Madaktari waanza kuikimbia nchi..

Mkuu tuweni objective na madai ya madaktari wetu (hapo kwa red). Wanachopigania ni maslahi yao, hili la vifaa ni kipandio tu ili wapate public support. Hivi unajua vifaa ni one point ktk orodha yao yenye madai 12?

madai yalikuwa 8,hayo mengine wameongeza kina mwinyi na wenzao. Hivi wewe, kupunguza viongozi kwenda nje ilid fedha ziboreshwe haikusaidii? Nyumba ya daktari ikiwa karibu na hosp ili asichelewe haikusaidii? Daktari akiwezeshwa vizuri ili akuhudumie with full conc haikusaidii? After all kila mtu atapigania haki yake.
 
Goodness me!

The government has already set aside Tsh200 billion ($100 million) to employ foreign doctors. The amount is way above the cost of training a doctor in the country —Tsh100 million ($64,034.4) over five years.
 
JAMANI WAAACHENI WAENDEEEE, HUENDA HII DHAHAMA YA KUTISHANA YA KITOTO KABISA ITAISHA
Mimi nakubali kabisa hawa madaktari walikuwa hawanisaidii ntabaki natibiwa hata na Manesi au MaMedical ambao walipita huko JKT wanaujua Uzalendo, hao wanaojidanganya eti ataenda Botswana wakati Leseni yake imefutwa ni uongo Mtupu hawatapokelewa,
  • Kwanza ni lazima Ubalozi wetu uwachuje,
  • Pili Nchi za wenzetu huwezi kumgusa Raia wao na kumuandikia sindano wakati huna Leseni toka nchi uliosomea au cheti cha Chuo husika
  • Hao Madaktari tuwaombee safari njema kuna kazi nyingi tu huko hata km si za Udaktari wakafanye
  • Ni kweli walikuwa sio wazalendo maana walitaka kujipima na wabunge, hivi na Wahasibu Mainjinia wanajeshi, Polisi wanasheria nao wafanye hivyo?
  • Acheni waende wametumwa hao tutawasiliana nao humuhumu JF wakitutukana lakini msg send na picha imefika THE END tusubiri mgomo wa wengine, Wakulima

Ni vyema ukasoma hoja za mwanzisha 'uzi' (thread) ukazielewa kabla ya kuchangia..ukikurupuka tuu ndio unajibu bla bla blaah kama hapo juu!

- Kwanza kabisa, posti imesema wazi maDaktari walioondoka na wanaopanga kuondoka ni 'medical specialists', yaani maDaktari bingwa...inakuchukua si chini ya miaka mi5 baada ya kumaliza digrii ya kwanza ya uDaktari mpaka kuwa specialist. Hawa wote wana vyeti na leseni halali!

NB: Waliofutiwa leseni za muda (provisional registration) ni maDaktari walio katika mafunzo ya vitendo (intern doctors), sio maSpecialists.

- Kuna maDaktari wengi sana maSpecialists ambao wanafanya kazi Botswana, Namibia, Swaziland na South Africa ambao hawajachujwa na balozi zetu, ni ubalozi wa Tanzania - Rwanda ndio huwa unakeep record ya waTanzania (maDaktari) walioajiriwa huko....niana maRafiki wengi maSpecialist wanafanya kazi huko na wengine wako kwenye process za kwenda huko.

Nashukuru kwa kuwaombea safari njema wahanga hawa wa kitaaluma..baraka zako kwao zitafika tu na watafanikiwa katika malengo yao!
 
wangesema hivyo tangu mwanzo wangepata support kubwa, tuliwadharau walipotaka kujilinganisha na wabunge...

Kwani wabunge sio watanzania kama mimi na wewe? Tunajenga matabaka halafu matatizo yakitokea tunatumia nguvu kuyazima? Hatujiulizi tutaweza kufanya hivyo kwa muda mrefu kiasi gani!
 
