Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,811
- 15,404
Mama mkwe wangu alilazwa Muhimbili kwa wiki moja, lakini jana nililazimika kumtoa kutokana na kile nilichokishuhudia pale. Pamoja na vituko vingi tu tulivyoviona kutoka kwa manesi wa ward ya Mwaisela, lakini nisingependa kuzungumzia hayo kwa kuwa si mageni masikioni mwa wengi. Tulimpeleka mgonjwa wetu kufanyiwa uchunguzi zaidi kutokana na kuwa na complication nyingi nadhani ni kutokana na uzee (mkwe wangu ana miaka 70 hivi sasa)
Tulipofika pale alichukuliwa vipimo vyote ikiwapo x-ray, tatizo lilikuwa ni pale madaktari wanapopita round kuona wagonjwa. kwanza walikuwa wamemgeuza mama mkwe wangu kama vile ni darasa la kufundishia wanafunzi, kila daktari alikuwa anafika na wanafunzi wake na kufungua darasa. Cha kushangaza walikuwa wameyakalia majibu ya mgonjwa wetu huku wakiendelea kumuweka pale kama mtu wa kufundishia wanafunzi.
Sikatai mgonjwa kutumika kufundishia wanafunzi, hawa ni ndio madaktari wetu wa kesho wakajifunzie wapi. Lakini pale dakatari anapowaambia wanafunzi wake kwamba huyu mgonjwa aliyeko mbele yao yuko katika TERMINAL STAGE huku wanaomuuguza wakiwa karibu na hata mgonjwa mwenyewe akisikia, huu ni uuaji. Daktari huyo aliendelea kuwaonyesha wanafunzi wake dalili zinazothibitisha kuwa mgonjwa wetu yuko kwenye terminal stage.
Kitu ambacho madaktari wale walikuwa hawakijui ni kwamba mke wangu pamoja na dada yake ni wauguzi by professional na wanazijua hizo terminology vizuri sana. Sasa iweje waropoke hivyo bila kuangalia walioko karibu. kitendo hicho kilifanyika muda wa kuona wagonjwa na nadhani ndio walikuwa wanamalizia round.
Tumelazimika kumchukua mgonjwa wetu kwa ajili ya kuangalia ustaaarabu mwingine.