Watanzania tuache ushabiki wa kinafiki kana kwamba hatujazaliwa hapa nchini kwa kutetea vitu ambavyo dhairi kila ambae alishawahi kufika hospital za serikali ni shahidi. Hali za hospitali zetu zinatisha, wagonjwa wanalala chini, wakinamama wanajifungua katika hali hatarishi na wengi wao wanapoteza maisha kwa kuvuja damu nyingi baada ya kujifungua kwa kuwa imekosekana sindano ya kuzuia damu, wenzetu wanakufa mapokezi kwa kukosa huduma staili.
Madaktari wanadai vitu vya msingi kabisa ila sie ambao hayajatukuta na wala hatujui kinachoendelea katika vituo vya afya tumekalili madai ya madaktari ni posho na mishahara.
Hizo 200 bilioni za kuwaleta madaktari kutoka nje zimetoka wapi kama serikali imekiri kupitia kwa rais wetu kwamba haina pesa ya kushughulikia matatizo ya madaktari? Hawa wanaojiita madaktari by experience wanaokuja hawajui kiswahili na isitoshe kuna wengi wao pia hawajui hata kiingereza. Unategemea nini hapo? Na hata kama wakija na vitendea kazi visipoletwa hakuna kitakachofanyika zaidi ya kubebeshwa lawama etc.
Tuache ushabiki wa siasa bali tuchambue uhalisia wa tatizo lenyewe kwa kutazama ukweli halisi.