Hawa madaktari wetu serikali ikitaka kuleta Madaktari kutoka nje wanalalamika wanasema ni aibu kuleta madaktari kutoka nje halafu wenyewe wanasema wanaenda Botswana, Lesotho, Swaziland, South Africa, sasa raia wa hizo nchi hawasemi ni aibu kutibiwa na wageni...
Wanaweza nao wakasema hivo kama wenyeji wamegoma kwa kudai mazingira bora,na mishahara. Hi dr. Wa kigeni anaweza kulipwa sh.ngapi?
 
Mkuu tuweni objective na madai ya madaktari wetu (hapo kwa red). Wanachopigania ni maslahi yao, hili la vifaa ni kipandio tu ili wapate public support. Hivi unajua vifaa ni one point ktk orodha yao yenye madai 12?

sion kama kuna ubaya kama madai ya vifaa yamejitokeza mara moja,,,,,,,hakuna asotaka maisha mazuri bhana,,,,waache wapigane nao waishi kama wanavoishi wezi halali(wanasiasa)
 
madai yalikuwa 8,hayo mengine wameongeza kina mwinyi na wenzao. Hivi wewe, kupunguza viongozi kwenda nje ilid fedha ziboreshwe haikusaidii? Nyumba ya daktari ikiwa karibu na hosp ili asichelewe haikusaidii? Daktari akiwezeshwa vizuri ili akuhudumie with full conc haikusaidii? After all kila mtu atapigania haki yake.

sure,sijawah kusikia wabunge wakiongelewa suala la mishahara yao,,,,,,,ila hujiongelea wenyewe
 
Inauma lakini tujiulize
kwa nini wanaondoka leo

moja, ni kutokana na mlolongo wa matukio migomo kutaka maslahi bora kwa kila mtanzania /uboreshaji wa huduma za afya unawagusa watanzania wote hata mafisadi kwani ndugu zao hutibiwa humu humu nchini/
daktari akilipwa vizuri hakika kazi yake itakuwa nzuri pia atapata muda wa kujisomea kwani kutakuwa hakuna sbb za msingi za yeye kutangatanga kwenye hospitali zingine....

Faida za wao kuondoka
wanakoenda taaluma yao inathaminiwa,vitendea kazi vinapatikana hivyo kazi yao itakuwa imerahisishwa watapumzika kupiga ramli kitu ambacho hawakusomea..,watapumzika kuona wat wanakufa kwaukosefu wa vifaa ambavyo mara nyingine hugharimu sh 1500/ tu pia kuona watu wanakufa kwa sababu tu mazingira ni machafu na hakuna dawa za kusafishia lakini wananchi hawajui hili na wao wanaona ni sawa tu .
Tukiangalia ktk masuala ya utaalamu watafaidika sana in terms of resources ambazo kule zipo hivyo kama baada ya muda wataamua kurudi nyumbani basi watarudi na utaalamu wa kutosha ambao utasaidia watz kwa ujumla

hasara watakayoipata madr
bwana we nyumbani ni nyumbani
huko wanakoenda wao watakuwa wageni tu
 
JAMANI WAAACHENI WAENDEEEE, HUENDA HII DHAHAMA YA KUTISHANA YA KITOTO KABISA ITAISHA
Mimi nakubali kabisa hawa madaktari walikuwa hawanisaidii ntabaki natibiwa hata na Manesi au MaMedical ambao walipita huko JKT wanaujua Uzalendo, hao wanaojidanganya eti ataenda Botswana wakati Leseni yake imefutwa ni uongo Mtupu hawatapokelewa,
  • Kwanza ni lazima Ubalozi wetu uwachuje,
  • Pili Nchi za wenzetu huwezi kumgusa Raia wao na kumuandikia sindano wakati huna Leseni toka nchi uliosomea au cheti cha Chuo husika
  • Hao Madaktari tuwaombee safari njema kuna kazi nyingi tu huko hata km si za Udaktari wakafanye
  • Ni kweli walikuwa sio wazalendo maana walitaka kujipima na wabunge, hivi na Wahasibu Mainjinia wanajeshi, Polisi wanasheria nao wafanye hivyo?
  • Acheni waende wametumwa hao tutawasiliana nao humuhumu JF wakitutukana lakini msg send na picha imefika THE END tusubiri mgomo wa wengine, Wakulima

