DOKEZO Madaktari wa kizazi hiki mnatia aibu sana

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hii ndiyo hali ninayo sasa.
Mbavu zinabana na kuachia, kichwa, mwili na viungo vinauma uma tuu.. Muda wote mwili una uchovu.

Na hapa nimeshamaliza Dozi ya UTI na Typhoid zaidi ya Wiki sasa ila sijaona mabadiliko yoyote.

Huenda hii kitu ipo kweli mtaani huku..
Internal pain , inategemea na shughuli unazofanya hasa kuji expose ktk moshi mzito wenye cabon nyingi,
Kupungukiwa madini muhimu yanayoipa misuli nguvu, ukiwa upo vizuri kawekewe ka oksijeni uvute vute kidgo, kunywa maziwa, meza dawa za maumivu
 
Naandika uzi huu kwa uchungu na majonzi makubwa.

Siku za hivi karibuni nikiwa mkoa wa ugenini mishale ya usiku nilianza kujisikia hovyo sana kwa ghafla tu. Hali ilianza kubadilika mida ya saa sita za usiku. Nilianza kujisikia hali ya ganzi upande wa kushoto wa kifua, na mapigo ya moyo kwenda mbio hasa.

Nikapambana na kujitahidi huku nikimuomba Mungu anifikishe tu asubuhi salama, kisha niwahi hospitali asubuhi hiyo. Lakini, kwa bahati mbaya hali ilizidi kuwa tete kadri muda unavyosonga. Basi, hadi kufika mida ya saa tisa hali bado ilikua ngumu, sasa nikaanza kusikia hali ya kifua kuwa kizito na kama hali ya kukosa hewa hivi.

Nikasema hapa sina namna, la sivyo wenyeji wanaweza kukuta mwili tu asubuhi hapa, maana nilikua peke yangu. Nikampigia simu mwenyeji wangu bahati nzuri akapokea nikamwambia naona hali yangu si nzuri, akaja fasta na gari, akashauri kuwa kwa vile ni usiku sana anipeleke tu health center ya binafsi ambayo si mbali sana kutoka hapo, kisha kama wataona umuhimu wa kutoa rufaa kwenda hospitali ya juu zaidi ndo twende, nikasema, sawa haina shida.

Aka drive hadi hapo health center, nikashuka nikaingia mapokezi nikaandikisha jina vizuri, nikaingia kwa daktari.

Kufika kwa daktari, akaniuliza shida nikampa historia yangu vizuri kabisa, sasa cha kushangaza yaani yule daktari hata kunifanyia physical examination hakutaka!! Yaani nampa dalili za moyo kwenda mbio, kifua kubana ila yeye hata kusema asikilize mapigo ya moyo, asikilize kifua (mapafu) kama hewa inaingia vizuri, asikilize pulse rate na rythym, wala!! Alichofanya tu alimuita nurse, akamwambia anipime presha, nikapimwa presha kwa automatic blood pressure machine. Karudia pale kama mara tatu, anapata readings tofauti tu hadi kachanganyikiwa achukue reading ipi. Yaani hata ugonjwa uliisha ghafla nikawa nawaza what is this? Ila ikabidi niwe mpole tu, maana sikutaka kujitambulisha kama daktari wala kujimwambafai. Baada ya nesi kuondoka, nikajua atanifanyia physical examination sasa asikilize hata kifua na mapigo ya moyo.Walaaaahhh hakuwaza kabisa!

Basi, akaandika vipimo vya lab pale, nikasubiri kidogo nikaja kutolewa damu,zikapelekwa maabara. Majibu yamerudi, nikaitwa tena kwa daktari, akaniambia majibu yangu na kuniandikia dawa za uongo na kweli. Nimetoka pale, hata pharmacy sikwenda, nikatoka nikamshtua jamaa yangu nikamwambia twende zetu, I was so disappointed hasa kwa sababu wakati yule daktari anajaza fomu yangu ya bima, niligundua kuwa kumbe ni MD kabisa (kwa maana ya kwamba ana shahada ya udaktari), yaani ndo nilichoka kabisa, maana mwanzoni nilidhani ana diploma tu (CO).

Tumetoka pale tayari saa kumi na moja alfajiri, jamaa akanirudisha tu home ila niliwaza sana aisee, kama MD ndo anakua hivyo, nikasema tuna shida kubwa sana nchini.

Ndio maana kila siku naona nyuzi humu madaktari tunatukanwa, aisee kumbe we deserve it kama madaktari wenyewe ndo sampuli ile niliyokuta pale. Waalimu mliopo vyuo vya udaktari mnawaandaaje hawa vijana huko vyuoni aisee? Daktari gani, a whole MD unakua hovyo hivyo?
We are doomed kwa kweli.

Ilibidi tu kulipokucha nicheki na jamaa yangu cardiologist yupo hospitali fulani ya rufaa ya zonal nikaenda pale kutibiwa, naendelea fresh now.

I am not saying kuwa I expected pale nifanyiwe vipimo vya hali ya juu vya moyo labda, no..!! ila daktari unapata mtu ana complain moyo unaenda mbio na kifua kizito, hata kumsikiliza moyo haumsikilizi, hausikilizi sauti za kwenye mapafu, hau palpate hata pulse..?? A whole MD?

We are doomed.
Ulifanya vema
 
Hatar sana kuna dada mmoja alikuwa anasumbuliwa na kizunguzungu kikali non stop miez mitatu, usingizi hapati hata lepe alikuwa anaenda hospitl flan ya private kubwa tu, alikuwa anatundikwa dawa za kutosha ugonjwa upo pale pale hadi nakutana nae yule. dada kashakata tamaa depression ishamkamata, katajiwa magonjwa yote makubwa😂😂,

Hadi kwa waganga kafika shida ipo pale pale
Alivyonielezea tu japo udaktari umebaki kama passion tu nikamwambia unatatizo la sikio twede ukachukuwe vipimo ila sikio ukilitazma halina shida yoyote kwa nje ila kwa ndani akakutwa na uvimbe mkubwa tu akapewa matibabu hadi akapona

Md sikuizi wwanaza pesa na mambo mengine kutibu wala wanalipuwa lipuwa ilimradi pesa
 
Sasa hivi naona bora nikapange foleni serikalini hukoo kuliko hizi private utopolo mtupu
Halafu daktari namuuliza mbona huniangalii chochote(mimi nishazowea kupimwa kwa kuangalia macho,ulimi,masikio,mapigo ya moyo kifuani/mgongoni, magoti) huyu daktari hata kunigusa hajanigusa. Kaandika tu dawa na kunambia nenda kachukuwe dawa pharmacy yao na kuondoka.
 
Hadi hapo inakuwa ni uongo, privacy ya kitu gani kwamba wewe pekee ndo mgonjwa hospital nzima?
Mkuu hayajakufika kuna sehemu niliwahi kuwasema wale wana wakaniwekea mwanasheria wao. Kwa kesi ya kuwaharibia biashara mahakama ilinitaka niwalipe wale watu fidia mpaka leo sina mambo ya kutaja majina ya sehemu husika.
 
Huu ni uongo unaofana na ukweli labda ungesema kuna mahali kuna shida ila sio kuwa Vyuo vyetu vyote uozo hawa Proff wetu waliojaa vyuoni kwetu ndio hawahawa wamesoma Sijui Calgarly mara KUMAMOTO, sijui Zhengjeng na ndio hufundisha na kuandaa mitaala huku vyuoni inamaana nawenyewe ni UOZO japo wamesoma hukohuko Nje ambako wewe unaona wako vizuri

Mara kadhaa nimekuwa naona Gynacologist sijui Cardiologist(toka nje) wanakuja fanya kambi katika vituo ambavyo nakuwepo pia mbona wenesomagi wamekuwa wakiwakubali sana baadhi ya wataalam wetu wandani wako vizuri!??
aliyesoma Kumamoto ni ng'walali tu .
 
Mkuu hayajakufika kuna sehemu niliwahi kuwasema wale wana wakaniwekea mwanasheria wao. Kwa kesi ya kuwaharibia biashara mahakama ilinitaka niwalipe wale watu fidia mpaka leo sina mambo ya kutaja majina ya sehemu husika.
Acha kutudanganya hapa
 
Ndugu yngu kafanya vipimo tukaambiwa ana tatizo la brucella, daktari anasema ili apone anatakiwa anywe doze ya TB akichanganya na dawa inaitwa Doxycycline vindonge mamia kwa mamia.

Baadhi ya madaktari wa siku hizi ni changamoto
Daktar yupo sahihi
Punguza ujuaji mkuu
Brucellosis inatibiwa hivyo kwa combined therapy
 
It's true!
Wakati mama angu anakaribia kustaafu;akiwa wodini na hao internship wa kutoka UDOM ,aisee si akakuta dada anachanganya dawa(Ile ya unga ya sindano) na maji ya uhai 😳...wakati zile Zina maji yake ya kuchanganyia....
Ndo mama anamuuliza,ndo mnavyofundishwa? Hana la kujibu ...
Ilibidi mama angu afanye mwenyewe Ili kumchoma sindano huyo mgonjwa!
Km huna Dr ,nesi unaemfahamu vzr kwakweli ni balaa
Hii ni Tatepa yenye tangawizi
 
Nimefanya utafiti Kwa nyakati tofauti tofauti kwenye hospitali na vituo vyetu vya Afya iwe binafsi au vya serikal, Kwa Kila mgonjwa wanayempima wakikosa tatizo lazima azawadiwe kwa kuambiwa (mkojo mchafu Una UTI)...
Hii Tabia ni mbovu mno na imeshika kasi
 
Naandika uzi huu kwa uchungu na majonzi makubwa.

Siku za hivi karibuni nikiwa mkoa wa ugenini mishale ya usiku nilianza kujisikia hovyo sana kwa ghafla tu. Hali ilianza kubadilika mida ya saa sita za usiku. Nilianza kujisikia hali ya ganzi upande wa kushoto wa kifua, na mapigo ya moyo kwenda mbio hasa.

Nikapambana na kujitahidi huku nikimuomba Mungu anifikishe tu asubuhi salama, kisha niwahi hospitali asubuhi hiyo. Lakini, kwa bahati mbaya hali ilizidi kuwa tete kadri muda unavyosonga. Basi, hadi kufika mida ya saa tisa hali bado ilikua ngumu, sasa nikaanza kusikia hali ya kifua kuwa kizito na kama hali ya kukosa hewa hivi.

Nikasema hapa sina namna, la sivyo wenyeji wanaweza kukuta mwili tu asubuhi hapa, maana nilikua peke yangu. Nikampigia simu mwenyeji wangu bahati nzuri akapokea nikamwambia naona hali yangu si nzuri, akaja fasta na gari, akashauri kuwa kwa vile ni usiku sana anipeleke tu health center ya binafsi ambayo si mbali sana kutoka hapo, kisha kama wataona umuhimu wa kutoa rufaa kwenda hospitali ya juu zaidi ndo twende, nikasema, sawa haina shida.

Aka drive hadi hapo health center, nikashuka nikaingia mapokezi nikaandikisha jina vizuri, nikaingia kwa daktari.

Kufika kwa daktari, akaniuliza shida nikampa historia yangu vizuri kabisa, sasa cha kushangaza yaani yule daktari hata kunifanyia physical examination hakutaka!! Yaani nampa dalili za moyo kwenda mbio, kifua kubana ila yeye hata kusema asikilize mapigo ya moyo, asikilize kifua (mapafu) kama hewa inaingia vizuri, asikilize pulse rate na rythym, wala!! Alichofanya tu alimuita nurse, akamwambia anipime presha, nikapimwa presha kwa automatic blood pressure machine. Karudia pale kama mara tatu, anapata readings tofauti tu hadi kachanganyikiwa achukue reading ipi. Yaani hata ugonjwa uliisha ghafla nikawa nawaza what is this? Ila ikabidi niwe mpole tu, maana sikutaka kujitambulisha kama daktari wala kujimwambafai. Baada ya nesi kuondoka, nikajua atanifanyia physical examination sasa asikilize hata kifua na mapigo ya moyo.Walaaaahhh hakuwaza kabisa!

Basi, akaandika vipimo vya lab pale, nikasubiri kidogo nikaja kutolewa damu,zikapelekwa maabara. Majibu yamerudi, nikaitwa tena kwa daktari, akaniambia majibu yangu na kuniandikia dawa za uongo na kweli. Nimetoka pale, hata pharmacy sikwenda, nikatoka nikamshtua jamaa yangu nikamwambia twende zetu, I was so disappointed hasa kwa sababu wakati yule daktari anajaza fomu yangu ya bima, niligundua kuwa kumbe ni MD kabisa (kwa maana ya kwamba ana shahada ya udaktari), yaani ndo nilichoka kabisa, maana mwanzoni nilidhani ana diploma tu (CO).

