Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Doto Biteko ateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Makamba Mambo ya Nje, Pindi Chana Katiba na Sheria...

Na salary anachukua mbili au atabeba ya unaibu PM ,then ya wizara inakua POSHO?
Hapo ni double double mkuu- kuna ya Ubunge, ya waziri, na ya deputy pm, haya mambo NI ufujaji wa malinz umma- period/ Kwa nini mtu mmoja anarundikiwa ma vyeo yote hayo na tuko Million 60 na zaidi?
 
Hiki cheo mara ya mwisho alikishika Mrema kama sikosei enzi za Mwinyi.

Kiuhalisia ni cheo cha utashi wa raisi, hakipo kikatiba.

Ila kinachotafakarisha hapa ni pale Biteko atakapokosea kama Naibu Waziri wa Nishati, je waziri akimuadhibu si itakuwa anamuadhibu Boss wake ambae ni Naibu Waziri Mkuu? Maelekezo ya Waziri wa Nishati yatakuwa na mashiko kwa Naibu wake ambae kiuhalisia ni Boss wake?
Nadhan ni naibu mara moja tuu...Wizarani ni Waziri kamili
 
Tamisemi naona iko wazi je Majaliwa ndiyo inamsubiri
hHapana, Majaliwa akitoka hapo au analamba mshiko wake mrefu, anafanya miradi yake na huku anakuwa mshauri tu.

Mafao na maisha ya waziri mkuu mstaafu Tanzania siyo ya kitoto.

Huyo bado ataendeelea kupata walinzi, ma dereva, magari mapya, tiketi za ndege, kula, kulala, heshima. mpaka kufa kwake au katiba ibadilike.
 
Kikatiba cheo hakipo lakini Katiba inampa Rais uwezo wa kuunda Baraza la Mawaziri kadri anayoona inafaa
Ndiyo maana Rais anaweza kuziunganisha au kuzigawa Wizara n.k.
Cheo cha Naibu Waziri Mkuu ni sehemu tu ya 'idara' kuleta ufanisi kadri anavyoona
Duh! Mbona Mzee Mrema sasa waligoma kumlipa mafao yake ya unaibu waziri mkuu ?....
 
Rais Samia Suluhu amefanya mabadiliko na teuzi za sura mpya kwenye baraza la mawaziri. Uapisho utafanyika September 1, Ikulu ndogo Zanzibar saa tano kamili asubuhi.
1. Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Doto Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Awali alikuwa Waziri wa Madini.

2. Amemteua January Makamba kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Awali alikuwa Waziri wa Nishati.

3. Amemhamisha Balozi Pindi Chana kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Awali alikuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.

4. Amemhamisha Steven Byabato kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Awali, Byabato alikuwa Naibu Waziri wa Nishati.

5. Amemteua Jerry Silaa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Silaa ni Mbunge wa Ukonga, Dar es Salaam.

6. Rais amemteua Anthony Mavunde kuwa waziri wa madini, mwanzo alikuwa naibu waziri wa kilimo.

7. Prof Makame Mbarawa aliyekuwa waziri wa ujenzi na uchukuzi amekuwa waziri wa uchukuzi.

8. Innocent Bashungwa amekuwa waziri wa ujenzi, mwanzo alikuwa waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa.

9. Godfrey Kasekenya aliyekuwa Naibu waziri wa Ujenzi na uchukuzi ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa Ujenzi

10. Alexander Mnyeti ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa Kilimo

11. David Mwakiposa Kihenzile ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa Uchukuzi. Ni mbunge wa Jimbo la Mufindi

12. Judith Kapinga ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa nishati, ni mbunge wa viti maalum Ruvuma.

13. Dunstan Kitandula ameteuliwa Naibu Waziri wa maliasili na Utalii, ni mbunge wa Mkinga

14. Stergomena Tax amehamishwa wizara ya mambo ya Nje kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

15. Angellah Kairuki amehamishwa kutoka TAMISEMI na kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii

16. Dkt. Damas Ndumbaro amehamishwa kutoka Wizara ya Katiba ba Sheria na kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.




View: https://www.youtube.com/watch?v=7bLEuvgVGG4

======

View attachment 2733279
View attachment 2733280
View attachment 2733281
View attachment 2733282

Kama amefany aunafiki kupata cheo kanda ya ziwa hawashawishiwi na zawadi ya ubwabwa. Jamii gani hasa anayoiwakilisha kanda ya ziwa zaidi ya Wasumbwa wa Kahama mchaanganyiko na Wasubi wa Kagera?

Kama alifanya usaliti kumsema vibaya JPM ili apendwe na hatimaye kuzawadiwa hicho cheo laana itamtafuna. Au sababu ya kauli aliyoitoa juzi akisema ".......viongozi tusikubali rais kutweza utu na heshima yake...."
 
Ni wazi mama anamuandaa kijana wao ili ampishe kiti cha Urais 2025

Hatagombea

Hawa watu wamejipanga wanata kijana wao akae kwenye wizara isiyo kuwa na heka heka Ili asichafuke isije kumuharibia kuelekea 2025.

Ndio maana awamu hii wanataka wasaini mikataba yote mibovu kwasababu samia anajua hana cha kupoteza kwa kuwa 2025 anamuandaa kijana fulani

Watanganyika tujiandae kwa mateso mengine makubwa kuanzia 2025-2035

TANGANYIKA tulimkosea nini Mungu?
 
Huyu naye anayetangaza na Mchechu wa Hazina ni mizigo, wawekwe kando! Haya mambo ya ushirika wa kikabila unaharibu taifa.
Hizo nongwa zako binafsi najua Kuna jina linakuchanganya lakini hao wawili sio kablia moja
 
Gabon tayari leo wanajeshi wamefuta uchaguzi wa kitapeli na kuchukuwa nchi.

Hizi utawala za kijanjajanja Dawa yao ni Jeshi tu, sema kwetu tatizo la Jeshi wanakula nao pamoja kwahiyo hilo haliwezi kutokea.
Jeshi letu ni kubwa na wapo makini sana, ninauhakika "mambo yakiharibika" wanauwezo, wanaupeo, wanadhamira na uweledi.....wa kulinda Katiba na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Vilevile,natamani nijue hali halisi ya kuwafanya Jeshi wawe kwenye hali waliomo sasa, ukizingatia walivyojitokeza majuzi kuhusiana na suala la "Mavazi" yanaoyofanana na wao, ukiniuliza mie kwanini walikurupuka, nasema labda wapo kwenye utayari tayari, yaani wana kaintelijensi kwamba kuna watu wamo na hayo magwa
nda na wanaweza kufanya jambo? Je, ni kujiandaa na tetesi za yanayojiri huko magharibi? manake saa nyingine taarifa zinawezwa kunaswa(intelligence) kuhusu "jaribio" bila ya kuwepo Nchi husika, anyways its all speculation in my part.

So far, kuhusiana na hawa "janja janja" na hii tifua tifua-Kuanzia Wakubwa wa TISS, na Wizara ya Ulinzi, Mambo ya Nje n.k ndio najiuliza bado, Je huko juu wanatikiswa? Wanahadaa(mbinu ya kuteka headlines kama kawa) au ni kujiandaa Kisiasa, yaani ndani ya CCM kuelekea 2024-2025?

Hatahivyo ni ngumu katikati ya chemichemi na vuguvugu hizi, yani pindua pindua za Ukanda wa Sudan-Guinea kujua lipi ni lipi na hili la kwetu kuzima mzozo wa DPW na Loliondo Ngorongoro saga n.k n.k

Naiombea Nchi, hao wengine watafute miungu yao
 
Ni wazi mama anamuandaa kijana wao ili ampishe kiti cha Urais 2025

Hatagombea


Hawa watu wamejipanga wanata kijana wao akae kwenye wizara isiyo kuwa na heka heka Ili asichafuke isije kumuharibia kuelekea 2025

Ndio maana awamu hii wanataka wasaini mikataba yote mibovu kwasababu samia anajua hana cha kupoteza kwa kuwa 2025 anamuandaa kijana fulani


Watanganyika tujiandae kwa mateso mengine makubwa kuanzia 2025-2035


TANGANYIKA tulimkosea nini Mungu?
Wasi wasi wako tu. Makamba ni mtendaji mzuri sana na mama analijua Hilo ndo mana Huwa hasikilizi kelele za mataahira kama wewe na TEC yako. Mama is there to stay till 2035
 
Back
Top Bottom