Mabadiliko TRA: Kamishna wa Forodha Mtanganyika Said Athuman Kiondo aondolewa awekwa Juma Bakari Hassan kutoka Zanzibar

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
Washauri wa Rais wameshindwa kujua Bandari na TRA ambazo ndio roho za Tanganyika hazipo kwenye Muungano au ni amri kutoka juu kwa ajili ya ujio wa DPW

ZPA - ZANZIBAR PORT AUTHORITY

TPA - TANZANIA PORT AUTHORITY

ZRA- ZANZIBAR REVENUE AUTHORITY

TRA - TANZANIA REVENUE AUTHORITY
===

Kamishna wa forodha Said Athuman Kiondo, ameondolewa nafasi yake na kuchukuliwa na Juma Bakari Hassan.

Kamishna Juma Bakari ndiye atahusika na ushuru wa Forodha TRA (customs) ndani ya ofisi ya meneja wa Bandari.

Idara ya Ushuru na Forodha inasimamia kodi zote zinazohusu biashara ya kimataifa. Kodi hizo ni pamoja na Kodi ya Uingizaji Bidhaa, Ushuru na Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa bidhaa ziingizwazo nchini. Kodi ya uingizaji bidhaa ni kodi inayotozwa kwa bidhaa zinazoingizwa nchini.
 
Hueleweki
Unelewa vizuri sana sema umeamua kujitia ujinga.

Zanzibar wana Bandari zao kwaajili ya Wazanzibari.

Zanzibar wana Mamlaka yao ya kodi kwaajili ya Wazanzibari.

TPA & TRA ni kwaajili ya watanganyika kutuletea Wazanzibari huko ni kuwadharau watanganyika million 61.

Kwakuwa hakuna mtanganyika ZPA & ZRA ni ujinga wa kiwango cha SGR kutuletea Wazanzibari kuongoza taasisi ambazo zipo Tanganyika.
 
imefika wakati tufungue kesi za kuwaondoa Hawa wazanzibar kwenye nafasi wanazopewa ambazo SI za Muungano kama yule Shaka ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya. Hawa watu wamezoea Chao Chao Chao kwetu ni Cha wote.
Masharti ya muungano ndiyo yanavyosema hivyo. Kwahiyo hapa wa kulaumiwa ni watanganyika wenyewe walioamua kuingia kwenye muungano wa "chetu ni chao na chao ni chao"
 
Kwani Zanzibar hakuna TRA?

Nijibu tafadhali
Unalijua aliloliandika mwandishi? Bandari ni swala la muungano kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri. Lakini Zanzibar walijizima data wakavunja katiba na wakaanzisha mamlaka yao. TRA pia inatakiwa kukusanya ushuru hadi Zenji lakini hapo pembeni kuna ZRA. Sasa waziri anayesimamia bandari ni Mzenji na ndo Kasaini DPW baada ya kunyofoa bandari za SMZ.

Sasa mleta uzi anashangaa kuweka boss wa Zenji wakati wana ZRA.
 
Washauri wa Rais wameshindwa kujua Bandari na TRA ambazo ndio roho za Tanganyika hazipo kwenye Muungano au ni amri kutoka juu kwa ajili ya ujio wa DPW

ZPA - ZANZIBAR PORT AUTHORITY

TPA - TANZANIA PORT AUTHORITY

ZRA- ZANZIBAR REVENUE AUTHORITY

TRA - TANZANIA REVENUE AUTHORITY
The United Republic of Tanzania imeundwa na pande mbili kwa gharama ya upande mmoja kuji dissolve huku upande mwingine ukibaki. Tanganyika ilijigeuza mshumaa, ilijiangamiza kwa lengo la kuangazia wengine.
Hivyo, Muungano huu unampa Zanzibar kuwa access ya nafasi zote, maana Tanganyika ilishajiua hivyo kukabidhi kila kitu kwa Zanzibar, maana katika Muungano huu Zanzibar ndiye pekee aliye hai.
So, unapoongelea maliasili, taasisi, n.k Zanzibar ana mamlaka nazo zote, kama mmiliki upande mmoja, huku upande mwingine akiwa kama msimamizi maana Tanganyika ilipojiua iliacha watoto na wake kadhaa ambao wote walendelea kulelewa na Zanzibar. Hapo ndipo hesabu za nyerere zilipopotea na kuvurunda kila kitu.
Laiti Tanganyika ingekuwepo au ingefufuka leo, basi hapo itakua sawa kusema kuna vitu vya Muungano. Ila kwa sasa, Zanzibar ndiye anayetambuliwa ni vile tu hawaijui nguvu yao.
Sasa hivi Zanzibar wana nguvu ya kuamua lolote ndani ya Muungano na watoto na wa tanganyika wakatakiwa kupokea tu maelekezo.
Kwa kuwa Tanganyika ilishakufa, sasa hivi serikali ya Muungano inabaki kuwa chombo kinachomsikiliza zaidi Zanzibar kabla ya kufanya maamuzi yoyote yale. Maana ndiye pekee aliye hai.
 
Back
Top Bottom