...nazani haujui maana ya ''LESENI NA CHETI/CERTIFICATE'',ngoja nikutofautishie kidogo ili uelewe na pia ukawaeleweshe na wengine walio na kichwa kama chako,
1) Leseni anayoipata Daktari baada ya kufanya Intern inamuwezesha kufanya kazi nchi husika iliyopatia leseni,kwa kuangalia vyeti vyake pia na kuhakiki kuwa vinakidhi viwango vya Elimu ya Udaktari kutokana na nchi husika!!!
2) Cheti/certificate ni sawa na kile cheti chako cha form four au six,unakipata shuleni/chuoni,hakiingiliani na leseni,ila KUPATA LESENI NCHI YOYOTE ile ni lazima uwe na cheti/certificate yako,NAKUULIZA SWALI-HIVI WEWE UNAPOSEMA HAWATAKUWA NA VYETI,BAADA YA KUFUTIWA LESENI ZAO,KWANI SEHEMU UNAZOOMBAGA KAZI HUWA UNAPELEKA VYETI ORIGINAL AU FOTOCOPY YA VYETI!!!??(NADHANI JIBU UNALO-NA USHAJITAMBUA KUWA HUKUSHIRIKISHA KICHWA KABLA YA KUANDIKA ULICHOANDIKA).
Kwa taarifa yako,Intern inakuwezesha kusajiriwa ktk Bodi ya Madaktari wa nchi husika kwa kukupatia Leseni ya kupractice nchi husika na WORLD WIDE Mkuu!!!

Au haujawahi kusikia kuwa nchi fulani haitambui elimu ya fani fulani kutoka nchi fulani,ingawa hao watu wanaprctice bila tatizo kwao!!??
 
Ndani ya siku 9 zijazo kutasikia jambo la ajabu msilotegemea kwa nchi ya Tanzania. Na huo ndio utakuwa mwanzo tu wa hayo mambo yasiyotarajiwa.

Ondoa habari za mafumbo na za kusadikika, kama una jambo lete hoja watu wajadili na si kuficha ficha, hii siyo facebook!
 
Mkuu Mpayukaji, umeshapayuka tayari kusema mitanzania ni mizezeta, uzezeta wetu ndiyo turufu wanayoitumia ccm kuchezea haki zetu. mfano mzuri humu jf. wanazi wa ccm watakuwa tayari kushabikia jambo lolote hata kama serikali yao itapitisha kwamba wanaume wote wa tz tuwetunalawitiwa, manazi wa ccm wao wataunga mkono.

Mweee!
 
JAMANI WAAACHENI WAENDEEEE, HUENDA HII DHAHAMA YA KUTISHANA YA KITOTO KABISA ITAISHA
Mimi nakubali kabisa hawa madaktari walikuwa hawanisaidii ntabaki natibiwa hata na Manesi au MaMedical ambao walipita huko JKT wanaujua Uzalendo, hao wanaojidanganya eti ataenda Botswana wakati Leseni yake imefutwa ni uongo Mtupu hawatapokelewa,
  • Kwanza ni lazima Ubalozi wetu uwachuje,
  • Pili Nchi za wenzetu huwezi kumgusa Raia wao na kumuandikia sindano wakati huna Leseni toka nchi uliosomea au cheti cha Chuo husika
  • Hao Madaktari tuwaombee safari njema kuna kazi nyingi tu huko hata km si za Udaktari wakafanye
  • Ni kweli walikuwa sio wazalendo maana walitaka kujipima na wabunge, hivi na Wahasibu Mainjinia wanajeshi, Polisi wanasheria nao wafanye hivyo?
  • Acheni waende wametumwa hao tutawasiliana nao humuhumu JF wakitutukana lakini msg send na picha imefika THE END tusubiri mgomo wa wengine, Wakulima

Mkuu, jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza, ndivyo walivyosema wahenga hapo kale.
Hiyo leseni unayoizungumzia si kitu bali ni kibali tu cha kufanyia kazi TZ.

