Haki za wagonjwa zinawezaje kuhakikishwa hospitalini? Wanasheria wekezeni na upande wa afya ili kudhibiti matatizo yanayotokana na uzembe

Nyafwili

JF-Expert Member
Nov 27, 2023
2,774
6,885
Wagonjwa wana haki zao. Nchi nyingi duniani kama Denmark, Hungary, Japani, Marekani, Afrika Kusini na Uingereza wanayo maandiko ya kitaifa ambayo yanaainisha haki za mgonjwa. Maandiko kama hayo yanaelezea haki za kila mtu/mgonjwa anayehitaji huduma za tiba ili kulinda hadhi, utu wake na heshima yake.

Shirika la Afya Duniani (The World Health Organization-WHO), linafahamu na kubaini kuwa unyanyasaji na unyanyapaa unaweza kujitokeza katika masuala ya tiba, hivyo basi liliandaa siku za awali kwenye miaka ya 1948, haki za mgonjwa zenye vipengele 12.

[1] Mgonjwa ana haki ya kupewa tiba anayostahili na yenye heshima.

[2] Mgonjwa anayo haki ya kupata taarifa kamili na iliyo sahihi kutoka kwa tabibu anayemtibu kuhusu ugonjwa wake katika njia atakayoweza kuelewa. Endapo taarifa hiyo ni tete na itamletea mgonjwa usumbufu, taarifa hiyo apewe mtu aliye karibu na anayemhusu kwa niaba yake.

[3] Mgonjwa anayo haki ya kumfahamu kwa jina daktari wake ambaye anamtibu na ambaye pia ndiye anayeratibu matibabu yake.

[4] Mgonjwa anayo haki ya kupewa taarifa kutoka kwa tabibu/daktari wake, habari ambazo zitamuwezesha kutoa idhini/rai kuhusu uchunguzi na tiba yoyote kabla kufanyika. Endapo ipo haja ya kujadili au kutoa tiba tofauti na ile ya awali kama ipo. Mgonjwa ana haki ya kupewa taarifa hiyo. Mgonjwa ana haki ya kumjua kwa jina atakayefanya tiba/uchunguzi huo unaotarajiwa kufanyika. Mgonjwa anayo haki ya kukataa tiba kwa mujibu wa kanuni na sheria zilizopo na pia anapaswa kuelezwa nini hatma yake kitiba, kwa hatua aliyoichukua.

[5] Mgonjwa ana haki ya kufikiriwa kuhusu usiri wa tiba na huduma zake kwa ujumla katika maendeleo ya matibabu yake. Kuzungumzia hadharani/kwa njia ya ushauri na pia kumpima ni siri ya mgonjwa. Wale ambao hawahusiki na mgonjwa hususan wanafunzi/jopo la madaktari wanapaswa kupata ridhaa ya mgonjwa au mlezi wake.

[6] Mgonjwa anayo haki ya kutarajia kuwa mawasiliano yake na kumbukumbu zake zote zinazohusu ugonjwa na tiba zitahifadhiwa kama nyaraka za siri (confidential).

[7] Mgonjwa anayo haki ya kutarajia kuwa kutokana na uwezo wake hospitali lazima ifanye jitihada za kuweza kumhudumia mara anapohitaji tiba/huduma. Hospitali lazima ifanye tathmini kuhusu huduma na kama ilivyo wakati wa dharura ikibidi rufaa iwe ni kitu cha haraka. Na inapobidi kama mgonjwa atapewa rufaa ya kwenda hospitali nyingine, hayo yafanyike baada ya mgonjwa kupewa taarifa kamili kuhusu sababu ya rufaa iliyopendekezwa na endapo kuna huduma nyingine badala ya hiyo rufaa. Taasisi au asasi itakayopokea uhamisho wa mgonjwa lazima ikubali kwanza kumpokea.

[8] Mgonjwa anayo haki ya kupata uhusiano uliopo kati ya hospitali inayomtibu na huduma nyingine zilizopo kama vyuo vya taaluma. Mgonjwa anayo haki ya kujua uhusiano uliopo kitaaluma kati ya wataalamu wanaomtibu kwa majina.

[9] Mgonjwa anayo haki ya kupewa ushauri kama hospitali ina mpango wa kufanya utafti wowote au majaribio yoyote yanayohusu binadamu ambayo huenda yakaathiri tiba na huduma anazopewa hapo hospitali. Mgonjwa anayo haki ya kukataa kushiriki katika tafiti hizo.

[10] Mgonjwa anayo haki ya kutarajia kuwa tiba yake itakuwa endelevu isiyo na kikomo. Mgonjwa ana haki ya kujua ni muda gani amepewa ahadi ya kumuona daktari/ mtoa huduma na itamlazimu mtoa huduma awepo kwa wakati uliopangwa. Mgonjwa katika haki alizonazo apangiwe atakayechukua nafasi ya tabibu mhusika endapo yeye tabibu hayupo. Haki za mgonjwa hazikomi njiani bali wakati akipewa ruhusa kwenda nyumbani apewe nyaraka zote za kutoka hospitali (discharge summary certificate).

[11] Mgonjwa katika tiba anayopewa kwenye hospitali binafsi, anayo haki ya kujua na kuelezwa mchanganuo wa gharama anazopaswa kuzilipa, na si lazima ijulikane fedha hizo zitatoka wapi. Inawezekana kuna mtu atakaye mlipia hata kama unamuona hana uwezo mpe bili yake.

[12] Mgonjwa anayo haki ya kujua kanuni/ sheria na utaratibu uliopo katika hospitali anayotibiwa, ili azifahamu kama mgonjwa anavyostahili.

Kwa wauguzi wote na wahudumu wote wanaotoa tiba/ huduma kwa wagonjwa. Majukumu yao ni makubwa mawili kama watoa huduma na pia na wao ni wagonjwa watarajiwa. Wanapaswa kujua sheria/kanuni hizo za haki ya mgonjwa.

Ndugu msomaji wa makala haya utajiuliza kama haki za mgonjwa zipo hapa Tanzania tunazo? Sina jibu la haraka. Ukitazama nchi zilizoendelea haki za mgonjwa zimepewa kipaumbele kwa sababu ya ELIMU. Kwa wenzetu Elimu kwanza hususa kujua wajibu na haki za kila mmoja. Sio wote wanaojua haki za mgonjwa. Rushwa inapojitokeza katika huduma za jamii, haki za mgonjwa zitatiwa mfukoni. Una haki wewe mgonjwa ujue haki zako.

Endapo una fikiri elimu ina gharama kubwa umekosea, ujinga una gharama kubwa sana. Gharama zako za maisha zinaongezeka sana katika nchi ambayo ni masikini. Kuwa maskini ni mzigo wa gharama.

Prof. Kisali Pallangyo aliyekuwa Makamu wa Mkuu wa Chuo cha Muhimbili cha Sayansi na Tiba, Julai 5 mwaka wa 2012 alitoa taarifa kwa vyombo vya habari wakati wa migomo ya madaktari, kama alivyonukuliwa na gazeti la Serikali – Daily News ukurasa wa mbele kuwa:

”Tafsiri yake isiyo rasmi: “Iko haja kwa sisi tukiwa madaktari/ matabibu kufuata maadili yetu ya kidaktari kwa kuwajali na kuwahudumia wagonjwa na kuhakikisha kuwa tunawaondelea maumivu wanayoyapata wakiwa pia wanategemea tutaboresha siha zao na kuokoa maisha maisha yao.”
 
Wagonjwa wana haki zao. Nchi nyingi duniani kama Denmark, Hungary, Japani, Marekani, Afrika Kusini na Uingereza wanayo maandiko ya kitaifa ambayo yanaainisha haki za mgonjwa. Maandiko kama hayo yanaelezea haki za kila mtu/mgonjwa anayehitaji huduma za tiba ili kulinda hadhi, utu wake na heshima yake.

