Barua ya Wazi kwa Rais John Pombe Magufuli - Madaktari Bingwa Wabobezi na TCU

DidYouKnow

JF-Expert Member
Jul 28, 2019
1,094
1,691
Mheshimiwa Rais!

Hongera na Pole kwa majukumu makubwa uliyopewa na Watanzania.

Nikiri kwamba barua yangu hii, imechagizwa na Mkutano wa Madaktari Tanzania wa mwaka huu. Bahati mbaya Dr. Elisha Osati alisahau kuwasilisha hili.

Mheshimiwa Rais, toka umeingia madarakani umeokoa kiasi kikubwa cha fedha kilichokuwa kikitumika kutibu wagonjwa nje ya nchi. Kwa muda mrefu sana kulikuwa na malalamiko dhidi ya hospitali za India kama Appolo Hospitals, ambapo wagonjwa wengi walikuwa wakilalamika kwamba kuna inflation kubwa ya gharama za matibabu waliyopata ambao ulikuwa ni mzigo mkubwa kwa serikali.

Mheshimiwa Rais, pamoja na kuokolewa kwa kiasi kikubwa cha gharama za kupeleka wagonjwa nje ya nchi, tunaweza kuokoa zaidi na zaidi. Kitu kikubwa kinachozuia ni kwamba bado tuna madaktari wachache sana wenye sifa za juu za kutibu kwa maana ya madaktari bingwa wabobezi (Super specialists) kwani tuna wataalam wachache wenye elimu kama hiyo wanaoweza fundisha katika vyuo vyetu vikuu. Kwa sasa tuna upungufu mkubwa wa wataalamu wabobezi kwenye magonjwa mbalimbali kama rheumatologia, utumbo, moyo, ini, mfumo wa upumuaji, upasuaji wa moyo, figo n.k.

Moja ya watu ambao wangekuwa vinara wa kusomea superspecialization, ni walimu wa vyuo vikuu vya tiba hapa Tanzania. Vyuo hivyo ni kama Muhimbili, UDOM, na UDSM. Bahati mbaya sana walimu hawa wanaathirika na miongozo ya TCU. Baadhi baada ya kurudi kusoma superspecialization walirudi chuo nankuwa feustrated, kwani hawakupata promotion - kwanini? Ati hawakwenda kusomea PhD.

Baada ya daktari kusomea digrii ya kwanza ya udaktari (miaka mitano hadi sita), hufanya kazi mwaka mmoja wa mazoezi (internship, wenzetu wanafanya kwa miaka miwili). Miaka yetu ya tisini, ilikuwa ukimaliza internship ni lazima uende kufanya kazi walau miaka mitatu kabla hujapata nafasi ya kwenda kusoma digrii ya pili ili kupata uzoefu na kutambua matakwa yako ya digrii ya pili. Siku hizi nasikia wanaweza pata nafasi ya kusoma digrii ya pili straight after internship.

Daktari anapokwenda kusoma digrii ya pili, huwa na chaguzi zisizopungua tatu 1. Kusomea udaktari bingwa (clinical subjects) kama wa magonjwa ya upasuaji, watoto, magonjwa ya ndani, kansa, mifupa, kansa n.k. 2. Kusomea masomo ya basic science ambayo pia yana upungufu mkubwa wa staff kama Physiology, Anatomy, Pharmacology, Pathology n.k 3. Kusomea digrii ya afya ya jamii na hizo digrii nyingine za uongozi.

Kwa yule daktari atakayesoma ubingwa wa clinical subjects - huitwa Master of Medicine (atatumia miaka mitatu hadi minne) atakuwa daktari bingwa wa kile alichosomea. Mfano atakuwa daktari bingwa wa upasuaji.

Mheshimiwa Rais, baada ya digrii ya pili ya udaktari bingwa, kwa sasa vyuo vingi duniani vimeanzisha kitu kiitwacho fellowship. Hii ni competent based training. Mfano daktari wa upasuaji anaweza kwenda kwenye fellowship ya upasuaji wa ubongo. Akimaliza anakuwa daktari bingwa mbobezi (superspecialist) wa upasuaji wa ubongo.

Kwa Tanzania wanatoa Muhimbili kama Master of Science, kwa Afrika ya Kusini wanatoa kama Certificate, kwa India wanatoa kama Doctor of Medicine (DM). Hii fellowship huwahusu madaktari wanaotibu (clinicians) na hutumia angalau miaka miwili. Na hii ndio njia sahihi ya daktari anayetibu kupita.

Miaka ya nyuma kozi hizi hazikuwapo kwenye nchi nyingi za Afrika. Lakini kuna watu wachache walifanikiwa kwenda kusoma ng’ambo baada ya kumaliza Master of Medicine hapa nchini, na wakarudi wakiwa wabobezi. Lakini siku zote, digrii ya pili ya ubingwa wa magonjwa imekuwa ikifananishwa na PhD vyuoni, na kiuhalisia units za Master of Medicine zinazidi units za PhD.

Kwa bahati mbaya sana, wale madaktari wanaofundisha masomo ya kutibu vyuo vikuu, wakienda kufanya hiyo fellowship kwa miaka miwili hadi mitatu kwa lengo la wao kuwa wabobezi katika nyanja fulani, huwa hawapandishwi madaraja kwa kuwa mtazamo wa TCU ni kuwa baada ya kufanya Master of Medicine, hawa walimu wanapaswa wakafanye PhD, jambo ambalo si sahihi hata chembe.

Daktari bingwa aliyesomea Ubingwa Wa Upasuaji, hawezi akafanya PhD ili awe bingwa wa upasuaji wa ubongo. Ukifanya PhD kwenye surgery utakuwa vizuri sana kwenye kitu kidogo kile ulichokuwa ukikifanyia utafiti, lakini hakitakufanya uwe guru kwenye mfumo mzima. Haya masomo lazima yawe ya course work ambapo kwa bahati mbaya sana, sijawahi ona PhD by Coursework katika udaktari.

Lengo kubwa la daktari bingwa anayefundisha chuoni ni kuongeza ubora wa matibabu kwa wagonjwa na kutoa elimu bora kwa wanafunzi na pia kama mwalimu kufanya utafiti ambako hakuhitaji mpaka awe na neno PhD mbele ya jina lake ili afanye utafiti bora.

Utahitaji watu kumi wenye PhD ili kuweza kumtibu mgonjwa mmoja mwenye Tatizo la Moyo, kwa sababu kwenye PhD focus inakuwa ni kwenye vitu vidogovidogo ambavyo daktari bingwa au mbobezi atavifanya kwa ujumla na kwa undani zaidi.

Kitendo cha TCU kutotambua qualification ya ubingwa ubobezi na kusisitiza madaktari wanaofundisha na kutibu kufanya PhD ni kosa kwa sababu ule ubingwa wao tayari una level ya PhD lakini pia unapunguza morali ya walimu walioko vyuoni kwenda kusomea ubingwa ubobezi na hivyo kusababisha ubora wa matibabu nchini kutoendelea, kwa kuwa madaktari bingwa wanaofundisha vyuoni wanaamua kwenda kusoma PhD ambayo haisaidiii kuboresha huduma za mafunzo na matibabu kwa wanafunzi na wagonjwa wao.

Mheshimiwa Rais, Hivyo mfano Daktari bingwa (ambaye sio superspecialist) wa upasuaji akienda kufanya PhD kwenye kitu kilichomo ndani ya Neurosurgery, hakitamfanya yeye kuwa Neurosurgeon kwa sababu ndani ya Neurosurgery kuna magonjwa mengi yanayomfanya mtu kuwa Neurosurgeon ambayo atakuwa hayafahamu.

Mheshimiwa Rais, Bahati mbaya sana ulimwengu tunaoenda tunahitaji superspecialists wengi. Kuna madaktari bingwa waliosoma hadi PhD, sasa wanaenda kuomba nafasi za Superspecialization ili kuwa competent.

Ukitaka watu wasome PhD mfano kwenye hiyo topic ya Neurosurgery basi utahitaji kuwa na madaktari wengi wenye PhD katika maeneo tofauti ya Neurosurgery ili mwisho wa siku waweze kumfundisha mwanafunzi wa Neurosurgery kwa sababu watakuwa hawana competence ya magonjwa mengi. Pia hata matibabu kwa wagonjwa itapaswa yatolewe na madaktari wenye PhD wengi kwani kila mmoja atakuwa ana ufahamu wa sehemu ndogo tu ya ugonjwa aliousomea. Ni ngumu sana kumegamega mgonjwa kwa kusomea PhD ya kila sehemu ya ugonjwa.

Mheshimwa Rais, naona ni wakati muafaka sasa wa TCU kuipitia upya miongozo yake kwa haraka ili walimu wa vyuo vikuu ambao ni madaktari wa kutibu waweze kufuata njia sahihi za kuboresha elimu zao na hivyo kusaidia kufundisha madaktari wa kesho katika level mbalimbali na kwa ubora mkubwa.

Binafsi ninawafahamu baadhi ya walimu waliokwenda nje ya nchi kusomea udaktari bingwa ubobezi, lakini baada ya kufika kule na kuona kuna nafasi ya kufanya PhD basi wakaachana na superspecialization, ili wakirudi waweze pata promotion kupitia PhD kwani superspecialization haitawapa promotion.

Tungependa zaidi hawa madaktari wasome superspecialization (fellowship) ili waweze kuwafunza wanafunzi wetu kiundani. Lakini tukitaka walimu wenye PhD weeengi sana, basi hawataweza kufundisha kitu superspecialist mmoja anaweza fundisha. PhD zifanywe na madaktari wanaotibu ili kuongeza experience ya Research, lakini isiwe kigezo namba moja cha kutambulika.

Madaktari bingwa wanaotibu hawahitaji PhD ila wanahitaji superspecialization. PhD ziachwe kwa madaktari wa basic science tu au kwa madaktari wanaotibu wenye interest ya research.

Mwisho mheshimiwa Rais, nina ushauri wa ziada
1. Tuone namna wasajili wa vyama vya kitaaluma wakawa na ushirikiano na TCU. Tabia ya TCU ku consult madaktari toka sehemu tofautitofauti kuna wakati inaweza ikawa na mgongano wa kimaslahi.
2. Ni vyema vyuo vikuu vya afya vikaachana na kuangalia GPAs kwa madaktari. Nchi nyingi daktari anayefundisha chuo kikuu haangaliwi kwa GPA. Kila daktari aliyepo katika teaching hospital anakuwa ni faculty member. Hii inafanyika Afrika ya Kusini na inasaidia. Ni ngumu sana daktari katika miaka yake mitano hadi sita ya kusoma digrii ya kwanza akapata GPA kubwa ambazo zimewekwa na TCU. Lakini hata hivyo umahiri wa kufundisha na kutibu hauendani na GPA. Hizo GPA zifanyike kwa courses nyingine. Madaktari digrii zao ziendelee na mfumo wa zamani kuwa unclassified. Ni ama PASS au FAIL.

Mimi mwenyewe nashangaa kwamba mambo kama haya hayakupaswa kuandikwa kwa Rais, lakini nchi hii viongozi wengi hawawezi kujiongeza.
 
Hilo suala la GPA sikubaliani nalo...naomba uelewe kwamba kama huwezi kupata hiyo GPA wewe ni average student na ukubali hivyo.
Suala la Msc pia halina tija..utakuta mtu katambaa na masupp kibao toka Md mpaka Mmed hivyo mtu kama huyu hana capacity ya kufundisha mtu.
Hitimisho.
Sio lazima watu wote wawe walimu hata hivyo unaweza ukawa mwalimu wa familia yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mhadhiri wa Chuo Kikuu lazima awe na PhD.. Vigezo vya kupata PhD viko wazi
- Lazima aandike proposal ya kufanya utafiti ambao matokeo yake yatamapatia sifa ya kupata PhD..

- Lazima afanye utafiti katika eneo husika, hata kama anatafiti neuron moja tu, ndo maana ya uzamivu (kubwa ka isa kuliko ubobevu)..

- Lazima afanye mtihani wa mwisho unaitwa viva voce.. huu ni mtihani unaolenga kupima uzamivu wa mhusika na uwezo wake kama mtafiti anayeibukia..

Sasa mtoa hoja unaposema kuwa daktari tu afanye makorokocho gani sijui ambayo ni nje ya vitu vitatu nilivyovitaja.. hawezi kulinganishwa na PhD.. kwa hiyo TCU wako sahihi kabisa kwa sababu duniani kote, utaratibu wa PhD uko hivyo.

Swala la pili, siyo lazima mhadhiri wa PhD awe clinician.. huyu tayari ni mtafiti.. mambo ya kuattend clinical subjects yaachiwe watu wa ngazi za chini kama hao specialists.. ambao hawana sifa za kuwa academicians..

Nakamilisha kwa kusema kuwa hoja za mleta mada ni dhaifu kwa sababu vyuo vikuu siyo hospitali.. kule hakuna wagonjwa bali kuna wanafunzi wanaohitaji elimu. TCU inatenda kulingana na sheria za nchi.. labda ulete hoja mpya za kupitia sheria iwapo sheria zinazotumika zina kasoro..

Ni hayo
 
Noted
 
Noted.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom