Madaktari waipiga changa la macho serikali

Tuko pamoja Mkuu! Badala ya sisi wanachi kuwalalamika madaktari ambao kimsingi madai yao yana hoja, ni wajibu wetu kuidai serikali tunayoilipa kodi huduma nzuri ya afya! Hatuna mkataba na wadaktari bali na serikali!
madaktari ni muhimu watafakari upya ajenda yao ya mgomo. mgomo wao wangeuitisha mwezi wa tisa baada ya kuangalia utekelezaji wake wa bajeti. wakumbuke even today ktk watumishi wa umma wao wanalipwa vizuri kuliko wengine.

hata madai yao mengi yametekelezwa, waipe muda serikali
 
Watumie vizuri nafasi yao ya kupiga kura ili wachague serekali makini itakayotumia vizuri rasilimali tulizojaliwa ili wafanyakaze wote walipwe vizuri..

Ambacho sikubaliani nacho hapa ni kushabikia matendo yatakayopelekea madhara kwa wasioukuwa na hatia kwa sababu tu tunataka kuiadhibu serekali ambayo to my opinion haiathiriki katika hili...
Mkirua unaudhi ile mbaya,nadhani unaongea kishabiki wewe,na sio hao unawasema wanashabikia,wewe ndo unashabikia kishabiki na ushabiki huu ni ule wa Nyinyiemu-CCM.for sure wewe umetumwa na Nape,unaangalia matokeo badala ya kuangalia chanzo cha tatizo.hivi reflect hili suala la madaktari ambalo ni lao wao,naaminisha maslahi yao kama wao,Je ungelikuwa wewe unaefanyiwa hayo ungeliona ni sawa tu?hivi ni kweli serikali haina pesa ya kuwaongezea mishahara na posho zingine wanazoziomba,je matumizi ya anasa ya hizo pesa zinazo fujwa na viongozi mafisadi chini ya CCM zinatoka wapi?wewe uko tayari kulipwa ujira kidogo wakati unafanya kazi kubwa?
Kingine sidhani kama huwa unaenda hospitali zetu sisi walala hoi,madktari wanadai mazingira ya kufanyiia kazi yaboreshwe,kinachomaanishwa hapa wanataka vifaa tiba vya kutosha na vya kisasa,wanataka majengo ya kutosha wanataka vitanda vya kutosha mahospitalini na vitu vingine ambavyo ni essential katika utendaji wao wa kazi.sasa haya yote unaona ni upuuzi au,haya yote unaona tunashabikia sio,hujawahi kuuguliwa au kuugua kiasi kwamba ikabidi ulazwe ndio maana unaropoka.ujinga huu unaofanywa na chama chako hauwezi kuisha bila watu ku-sacrifice.najua tutakufa,na huenda ikawa ni mimi lakini ni vema saratani hii iitwayo CCM iondoke.maana haya yote ni sababu ya udhaifu wa chama cha magamba.wacha tushabikie lakini one day yes ukombozi utapatikana.
chonde chonde madaktari msi-beep tafadhalini pigeni
 
Sikubaliani nawewe kuhusu madaktari kulipwa vizuri kuliko watumishi wengine wauma,Fanya utafiti utaliona hili.Sivizuri kuweka bayana yamalipo yawatumishi wauma hapa ila nakuhakikishia wapo wanaolipwa zaidi kuliko madaktari ingawa kielimu wako sawa!
 
Sio tu tunaweza mkuu Ciril, pia ni haki yetu kuandamana kuzidai haki hizo zinazoambatana na huduma za afya, hatimaye kukiadhibu kwa kukifuta chama kinachowadharau wananchi ikibidi kuleni nyasi lakini lazima ndege ya rais inumuliwe this time wameongeza ukali wa adhabu kufeni, hatuongezi mishahara ya medical doctors kwani mishahara ya wabunge bado haitoshi, posho za wakurugenzi wateule wa jk ndio kipaumbele

Pana wakati ukifikiria mambo yanayotendwa na viongozi wa Serikali hii unaweza kushawishika kupindua uongozi kwa namna yeyote ile.Maisha yanayomgusa wananchi masikini Wa taifa hili yamekuwa yakiwekwa ktk nafasi za mwisho,na sasa nnayaamini maneno ya mwalimu Nyerere juu ya suala la Kitiba na alisema"kwa katiba ya hii ya Tanzania inaniwezesha kuwa dikteta"na juzi kati hapa Prof,Issa Shivji nae ktk kuichambua katiba yetu alisema Katiba ya Tanzania ni ya Kibepari.
 
Last edited by a moderator:
madaktari ni muhimu watafakari upya ajenda yao ya mgomo. mgomo wao wangeuitisha mwezi wa tisa baada ya kuangalia utekelezaji wake wa bajeti. wakumbuke even today ktk watumishi wa umma wao wanalipwa vizuri kuliko wengine.

hata madai yao mengi yametekelezwa, waipe muda serikali

Kauli nzuri ni utajiri. siku zote serikali imekuwa ikitumia polisi na mahakama kididimiza au kupoka haki za watu. serikali haiwajibiki kwa kua inajua ina mahakama na polisi kuwalinda. Mia
 
Nakwataarifa tu wana Jf nikwamba zile posho zinazotamkwa basi kama zililipwa nikwamadaktari wa Muhimbili,Moi labda nakwingine kwenye hospitali kubwa!Hospitali za Halmashauri nyingi mnazozifahamu malipo yameendelea kuwa yaleyale kwakisingizio kuwa serikali haijatoa waraka nawatendaji wachini hawawezi kutekeleza kauli za viongozi kwenye vyombo vyahabari!Msione kimya ,inaumiza mno!
 
Tuache kusapoti u jinga na u huni unaofanywa na hawa jamaa....Hiyo kamati imesajiliwa wapi?? Kwahili sijawahi kuunga na wala sitoliunga mkono....Ninyi shabikieni lakini athari zitakazowapata mama ana baba zenu wakiwamo bibi na babu zenu ambao hamuishi nao ndo mtajua.....hata kama tunadhani tunaikomoa CCM na serekali..nadhani strategy hii ni mbovu na haifai na wala haitatufikisha popote....Nakaribisha matusi na kejeli kama ilivyo kawaida ya baadhi ya wana JF ambao hatutaki kusikia second opinion....

Wengi wanaosapoti madaktari kugoma hawatibiwi huko temeke,amana au m'nyamala.kama wangekuwa wanatibiwa huko na wanakosa huduma au ndugu zao kufa wasingesapoti hawa madaktari. Kwangu mimi madaktari na serikali wote sawa tu selfish individual! Maslahi binafsi mbele utendaji nyuma
 
Gharama/adhabu ya uhai ni kubwa mno haswa unapochanganya wanaohusika na wasiohusika....mimi na wewe tu wazima sas lakini unatoka kueleke morogoro njiani linatokea la kutokea ndipo utakapoelewa ninachokisimamia

Hata mazuri yana faida hata kwa watu wabaya, it goes on both sides with no excuse, unachokisimamia hakileti maana sahihi, the way this world operates ni kila kitu kina gharama yake ndg!
 
madaktari ni muhimu watafakari upya ajenda yao ya mgomo. mgomo wao wangeuitisha mwezi wa tisa baada ya kuangalia utekelezaji wake wa bajeti. wakumbuke even today ktk watumishi wa umma wao wanalipwa vizuri kuliko wengine.

hata madai yao mengi yametekelezwa, waipe muda serikali

Nikukumbushe mkuu jambo hapa,mashine ya T'Scan zipo mbili ktk hospitali za Serikali hapa Tanzania na pia hiyo iliyopo katika Hospital ya Muhimbili imeharibika ni mwezi Wa Sita sasa haijatengenezwa na papo hapo wagonjwa wanaohitaji Huduma hiyo hawaipati zaidi ya kwenda hospital za private ambako gharama ni kubwa.Italeta tija gani Kama utamlipa daktari mshahara mkubwa pmj na posho lakini vitendea kazi akavikosa?Tunachotaka wananchi wa Tanzania tunahitaji Serikali iboreshe mazingira ya hospitali zetu kuanzia uwepo Wa dawa kwa wakati/vitendea kazi vyote vinavyohitajika/uongozi imara unaofuatilia mambo kwa wakati ktk wizara hii ya afya nk.Wananchi tunaomkataba na Serikali na hatuna mkataba na madokta,Serikali iwajibike ipasavyo kwa madokta papo hapo itakuwa imewajibika kwetu sie wananchi.
 
Mkirua unaudhi ile mbaya,nadhani unaongea kishabiki wewe,na sio hao unawasema wanashabikia,wewe ndo unashabikia kishabiki na ushabiki huu ni ule wa Nyinyiemu-CCM.for sure wewe umetumwa na Nape,unaangalia matokeo badala ya kuangalia chanzo cha tatizo.hivi reflect hili suala la madaktari ambalo ni lao wao,naaminisha maslahi yao kama wao,Je ungelikuwa wewe unaefanyiwa hayo ungeliona ni sawa tu?hivi ni kweli serikali haina pesa ya kuwaongezea mishahara na posho zingine wanazoziomba,je matumizi ya anasa ya hizo pesa zinazo fujwa na viongozi mafisadi chini ya CCM zinatoka wapi?wewe uko tayari kulipwa ujira kidogo wakati unafanya kazi kubwa?
Kingine sidhani kama huwa unaenda hospitali zetu sisi walala hoi,madktari wanadai mazingira ya kufanyiia kazi yaboreshwe,kinachomaanishwa hapa wanataka vifaa tiba vya kutosha na vya kisasa,wanataka majengo ya kutosha wanataka vitanda vya kutosha mahospitalini na vitu vingine ambavyo ni essential katika utendaji wao wa kazi.sasa haya yote unaona ni upuuzi au,haya yote unaona tunashabikia sio,hujawahi kuuguliwa au kuugua kiasi kwamba ikabidi ulazwe ndio maana unaropoka.ujinga huu unaofanywa na chama chako hauwezi kuisha bila watu ku-sacrifice.najua tutakufa,na huenda ikawa ni mimi lakini ni vema saratani hii iitwayo CCM iondoke.maana haya yote ni sababu ya udhaifu wa chama cha magamba.wacha tushabikie lakini one day yes ukombozi utapatikana.
chonde chonde madaktari msi-beep tafadhalini pigeni

jigoku Pole sana kwa kukuudhi ingawa pia ninaposimamia kile ninachoamini kuwa kipo sahihi sina haja ya kumfurahisha yeyote...Kama naweza kufanya hilo kwa ninaoishi nao na kufanya nao kazi sembuse kwa avata inayojiita Jigoku?? Hiyo sio mission yangu....

Pili acha kukurupuka na soma between lines kuanzia mwanzo wa argument yangu. Mwisho tabia ya kuona kila unayetofautiana naye katumwa na Nape humu jukwaani inatushushia hadhi wana JF na ukome kunitusi kuwa mimi nimetumwa na nape....haya ni matusi kwangu.
 
Mkuu nafikiri nyakati hizi ambapo vijana wengi wamepiga shule ni muhimu kupigania kupinga hii trend iliyojengwa karibuni - kwamba siasa na wanasiasa wanathaminiwa na kutuzwa kuliko elimu+wenye elimu zao walizosotea kwa viwango mbalimbali!! Tumekuwa Taifa lisilo na dira ya vipaumbele!

Sijakuelewa mkuu?
 
Watumie vizuri nafasi yao ya kupiga kura ili wachague serekali makini itakayotumia vizuri rasilimali tulizojaliwa ili wafanyakaze wote walipwe vizuri..

Ambacho sikubaliani nacho hapa ni kushabikia matendo yatakayopelekea madhara kwa wasioukuwa na hatia kwa sababu tu tunataka kuiadhibu serekali ambayo to my opinion haiathiriki katika hili...

Mbona na wewe ni kama unaishabikia serikali ambayo imeshindwa kutimiza wajibu wake na kupelekea mgomo wa madaktari? Bila ushabiki, serikali pia ina madhambi yake makubwa tu katika hili. Haiwezekani serikali ikakosa hela ya kumlipa daktari vizuri lakini wakati huo huo ikawepo ya kumlipa mbunge. Kama inawezekana kugharamia safari za viongozi kadhaa (rejea kilichokuwa mbioni kuibwa wizara ya Membe) kwa bilioni kadhaa kwanini isiwe na uwezo wa kuwalipa madaktari. Hata hivyo waswahili walisema ''Kupanga ni kuchagua'' na nionavyo mimi, tumechagua mgomo!!
 
Msimu mwingine wa maumivu kwa raia wasio na hatia.
Nawashauri madaktari warudi mezani kwa mazungumzo.Siamini kama madokta wana hali ngumu kuliko kada zingine za utumishi wa umma.
Enyi madaktari vaeni uzalendo na kuthamini uhai wa binadam wenzenu.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Uko sahihi kabisa.....pata picha kila kitu kitakapokuwa kimesimama.....

