Mababu Zetu Wakifufuka leo! Wataona vizazi walivyoacha vimewatia aibu sana hapa Duniani

Arovera

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
11,176
29,240
Wakuu twende taratibu.

Wale mababu zetu wakifufuka leo watakufa haraka kwa mshituko maana hawatoamini watakayoyaona,
Kwanza watakuta mapambano dhidi ya wazungu ili kutetea ardhi yao ya asili hayapo tena na kiufupi ardhi mzungu anafanyia chochote anachotaka tena kwa kukaribishwa na kupewa mikataba.

Halafu watakuta tujitu hatuna afya twenye maumbile yasiyojaa misuli kwa wanaume na watakuta vijitu vifupi tu, hilo pia watashangaa. Watakuta maajabu mengine kwamba wao walikua wanapambana kumtimua mzungu kwenye ardhi ya africa , maana alikua anatawala kimabavu lakini ajabu leo tunawafuata kwao wazungu na kuwaita waje wawekeze afrika na masharti ni nafuu, yaani mzungu anakuja kama mwekezaji kiulaini kabisa.

Watakuta mila na desturi za mwafrika ni kama zimepotea kabisa maana kwa sasa hatuna ibada zetu za asili kama wao walivofanya aibu hii?

Watashangaa wao walitamani wabakie milele afrika na walipelekwa ulaya kwa nguvu lakini kwa sasa watu wanapambana waende ulaya tena wanalipa hadi pesa nyingi ili waende ulaya, wengine hupoteza maisha kabisa aibu hii.

Watakuta mifumo ya kiuongozi mibovu sana ambayo hawatoielewa maana koo mbali mbali zimevurugwa hivo watashangaa sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom