Mabeberu, Vibaraka wa Mabeberu, Wazalendo wa Hayati Magufuli, na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Na wanasahau ni huyu huyu ndie alituambia serikali wenyewe tuna uwezo wa kujenga copper smelter inayohitajika na Acacia. Na watu tuliposema kwamba hizo ni porojo tu, misukule yake kama kawaida ikaishia kumwaga matusi tu!

Matokeo yake, hadi umauti umemkuta, hata "tofali" moja hawajajenga!
Nchi hii inawajinga wengi sana

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
UTANGULIZI

Amini usiamini, wale wale ambao wamekuwa wakijivika uzalendo, linapokuja suala la Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, ndiyo hao hao wanaotumikia Mabeberu bila wao kujijua!

Nitajadili mada hii katika sehemu mbili:-
  • Kwanini wale wanaoitwa Mabeberu hawawezi kuwa tayari kuona miradi kama ya Bandari ya Bagamoyo inafanikiwa, na
  • Hoja zinazotolewa na Wazalendo Kupinga Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.
Kwa bahati, binafsi mwaka 2016 nilikuwa “Mbeba Mikoba” wa Researcher mmoja wa Kimarekani (Beberu?) aliyekuwa anafanya utafiti kuhusu Belt and Road Initiative (BRI).

Kazi yangu kubwa ilikuwa Literature Review!

Kwa wanaofahamu mambo ya Resech, ukifanya Literature Reviews, hususani ya wasomi kama huyu bwana, basi unapata fursa ya kufahamu mambo mengi zaidi yaliyopata kutokea hapo kabla kwenye eneo husika!

Kwa wasiofahamu, Mradi wa Bandari ya Bagamoyo ni matokeo ya (BRI) ambayo, Rais wa China, Xi, anailezea BRI kwamba:


Kwa lugha nyepesi, malengo ya China kupitia BRI ni kuiunganisha nchi hiyo na sehemu zingine duniani, hususani Asia, Afrika, na Ulaya! Uunganishaji huo ni kwa ujenzi wa miundombinu, hususani ya bandari, reli, na viwanja vya ndege.

Ndugu yangu MALCOM LUMUMBA alipata kuchambua kwa undani kabisa suala la Belt and Road Initiative!!

Na hapo sidhani kama mtu anahitaji kuwa na Shahada ya Diplomasia ya Uchumi na Ushikirikiano wa Kimataifa kunusa “threat” ya mpango huo wa China kwa mataifa makubwa, hususani Marekani!

Kutokana na ukweli huo, ndo maana haishangazi mara tu BRI ilipotangazwa, Waandishi na Watafiti mbalimbali kutoka nchi za magharibi wakaanza kulivalia njuga suala hilo.

Makala zikaandikwa, na tafiti zikafanywa kuhusu BRI, lakini makala nyingi kama sio zote zililenga kuyatisha mataifa mengine kuwa makini na BRI!

Watu hawa wakageuka kuwa “Wajomba Zetu” Afrika, huku wakituasa tusije tukaingia kwenye mtego huo hatari wa China!

Ni kupitia hizo tafiti ndipo nami nikajikuta nipo na huyo Mtafiti Msomi kweli kweli wa Kimarekani.

Huyu Bwana case studies zake zilikuwa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, Bandari ya Hambantota (Sri-Lanka), pamoja na Bandari ya Piraeus (Ugiriki).

Ukweli ni kwamba, ilinichukua chini ya dakika 3 kugundua Mtafiti huyu ni kama tayari alishakuwa na “matokeo” ya utafiti wake hata kabla kazi haijaanza! Kwa kifupi, alionesha dalili zote za kutounga mkono Mradi wa Bandari ya Bagamoyo!

Hata "beberu" niliyekuwa namtumikia, nae alikuwa pamoja na "Wazalendo" wetu!!

Binafsi, nilikuwa “in favor of” Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, kwahiyo tukaanzisha kimdaharo kisicho rasmi!

Baada ya kuona hoja zake nyingi nazipangua, akaishia kuuliza ikiwa nadhani ni busara kwa taifa maskini kama Tanzania kuwa na bandari kubwa kama ya Bagamoyo!!

Jibu langu kwake lilikuwa rahisi sana, kwamba: Bandari ya Bagamoyo itakuwa ni kubwa mno kwa Tanzania endapo tu unaamini Tanzania na majirani zake wataendelea kuwa maskini kwa miongo kadhaa ijayo, vinginevyo, huwezi kusema ni “kubwa mno”!

