Albedo
JF-Expert Member
- Feb 24, 2008
- 5,559
- 1,452
Mkuu ndege ya uchumi. mimi sioni kama marando anakosa kwa kutokukubaliana na sera za uburuzwaji za mrema maana wote ni watoto wa baba mmoja na walikuwa wanatimiza wajibu wao.
Kosa kubwa kwa CHADEMA ni kutupa karata ya uaminifu mapema kabla hawajamsoma mchumba mwenyewe kama kweli ni mzalendo kivile.
Unajua mimi sishabikii mabomu ya kisiasa yanavyorushwa, bali umakini wa mipango na uhakika wa mfumo uliojengwa na kuheshimiwa hata inapolazimu mabadiliko. Ndo maana ingawa huwa nawananga sana hapa hawa walumendago (UwT) lakini kiukweli ninawadmire mno kwa kazi ngumu wanazozifanya na jinsi mfumo wao ulivyokuwa settled ingawa haueshimiwi na watumiaji wa mfumo huo.
Pia nawasihi CHADEMA wajitahidi kuwaandaa vijana kushika hatamu ndani na nje ya chama kama walivyofanya kwa akina zitto, mnyika, mdee et all. Tupike chakula chetu tuache kudoea kwa jirani
Mkuu Msanii, mimi ssiko ndani ya CHADEMA, sina uhakika na wewe ila unaonesha na wewe hauko ndani ya CHADEMA, Katika Suala la Vetting sina shaka kabisa na CHADEMA ingawa wanaweza kabisa wasiwe 100% perfect pale wanapomchunguza mtu. Katika kipindi hiki cha Uchaguzi kuna wanasiasa wengi sana baada ya kupigwa chini CCM sasa wanagombea kwa CHADEMA, siwataji kwa majina maana naamini unawafahamu. Katika hao naamini kabisa CHADEMA wanafahamu ni yupi watakuwa naye baada ya Uchaguzi na ni yupi Atarejea CCM kama wakishindwa Ubunge, sasa katika wote CHADEMA kwa nini hawajaamini hao kama wana tabia ya Ukurupukaji? Mimi naamini kabisa kama kweli Marando ni mtu wa TISS na anawafahamu vyema wenzie wa TISS na akawa mwaminifu kwa CHADEMA basi hii ni Tunu nzuri sana kwa CHADEMA kwa sababu wamepata mtu wa kuwa alert yupi ni Kondoo yupi Chui.
Nitapinga mpaka naingia kaburini mtu yeyote atakayesema kwamba Marando ndiye aliyeivuruga NCCR-Mageuzi, Marando did a miatake kwa kumpisha Uenyekiti Mrema na baada ya Uchaguzi Mrema akaanza kuonesha Makucha yake Halisi