Cha muhimu ni cheti chako cha kuhitimu elimu husika na kama kinatambulika au chuo ulichosomea kinatambulika katika nchi hiyo. Nje ya Tz utaulizwa cheti, uwezo na ufahamu wako kwa taaluma yako na si leseni yako ya TZ.

Kwa hiyo kukosa leseni hakukubani wewe kushindwa kufanyakazi katika nchi nyingine nje ya TZ.
 
The government has already set aside Tsh200 billion ($100 million) to employ foreign doctors. The amount is way above the cost of training a doctor in the country —Tsh100 million ($64,034.4) over five years.

Hii serikali imechanganyikiwa sasa 200bn si ingeweza kuboresha maslai ya madakatari kwa kipindi cha hata miaka miwili wakati wakiendelea kutafuta fedha zingine.
 
waondoke tu - huduma yao ni tradable ina uwezo wa kuuzika nje. kuwepo kwao hapa ni sawa na bure maana wanatia kichefu chefu tu. wasepe tu kama nako kule watazifanya hospitali za serikali vijiwe vya kupoka wagonjwa na "kuwalazimisha" kwenda hospitali zao binafsi na maduka yao ya dawa zinazotoka bohari za dawa za serikali. wanasahau kuwa serikali muda wote imefumbia kanuni za utumishi na kuwaacha wajifanyie kazi zao binafsi za kutibu kwa kutumia muda na vifaa vya serikali na hivyo kuikosesha serikali mapato ya kusaidia kuendesha hospitali.

daktari uko hospitali ya serikali ulioifanya kijiwe unamwambia mgonjwa tuonane kwenye hospitali yangu ulipie laki tatu kwa kukufunga pop. umeinyima serikali chini ya laki na mshahara umeupata juu na bado unaamua kuuwa wa Tz kwa kugoma - shame!!!
 
Bahati nzui ni marufuku kutukanana humu, lakini wewe kama si mmoja wa wanaonufaika na matibabu ya bure nje ya nchi sijui ni nani tena. Yaelkea huna macho ya kuona na huna masikio ya kusikia. Udhalili wote unaowapata madaktari huuoni na wala huusikii? Lakini uko tayari ku-justify safari 360+ za nje ya nchi za rais wako, ia daktari akiomba dola 100 zaidi ni kituko? Ama kweli wee......lakini tupo, yatakufika hata wewe!

Ni vyema wakakimbia kabisa. Nchi hii kama huwezi kuwa fisadi basi utaishi maisha ya kubangaiza sana. Ni kwanini usome kwa shida kisha wewe na familia yako muishi kwa shida wakati uwezo wa kutafuta maisha mazuri uishi kama wenzako wenye nguvu na uwezo wa kufanya ufisadi?

Mtu yeyote ambaye anaona kuwa hawa madaktari wanaoondoka kutafuta greener pastures hawafanyi jambo sahihi, ni aidha mbinafsi au uwezo wake wa kudigest mambo ni mdogo sana. Ni vyema usichangie mada ungali na upeo mdogo wa kuelewa kinachozungumziwa.
 
Mwenyezi mungu amesikia kilio cha wanyonge, madaktari wakatili hao ametuepushia. Waende huko wakajiuze.
You have a very weird way of thinking. As much as it is your right to think differently, you are impeding development of your society if your have in you a feel of belonging here in Tanzania
 
Hii serikali imechanganyikiwa sasa 200bn si ingeweza kuboresha maslai ya madakatari kwa kipindi cha hata miaka miwili wakati wakiendelea kutafuta fedha zingine.

Mkuu huko ni kubangaiza - sustainable source inahitajika na sio hizi sunken costs - don't cry over spilled milk!!!!
 
Back
Top Bottom