Pili je, tunamuadhibu nani hapo?? serekali? Kwa maana ya nani?Kikwete Pinda au hussein Mwinyi wa wategemezi wao??.....
Mimi siyo daktari ila mke wangu ni daktari, MD! Hali iliyoko kwenye hospitali zetu ni afadhali mgomo kuliko hiyo hali. Nasema hivyo kwa sababu madaktari wapo, lakini vitendea kazi hakuna. Unategemea kila mgonjwa atatibiwaje kama hata sindano tu, visu vya kufanyia operation, pamba za kusafishia, mipira midogo ya kusaidia mtu kupumua wakati anapokuwa hajiwezi pamoja na mazingira magumu ya kufanyia kazi.
Pamoja na hilo la kudai nyongeza ya mishahara, lakini kuna madai ambayo ni msingi na ni ya faida kwa mtanzania si kwa madaktari tu. Bazi serikali kupitia kwa viongozi wahusika waseme ukweli waache siasa kwenye inshu sensitive kama za afya nini wanakifanya kuboresha hospitali hata kwa kuweka gharama fulani kwa ajili kutibu watu. Wakati nchi zingine zikiamini kila mtu anayo haki ya kuishi, kifo ni bahati mbaya tena kwa ajali au uzee, sisi watu tena nguvu kazi inapoteza maisha kizembe kabisa kwa daktari kukosa vitendea kazi kwa ajili ya kumsaidia mgonjwa.
Fikiria, mgonjwa anapoteza maisha mbele yako kwa kukosa kisindano! pengine huyu daktari kawasaidia watu zaidi ya kumi (mfano mke wangu) kwa kuwanunulia sindano sasa kaishiwa pesa, anamuona mgonjwa yule anahitaji kitu kidogo tu lakini hana jinsi inabidi akubali mtu yule apoteze maisha. Sasa, hapo unafikiria akili ya huyo daktari itakuwaje? kumbuka daktari naye ni binadamu.
Its too sad, wakati mtu mwenye kufanya maamuzi ya nini kifanyika kusaidia wananchi anapiga siasa pamoja na vitisho huku wengine wakiendekeza uzinzi. Ningekupa mifano ya jinsi wagonjwa wanavyopoteza maisha kizembe si kwakuwa daktari hawezi kumtibu lakini kwa kukosa vifaa vya kumsaidia yule binadamu mwenzako.
 
Msimu mwingine wa maumivu kwa raia wasio na hatia.
Nawashauri madaktari warudi mezani kwa mazungumzo.Siamini kama madokta wana hali ngumu kuliko kada zingine za utumishi wa umma.
Enyi madaktari vaeni uzalendo na kuthamini uhai wa binadam wenzenu.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Sijakuelewa mkuu?

Linapokuwa ni swala la mishahara au posho za wanasiasa wetu pesa zipo nyingi tu, ila linapokuja swala la maslahi halali ya watumishi wengine wa umma wa kada mbali mbali e.g walimu, madaktari, maprofesa nk nk inabidi kuvutana mashati wakati nyasi zikiumia! (Nyasi - wanafunzi, wagonjwa, wanachuo nk)
 
Haya ni matunda ya serikali inayoendeshwa kisanii. Najiuliza kuwa, je, serikali kukimbilia mahakamani kutawafanya madaktari wafanye kazi, au ndo kutawaongeza hasira? Unaweza kumlazimisha punda kwenda mtoni, lakini je unaweza kumlazimisha kunywa maji? Hakuna njia ya mkato hapa, ili hawa madaktari wafanye kazi kwa furaha, ni lazima muafaka ufikiwe kwa serikali kutekeleza madai yao na si vinginevyo! Nionavyo, kwenda mahakamani kunachochea hasira zaidi. Na lingine tunalopaswa kufahamu ni kuwa hakuna mgomo usiokuwa na athari, mbaya! Mgomo wa madaktari utapelekea watu kufa na hatupendi jambo hili. Kwa kuwa serikali inaleta usanii kwa kuyapuuza madai yao ya msingi, haya yatatokea na ni lazima serikali iwajibike kwa hili.
 
Msimu mwingine wa maumivu kwa raia wasio na hatia.
Nawashauri madaktari warudi mezani kwa mazungumzo.Siamini kama madokta wana hali ngumu kuliko kada zingine za utumishi wa umma.
Enyi madaktari vaeni uzalendo na kuthamini uhai wa binadam wenzenu.
Mungu ibariki Tanzania.

Kama nililielewa vema Tamko la madaktari ni kwamba wako tayari kurudi kwenye meza ya mazungumzo! Mie naona serikali haina utashi wa kweli wa kulimaliza hili jambo! Wanafanya siasa at the cost of innocent lives!
 
Back
Top Bottom