Mabere Marando Ateuliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA

Mimi ningependa zaidi kusikia maoni ya Mlalahoi katika hili la Marando kuteuliwa kamati kuu ya Chadema.

Binafsi simuelewi vizuri huyu bwana. Hivyo sina cha kuchangia.
 
Thanx kwa taarifa.

Nadhani makosa haya yasiendekezwe kwenye vyama vya upinzani. Naona imekuwa too fast to trust him to be there.

Simchukii lakini nahisi kuna utaratibu umeharakishwa sana hapo. Angefaa apewe nafasi ya kumpima na kumsoma kabla hajapewa majukumu makubwa zaidi.

Kuna kitu kinaniambia kichwani kwamba kuna something si sawa ktk hili

You are damn right my brother! Hii haijakaa sawa. Ninaamini kwamba wapo wanachama wakereketwa na wenye uwezo wengi tuu ambao wangeweza kufikiriwa kupewa hiyo nafasi kabla ya Mabere marando. Tatizo letu watazania walio wengi ni kutopenda kusumbua akili zetu japo kidogo tu. Iweje mtu huyu aliyeingia juzi tu kwenye Chama ndio aanze kurundikiwa madaraka ya kutoa maamuzi nyeti? Majuzi nimeuliza hapa kwa nini Marando awe ndio mwenye kauli ya mwisho kuhusu kumfikisha mahakamani JK watu wakajibu haraka haraka kuwa aliona ingetupotezea muda tu? jamani kumtingisha mpinzani wako kwa silaha yoyote uliyonayo nayo ni kupopteza muda?
Haya, imekuja kesi ya kumshitaki Mama Salma K kwa kutumia vibaya mali za umma kumpigia mumewe kampeni kama walivyofanya wenzetu wa Zambia, bado watu wanavuta vuta miguu...
Hakuna mtanzania wa kawaida asiyejua historia ya Marando. Kwa akili ya kawaida kabisa, huyu ni mtu ambaye kwa wakati huu wa majeruhi Chadema hawakupaswa kumgusa kwa a ten foot pole!!
Inashangaza ghafla bin vuu viongozi wa Chadema kumuona huyu mtu ni lulu.
Hivi mtu hawezi kusaidia chama akiwa mwanachama wa kawaida mpaka awe 'high table'???
Hivi wakiibuka baadhi ya wanachama wakaanza kupingana na maamuzi ya viongozi ya kumpapatikia Marando, wataitwa wakorofi??
Naanza kuhisi kuna watu wako kwenye payroll ya watu fulani kwa ajili ya kuivuruga Chadema. Mark my Words.
 
Nina hakika Uongozi wa Chadema unamfahamu Marando kuliko wengi wetu tunavyofikiria na nashauri tuwe na imani na maamuzi wanayoyachukua kwa niaba yetu. Hivi wana Chadema kwa nini hatujiulizi kwa nini hata watetezi wa CCM wasioitakia mema Chadema eti leo nao wajitokeze kutoa ushauri kwa Chadema, kwa lengo gani - kutuvuruga ? Humu kuna watu hata historia sahihi na kiini cha ugomvi wa Marando na Mrema hawakijui lakini wanakuwa wepesi kumhukumu kwa maneno ya mitaani. Hivi Dr. Slaa na umakini wake kama tunavyomkubali na alivyo na uwezo wa kupata nyeti za dola, tunashindwa kumwamini kwa hili la Marando ? Kweli kipimo chetu cha kutomkubali Marando kiwe Mrema ! of all the people, jeezus ! Mimi namkubali Marando 100%.
 
Marando si ndiye huyo aliiua NCCR na baadaye akapewa ubunge wa East Africa kwa kupitishwa na wabunge wa CCM. Mtamlaumu Mrema, lakini wakati wanamhitaji walimpa uenyekiti Mrema na kisha wakaongoza njama kibao za kutaka kumng'oa badala ya kuwaachia wanachama.

Simwoni Marando kama mtetezi wa wanyonge, ni opportunist na ambaye anapata pesa nyingi kwa kuwatetea mafisadi.

Kwanza yeye mwenyewe Marando ni fisadi.
 
Ndugu zangu, kama nilielewa vizuri ni kwamba amechaguliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu, Hili lisitupe shida sana. Haijatangazwawala kuainishwa popote kwamba amekuwa mjumbe wa kudumu wa kamati kuu, hapa tusichanganye mambo.

All in all, CHADEMA ni chama kilichojitosheleza kwa mipango madhubuti tena iliyojaa tija. Kutokana na hili mimi naamini CHADEMA kupitia viongozi wake wapo katika kufuatilia au hata wamesha jiridhisha juu ya doubts zilizo kuwa impossed kwa Mr. Mabere N. Marando. Ninaamini hawajalala ila kama wanachama wenye uchungu na chama pamoja na nchi yetu hatuna buni ku_question mambo mawili-matatu ambayo kwa namna moja au nyingine yanatupa wasiwasi juu ya mustakabali wa chama chetu.

Hivyo basi, mimi naona kuwa suala la kuwa mjumbe wa kamati kuu haimpi Marando nafasi ya kuwa na mamlaka ya juu katika chama, bali inampa changamoto ya ku
-show cooperation and supportiveness kwa viongozi wengine, tena ndio sehemu ambayo anaweza kuchunguzwa kwa umakini zaidi bila kuwa na madhara yoyote. Pia ninaamini kuwa zipo position katika chama ambazo kama likifanyika kosa hata kama ni dogo lazima litakuwa na impact makubwa sana ila si nafasi ya ujumbe katika kamati kuu.

Katika uhalisia wa mambo hasa katika kipindi hiki cha kampeni na uchaguzi, viongozi wetu wa juu (CHADEMA) wana kazi kubwa na wahitaji mipango madhubuti na ushirikiano, ili kufanikisha adhima yetu ya kuongoza nchi. Hivyo basi kama jambo hili limetoka kwa mwenyekiti na kamati yake na kupewa baraka zote sina shaka kuwa lazima utakuwa ni uamuzi uliozingatia misingi, tija, ufanisi na usafi wa moyo.

Mungu ibariki CHADEMA, wabariki wote wanaoiombea mema na watie upofu wote wanaowaza kuiharibu CHADEMA yetu, maana katika wewe kupitia CHADEMA tunaimani yapo matumaini yakupatikana kwa haki za watoto wako ziliyopotea. Amen
 
Thanx kwa taarifa.

Nadhani makosa haya yasiendekezwe kwenye vyama vya upinzani. Naona imekuwa too fast to trust him to be there.

Simchukii lakini nahisi kuna utaratibu umeharakishwa sana hapo. Angefaa apewe nafasi ya kumpima na kumsoma kabla hajapewa majukumu makubwa zaidi.

Kuna kitu kinaniambia kichwani kwamba kuna something si sawa ktk hili

Ningeomba maneno yako haya yahifadhiwe hapa JF, ninanvyofahamu viapo vya UWT havifutiki...kosa alilofanya Amran Kombe kushindwa kwa lugha nyepesi kuwahakikishia mabosi wake kuwa hilo halitatokea...jambo ambalo Marando ameliweza tokea walipoanza na vugu vugu la mageuzi na NCCR baadae NCCR-Mageuzi...this guy is too sharp to negotiate his way through!
 
Bahati mbaya huu uteuzi umeleta malumbano baina ya supporters wa CHADEMA wakati mbaya. Kwa sasa CHADEMA ina supporters wengi kuliko wananchama. Wengine tuko nje, na tungekuwa Tanzania tungejiunga rasmi.

Hofu iliyotupata inatokana na kukipenda CHADEMA, na kuogopa kisiingiliwe. Ila kuna upande ambao inawezekana wenye hofu hawajauona: Hakuna uwezekano kwamba angalau sehemu ya viongozi wa UWT wanaisapoti CHADEMA kipindi hiki? Maana kama kweli nia yao ni kulinda USALAMA WA TAIFA, basi wataweza sana kuiunga mkono CHADEMA. CCM inaangamiza Tanzania wakati huu. Mwaka huu, kukiunga mkono CHADEMA ni kuilinda Tanzania.

Kuna swali ambalo sijapata jibu lake: Marando alipotangaza kujiunga na CHADEMA alisema hapendi nafasi yoyote ya uongozi. Alikuwa anadanganya? Kwa nini CHADEMA haikusubiri mpaka angalau uchaguzi umalizike?
 
We hope for the bast!
I do not trust BN Marando either.
 
wakuu....!
kuna yule MTATIRO JULIUS wa CUF........

the guy is good jamani

chadema fanyeni linalowezekana mumchukue maanake kwa yule bwana mkubwa kukaa CUF ni kama ''BIG FISH IN A SMALL POND'':becky::becky:
 
Unataka CHADEMA iwe kama Real Madrid au ManCity? CUF nako kuzuri tu.
 
kilombero kuko vizuri, hali ya kisiasa si mbaya ni kujipanga kulinda kura na kubana mianya yeyote ya wizi.

Hi, hongera kwa kujitolea kuwapigania wana kilombero. Huu ni ujumbe wangu kwa wana kilombero. Mmepewa Jimbo tajiri sana na mwenyezi Mungu, ardhi yenye uwezo wa kuzalisha mpunga kwa mamilioni ya tani, mito inayotiririsha maji miaka nenda miaka rudi. Lakini kwanini ninyi ni masikini? Sera mbovu za CCM. Vipaumbele vya CCM ni kula miaka minne, honga upate kura mwaka mmoja. Wameshindwa kuwawezesha mlime kilimo cha kisasa, wameshindwa kuwatafutia masoko yenye tija. Mabadiliko ni sasa, chagua CHADEMA, Chagua madiwani wa CHADEMA, Chagua Regia (ubunge), Chagua Dr. Slaa(urais). Tanzania ni yetu sote na itajengwa na sisi wenyewe, tuwaondoe katika madaraka wanaodidimiza uchumi wa taifa letu na kuigeuza nchi yetu kuwa ombaomba.
 
Uteuzi sawa,lakini Marando bwana!!!!!!!!!!!!!! La msingi Chadema chonde chonde kuweni makini hasa!!!!!
 
kilombero kuko vizuri, hali ya kisiasa si mbaya ni kujipanga kulinda kura na kubana mianya yeyote ya wizi.
Siku hizi watu hawaibi katika maboksi....wanamkwiba mpiga kura! Akija kupiga kura anakua ameshakwibwa!
 
wakuu....!
kuna yule MTATIRO JULIUS wa CUF........

the guy is good jamani

chadema fanyeni linalowezekana mumchukue maanake kwa yule bwana mkubwa kukaa CUF ni kama ''BIG FISH IN A SMALL POND'':becky::becky:

Mtatiro ni Kamanda na kachero vilevile. Kazi yake uchaguzi wa mwaka huu tunaijua.

Kwa ufupi ni kwamba CCM wasahau jimbo la Ubungo mwaka huu.
 
wenye mauzoefu wananena sasa. siyo maneno yangu haya, ila nimehisi kuna tatizo ktk uamuzi wa CHADEMA kuharakisha kumpa degree ya kuaminika huyu jamaa.

Mkuu ingawa siombei mabaya lakini sisikii harufu nzuri ktk hili

Hata mimi siombei mabaya lakini rekodi yake ndio inatiashaka ukichanganya na uharaka.
 
Back
Top Bottom