Madaktari wa Muhimbili: This is unprofessional....!

Halo jamani mnachosema ni sahìhi ila kwa habari ya hicho ieleweke kuwa madaktari huwa wanajifunza kwa vitabu na kwa vitendo pia. Unajua ikiwa mgonjwa mmoja kwenye vipimo ana findings ambazo zimeonekana, hivyo ni muhimu awashirikishe wanafunzi maana ndo maspecialists wa kesho. Hivyo ukimkatalia leo asijifunzie mgonjwa wako, jua kesho itatokea wewe au jamaa yako au mtu mwingine kaugua ugonjwa huohuo na wa kumhudumia ni huyo daktari ambae leo ni mwanafunzi. Mpaka huyo daktari kuwakusanya wanafunzi wa udaktari alikuwa sahihi kabisa ili wawe exposed kwa ajili ya msaada wa kesho. Hebu tufikirie kabisa kwa upande mwingine ile ni teaching hospital ingekuwa labda anasema hivyo kwa watu ambao wake nje ya profession hilo ni kosa na si maadili ila kuwafundisha wengine hiyo ni hazina ya kesho ni lazima kuwekeza for future.
Tatizo sio kufundishia mgonjwa alliye wodini, tatizo ni misconduct katika presentation yake kwakuwa pale kulikuwepo mult audience na pia possibility ya kusikiwa na mgonjwa husika ilikuwa kubwa hivyo alikiuka Daktari ana kanuni ya Re assurance of the Patient hata kama anakaribia kukata roho hutakiwi kumwambia. Hivyo tatizo si kufundishia mgonjwa kwa sababu hata kwenye Anatomy Dissecting ni maiti zinatumika
 
pole sana ndugu wa mgonjwa, naomba tu upunguze jazba, hakuna m2 aliyezaliwa akijua kuongea wote wanajifunza na kufunzwa pia, katika hospitali kama muhimbili mgonjwa akishaingia wodini tayari ni kitabu kwa kuwa kuna madaktari wanofanya kazi kwa uangalizi wa wenzao na wapo wanaoongeza elimu na pasipo kutumia wagonjwa hatutaweza kutengeneza madaktari wengine.
kuna mida maalum yakuona wagonjwa na wakati madaktari wanakuwa na mgonjwa ni jambo la hekima kwa ndugu kutoa mwanya lakini kwa wa TZ wengi hawafuati utaratibu, hasa pale ndugu wa mgonjwa anapokuwa mtumishi wa afya au anavijisent na nafasi kidogo yakisiasa ndiyo wataomba vibali mpaka ikulu ili tu awe na mgonjwa wakati wote.

kuna magonjwa yanayoonekana kwa nadra na hivyo anapotokea mgonjwa mwenye tatizo kama hilo au mwenye dalili na alama kama kitabu hutumika sana kufundishia kwakuwa kusikia m2 husahau kwa asilimia nyingi, kuona huongeza kumbukumbu na kugusa huweka mihuri na uhakika katika jambo husika, fuatilia kisa cha tomaso.

matambue kuwa mgonjwa wa mgonjwa wapaswa kuwa siri kati yake na daktari/madaktari wake hivyo nawe ulipokuwa unataka majibu ya mgonjwa ulimuomba mgonjwa ruksa ya wewe kupokea majibu yake?

kama kawaida katika kila sekta huwezi kuwa na watu waaminifu katika mambo sensitive kama siri za wagonjwa hivyo kwa wale wanaotoa taarifa za wagonjwa wao wanapaswa kukemewa kwa nguvu zote kupitia katika masanduku ya maoni na kamati za afya za vijiji, kata........
uzi ni kwamba muda huo ulikuwa wa
jambo la msingi ni kushirikiana na kuheshimiana,
Kwa mujibu wa bwana muttabuzi ni kwamba muda huo ulikuwa wa kutizama wagonjwa na madaktari walikuwa wanamalizia round, I guess walichelewa kumaliza wakakutana na muda wa kutembelea wagonjwa
 
Mkuu hapo utakuwa umedandia Fastjet tena kwenye tairi bila kujua tairi huwa linaingia ndani na kuweza kuhatarisha maisha yako. Sielewi Kama tatizo hapa ni kusoma au kumuelewa bwana Mtambuzi alikuwa anaongelea nini!?

