Madaktari wa Apollo wawasili, Wagonjwa Wetu Wazidi Kwenda Ng'ambo

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,941
9,947
Wana JF nimesikia kupitia magazetini kwamba madaktari kadhaa toka India (Apollo) waliwasili nchini jana kwa ajili ya kutoa matibabu bure kwa wananchi wa nchii hii. Lakini pia nimesikia Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Ndg. Cleopa David Msuya naye jana amepanda pipa kwenda ng'ambo kwa matibabu!! Kwa maana hiyo basi wakuu wetu takribani watano (ambao japo wanafahamika) wapo ng'ambo kwa matibabu:
  • Mwandosya
  • Mwakyembe
  • Chami
  • Zitto
  • Msuya
Kazi kwelikweli. Bahati mbaya ni mmoja tu tumeweza kuambiwa (kupitia JF) kuwa anaumwa nini.

Kama hao madaktari bingwa wamekuja si wangewatibu hapahapa ya nini wansiasa wetu kuishia India? Huduma za afya hapa nchini ziko taabani kiasi hicho?
 
Mkuu, nguvu za jeshi ni aina ya silaha wanazomiliki na kujua jinsi ya kuzitumia. Leo hii ukimleta askari wa kimarekani mwenye uwezo wa ku-operate tomahawk aje kupigana na AK 47 Afrika atadundwa tu.

Mi nafikiri ubora wa madaktari si taaluma pekee bali na vitendea kazi. Kama madaktari hao wamekuja na meli iliyojaa vifaa vyote kama wanvyotumia huko kwao basi hakuna haja ya watu hao kwenda nje, wasiwasi utabakiwa tu kwenye umeme wa kufanya vifaa hivyo vifanye kazi. Hao wamekuja kutalii na PR baada ya kuona Viongozi wa Tanzania ni wateja wao wazuri sana katika biashara ya matibabu. Ukifuatilia sana utaambiwa wana ratiba ya kwenda mbuga za wanyama pia.

Hawa waheshima wanaopelekwa huko wangekuwa ni wazalendo wangekuwa wanauliza majina hata ya vifaa vya matibabu ili wakipona na kurudi salama waje wasimamie kuhakikisha vinapatikana. Tanzania tuna madaktari wazuri sana, ukiwapatia vifaa vya kisasa na mshahara kama wa wabunge basi hauna haja ya kutumia USD kupeleka watu India kwa matibabu.
 
wameona wengi mno wanakwenda huko hivyo wameamua kufuata kiini/source za ugonjwa uliko ili kupunguza mlundikano wa wagonjwa huko INDIA

siyo watatibu tu bali pia watoa elimu ya UBAYA WA KUPEANA SUMU na ATHALI zake kwa jamii
 
wameona wengi mno wanakwenda huko hivyo wameamua kufuata kiini/source za ugonjwa uliko ili kupunguza mlundikano wa wagonjwa huko INDIA

siyo watatibu tu bali pia watoa elimu ya UBAYA WA KUPEANA SUMU na ATHALI zake kwa jamii

aiseeee umesema..
 
Back
Top Bottom