Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Prof. Palamagamba aula, Mwakyembe achukua nafasi ya Nape Nnauye

Hiki ndicho nilichokitegemea taasisi kubwa ya urais imevamiwa na mtu asiye na utashi WA uongozi wala hekima na kama mkilinyamazia kimya Hili basi Mengi yatajitokeza.
Pole nape nenda Baba juhudi zako tumeziona na tumekuheshimu..
Ushauli wangu kwangu Nape wala usihuzunike na kusikitika nenda jimboni kwako kafanye kazi ya ubunge kwa ufanisi mkubwa sote tunafahamu wewe na Kinana ndiyo mliyofanikisha kufufua CCM Leo waliodandia treni wanajiona bora na kukuripa kwa hayo. achana nao sisi ndio waamuzi wamwisho yote uliyofanya tumeyaona na kuyathamini.
 
Alikuwa na nafasi kwenye vikao vya baraza la mawaziri kutoa ukosoaji huo.
Hivi uliwahi kujiuliza ni kwa nini unaenda kusali Kanisani kila Jumapili na si Msikitini Ijumaa? Au unaenda nyumbani Kigoma na sio Mtwara? Hii ni kwa sababu kuna kitu unachokiamini na ndio maana unakifanya lakini huna uhuru hata kidogo kumlazimisha mwenzio kutoamini vya kwake na kukufuata wewe eti kwa vile ndio 'uko sahihi'.
Huu mfano ni kwamba hata kwenye baraza la mawaziri unaenda kuhudhuria ukiwa na mawazo yako na katika kujadiliana ukiona mmepishana sana na wenzio ndio maana wazo la kujihudhuru liko wazi. Huenda Nape kaangukia hapo!
 
Upendo wa kimungu huu...
Daaah...hii nyota kaliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Sio nyota mkuu.

Ninachoona ni Makonda anaandaliwa kuja kuvuruga uchaguzi wa 2020.

Kama unavyojua Dar iliwaangusha sana CCM, kwahiyo makonda analelewa ili 2020 afanye fujo kwasababu he is crazy enough.
 
Typical Hollywood style, lakini tutamwelewa tu acha atunyoroshe, tuliimba wenyewe!
 
a012381d5b76ef33e87c456dc30bc7e6.jpg
 
Kuwa na hasira kidogo lakini furahi sana!! FUrahi sana kwa sababu; JPM angekuwa anatumia kichwa kufikiri angegundua kwamba Nape ulikuwa ni mtego uliojificha wa kumpima JPM ni mtu wa aina gani!!!

Kama ilivyotarajiwa; ameingia kichwa kichwa kutokana na kiburi chake!! Kumtumbua Nape ameshatoa picha halisi ya yeye ni mtu wa aina gani hasa!! Anaweza kujifanya hajali lakini hili litawafanya wengi waanze kuiona vizuri image iliyojificha ya huyu mzee jambo ambalo ni zuri kabisa kwa sasa! Wapo wanaodhani JPM ni malaika... sasa ndo waone Malaika anayemwacha anayestahili kushughurukiwa na kumshughulia ambae hakupaswa kushughulikiwa!!!

Sina shaka Nape alishijiandaa kwa hili hasa ukipitia tweets zake za nyuma... huyu alishachoka na alikuwa anatafuta sababu muafaka na JPM akajiingiza kichwa kichwa!!!
Umewaza nje ya box,asante kwa kunituliza munkari
 
Back
Top Bottom