Mtambuzi ametujuza yaliyomfika,ni kitu ambacho kinaweza kumtokea binadamu yoyote muda wowote. Nitamquote Bw. Mtambuzi ili iweze kukusaidia hapo mbeleni.
Mtambuzi aliandika "Lakini pale dakatari anapowaambia wanafunzi wake kwamba huyu mgonjwa aliyeko mbele yao yuko katika TERMINAL STAGE huku wanaomuuguza wakiwa karibu na hata mgonjwa mwenyewe akisikia, huu ni uuaji. Daktari huyo aliendelea kuwaonyesha wanafunzi wake dalili zinazothibitisha kuwa mgonjwa wetu yuko kwenye terminal stage".

Hakuna sehemu aliyoandika kulalamika au kukasirika kutokana na mgonjwa wao kuwa katika "TERMINAL CARE". Tatizo hapa lilikuwa ni kwa Ndugu wa mgonjwa kutojua au kupewa majibu kutoka kwa Madaktari.
Kutembea UK na kurudi sio tija siku hizi mkuu...wala hakumfanyi mtu awe mjuaji wa mambo.

Kwa taarifa yako katika hizo "Dunia" unazoongelea wewe Hilo Jambo lililotokea sio la kawaida. Kwa kuwa wenzetu wanajali sana na kuzingatia taarifa na hali ya mgonjwa. Isitoshe huko UK unakozungumzia hao jamaa wana kitu kinaitwa Code of conduct na accountability.

Sasa hapa sijui ni wewe uliyetembelea UK au Mtambuzi anayelalamika bila kujua!!???
r
Mkuu humu jf kuna watu wanaopenda kujibu hata mada wasizosoma kwanza, ila hata kwenye jamii wapo unaweza ukawa unamulekeza mtu jambo hakusikilizi ila anapanga atakujibu nini!!
 
pole ndugu Mtambuzi naamini kabla ya kumuondoa mgonjwa wako ulitoa mrejesho/malalamiko kwa wahusika hapo muhimbili.
 
Last edited by a moderator:
Haki ya mgonjwa jua kama yeye ni mgonjwa darasa vipi hapo?
Pole sana mtambuzi,lakini tatizo letu wabongo tunapenda kudanganywa mgonjwa akiambiwa ukweli hatupendi.Pili muhimbili ni hospitali ya kufundishia,kwahiyo huwezi kwepa mgonjwa wako kutumika kama kitabu.
 
walimueleza mgonjwa? Unadhani ni sahihi mgonjwa kujua hali yake kwa staili hiyo?

Pia utamtumiaje mhinjwa kama darasa bila idhini yake? Na watu kama nyie mnajaribu kahalalisha hilo?

It's a teaching hospital for gods sake ...
 
Kimaadili, katika hospitali ambayo kuna chuo cha kufundisha madaktari inatakiwa mgonjwa wakati analazwa apewe form ya kujaza kama anakubali au kukataa kutumika katika kufundishia madaktari. Je, fomu hii mlipewa?

Kuhusu daktari kutamka lugha hiyo mbele ya mgonjwa inasikitisha, lakini turudi nyuma kidogo. Je, mgonjwa alipewa taarifa kuwa yuko kwenye terminal stage kabla ya tukio hilo? if yes, je aliipokeaje taarifa hiyo? Iwapo mawasiliano kati ya mgonjwa na daktari yamefanikiwa, mgonjwa akajua hali yake na kuikubali, kunakuwa hakuna kosa kuwaambia wanafunzi mbele yake. Tatizo linakuja pale mgonjwa anapojua kwa maa ya kwanza kuwa yuko kwenye terminal stage kupitia maneno ya daktari akiongea na wanafunzi wake!!!

unakosea mnh ndugu haruhusiwi kuwepo wodini wakati wa round sema kuna relative wanakera mnapita round yy kwasababu anajuana na flan wale alinzi na manesi wakimtoa analetadharau ndo maana at the end wanakua wametega maskio dr atraongea nn jamaa ni mnafki tu
 
pole sana ndugu wa mgonjwa, naomba tu upunguze jazba, hakuna m2 aliyezaliwa akijua kuongea wote wanajifunza na kufunzwa pia, katika hospitali kama muhimbili mgonjwa akishaingia wodini tayari ni kitabu kwa kuwa kuna madaktari wanofanya kazi kwa uangalizi wa wenzao na wapo wanaoongeza elimu na pasipo kutumia wagonjwa hatutaweza kutengeneza madaktari wengine.
kuna mida maalum yakuona wagonjwa na wakati madaktari wanakuwa na mgonjwa ni jambo la hekima kwa ndugu kutoa mwanya lakini kwa wa TZ wengi hawafuati utaratibu, hasa pale ndugu wa mgonjwa anapokuwa mtumishi wa afya au anavijisent na nafasi kidogo yakisiasa ndiyo wataomba vibali mpaka ikulu ili tu awe na mgonjwa wakati wote.

kuna magonjwa yanayoonekana kwa nadra na hivyo anapotokea mgonjwa mwenye tatizo kama hilo au mwenye dalili na alama kama kitabu hutumika sana kufundishia kwakuwa kusikia m2 husahau kwa asilimia nyingi, kuona huongeza kumbukumbu na kugusa huweka mihuri na uhakika katika jambo husika, fuatilia kisa cha tomaso.

matambue kuwa mgonjwa wa mgonjwa wapaswa kuwa siri kati yake na daktari/madaktari wake hivyo nawe ulipokuwa unataka majibu ya mgonjwa ulimuomba mgonjwa ruksa ya wewe kupokea majibu yake?

kama kawaida katika kila sekta huwezi kuwa na watu waaminifu katika mambo sensitive kama siri za wagonjwa hivyo kwa wale wanaotoa taarifa za wagonjwa wao wanapaswa kukemewa kwa nguvu zote kupitia katika masanduku ya maoni na kamati za afya za vijiji, kata........

jambo la msingi ni kushirikiana na kuheshimiana,

Tatizo lako kubwa sana hujaelewa kinacholalamikiwa hapa. Halafu unaandika na kisirani.
 
Kuna chief mmoja tukiwa round akasema this is the dying patient,duh nilishtuka hata mi mwenyewe nikawaza wat if mgonjwa ameelewa maana yake.ndo ivo madr wetu uzoefu unamfanya asione ishu kutamka neno km hilo,its not ethical kwakweli
 
relative mkiambiwa mtoke nje wakati wa kuita round madokta mnakataa huo ndio mshahara , kimsingi walikuwa wanawafukuza kiujaja tu , poleni kwa kusikia hatma ya mgonjwa wako:-*
Mama mkwe wangu alilazwa Muhimbili kwa wiki moja, lakini jana nililazimika kumtoa kutokana na kile nilichokishuhudia pale. Pamoja na vituko vingi tu tulivyoviona kutoka kwa manesi wa ward ya Mwaisela, lakini nisingependa kuzungumzia hayo kwa kuwa si mageni masikioni mwa wengi. Tulimpeleka mgonjwa wetu kufanyiwa uchunguzi zaidi kutokana na kuwa na complication nyingi nadhani ni kutokana na uzee (mkwe wangu ana miaka 70 hivi sasa)

Tulipofika pale alichukuliwa vipimo vyote ikiwapo x-ray, tatizo lilikuwa ni pale madaktari wanapopita round kuona wagonjwa. kwanza walikuwa wamemgeuza mama mkwe wangu kama vile ni darasa la kufundishia wanafunzi, kila daktari alikuwa anafika na wanafunzi wake na kufungua darasa. Cha kushangaza walikuwa wameyakalia majibu ya mgonjwa wetu huku wakiendelea kumuweka pale kama mtu wa kufundishia wanafunzi.

Sikatai mgonjwa kutumika kufundishia wanafunzi, hawa ni ndio madaktari wetu wa kesho wakajifunzie wapi. Lakini pale dakatari anapowaambia wanafunzi wake kwamba huyu mgonjwa aliyeko mbele yao yuko katika TERMINAL STAGE huku wanaomuuguza wakiwa karibu na hata mgonjwa mwenyewe akisikia, huu ni uuaji. Daktari huyo aliendelea kuwaonyesha wanafunzi wake dalili zinazothibitisha kuwa mgonjwa wetu yuko kwenye terminal stage.

Kitu ambacho madaktari wale walikuwa hawakijui ni kwamba mke wangu pamoja na dada yake ni wauguzi by professional na wanazijua hizo terminology vizuri sana. Sasa iweje waropoke hivyo bila kuangalia walioko karibu. kitendo hicho kilifanyika muda wa kuona wagonjwa na nadhani ndio walikuwa wanamalizia round.
Tumelazimika kumchukua mgonjwa wetu kwa ajili ya kuangalia ustaaarabu mwingine.
 