Kwa ufupi, Mheshimiwa huyu, kama walivyokuwa wenzake wengine, nyimbo zao zilikuwa ni agenda ya siri ya China kuitumia BRI kama Mtego wa Madeni kwa nchi maskini!

Lilipokuja suala la Bandari ya Hambantota kule Sri-Lanka, propaganda zikasambazwa kwamba China IMEITWAA bandari ya Sri Lanka ili kufidia deni lake!

Wazalendo wetu nao wakazidaka propaganda hizo, na bila kufanya utafiti, wakaanza kutueleza kwamba “tukishindwa kulipa deni, Wachina wataichukua Bandari ya Bagamoyo kama walivyofanya kule Sri-Lanka.”

Kuweka kumbukumbu sawa, habari za Wachina KUITWAA bandari hiyo zilipotoshwa. Nitaeleza hili kinaga ubaga hapo baada kwenye makala hii.

Pamoja na suala la “Debt Trap”, watu hawa tunaowaita Mabeberu ambao kwa hili tunawaona wanajali maslahi yetu, pia wakawa wanatuambia agenda nyingine ya siri ya China ya kuanzisha “military base” kupitia BRI.

Hapa wakawa wanalenga kutuambia, hata mradi kama wa Bandari ya Bagamoyo, lengo lake ni Wachina kutaka kuweka kambi za kijeshi eneo hili la Afrika Mashariki!

Hata hivyo, hawatuambii ukweli kwamba, ni wao wenyewe ndio wanaozihofia hizo “military bases” za China endapo zitawepo!

Kila mfuatiliaji wa mambo duniani, anafahamu Marekani ina kambi za kijeshi sehemu kadhaa duniani, lakini linapokuja suala la China au mataifa mengine kufanya yale yale ambayo yeye keshayafanya kwa miongo kadhaa, hapo inageuka kuwa nongwa!

Waingereza wana msemo “If you can’t beat them, join them.”

Guys, amini usiamini, juzi yule Mtafiti niliyekuwa nae ametoa makala kwenye moja ya majarida maarufu sana duniani! Baada ya kuisoma makala ile, hapo hapo nikajisikia uchungu, na kumhurumia!

Yaani yule yule aliyekuwa anaipinga BRI, kwenye hiyo makala anaulaumu wazi wazi Utawala wa Trump kwa kutumia kete ya Debt Trap kama njia ya kuidhoofisha BRI.

Kwenye makala hiyo, kuna sehemu anahoji “Kama kweli BRI ni kitu kibaya kiasi hicho, ni kwanini basi China inaendelea kutafuta Washirika walio tayari kujiunga na BRI.”

Mwishowe, Mtafiti huyu anaisemanga serikali yake kwamba ”USA haitaweza kumzuia Rais wa China kuwekeza kupitia BRI endapo US haitakuwa na mbadala kwa mataifa yanayoshirikiana na China!

Ufaransa, imeanza kuliona hilo kama ilivyowahi kuripotiwa na France24 kwamba:


Desperation ya Mtafiti huyu bila shaka inatokana na vile anavyoona jinsi ambavyo nchi mbalimbali duniani jzinavyojiunga na BRI, kinyume na matarajio ya USA ambayo ilikuwa ina-lobby nchi zingine, hususani Washirika wake kutojiunga na BRI.

Kwa bahati mbaya sana, si Afrika, si Asia! Hadi baadhi ya nchi za Ulaya na Carribean zinaingia kwenye BRI. Mbaya zaidi, miradi ya BRI inaonekana kufanya vizuri sana!

Kwa mfano, mwaka 2016 Bandari ya Piraeus ilikuwa ndio ya kwanza barani Ulaya kubinafsishwa chini ya BRI. Bandari hii ndiyo bandari kubwa kuliko zote nchini Ugiriki, na ndio langu kuu la bahari linalounganisha nchi za EU na Asia!

Hapo kabla, bandari hii ilikuwa haifanyi vizuri, na ripoti za nyuma zilikuwa zinaiweka bandari hiyo kama bandari ya 17 barani Ulaya!

Baada ya Wachina kuchukua 51% ya hisa za bandari hiyo, na hatimae hisa hizo kufikia 67%; ripoti ya mwaka huu kupitia Port Economics inasema kwa sasa Bandari ya Piraeus ndiyo bandari kubwa zaidi (kwa kiwango cha makontena) kwenye ukanda wa Bahari ya Mediterranean, na ya 5 Barani Ulaya!!

Sasa haya ndo mambo ambayo watu hawakuyataka! Yaani bandari iliyo kwenye ardhi ya Mzungu, 67% imilikiwe na Mchina, na hapo hapo inaanza kutishia ushawishi wa bandari zingine zinazomilikiwa na Wazungu wenyewe!

JokaKuu
You never let us (great minds) down.
Kongole ndugu yangu Chige .
Mungu Baba wa Mbinguni aendelee kukubariki.
 
Mkuu umelipwa pesa ngapi ili kuupugia chapuo hivi huu mradi?,
Yuko sahihi kupigia chapuo mradi huu. "It is part of the DFI which is a key ingredient to any national economic development". Wanaopinga ni wale hawafahamu umhimu wa DFI kwa uchumi wa nchi.
 
Na mimi nlitaka kuuliza hichi kitu, je ameuona mkataba au anandika kwa hisia...
Kumtuhumu mtu km kakoko aliekua jikoni na mwenye access ya Mkataba kua ana toa Maoni ki Mataga ili hali mtoa uzi hajauona mkataba sio sawa...
Unaweka screenshot za mchina akikanusha...kwani ulitaka afanyeje, hio ndio PR yenyewe, does it prove anything? No, iv he has guts ange screeshoy vipengele vya mkataba aviweke then inge make sense, ila haya mambo ya his words aginst their doesnt prove anything.
Whatever it is huu mradi tuujenge wenyewe..km tumeweza kufanya miradi mingine mikubwa ht huu hautatushinda.
Alichosema Kakoko kina-prove nini?!

Mtu ambae hata mamlaka inamtilia mashaka kwamba ni mwizi, anatoa wapi uhalali wa kuongea bila kuweka mkataba halafu unataka bado ni yeye ndie aaminiwe na sio Moosa wala sie tuliofanya research!

Moosa katamka wazi wazi kwamba habari zilizosemwa ni UONGO, na Kakoko hakushiriki negotitions tangu mwanzo!!

Hivi kuna damaging news kama hiyo?!

Yaani Mkuu wa Taasisi kubwa kabisa anashutumiwa hadharani kwamba muongo... mbona hakutoka mbele kusafisha image yake na ya taasisi yake? Au Kakoko Mkurugenzi mzima hafahamu maana ya PR?

Btw, kuna PR ya kumshutumu mbia hadharani namna hiyo?!

Na tangu Kakoko atandikwe za uso, ushawahi kumsikia tena?!

In short, nyie mnaojificha kwenye mkataba hamna hoja kwa sababu niliyoyaandika wala hayahitaji kuona mkataba kuweza kuyachangia!!!
 
Mkuu nadhani haya mambo ameyafafanua. Wachina watakuja kujenga viwanda kwa ajili ya bidhaa zao hapo Bagamoyo....Sina hakika kama mizigo yetu pia itakuwa inapita hapo!
Sasa si mpaka hapo watakapo jenga hivyo viwanda, kama hakuna viwanda hakuna mzigo wa kutosha , hivyo basi viwanda ndio vianze, ndio hiyo Bandari ifuate
 
Alichosema Kakoko kina-prove nini?!

Mtu ambae hata mamlaka inamtilia mashaka kwamba ni mwizi, anatoa wapi uhalali wa kuongea bila kuweka mkataba halafu unataka bado ni yeye ndie aaminiwe na sio Moosa wala sie tuliofanya research!

Moosa katamka wazi wazi kwamba habari zilizosemwa ni UONGO, na Kakoko hakushiriki negotitions tangu mwanzo!!

Hivi kuna damaging news kama hiyo?!

Yaani Mkuu wa Taasisi kubwa kabisa anashutumiwa hadharani kwamba muongo... mbona hakutoka mbele kusafisha image yake na ya taasisi yake? Au Kakoko Mkurugenzi mzima hafahamu maana ya PR?

Btw, kuna PR ya kumshutumu mbia hadharani namna hiyo?!

Na tangu Kakoko atandikwe za uso, ushawahi kumsikia tena?!

In short, nyie mnaojificha kwenye mkataba hamna hoja kwa sababu niliyoyaandika wala hayahitaji kuona mkataba kuweza kuyachangia!!!
Kakoko haaminiki!

Haya na wewe unataka tukuamini kwa kipi?


Weka mkataba tukuamini.
 
Nakupotezea muda kivipi, nimeku tag ?

HUNA MKATABA !
Bwah! Bwah! Bwah!

Umesahau kwamba post yako ya kwanza tu, moja kwa moja ulii-direct kwangu?

Na kama ulii-direct kwangu, wakati hakuna cha maana unachoongea, ni kama umekaririshwa kwamba ukiona mada ya Bandari ya Bagamoyo tu, sema "lete mkataba"!!

Hivi hujui kwamba hapo unapotezea watu muda?!

Ukweli mchungu ni kwamba, hii mada imekuzidi umri, ndo maana umekuwa kama robot.... "Mkataba"! Huna ubavu wa kujenga hoja, na hata huo ubavu wa kusoma kwa mapana na marefu threads za aina hii HUNA!
 
Kakoko haaminiki!

Haya na wewe unataka tukuamini kwa kipi?


Weka mkataba tukuamini.
We nimeshakupuuza bhana manake upo hapa kumtetea Jiwe hata kama hakuna alipotajwa Jiwe! Lakini kwavile unajua ni Jiwe ndie kashindwa kufanyia kazi mradi, basi hapo hapo unaona ndo kama anasemwa Jiwe!!

Pole sana, lakini narudia tena... KAZI UNAYO!!! Na ukweli mchungu ni kwamba, sawa na wenzako, huna ubavu wa kujadili mada za aina hii, NEVER!!!
 
We nimeshakupuuza bhana manake upo hapa kumtetea Jiwe hata kama hakuna alipotajwa Jiwe! Lakini kwavile unajua ni Jiwe ndie kashindwa kufanyia kazi mradi, basi hapo hapo unaona ndo kama anasemwa Jiwe!!

Pole sana, lakini narudia tena... KAZI UNAYO!!! Na ukweli mchungu ni kwamba, sawa na wenzako, huna ubavu wa kujadili mada za aina hii, NEVER!!!
Wewe unaumwa ugonjwa unaitwa jiwe!

Tangu huko juu page kwanza watu wamedai haya uliyoandika ni kwa mujibu wa mkataba uliouona au ni kwa hisia zako tu? Wewe unasema hoo umefanya research!

Tumekwambia hakuna anaekataa kama huo mradi ni mzuri na una manufaa kwa nchi lakini ishu ni mkataba umekaa kinyonyaji ndio kilichofanya huo mradi kushindwa kuanza,!

Tukikwambia hivi hoo tunamtetea jiwe! Basi wewe usiemtetea jiwe weka mkataba basi tuuone ili tuungane wote kumpnda jiwe na kudai bandari kuanza haraka! Hoo kwani Kakoko alikuwekea mkataba.?

Sasa unataka tumwamini nani kati yako na kina Kakoko waliokuwa na mkataba wenyewe?
 
HITIMISHO

Tukubali tusikubali, fursa ya Bandari ya Bagamoyo ikituponyoka tutakuja kuijutia pale Mchina atakapoamua kurejea tena Lamu, au popote pale kwenye ukanda huu wa Bahari ya Hindi!

Inashangaza sana karne ya 21 bado kuna Watanzania wana mawazo yale yale ya Ujima kwamba, eti “madini hayaozi”, na tutakuja kuchimba wenyewe tukishapata uwezo!

Injinia Kakoko na mwenyewe aliwahi kunukuliwa akisema “…na sisi bandari ile (Bagamoyo), tulifanya feasibility study na TPA. Na TPA kupitia serikali, itawekeza na kuijenga wakati utakapokuwa umefika.

Ni wazo zuri kama serikali itakuwa na uwezo wa kujenga hiyo bandari wao wenyewe haidhuru hata kama tumeshindwa kujenga bandari yoyote ndani ya miaka 60 ya uhuru!

Hata hivyo, Kakoko na wengine wanatakiwa kufahamu kwamba, hoja sio kuwa na uwezo wa kujenga bandari bali uwezo wa ku-utilize bandari husika!

Nimetoa mfano wa Bandari ya Piraeus huko Ugiriki ambayo kabla ya uwekezaji wa China, bandari hiyo ilikuwa haifanyi vizuri. Hata hivyo, baada ya Mchina kuingia, Bandari ya Piraeus imegeuka na kuwa ndiyo bandari kubwa kuliko zote Ukanda wa Mediterranean, huku ikichukua nafasi ya 5 Barani Ulaya!

