DOKEZO Madaktari wa kizazi hiki mnatia aibu sana

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
2,858
7,847
Naandika uzi huu kwa uchungu na majonzi makubwa.

Siku za hivi karibuni nikiwa mkoa wa ugenini mishale ya usiku nilianza kujisikia hovyo sana kwa ghafla tu. Hali ilianza kubadilika mida ya saa sita za usiku. Nilianza kujisikia hali ya ganzi upande wa kushoto wa kifua, na mapigo ya moyo kwenda mbio hasa.

Nikapambana na kujitahidi huku nikimuomba Mungu anifikishe tu asubuhi salama, kisha niwahi hospitali asubuhi hiyo. Lakini, kwa bahati mbaya hali ilizidi kuwa tete kadri muda unavyosonga. Basi, hadi kufika mida ya saa tisa hali bado ilikua ngumu, sasa nikaanza kusikia hali ya kifua kuwa kizito na kama hali ya kukosa hewa hivi.

Nikasema hapa sina namna, la sivyo wenyeji wanaweza kukuta mwili tu asubuhi hapa, maana nilikua peke yangu. Nikampigia simu mwenyeji wangu bahati nzuri akapokea nikamwambia naona hali yangu si nzuri, akaja fasta na gari, akashauri kuwa kwa vile ni usiku sana anipeleke tu health center ya binafsi ambayo si mbali sana kutoka hapo, kisha kama wataona umuhimu wa kutoa rufaa kwenda hospitali ya juu zaidi ndo twende, nikasema, sawa haina shida.

Aka drive hadi hapo health center, nikashuka nikaingia mapokezi nikaandikisha jina vizuri, nikaingia kwa daktari.

Kufika kwa daktari, akaniuliza shida nikampa historia yangu vizuri kabisa, sasa cha kushangaza yaani yule daktari hata kunifanyia physical examination hakutaka!! Yaani nampa dalili za moyo kwenda mbio, kifua kubana ila yeye hata kusema asikilize mapigo ya moyo, asikilize kifua (mapafu) kama hewa inaingia vizuri, asikilize pulse rate na rythym, wala!! Alichofanya tu alimuita nurse, akamwambia anipime presha, nikapimwa presha kwa automatic blood pressure machine. Karudia pale kama mara tatu, anapata readings tofauti tu hadi kachanganyikiwa achukue reading ipi. Yaani hata ugonjwa uliisha ghafla nikawa nawaza what is this? Ila ikabidi niwe mpole tu, maana sikutaka kujitambulisha kama daktari wala kujimwambafai. Baada ya nesi kuondoka, nikajua atanifanyia physical examination sasa asikilize hata kifua na mapigo ya moyo.Walaaaahhh hakuwaza kabisa!

Basi, akaandika vipimo vya lab pale, nikasubiri kidogo nikaja kutolewa damu,zikapelekwa maabara. Majibu yamerudi, nikaitwa tena kwa daktari, akaniambia majibu yangu na kuniandikia dawa za uongo na kweli. Nimetoka pale, hata pharmacy sikwenda, nikatoka nikamshtua jamaa yangu nikamwambia twende zetu, I was so disappointed hasa kwa sababu wakati yule daktari anajaza fomu yangu ya bima, niligundua kuwa kumbe ni MD kabisa (kwa maana ya kwamba ana shahada ya udaktari), yaani ndo nilichoka kabisa, maana mwanzoni nilidhani ana diploma tu (CO).

Tumetoka pale tayari saa kumi na moja alfajiri, jamaa akanirudisha tu home ila niliwaza sana aisee, kama MD ndo anakua hivyo, nikasema tuna shida kubwa sana nchini.

Ndio maana kila siku naona nyuzi humu madaktari tunatukanwa, aisee kumbe we deserve it kama madaktari wenyewe ndo sampuli ile niliyokuta pale. Waalimu mliopo vyuo vya udaktari mnawaandaaje hawa vijana huko vyuoni aisee? Daktari gani, a whole MD unakua hovyo hivyo?
We are doomed kwa kweli.

Ilibidi tu kulipokucha nicheki na jamaa yangu cardiologist yupo hospitali fulani ya rufaa ya zonal nikaenda pale kutibiwa, naendelea fresh now.

I am not saying kuwa I expected pale nifanyiwe vipimo vya hali ya juu vya moyo labda, no..!! ila daktari unapata mtu ana complain moyo unaenda mbio na kifua kizito, hata kumsikiliza moyo haumsikilizi, hausikilizi sauti za kwenye mapafu, hau palpate hata pulse..?? A whole MD?

We are doomed.
 
Sasa wewe MD ulishindwa hata jua tatizo linalokusumbua kabla hujaenda huko zahanati?

Kingine

Madaktari wengi vijana hawana uzoefu
Mganga hajigangi mkuu. Maana ili kujua tatizo lako lazima usikilize sauti za moyo zikoje, unadunda vipi, usikilize kifua, ucheki pulse, na kadhalika. Unaweza kujifanyia hayo ukiwa hata kupumua vizuri ni shida?

Hapana, ile sio shida ya uzoefu mkuu. Medical school mnafundishwa, mtu akiwa na shida ya kupumua/moyo; Kati ya basics za kwanza ni kusikiliza sauti za moyo wake, kusikiliza kifua chake kinasemaje. Hivyo sio vitu vya kujifunzia kazini, ni vitu vya kujifunzia medical school na wakati wa internship.

Kama tumefika hatua ambayo hizo basics daktari anajifunzia kazini, basi tuna tatizo kubwa mkuu!!
 
Swala sio mganga hajigangi.

Swala ni kuwa unaweza jua tatizo kwa kuhisi tu maana tayari wewe ni daktari unajua kabisa kuwa hapa tatizo ni hili na lile na sio swala la kuona pulse rate au kutumia steto kusikiliza mapigo ya moyo na sauti.

Mi si daktari ila huwa naweza fanya diagnosis ya mwenyewe.

Kama matatizo ya moyo unayo maana yake utakuwa na dawa ndani.
 
Swala sio mganga hajigangi.
Swala ni kuwa unaweza jua tatizo kwa kuhisi tu maana tayari wewe ni daktari unajua kabisa kuwa hapa tatizo ni hili na lile na sio swala la kuona pulse rate au kutumia steto kusikiliza mapigo ya moyo na sauti.

Mi si daktari ila huwa naweza fanya diagnosis ya mwenyewe.

Kama matatizo ya moyo unayo maana yake utakuwa na dawa ndani.
Kuhisi sawa.
Ila hadi kufikia hatua ya kujitibu mwenyewe, hapana. Sijawahi kuwa na tatizo la moyo kabla.
Nilishahisi shida ni moyo, ila nilitaka mtu mwingine ani examine na kufikia conclusion na kunishauri cha kufanya. Huwa hakuna kitu sipendi kama kujitibu mwenyewe, unless labda kama sina option kabisa. Tena ugonjwa wa kuhusu moyo, siwezi hata kujaribu kujitibu.
 
Siku hizi wanaangalizia. Wakienda internship hawafanyi kazi chini ya uangalizi, no wonder hata basics hawazifahamu!

We need an overhaul kuanzia mtu binafsi mpaka mifumo ya kuwaandaa wataalamu wetu wa kada zote siyo afya pekee, otherwise, tutaendelea kupoteza Watanzania.

Sadly, voda fasta za Kikwete zimeendelezwa na awamu zote zilizofuata. Tunateketea kama taifa.
 
Kuhisi sawa.
Ila hadi kufikia hatua ya kujitibu mwenyewe, hapana. Sijawahi kuwa na tatizo la moyo kabla.
Nilishahisi shida ni moyo, ila nilitaka mtu mwingine ani examine na kufikia conclusion na kunishauri cha kufanya. Huwa hakuna kitu sipendi kama kujitibu mwenyewe, unless labda kama sina option kabisa. Tena ugonjwa wa kuhusu moyo, siwezi hata kujaribu kujitibu.
Kafanye ECHO na vipimo vingine vya MOYO,watu wengi hufa ghafla
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom