apolycaripto
JF-Expert Member
- Feb 11, 2011
- 644
- 225
Huu mgomo kama unavyosemekana na undani wa madai yake "details" (haijajulikana kiasi gani wanataka) nadhani hautokwisha kirahisi. Nimezungukia Hospitali binafsi mbili hapa Jijini ama kweli kufa kufaana. Baadhi ya Madaktari wa Muhimbili wako huku wanapiga mzigo kama kawaida na fungu wanapata.Wangonjwa ni wengi na dau nahisi liko juu ama ni "peace of mind".
Tokea mgogoro huu uanze napata kizunguzungu hasa juu ya madai yao na kwanini Serikali imekuwa na kigugumizi. Kama alivyosema Pinda kuwa kwa anae anza kazi anadai alipwe 7,500,000 na wale nguri mpaka 17,000,000 du!.Hili mpaka sasa madaktari hawajakanusha hili binafsi naamini ni sehemu ya madai yao.
Kama ni hivi Serikali imeshikwa pabaya hapa bado polisi,walimu (wanadai isiwe chini ya 900,000 kwa graduate),na sekta binafsi ndio balaa tupu linakuja.
Kimsingi mgomo wa madaktari hautakwisha kama wanapo pa kushika na huko (private) kutokana na population ya wagonjwa kuongezeka bila shaka the law of marginal productivity ina apply (kwa maana ya pay as you earn).
Nashauri busara na uzalendo utumike kwa pande zote mbili katika kuokoa maisha ya sisi masikini (fast track inanyima haki kwa masikini). Binafsi niko skeptical na mgomo huu kwani hasara ni kwa sisi masikini .Tazama wenzetu wamesomeshwa kwa muda mwingi na kwa fedha zetu (100%), mioyo hii migumu wametoa wapi? je sisi wa 20% (kulipiwa na serikali inakuwaje)? .Ama ndio zile za bora punda afe (masikini) lakini mzigo ufike (maslahi).
Tumewapigia kelele Wabunge juu ya posho na hawa sasa inabidi tuwatizame kama wanachokidai in reality kinatekelezeka?. Kama kinatekelezeka basi Serikali iwajibike.