Mabillioni ya JK

ureni

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
1,261
526
Wakuu ile issue ya mabillioni ya JK aliowakopesha watazania iliishia wapi?waliokopa wamesharudisha au ilikua kama bonus?kuna mwana JF yeyote aliyefanikiwa kuipata au ilikuwa ni politics?
 
Kwa hiyo ilikuwa ni sanaa?lakini nakumbuka watu wengi sana walipanga foleni NMB na CRDB kwa ajili ya hayo mabilioni inamaana hawakupata kitu?
 
Zote alikopeshwa RZ1

Kwa nini wabunge wetu tuliowapeleka bungeni wasihoji hizi fedha matumizi yake yalikuwa vipi tupate kujua na zitarudije na walikopeshwa wakina nani na kwa kiasi gani?
 
Riz1 ni nomaaa kachukua bil 64 za EPA huyo dogo ana hekari 290 mkulanga!

Akibisha nawapeleka hadi kwenye shamba lake hilo la mkulanga!

Amelima nini ktk shamba hilo ? au ana pori la eka 290? Kama ana pori la eka 290 ni sawa na Watz wengi tu ambao wana mapori huko huko Mkuranga. Kibaya zaidi wengine wanayo zaidi ya huyo dogo.
 
Haya Mabilioni ya kikwete yananisikitishaga sana wakuu, waliopata ni wale wasio stahili na walio stahili kupata hawakupata, Mpaka leo na kesho sijajua dhumuni lake lilikuwa ni nini hasa,

wapo walio kopa wakaenda kuezekea nyumba zao, wapo waliokopa wakaenda kufanyia harusi, na hapo hapo viongozi wanajitapa wana mpango wa kuzifikia nchi kama thailand na zinginezo za asia,

Nchi hii imejaa siasa za kufa mtu na hatuwezi piga hatua za kuzalisha wajasiriamali ambao baadae watakuja kuwa ndo wanashikilia uchumi wa nchi kwa mwendo huu, hayo mabilioni bora hata wangetafutwa wajasirimali kumi pekee hapa nchini wenye muelekeao mzuri wakapewa kuliko kugawa mikopo kama pipi na bila kuangalia wanao pewa na wafanya biashara au la
 
Hii nchi ni kashfa tu zitakuwa zinafuatana...kweli kila kukicha afadhali ya jana
 
Back
Top Bottom