Mabadiliko TRA: Kamishna wa Forodha Mtanganyika Said Athuman Kiondo aondolewa awekwa Juma Bakari Hassan kutoka Zanzibar

Unelewa vizuri sana sema umeamua kujitia ujinga.

Zanzibar wana Bandari zao kwaajili ya Wazanzibari.

Zanzibar wana Mamlaka yao ya kodi kwaajili ya Wazanzibari.

TPA & TRA ni kwaajili ya watanganyika kutuletea Wazanzibari huko ni kuwadharau watanganyika million 61.

Kwakuwa hakuna mtanganyika ZPA & ZRA ni ujinga wa kiwango cha SGR kutuletea Wazanzibari kuongoza taasisi ambazo zipo Tanganyika na Zanzibar.
Hoja ya msingi hapo, mzanzibari hastahili kupewa nafasi yoyote kwenye serikali kwenye nafasi ambayo siyo ya Muungano.
 
Ndugu yangu, mbona hoja ipo wazi sana. Hujaelewa nini?
Tanzania Revenue Authority iko Zanzibar na inafanya Kazi, sasa Kamishna wa Ushuru na Forodha akitoka Zanzibar kuna Ubaya gani?

Tuwe halisia, bila Katiba Mpya tutaendelea kuwachukia Wazanzibari kwa uzembe wetu sisi wenyewe
 
Washauri wa Rais wameshindwa kujua Bandari na TRA ambazo ndio roho za Tanganyika hazipo kwenye Muungano au ni amri kutoka juu kwa ajili ya ujio wa DPW

ZPA - ZANZIBAR PORT AUTHORITY

TPA - TANZANIA PORT AUTHORITY

ZRA- ZANZIBAR REVENUE AUTHORITY

TRA - TANZANIA REVENUE AUTHORITY
Sio zra ni zrb -zanzibar revenue board
 
Marehemu Tanganyika lazima afufuke,iwe mzimu au roboti lazima afufuliwe na apewe haki zake sawasawa na Zanzibar.
Na kule Zanzibar wanalisubiri hili kwa hamu kwan wao walsasema zamani wakaambiwa siasa kali hivyo lazima wadhibitiwe. Bahati mbaya hili lilisemwa mchana kweupe, tena kanisani. Sasa imekuja nafasi na fursa itumieni kwa faida yetu sote.
 
Unelewa vizuri sana sema umeamua kujitia ujinga.

Zanzibar wana Bandari zao kwaajili ya Wazanzibari.

Zanzibar wana Mamlaka yao ya kodi kwaajili ya Wazanzibari.

TPA & TRA ni kwaajili ya watanganyika kutuletea Wazanzibari huko ni kuwadharau watanganyika million 61.

Kwakuwa hakuna mtanganyika ZPA & ZRA ni ujinga wa kiwango cha SGR kutuletea Wazanzibari kuongoza taasisi ambazo zipo Tanganyika na Zanzibar.
Unajua sa100 mwenyewe hapendi muungano huu jinsi ulivyo. Anachotaka kufanya ni kusaidia muungano uwe kwa jinsi Wazanzibari wanataka. Hivi afanyavyo ni ili muongee, mwanzo si mlikuwa mnakaa kimya sasa mtaongea ili tukiijadili katiba mpya muda huo akili iwakae sawa. Na bado wakuu wa mikoa wanakuja Wazenji
Kuna kitu nyuma ya kiti kinasukuma mambo. Hivi mumewe sijawahi kumsikia akiongea popote.
 
Back
Top Bottom