Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,329
- 33,139
Walemavu wa ngozi
Mabalozi wa nchi za Jumuiya ya Ulaya (EU) nchini Tanzania, wamelaani mauaji yaliyofanywa kwa mwanamke mmoja na watu wasiofahamika katika Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Mei 12, 2014 aliyekatwa baadhi ya viungo vya mwili wake akiwa nyumbani kwake na kuitaka Ofisi ya Waziri Mkuu kufanya uchunguzi wa kina ili kukomesha mauaji hayo ambayo yameibuka upya nchini mwaka huu.
Katika waraka ulioandaliwa na Mabalozi hao (FikraPevu tunayo nakala), Mei 20, 2014 wamesema pamoja tukio hilo kuwa la kwanzai hapa nchi kwa mwaka huu, kufuatia kifo cha mwanamke, Munghu Lugata (40), aliyeuwawa hivi karibuni katika mkoa huo, ambapo kifo hicho kimekuwa cha 73 kunzia mwaka 2000 huku wakijua kuwa watu wawili walioshikiliwa watatoa ushirikiano kwa Vyombo vinavyohusika ili kutokomeza mauaji hayo.
Aidha, wamesema pamoja na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuwa katika mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya vitendo hivyo, wanahitaji kukutana kwa mara nyingine na Ofisi yake ili kujadili namna ya kuimarisha dhamira ya kutatua tatizo hilo nchini.
Wamebainisha kuwa Serikali inatakiwa kuchukua hatua muhimu ili kuzuia matukio hayo na kuhakikisha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi Albino yanaisha hapa nchini pamoja na uchunguzi kufanyika ili kutokomeza dhana potofu iliyojengeka miongoni mwa jamii kuwa viungo vya walemavu wa ngozi Albino vikitumiwa na waganga wa jadi wanapata fedha nyingi.
Tukio la kuuwawa kwa mwanamke huyo ambalo liliwahi kuripotiwa na FikraPevu, tukio hilo lilitokea katika kitongoji cha Chalala kijiji cha Gasuma Kata ya Nkololo Wilayani Bariadi mkoani humo saa 12 jioni, kwa kukatwa mguu wake wa kushoto sehemu ya goti, vidole 2 mkono wa kushoto pamoja na ukucha wa kidole gumba, na wahusika kutoweka na viungo hivyo.
Hata hivyo, katika mahojiano ya FikraPevu na Jeshi la Polisi mkoani humo lilisema linawashikilia baadhi ya waganga wa jadi, ambao wamekuwa wakiwadanganya wananchi kuwa viungo vya mlemavu wa ngozi Albino vinaleta utajiri hali ambayo inawafanya baadhi ya wananchi kuamini hali hiyo na kuendeleza mauaji ya Albino katika maeneo mbalimbali nchini.
Kwa habari zaidi:
Mabalozi wa Nchi za Jumuiya ya Ulaya walaani mauaji ya Albino Kanda ya Ziwa