesti, hoteli na madanguro hatari sehemu tofauti jijini Dar.
Ilibainika kuwa sehemu hizo ni pamoja na hoteli maarufu zilizopo Sinza Madukani, Sinza-Mori, Sinza Afrikasana, Ubungo External, Makuburi, Mbezi, Majumba Sita-Ukonga, Uwanja wa Taifa, Saba Saba, Kawe, Kunduchi, Buguruni na Magomeni.
Pia, kuna hoteli maarufu za nyota tatu katikati ya jiji maeneo ya Posta na Kariakoo katika viunga vya Mnazi Mmoja zinazofanya biashara hiyo hasa kwa wanandoa wanaofanya kazi maeneo hayo ‘wanaocheza nje kapu’ kwenye ndoa zao.

WAZIRI SOFIA SIMBA ANASEMAJE?
Akizungumzia ishu hiyo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sofia Simba (pichani), mbali na kukiri kuwepo kwa hatari hiyo, alidai kuwa wizara yake inajitahidi kutekeleza na kulinda maslahi ya watoto ingawa hakueleza jinsi wanavyokabiliana nayo.

KUTOKA RISASI JUMAMOSI
Ukweli ni kwamba hali ni mbaya kupita maelezo.
Tunatoa wito kwa idara zote zinazohusika kunusuru kizazi cha kesho kwa kuwaepusha na mateso wanayoyapata huku janga la ukimwi likichukua kasi. Pia, tunaiomba jamii kupinga kwa nguvu zote kwa kuripoti kwenye vyombo husika uwepo wa biashara hiyo haramu.

Chanzo: Global Publishers

mbona sisi tunaoishi Makuburi hatujawahi sikia haya madanguro eneo hili?
 
kuna mambo mengine ukisoma kama hivi huwezi amini,amazing jana nilipita uwanja wa fisi yaani kujithibitishia hali ikoje nilichokikuta sikuamini yaani nimefika nikaingia chumbani baada ya kumchagua binti mmoja hivi nikamuuliza sh ngapi kaniambia buku mbili toba,ikabidi nizuge ili nitoke akaningangania pungufu tunaongea nikamwambia nina buku akaniambia ahilipi ile naondoka akaniambia lete hiyohiyo ikabidi nizuge tena hata hiyo buku sina nina jero tu akanipa bonge la tusi huyo nikatoka zangu ajabu hawavai hata nguo za ndani yaani mkifika chumbani anachuma mboga mnamaliza unasepa tena pesa kwanza,nawaza tu hivi watu wangapi huwa wanaenda pale maana kwa tsh 2k mpk wapate 15k lazima waandike seven sana tu ila dah kizazi kinapotea jitihada za makusudi zinahitajika kwa kweli.unless otherwise vijana wetu wengi watapotea hasa wale ambao wale ambao wanabalehge coz kipindi kile wanakuwa madomo zege naa huwa na hamu sana ya tendo bila ya kujua outcome yake
 
Hali si inatisha tu, ila inahuzurisha, kusikitisha na pia unafikia hatua ya kuwaonea huruma watu hawa. Unaeza kufikiria tu kwa nini wafikie hatua hiyo na kuweka kando utu wao. Nikikaa na kufikiri naona kuna tatizo ambalo linatakiwa kufanyiwa kazi nalo ni malezi ya msingi na elimu ya msingi ya maisha kwa vijana wa kizazi cha leo. Kwamba hali hiyo imekuwepo kwa miongo yote, lakini kwa sasa inafikia kiasi kisicho cha kawaida na tishio kwa usalama wa vijana wengye ambao ndio nguzo ya taifa.

Hata kesi kadhaa zikifikishwa katika idara na wizara husika ya jinsia na watoto utaona wananusa na kurudi maofisini badala ya kufanyia kazi.

Pengine nawapongeza wanaoamua kuweka kijimeza na kuuza iwevocha, maandazi, vitumbua nk lakini hili la kugeuza miilia yao kibiashara kwa kukodisha kutumiwa kifuska kwa ujira wa shiillingi 2000 imefikia hatua ya hali ya kawaida ya ubinadamu kutoweka maana hata mnyama tu hafanyi hivyo bali pale tu silika inaporuhusu na mazingira ya mnyama mwenzake yanaporuhusu, maana sijaona force ya ubakaji maana hunusa kwamba kuona kama ni majira mwafaka.
 
yaani kuna watu humu umewasaidia sana...

Yani mkuu ame solve kila k2, ila buguruni kuna watoto wazuri nyie Acha! Watoto wadogo maskini ya mungu Eti! sasa? hatuendi ku... dah! unamwambia wew ulitakiwa ulale kesho uwe shule

Mungu ulie juu jahazi hili ni wew tu uanaeweza kukoa
 
Back
Top Bottom