Mabomu yarindima chuo cha uhasibu Arusha IAA baada ya wanafunzi kugoma

Manhunt

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
218
26
Kufuatia tukio la kuuawa mwanafunzi wa chuo cha uhasibu Arusha jana usiku, wanafunzi wameanzisha mgomo ambao umepeleka FFU kupelekwa chuoni hapo ambapo hadi sasa wanawatawanya wanafunzi hao kwa mabomu ya kutolea machozi.
Wanafunzi wanasisitiza serikali kuchukulia hatua madai yao ya usalama ambapo wamedai huwa wanaripoti polisi lakini hakuna kinachofanyika.

Mbunge Godbless Lema, mkuu wa chuo, Mkuu wa mkoa na OCD wako shuleni hapo kujaribu kupata suluhu ya suala hilo
Updates; mbunge Godbless Lema akamatwa baada ya kuonekana yupo upande wa wanafunzi hii ni baada ya Mkuu wa mkoa kutoa ahadi sawa na aliyowahi kuitoa yalipotokea mauaji kama hayo ambayo hadi leo majibu yake hayajatolewa

attachment.php

attachment.php

24042013612.jpg
GAri ya mbunge wa Arusha Godbless Lema ikipelekwa kituo cha Polisi
 
Attachments

  • IMG-20130424-WA0003.jpg
    IMG-20130424-WA0003.jpg
    86.6 KB · Views: 1,690
  • img-20130424-wa0001(01).jpg
    img-20130424-wa0001(01).jpg
    102.6 KB · Views: 1,723
Kufuatia tukio la kuuawa mwanafunzi wa chuo cha uhasibu Arusha jana usiku, wanafunzi wameanzisha mgomo ambao umepeleka FFU kupelekwa chuoni hapo ambapo hadi sasa wanawatawanya wanafunzi hao kwa mabomu ya kutolea machozi.
Wanafunzi wanasisitiza serikali kuchukulia hatua madai yao ya usalama ambapo wamedai huwa wanaripoti polisi lakini hakuna kinachofanyika.
Mbunge Godbless Lema, mkuu wa chuo, Mkuu wa mkoa na OCD wako shuleni hapo kujaribu kupata suluhu ya suala hilo

Aisee niko jirani nasikia jinsi yanavyorindima.

Swali ninalojiuliza kunahaja ya kutumia mabomu kwenye hili swala?
Kwani si wangewasikiliza nakutafuta jinsi ya kuwatuliza bila mabomu....njia ya mabomu:nono:
 
muda huu mabomu yamepigwa chuo cha uhasibu arusha baada ya wanafunzi kutaka kuandamana kutokana mwanafunzi mmoja wa mwaka wa pili kuchomwa kisu cha shingo na kufariki dunia jana usiku saa 3 pembeni kidogo na chuo.
 
Agghhrrr...Mapoliccm uwezo wao wa kufikiri upo kwenye mauvimbe ya chini kwa nyuma. Diplomac imekataa kwani kwenye swala hili??? Natamani nijiuzulu kuwa Mtanzania.
 
natumaini kama lema yuko mambo yatakuwa poa maana jamaa anatumia sana busara
 
Siku hizi mafunzo ya polisi yanakuwa jinsi gani ya kutumia mabomu ya machozi. Sio Kulinda na kuhudumia Watanzania, wao vita kwenda mbele
 
Kwani hawa polisi wetu wameambiwa hayo mabomu yamekaribia kuharibika maana wao kila tukio lazima wayalipue ovyo tu.

Kweli hawa jamaa hawana mbinu yoyote mbadala kutuliza mtafaruku wowote isipokuwa ni mabomu tu, au wameagiziwa mengi sana wanaona wayapunguze kwa kila linapotokea jambo lolote.

Kazi tunayo kubadilisha fikra za hawa jamaa especially pindi wakiwa mbali na ofisi zao
 
Yani niko kwangu na bado nayasikia hayo mabomu

We nae hata hueleweki.... Mara uko kwako afu bado umeweza kumwona Lema akikimbia.... Hebu be serious kidogo manake tuna ndugu zetu huko! Acha wenye uhakika waandike we toa porojo zako hapa
 
We nae hata hueleweki.... Mara uko kwako afu bado umeweza kumwona Lema akikimbia.... Hebu be serious kidogo manake tuna ndugu zetu huko! Acha wenye uhakika waandike we toa porojo zako hapa

Anasikiliza Sunrise Redio huyo...................... taarifa zake ni za kuunga unga
 
Back
Top Bottom