Tumetoka pale tayari saa kumi na moja alfajiri, jamaa akanirudisha tu home ila niliwaza sana aisee, kama MD ndo anakua hivyo, nikasema tuna shida kubwa sana nchini.

Ndio maana kila siku naona nyuzi humu madaktari tunatukanwa, aisee kumbe we deserve it kama madaktari wenyewe ndo sampuli ile niliyokuta pale. Waalimu mliopo vyuo vya udaktari mnawaandaaje hawa vijana huko vyuoni aisee? Daktari gani, a whole MD unakua hovyo hivyo?
We are doomed kwa kweli.

Ilibidi tu kulipokucha nicheki na jamaa yangu cardiologist yupo hospitali fulani ya rufaa ya zonal nikaenda pale kutibiwa, naendelea fresh now.

I am not saying kuwa I expected pale nifanyiwe vipimo vya hali ya juu vya moyo labda, no..!! ila daktari unapata mtu ana complain moyo unaenda mbio na kifua kizito, hata kumsikiliza moyo haumsikilizi, hausikilizi sauti za kwenye mapafu, hau palpate hata pulse..?? A whole MD?

We are doomed.
Mimi kanichosha daktari wa Membe, Dr Nyagori. Kasema on live TV marehemu kafa na Pulmonary Embolism iliyosababishwa na virusi. Toka lini cardiovascular case kama PE ikasababishwa na kirusi wakati inajulikana inasababishwa na DVT blood clots za miguuni 95% of the times na hizo 5% zilizobaki hakuna kirusi kinachohusika?? Na anajiita Profesa tena. Na yeye yuko Muhimbili, Membe alipelekwa Kairuki, amepata wapi hayo ma diagnosis yake?
 
Mimi kanichosha daktari wa Membe, Dr Nyagori. Kasema on live TV marehemu kafa na Pulmonary Embolism iliyosababishwa na virusi. Toka lini cardiovascular case kama PE ikasababishwa na kirusi wakati inajulikana inasababishwa na DVT blood clots za miguuni 95% of the times na hizo 5% zilizobaki hakuna kirusi kinachohusika?? Na anajiita Profesa tena. Na yeye yuko Muhimbili, Membe alipelekwa Kairuki, amepata wapi hayo ma diagnosis feki ?
kuna interview kasema PE? au vita ni vita mura?
 
kuna interview kasema PE? au vita ni vita mura?

ndio, interview zake zote nilizoziona "daktari wa famlia" Dr Nyagori kasema marehemu kafa kwa Pulmonary Embolism iliyosabishwa na virusi

hivi tunavyoongea mwanafamilia amejitokeza akipinga vikali taaluma aliotumia huyu "daktari wa familia" katika kutaja sababu za kifo cha Membe. Amejimbulisha kama mdogo wake Membe toka nitoke na amefanya kazi za taaluma hii kwa serikali ya Canada miaka 12.

ameongea yale yale niliyoyasema, toka lini kirusi cha mapafu kikasababisha Pulmonary Embolism, gonjwa namba tatu la moyo kwa kuuwa watu duniani, limeshafanyiwa sana utafiti, hakuna unaeweza kumdanganya kuhusu huo ugonjwa.... hapo ndio nilipoanza kum doubt huyu daktari anaejiita professa wa Jakaya Kikwete Institute....

Mkuu mimi kila miezi 6 nafanya physical checkup, sasa nikaenda hospital tofauti safari hii. Kupima wakasema mkojo mchafu nikauliza kwanini mkojo mchafu wakasema kunywa maji mengi. Na wakanipa madawa nikatumia yale madawa ya kawa yananizidi nguvu wiki 2 sijatoka ndani. Nikaanza kufanya ganzi mkono mara ganzi ya mguu sijui kiuno kimeganda. Nikaona acha nitoke nje ya nchi nimekwenda huko nimeambiwa nina protein nyingi kwenye mkojo, kwahio niangaliwe liver na kidney naam hilo ndio lilikuwa tatizo. Lakini huku nyumbani nimeambiwa mkojo mchafu tena ninywe maji tu
Pole sana kwahyo walikuta shida kwenye figo?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom