Mabomu Zanzibar.

Hali haijatulia, mabomu yanaendelea. Hamkani si shwari. Kuna baadhi ya mabomu yameingia katika nyumba za Michenzani (FLATS). Moto unawaka. Habari zaidi kufuata.
 
Safi sana uamsho lianzisheni tu mpaka kieleweke'kuungana na li nchi lisilo na mila wala desturi ndio tabu yake hyo'mimi mbara pyua ila pia sipendi limuungano hili naomba kila siku life tu'

Uko sawa kabisa, ila jitahidi uwe na HOJA za msingi.
 
Huenda wameamka baada ya kugundua kuwa serikali, kwa uzembe na ufisi wake, inawaua bila sababu tokana na kuruhusu vyombo visivyofaa kusafirisha abiria. Ndani ya mwaka mmoja meli mbili zimezama na mamia ya watu wasio na hatia wamepoteza maisha yao. Kama si hilo basi huenda wanaaanzisha changamoto la mageuzi ya kweli baada ya kuona nchi nyingine zikifanikiwa. Tuwaunge mkono maana ni kwa ajili ya ukombozi wetu bara na visiwani. Kama sababu ni kuchukia au kutotaka muungano, bado wana haki kwanini kulazimisha ndoa isiyo na faida?
 
Nadhani mwandishi muongo anatudanganya......wapigwe mabomu kwani zenji kuna chadema?
 
Habari nilizozipata muda huu kutoka kwa jamaa walioko huko, kwamba eneo la Darajani kumetokea vurugu na sasa hivi jeshi la polisi wanatuliza fujo kwa mabomu.
Mkuu Mgombezi.

Polisi wanatuliza fujo au polisi wameanzisha fujo?

Umesema kumetokea vurugu. Nani ameanzisha vurugu? Chanzo cha vurugu ni nini?
 
Kwa nini Msangi asipelekwe huko akamshughulikie kiongozi wa Uamsho?
 
Kunani tena huko??
Muungano uvunjwe tu, jamaa watafanya mauaji ya kutisha wasingizie muungano.
 
Katiba mpya iwape nchi yao na sisi tubaki na Tanganyika yetu. Hawa tunawaendekeza ila siku si nyingi tutajuta. Wao wameshakatazwa mikusanyika isiyo rasmi, watu wako katika maombolezo siku tatu lakini wao wanakaidi amri ya serikali. Halafu tena hii meli ilikataliwa usajili na SUMATRA wao Zenji wakaamua kuisajili!!!! Let us have talaka tatu na huu muungano.
 
Hali si shwari, polisi Unguja waaza kupiga mabomu ya machozi kila kona ya Mji. Habari zaidi kufuata.

embu cheki foto yake..
attachment.php
 

Attachments

  • mabomu zenji.jpg
    mabomu zenji.jpg
    82.5 KB · Views: 314
Mpaka muda huu mji wa Unguja uko kimya, kila mtu amejificha anakokujua. Mabomu ya hapa na pale yanaendelea.
 
Back
Top Bottom