Na ndivyo hivyo kwa Bandari ya Hambantota ambayo na yenyewe ilikuwa haifanyi vizuri lakini hivi sasa hali imebadilika.

Na sababu kubwa ya China kuwa na uwezo wa kuzifanya bandari anazoendesha kufanya vizuri inatokana na ukweli kwamba China ina-handle biashara kubwa sana duniani. Kwa maana nyingine, China ina uwezo wa ku-utilize bandari zake kupitia mizigo yake tu.

Lakini kwa upande mwingine, Mradi wa Bandari ya Bagamoyo pia unahusisha Industrial Complex kubwa sana! Lengo la Mchina ilikuwa ni kujenga viwanda kwenye eneo la bandari, ili baadhi ya bidhaa zake anazosafirisha kutoka China hadi Afrika ziwe zinazalishwa Bagamoyo.

Ninachotaka kusema ni kwamba, pamoja na suala la kodi, mradi huu endapo ungekamilika, ungekuwa chanzo kikubwa cha ajira kwa wananchi!

Bandari ya Bagamoyo sio kama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chato! Hivyo basi, hata kama tuseme Mzee wa Msoga alilenga kupendelea kwao, hivi kuna mwenye akili timamu anayeweza kuthubutu na kudai kwamba, watakaofaidika na bandari hiyo ni Wakwere na Wazaramo wa Bagamoyo?

Halafu hii nchi ilivyo na viumbe wa ajabu, hao hao wanaosema JK alikuwa anataka kupendelea kwao, kwa kiasi kikubwa ndo hao hao wanaodharau watu wa Pwani kwamba HAWAJASOMA, na kwamba wanaishia kuendekeza madrasa!

Sasa kwavile nyie ndio mliosoma, hamuoni kwamba ni nyinyi wenyewe ndio mtakaofadika na mradi huo huku Wakwere na Wazaramo wakiishia kuwauzia kahawa?

Ukubwa wa mradi ule unaweza kuzalisha Pay As You Earn (PAYE) kutoka kwa wafanyakazi ambayo ni kubwa kuzidi hata thamani ya ukodishaji wa ardhi!

Na hii PAYE ni endelevu kwa miaka na dahari!

Pamoja na yote hayo, katu simaanishi kwamba Mkataba wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo upo PERFECT, au ni mkataba bora… la hasha!! Tanzania haijawahi kusaini mkataba ulio bora!

Ambacho ningependa kukiona kwenye hili ni Watendaji na Wafanya Maamuzi kuwa “objective”, na pia waache kusambaza habari za uongo ili mradi tu kuhalalisha ajenda zao.

Wengine ajenda zao ni aibu hata kuzitaja hadharani!

Watu hawa wanatakiwa kukaa na wadau, na kuangalia ni kwa namna gani huu mradi unaweza kufanyika huku tukiacha kile kiburi chetu cha Uzalendo Fake Uliopandikizwa na Mfumo wa Ujamaa!

Aidha, wanatakiwa kukaa na wadau kuangalia ni mfumo upi utaweka mbele maslahi mapana ya taifa.

Na kama nilivyosema kwenye utangulizi wangu, Wapinzani wa Bandari ya Bagamoyo wanawatumikia wale wale wanaowaita Mabeberu bila wao kujijua! Mabeberu walianza kuipinga Belt and Road Initiative ya China tangu kuanzishwa kwake!

Kwa bahati mbaya sana, hao hao waliokuwa wanapinga BRI, hivi sasa wanaanza kuingia mmoja mmoja! Kuna dalili zote kwamba Marekani imeanza kusalitiwa na Washirika wake, hata wale wa Jumuiya ya Ulaya.

Kwa mfano, Jarida la The Diplomat la March 23, 2021 linatueleza kwamba:-


Aidha, wakati Marekani ikihangaika na BRI, mwaka juzi tu hapa, huko China ulifanyika mkutano mkuuubwa wa BRI kama ilivyoripotiwa na UNDP-Asia kwamba:-



Na kwa mujibu wa Serikali ya China, kupitia Belt and Road Portal, wanasema kwamba:-

Mzee wa Msoga aliwahi kutujuza kwamba: Akili za Kuambiwa, Changanya na Zako!
Asante sana kwa article hii. Inafundisho sana. Swali langu ni moja tu, kwanini wazalendo wetu hawakuona hili ulilosema hapa? Walitaka nini hasa?
 
Wewe unaumwa ugonjwa unaitwa jiwe!

Tangu huko juu page kwanza watu wamedai haya uliyoandika ni kwa mujibu wa mkataba uliouona au ni kwa hisia zako tu? Wewe unasema hoo umefanya research!

Tumekwambia hakuna anaekataa kama huo mradi ni mzuri na una manufaa kwa nchi lakini ishu ni mkataba umekaa kinyonyaji ndio kilichofanya huo mradi kushindwa kuanza,!

Tukikwambia hivi hoo tunamtetea jiwe! Basi wewe usiemtetea jiwe weka mkataba basi tuuone ili tuungane wote kumpnda jiwe na kudai bandari kuanza haraka! Hoo kwani Kakoko alikuwekea mkataba.?

Sasa unataka tumwamini nani kati yako na kina Kakoko waliokuwa na mkataba wenyewe?
Mpaka siku Mradi unanza, watu makumi Elfu watakuwa wameshakula za mchina wengi Sana!!

Tulianza kutilia mashaka Kwa speeker, na sasa zamu ya Wana JF

Huyu naye ana kila Aina ya dalili za kulishwa uji na kilichobaki ni kuutetea huo uji!!

Mpaka hapa, bado sjafahamu anachotaka tuungane naye, kaponda wote waliojaribu kutuelezea ubaya na uzuri wa mkataba tena wao waliousoma, yeye badala ya kuja na vielelezo vya Mkataba, anakuja hapa na manenomaneno matamu ya Mao, tutajuaje, Je kama Mao kutengenezwa Kutokea Tz...?

Akitaka tuwapuuze aliotaka tuwapuuze, aweke Mkataba hapa
 
Unajua nini?

I can understand you guys... thread yangu ni ndefu mno, na wengi wenu mmeshindwa kuisoma yote!!! Maswali uliyouliza nimeshayadili tayari!!!

Lakini kwavile I usually respect anayetoa hoja, tofauti na wale wengine wanaokuja hapa na kuanza matusi, bila kuzungumzia hoja yoyote, wacha niseme kwa uchache!

Nimeshasema plan ilikuwa kuifanya bandari kuwa transshipment port, na pili, ku-handle cargo itakayotokana na Industrial Complex.

We all know kwamba bidhaa za China ndizo zimesambaa kila kona Afrika kama sio duniani. Sasa kwa mfano, ukiona meli inatoka US kufuata mzigo China, usidhani zote zinafika China bali zinaishia Singapore ambayo ndiyo largest transshipment port!

Kinachotokea ni kwamba, mega ships kutoka Mashariki ya Mbali zinapakia mzigo China, Korea Kusini na Japan hadi Singapore ambako mzigo utapakuliwa na kuingizwa kwenye meli zingine kutoka sehemu mbalimbali duniani!!

Lengo la Bagamoyo, ilikuwa ndio hilo! Kwamba, badala ya meli kutoka SA, Mozambique, Kenya na sehemu zingine Afrika kwenda hadi Singapore au China, meli hizo zitafuta mzigo Bagamoyo unaoshushwa na meli kubwa kutoka Uchina!!

Lakini hata suala la transshipment lisipoanza mapema, bado tukumbuke bidhaa nyingi zinazoingia Afrika Mashariki na Kati, pamoja na Ukanda wa Maziwa Makuu zinatoka China!

Ni kutokana na hilo ndo maana mradi wa bandari ulikuwa uende sambasamba na ujenzi wa SGR ambao ingeiunganisha Bagamoyo, na zingine! Which means, mizigo ya China inayotoka China kuingia ukanda wetu, yote ingeshushwa Bagamoyo, na kutokea hapo ingesambazwa kwa njia ya reli kwenda nchi mbalimbali!

Lakini kwa upande mwingine, mradi pia ilikuwa uende sambasamba na ujenzi wa industrial complex kubwa sana. Kama plan ingeenda kama ilivyotarajiwa, ile complex ingezalisha bidhaa nyingi sana ambazo zingine zingesafirishwa kwa meli for export!

Nimeshasema, Mtwara ipo reserved for gas tankers, Tanga kuna miradi miwili. Je, HAZITOSHI?

Kwavile nimeshataja Tanga na Mtwara, swali liwe je, Dar haitoshi?!

Ngoja nikuulize: Tanzania ni maskini! Malawi ni Maskini! Rwanda, Burundi na Uganda ni maskini! In short, nchi zote zinazotumia bandari ya Dar es salaam ni maskini!

Pamoja na umaskini wetu huo, lakini bado bandari ya Dar wakati mwingine huelemewa! Sasa jiulize, endapo uchumi wa nchi unafikia angalau kama tu ule wa South Africa ambayo na yenyewe ni maskini; je unaamini Bandari ya Dar itaweza ku-handle uchumi kama huo?

REMEMBER... uchumi wa nchi hizi ukikua, utachochea more imports and exports! That being said, kama tunataka kuangalia miaka 50 ijayo, au angalau 25, I can confidently say HAZITOSHI!

Sijakuelewa! Halafu tukishajenga in phase ndo inakuaje?! Kwamba ili tuijenge wenyewe, au?! Kama ndiyo, rudia swali lako la kwanza, kwamba, je, tutaweza kui-utilize?

Kumbuka, Mchina tayari ana mzigo unaosubiri kwenda sehemu mbalimbali duniani!! So, kama nasi tutakuwa na assurance ya mzigo, kujenga wenyewe itakuwa ni jambo bora lakini Sri Lanka walishindwa kui-utilize bandari yao, na hata Piraeus ya Ugiriki ilianza kupata mzigo wa kutosha baada ya kuingia Mchina!

Nashukuru tena kwa hadithi yako, hii issue bado ipo dependent na vitu vingi ili iweze kuwa a success
Ndio maana nika shauri kama kuna ulazima ianze in phases, hata hizi Bandari kubwa iwe ya Singapore etc hazikufika hapo overnight , na kwa kuwa hao merchant n.k wakawa wameweka hizo condition za jinsi watakavyo rudisha fedha zao.
Yaani wao wana jikinga na kutengeneza hasara kwa kutuwekea masharti ya hiyo miaka ya kurudisha fedha zao. Inaweza kuwa 30 years kwenda 99 years .
Ndio maana nitarudia tena , inabidi twende in phases.
Ukija issue ya industrial park n.k mbona hivyo viwanda hatuvioni hiyo Bagamoyo au sehemu zingine za Tanzania ikaonyesha hata dalili za kuongezeka kwa mizigo , kwa mfano Tuna mbao, umemuona Mchina yeyote kaweka kiwanda cha furniture , tuna chuma liganga nk, umeona mwekezaji yeyote kawekeza kwenye viwanda vya chuma au magari


brand

search



#worlds-top-5-ports
LinkedIn
Twitter
Facebook
Email
Reddit

World's Top 5 Ports​

Sea freight and port operations form a vital part of the supply chain. In fact, more than 90 percent of the worlds trade is carried by sea, according t...

Freddie Pierce
Aug 27
magazine
10 min read



Sea freight and port operations form a vital part of the supply chain. In fact, more than 90 percent of the world’s trade is carried by sea, according to the Maritime and Port Authority of Singapore. Elsewhere in this issue, industry expert Liz Wells takes a closer look at the state of the global shipping industry. In this article though, we identify the world’s five largest ports based on container traffic: Singapore (Singapore), Shanghai (China), Hong Kong (Hong Kong), Shenzhen (China) and Busan (South Korea).

1. Port of Singapore

Established in 1996, the Port of Singapore has since become a global hub port and international maritime center. The Maritime and Port Authority of Singapore is the driving force behind port operations and is responsible for regulating port activities. On average, the Port of Singapore attracts 140,000 vessel calls annually. In terms, of shipping tonnage, it is the busiest port in the world.

Vital statistics
2-3 ships arrive or leave Singapore every minute.
There are 1,000 vessels in the port at any one time.
It is connected to more than 600 ports worldwide.
120,000 ships call at Singapore every year.
5,000 maritime companies contribute approximately 7 percent to Singapore’s gross domestic product.

2. Port of Shanghai

The Port of Shanghai is one of China’s most vital gateways for foreign trade, as its location suggests. Situated in the center of the country’s coastline, it sits where the Yangtse River meets the sea. According to the Shanghai International Port Group (SIPG), which operates all public terminals at the port, annual import and export trade through Shanghai accounts for a quarter of China’s total foreign trade.

Vital statistics
Container throughput reached 21.71 million TEUs in 2006, which saw it ranked the third largest container port in the world for three consecutive years.
Over 2,000 container ships depart from the port every month.
SIPG operates 125 berths on a total quay length of about 20km.
SIPG also owns 5,143 units of cargo handling equipment.

3. Port of Hong Kong

One of the busiest international container ports in the world, Hong Kong is the location for major cargo handling facilities. It is more commonly known as the “fragrant harbor” and is situated in close proximity to the Pearl River Delta Region. The Hong Kong Port Development Council (PDC) was started in 2003 and is focused on port planning and promotion. The port is vital to the economic growth of both Hong Kong and southern China, and handles 89 percent of Hong Kong’s total cargo throughput.

Vital statistics
The port handled 21 million 20 foot TEUs.
In 2009, 205,510 ships visited the Port of Hong Kong.
It provided about 400 container liner services per week last year, which connected to over 500 destinations globally.
The Kwai Chung-Tsing Yi Container Terminals handled 15.2 million TEUs in 2009, accounting for 72 percent of the port’s total container throughput.

4. Port of Shenzhen

Shenzhen Port is adjacent to Hong Kong and south of the Pearl River Delta. Over 30 billion Yuan was invested in the port between 1979 and 2004 in order to construct port infrastructure facilities. By 2004, cargo throughput reached 135 million tons, an increase of 20.33 percent on 2003. While the port serves the Shenzhen area and makes an important economic contribution, it is also a vital hub for Guangdong Province, South China, Hong Kong and international container transhipment.

Vital statistics
Annual handling capacity is 83.764 million tons, including 6.2 million TEUs.
The total length of the port’s coastline amounts to 22,149.7 meters.
On a monthly basis, 560 ships call at the port.

5. Port of Busan

The largest transhipment port in northeast Asia, Busan Port has been developed by Busan Port Authority (BPA) since 2004. It is located on the main trunk route and has a feeder network connecting to ports in China, Japan and Russia. The BPA has overseen the implementation of technologies such as the U-Port system and speedy screening system at the port. It is also investing heavily in overseas projects, including Russia’s Nakhodka Port and logistics projects in Hunchun and Zarubino in China.

Vital statistics
Busan Port handles over 13 million TEUs annually.
The port is deep enough to accommodate more than 10,000 TEU container vessels.
It is also in active echange with 500 ports in 100 countries.
 
Wewe unaumwa ugonjwa unaitwa jiwe!

Tangu huko juu page kwanza watu wamedai haya uliyoandika ni kwa mujibu wa mkataba uliouona au ni kwa hisia zako tu? Wewe unasema hoo umefanya research!
Kwahiyo research inawakilishwa na hisia?
Tumekwambia hakuna anaekataa kama huo mradi ni mzuri na una manufaa kwa nchi lakini ishu ni mkataba umekaa kinyonyaji ndio kilichofanya huo mradi kushindwa kuanza,!
Mimi hata ukikataa, sioni tatizo hata kidogo lakini ukatae kwa hoja kuzipinga hoja nilizoweka!!

Kung'ang'ania eti nikuoneshe mkataba ni ushahidi tosha kwamba huna hoja, kwa sababu hoja nilizoweka kuhalalisha madai yangu, zinapingika vizuri sana kwa kutumia hoja tu bila ya kutumia mkataba!!!

Kwa mfano, nimesema wazi kwamba utafiti umebaini Mchina ana kawaida ya kutaka income tax exemption! Na nimesema wazi kwamba, VAT inaweza kuwa exempted kwenye capital goods au kwenye bidhaa ambazo sheria imeshazitaja!!

Uhitaji kuona mkataba kuzipinga hizo hoja!!!!

Simple like that!
Tukikwambia hivi hoo tunamtetea jiwe! Basi wewe usiemtetea jiwe weka mkataba basi tuuone ili tuungane wote kumpnda jiwe na kudai bandari kuanza haraka! Hoo kwani Kakoko alikuwekea mkataba.?
Labda umeshasahau kwamba kuna posts angalau mbili umenituhumu kwamba kila siku mimi kazi yangu ni kumpinga Jiwe! Ukafikia hadi kusema nimeleta hii mada ili kumchafua Jiwe!!

Sasa kama lengo sio kumtetea Jiwe ni nini?! Kwenye core issue ya Bandari ya Bagamoyo hakuna popote niliopomshutumu Jiwe... sana sana nimemshutumua Kakoko na Wazalendo wa Jiwe!!

Sasa hizo habari za mara kazi yangu ni kumpinga Jiwe, mara nimeleta mada kumkashifu Jiwe... umeyatoa wapi hayo?
Sasa unataka tumwamini nani kati yako na kina Kakoko waliokuwa na mkataba wenyewe?
Sijakuambia umuamini yeyote, nimekuambia jadili hoja!!!
 
Back
Top Bottom