Shirika la Afya Duniani (The World Health Organization-WHO), linafahamu na kubaini kuwa unyanyasaji na unyanyapaa unaweza kujitokeza katika masuala ya tiba, hivyo basi liliandaa siku za awali kwenye miaka ya 1948, haki za mgonjwa zenye vipengele 12.

[1] Mgonjwa ana haki ya kupewa tiba anayostahili na yenye heshima.

[2] Mgonjwa anayo haki ya kupata taarifa kamili na iliyo sahihi kutoka kwa tabibu anayemtibu kuhusu ugonjwa wake katika njia atakayoweza kuelewa. Endapo taarifa hiyo ni tete na itamletea mgonjwa usumbufu, taarifa hiyo apewe mtu aliye karibu na anayemhusu kwa niaba yake.

[3] Mgonjwa anayo haki ya kumfahamu kwa jina daktari wake ambaye anamtibu na ambaye pia ndiye anayeratibu matibabu yake.

[4] Mgonjwa anayo haki ya kupewa taarifa kutoka kwa tabibu/daktari wake, habari ambazo zitamuwezesha kutoa idhini/rai kuhusu uchunguzi na tiba yoyote kabla kufanyika. Endapo ipo haja ya kujadili au kutoa tiba tofauti na ile ya awali kama ipo. Mgonjwa ana haki ya kupewa taarifa hiyo. Mgonjwa ana haki ya kumjua kwa jina atakayefanya tiba/uchunguzi huo unaotarajiwa kufanyika. Mgonjwa anayo haki ya kukataa tiba kwa mujibu wa kanuni na sheria zilizopo na pia anapaswa kuelezwa nini hatma yake kitiba, kwa hatua aliyoichukua.

[5] Mgonjwa ana haki ya kufikiriwa kuhusu usiri wa tiba na huduma zake kwa ujumla katika maendeleo ya matibabu yake. Kuzungumzia hadharani/kwa njia ya ushauri na pia kumpima ni siri ya mgonjwa. Wale ambao hawahusiki na mgonjwa hususan wanafunzi/jopo la madaktari wanapaswa kupata ridhaa ya mgonjwa au mlezi wake.

[6] Mgonjwa anayo haki ya kutarajia kuwa mawasiliano yake na kumbukumbu zake zote zinazohusu ugonjwa na tiba zitahifadhiwa kama nyaraka za siri (confidential).

[7] Mgonjwa anayo haki ya kutarajia kuwa kutokana na uwezo wake hospitali lazima ifanye jitihada za kuweza kumhudumia mara anapohitaji tiba/huduma. Hospitali lazima ifanye tathmini kuhusu huduma na kama ilivyo wakati wa dharura ikibidi rufaa iwe ni kitu cha haraka. Na inapobidi kama mgonjwa atapewa rufaa ya kwenda hospitali nyingine, hayo yafanyike baada ya mgonjwa kupewa taarifa kamili kuhusu sababu ya rufaa iliyopendekezwa na endapo kuna huduma nyingine badala ya hiyo rufaa. Taasisi au asasi itakayopokea uhamisho wa mgonjwa lazima ikubali kwanza kumpokea.

[8] Mgonjwa anayo haki ya kupata uhusiano uliopo kati ya hospitali inayomtibu na huduma nyingine zilizopo kama vyuo vya taaluma. Mgonjwa anayo haki ya kujua uhusiano uliopo kitaaluma kati ya wataalamu wanaomtibu kwa majina.

[9] Mgonjwa anayo haki ya kupewa ushauri kama hospitali ina mpango wa kufanya utafti wowote au majaribio yoyote yanayohusu binadamu ambayo huenda yakaathiri tiba na huduma anazopewa hapo hospitali. Mgonjwa anayo haki ya kukataa kushiriki katika tafiti hizo.

[10] Mgonjwa anayo haki ya kutarajia kuwa tiba yake itakuwa endelevu isiyo na kikomo. Mgonjwa ana haki ya kujua ni muda gani amepewa ahadi ya kumuona daktari/mtoa huduma na itamlazimu mtoa huduma awepo kwa wakati uliopangwa. Mgonjwa katika haki alizonazo apangiwe atakayechukua nafasi ya tabibu mhusika endapo yeye tabibu hayupo. Haki za mgonjwa hazikomi njiani bali wakati akipewa ruhusa kwenda nyumbani apewe nyaraka zote za kutoka hospitali (discharge summary certificate).

[11] Mgonjwa katika tiba anayopewa kwenye hospitali binafsi, anayo haki ya kujua na kuelezwa mchanganuo wa gharama anazopaswa kuzilipa, na si lazima ijulikane fedha hizo zitatoka wapi. Inawezekana kuna mtu atakaye mlipia hata kama unamuona hana uwezo mpe bili yake.

[12] Mgonjwa anayo haki ya kujua kanuni/sheria na utaratibu uliopo katika hospitali anayotibiwa, ili azifahamu kama mgonjwa anavyostahili.

Kwa wauguzi wote na wahudumu wote wanaotoa tiba/huduma kwa wagonjwa. Majukumu yao ni makubwa mawili kama watoa huduma na pia na wao ni wagonjwa watarajiwa. Wanapaswa kujua sheria/kanuni hizo za haki ya mgonjwa.

Ndugu msomaji wa makala haya utajiuliza kama haki za mgonjwa zipo hapa Tanzania tunazo? Sina jibu la haraka. Ukitazama nchi zilizoendelea haki za mgonjwa zimepewa kipaumbele kwa sababu ya ELIMU. Kwa wenzetu Elimu kwanza hususa kujua wajibu na haki za kila mmoja. Sio wote wanaojua haki za mgonjwa. Rushwa inapojitokeza katika huduma za jamii, haki za mgonjwa zitatiwa mfukoni. Una haki wewe mgonjwa ujue haki zako.

Endapo una fikiri elimu ina gharama kubwa umekosea, ujinga una gharama kubwa sana. Gharama zako za maisha zinaongezeka sana katika nchi ambayo ni masikini. Kuwa maskini ni mzigo wa gharama.

Prof. Kisali Pallangyo aliyekuwa Makamu wa Mkuu wa Chuo cha Muhimbili cha Sayansi na Tiba, Julai 5 mwaka wa 2012 alitoa taarifa kwa vyombo vya habari wakati wa migomo ya madaktari, kama alivyonukuliwa na gazeti la Serikali – Daily News ukurasa wa mbele kuwa:

”Tafsiri yake isiyo rasmi: “Iko haja kwa sisi tukiwa madaktari/matabibu kufuata maadili yetu ya kidaktari kwa kuwajali na kuwahudumia wagonjwa na kuhakikisha kuwa tunawaondelea maumivu wanayoyapata wakiwa pia wanategemea tutaboresha siha zao na kuokoa maisha maisha yao.”
Wewe ni member mpya mwenye tija katika jukwaa hili tofauti na vijana wa hovyo kama akina Mpwayungu Village
 
Usemayo ni kweli ila hebu jitahidi ukiwa na mgonjwa basi uwe na hela ahudumiwe atoke chap mbali na hapo haki itamkuta kaburini
 
Hapa Tanzania Daktari Mmoja anahudumia mamia ya wagonjwa Kwa siku unapata wapi Muda wa hayo Yote?

Lakini Inawezekana
 
Mkuu, ujue siyo wote wenye Kipato cha kufanya hivyo (Rushwa), watu wa aina hii tuendelee kuwaacha wazidi kuteseka??
 
Hapa Tanzania Daktari Mmoja anahudumia mamia ya wagonjwa Kwa siku unapata wapi Muda wa hayo Yote?

Lakini Inawezekana

. Sekta ya afya ni ya mhimu sana, ni vizuri kuwa na wanasheria kwenye hii sekta , ili hawa madaktari, wauguzi wazembe wawe wanashitakiwa
 
Back
Top Bottom