Hapo naona makosa mawili.moja kupita round huku ndugu zako wakiwepo na kutaja hali ya mgonjwa kabla yeye hakaambiwa privately na kufanyiwa counselling.kama mgonjwa wako alishawahi kufanya kazi in a medical setting its most likely alishajua amefika terminal stage.hospital za govt zenye vyuo hii ndo trend na ukisusa kutumiwa as a guinea piguea for teaching unaweza ukasusiwa pia in terms of care.usiogope kuingia cost nxt time nenda private coz wao wapo very ethical in such matters wakiogopa kupoteza wagonjwa.all in all poleni sana
 
Pole sana mkuu, ingekuwa vizuri kufuata uongozi wa hospitali, inawezekana ukasaidia kuboresha utoaji wa huduma pale MUHIMBILI kuliko kuleta malalamiko hapa kwenye jamvi
 
relative mkiambiwa mtoke nje wakati wa kuita round madokta mnakataa huo ndio mshahara , kimsingi walikuwa wanawafukuza kiujaja tu , poleni kwa kusikia hatma ya mgonjwa wako:-*

Halafu jibu la kiporipori namna hii linaweza kuwa limetolewa na mtu mwenye hata elimu ya chuo kikuu... ndio ujue kweli waafrika tuna safari ndefu! Kwanini wasiwaambie tu ondokeni na watumie uhuni kama unaofikiria wewe?
 
r
Mkuu humu jf kuna watu wanaopenda kujibu hata mada wasizosoma kwanza, ila hata kwenye jamii wapo unaweza ukawa unamulekeza mtu jambo hakusikilizi ila anapanga atakujibu nini!!
Mkuu Mulama....inakwaza sana lakini ndio ukweli wenyewe watu utafikiri wamedhurika akili kwa kukremu table ya 12 ( 12mara1=12...12mara2=24) shule ya msingi. Yaani mtu kutumia akili na busara kutafakari jambo ni Issue.
 
Hapo naona makosa mawili.moja kupita round huku ndugu zako wakiwepo na kutaja hali ya mgonjwa kabla yeye hakaambiwa privately na kufanyiwa counselling.kama mgonjwa wako alishawahi kufanya kazi in a medical setting its most likely alishajua amefika terminal stage.hospital za govt zenye vyuo hii ndo trend na ukisusa kutumiwa as a guinea piguea for teaching unaweza ukasusiwa pia in terms of care.usiogope kuingia cost nxt time nenda private coz wao wapo very ethical in such matters wakiogopa kupoteza wagonjwa.all in all poleni sana
Mkuu,
Coming out from the Dr,this statement is absurd. Au Udokta wako ni Kama wa kina Dr. Love Pimbi????
Hata Kama hospitali za Govt zenye vyuo hiyo ndio trend Yao unasahau kwamba hizo Hospitali zinaendeshwa na walipa kodi!!?? Na walipa kodi ndio sisi. Unaposema kwamba ukikataa kuwa "Guinea Pig" unaweza kususiwa huduma Unamaanisha nini?? Kwanza wewe Kama Daktari ungejua unatakiwa uelewe kwamba Hiyo statement yako ya kumfananisha mgonjwa na Guinea Pig umekosea sana na hauna maadili ya kitabibu. Guinea Pig ni aina ya rodents ambao huwa wanatumiwa kwa ajili ya Scientific experimentation and so forth. Ina maana hapo Muhimbili au hizo hospitali za serikali unazozungumzia mnatutumia sisi wagonjwa (Walipa Kodi na mishahara yenu) kwa kufanyia experiments??????

Kwa nini Mtanzania anayelipa Kodi aende private hospital Kama unavyoshauri kwa dharau ilhali ana HAKI ya kutibiwa katika hospitali ya serikali? Au kwa kuwa kuna Madaktari wachache Kama wewe ni Miungu watu kwenye sehemu zenu za kazi na mnasahau kwamba sio Kikwete anayewalipa mshahara ni sisi walala hoi tunaokatwa makato kila kukicha ili kuwalipa mishahara!!
Jipange Dr. Chichi ....hapa sio kwenye mgahawa wenu hapo Muhimbili unapokunywa supu ya sh 500 mkiwa mnajadili matatizo ya wagonjwa kwa kejeli.
 
Pole mkuu kwa yote,lakini watanzinia inatupasa kutambua kwamba unapoingia teaching hospital umeshasign conset ya kuwa teaching model,hakuna conset zaidi ya ile kuwa teaching hospital.Kama hautaka mgonjwa wako afundishiwe wanafunzi please mpeleke hospitali isiyokuwa teaching hospital,tena ukikataa mgonjwa wako kufundishiwa inapaswa ufukuzwe kwenye teaching hospital.

Kwa muhimbili kama hutaki mgonjwa afundishiwe mpeleke first grade uone kama kuna mwanafunzi hatakuja huko kumgusa mgonjwa wako,hata intern doctor akija unamfukuza.

Hili la madaktari kufanya teaching round wakati relative wapo ndani ni uzushi wa mleta mada,hakuna daktari anayekubali kufanya round wakati relative wapo ndani,utapata usumbufu usio na mfano wake,utazingukwa na relative wewe mpaka ukome.
Ninachokiona mimi labda kwa kuwa mke wa mleta mada ni nesi pengine aliingia ndani kwa huo unesi wake baati mbaya akakuta watu wanpigwa shule,kulikuwa hakuna jinsi ispokuwa daktari kuwaonesha wanfunzi wake the real symptoms and signs za terminal stages,sasa nyinyi mulitaka wakazione wapi kwenye lecture room?

Kuhusiana na majibu,inawezekana utafiti ulikuwa bado unaendelea au kwa vile mgonjwa yupo kwenye terminal stage baada ya round doctor angemuambia nesi ili awashauri ndugu wa mgonjwa,mara nyingi manesi ndio wanaoongea na ndugu za wagonjwa isipokuwa pale nesi hasipoeleweka na ndugu wa mgonjwa ndio daktari uzungumza na ndugu wa mgonjwa.

Pamoja na maelezo yangu yote nakubaliana na wadau wengine ya kwamba system yetu ya afya inamatatizo,madaktari wamezidiwa na wagonjwa wengi mpaka wote wanakuwa na kisirani na hasira za karibu,plus maisha magumu kulinganisha na kazi wanayoifanya,so ukimvaa daktari kichwa kichwa na yeye atakutoa nduka kwa maneno makali,ni stress za kazi,we acha tunajuta kusomea hizi kazi hapa tz.
 
Mama mkwe wangu alilazwa Muhimbili kwa wiki moja, lakini jana nililazimika kumtoa kutokana na kile nilichokishuhudia pale. Pamoja na vituko vingi tu tulivyoviona kutoka kwa manesi wa ward ya Mwaisela, lakini nisingependa kuzungumzia hayo kwa kuwa si mageni masikioni mwa wengi. Tulimpeleka mgonjwa wetu kufanyiwa uchunguzi zaidi kutokana na kuwa na complication nyingi nadhani ni kutokana na uzee (mkwe wangu ana miaka 70 hivi sasa)

Tulipofika pale alichukuliwa vipimo vyote ikiwapo x-ray, tatizo lilikuwa ni pale madaktari wanapopita round kuona wagonjwa. kwanza walikuwa wamemgeuza mama mkwe wangu kama vile ni darasa la kufundishia wanafunzi, kila daktari alikuwa anafika na wanafunzi wake na kufungua darasa. Cha kushangaza walikuwa wameyakalia majibu ya mgonjwa wetu huku wakiendelea kumuweka pale kama mtu wa kufundishia wanafunzi.

Sikatai mgonjwa kutumika kufundishia wanafunzi, hawa ni ndio madaktari wetu wa kesho wakajifunzie wapi. Lakini pale dakatari anapowaambia wanafunzi wake kwamba huyu mgonjwa aliyeko mbele yao yuko katika TERMINAL STAGE huku wanaomuuguza wakiwa karibu na hata mgonjwa mwenyewe akisikia, huu ni uuaji. Daktari huyo aliendelea kuwaonyesha wanafunzi wake dalili zinazothibitisha kuwa mgonjwa wetu yuko kwenye terminal stage.

Kitu ambacho madaktari wale walikuwa hawakijui ni kwamba mke wangu pamoja na dada yake ni wauguzi by professional na wanazijua hizo terminology vizuri sana. Sasa iweje waropoke hivyo bila kuangalia walioko karibu. kitendo hicho kilifanyika muda wa kuona wagonjwa na nadhani ndio walikuwa wanamalizia round.
Tumelazimika kumchukua mgonjwa wetu kwa ajili ya kuangalia ustaaarabu mwingine.
Tafuta wakili, nenda mahakami ukawashitaki. Sheria hairuhusu kutoa siri ya mgonjwa. Ni wajinga, mbona watu wanaishi mpaka 100+
 
Back
Top Bottom