Mabasi ya UDART ndani ya maji tena, watu wawajibike hapa

Dr Guitar tz

JF-Expert Member
Jan 23, 2018
312
247
Ilitokea kama miezi 4 nyuma,Gari zilizokua parking katika majengo yao pale jangwani ziliingiliwa mafuriko Na kusababisha hasara kubwa
Sijui viongozi hawakujifunza lolote kwa hasara ile hadi imefikia tena Gari nyingine nyingi zimelowa? tena tahadhari ya mvua kubwa kunyesha ilitangazwa,viongozi wa kampui walikua wapi mpaka kushindwa kuondoa mabasi Yale?hata kwa kuyavuta kwa breakdown kama ni mabovu?
Serikali ni mbia mkubwa ktk kampuni hii hivyo ni dhahiri kabisa uzembe huu umelisababishia taifa hasara kubwa,safari hii waliokua wazembe wachukuliwe hatua Kali.
 
Hii kampuni naona inaogopwa sana kama ukoma hata viongozi kuiongelea tu wanashindwa.
 
Naona kwenye hiyo kampuni hakuna mgawanyo wa kazi. Kungekuwa na mtu anashughulikia usalama wa magari asingeacha kwa uzembr. Weka picha.
 
Tatizo sio kuyaondosha,tatizo kampuni ilifanyaje maamuzi kujenga depot wneo hatarishi ambalo linajulikana kila mwaka linafurika maji?
 
nakumbuka zilihitajika mil 400 kuyatengeneza ss hv sijui itahitajika mil mia ngapi tena
 
Ni namna ya upigaji dili mkuu. Wala usijihangaishe sana kufikiri. Utafukuzaje wananchi wahame eneo hatarishi alafu wewe unaenda kujenga hapo. Serikali ya mwendo kasi nayo.
 
Anayepaswa kuwajibishwa haswa no yule aliyekuwa Waziri wa ujenzi kwani hasara zote hizo na zitakazoendelea kuja ikiwemo kuja kubomolewa barabara ya jangwani ni yeye ndio kasababisha!!!

Kivuko alinunua bomu akakigawa jeshini,labda na barabara nayo ataigawa!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom