Maaskofu wasusia mwaliko wa JK

Ni pigo kubwa kweli kweli kwa JK kutoka kwa maaskofu hawa. Ni kubwa kweli kweli. Jk afahamu kwamba mialiko ya namna hii wakati wa kampeni ni unethical, inaweza kutafsiriwa vibaya, lakini yeye huwa hajui mambo hayo. Kweli ana washauri!
 
Waliogopa asije kuwaangukia katika karamu hiyo na wao kulaumiwa! Lakini hata hivyo ni lini JK alianza kufunga tena? Mbona hajasema? Maana baada tu ya kurudi jukwaani pale Jangwani kitu cha kwanza kuwatangazia Wananchi ni "Nimefungulia!" Inawezekana maaskofu wanaona anawadhihaki kwa kualika futari huku yeye hata hafungi! He he he!!!!
 
Maaskofu na wachungaji koani Mbeya walikata mwaliko wa JK wa kushiriki futari wakati kampeni mkoani mbeya. Viongozi hao walidai kukataa kwao kunatokana na kwamba wakati huu JK ni mgombea hivyo isingekuwa ni picha nzuri mbele ya umma wa kushiriki kwani ingeonekana wanapokea takrima.

Vile vile walidai futari ni kwa ajili ya waliofunga na wao hawakuwamefunga hivyo hamna sababu ya kushiriki.

Naona awamu hii viongozi wameshtuka mapema janja ya Kikwete kutumia cheo cha urais kuhadaa watu.

Hongereni kwa maamuzi yenu mazuri.
 
'Viongozi wa Dini' na CCM wote ni tabaka tawala tu, they care very little to what happens to the common mwananchi hawawezi kuwa na jipya..Nikionacho ni kuwa wanafanya sarakasi kipindi hiki katika kutafuta ushawishi ili waendeleze status quo baadaye..they are all manipulating witches.

I doubt if they are after harmonious society
I'm afraid this election will bring more religious hatred......creating dangerous future.
 
Maaskofu hatuzitaki KURA ZENU!!! Na bado ushindi utakuwa kishindo mwaka huu...:becky::becky:!
 
I doubt if they are after harmonious society
I'm afraid this election will bring more religious hatred......creating dangerous future.
Harmonious society inapatikana kwa maaskofu 'kufuturu' na 'Dr. Mkwere'..sivyo?hata kama hawajafunga? lol

BTW, dini ni kisingizio tu cha watu kutumia kama ngao ya kutotekeleza majukumu yao. Nina hakika watz wanaofuata dini hawajai hata kigangani..hivo mtu yeyote anayejishughulisha na makelele ya dini mi namuona hamnazo tu amekosa ya kazi ya kufanya.
 
Aliwaalika lini,
wapi
kwa ajili gani?
source?
(isije ikawa aliwaalika kwa futari au sala ya taraweh hao maaskofu)
fanya homework yako vyema kabla hujapost shekhe.

ndo hata kama kawaalika kwa futari ndo wamegoma hivo..kwanza si alifungulia huyu toka ile siku pale jangwani sasa mafutari ya nini ..heheeeee beki hazikabi mwaka huu kipa analalamika mashuti yamezidi langoni mwake
 
Anaye taka kujidanganya ama kujipa moyo anayo haki lakini kwa mujibu wa Lewis Makame munapoteza time zenu tu hakuna chama chengine kitakacho pewa kura zaidi ya CCM na CHADEMA mutapewa viti viwili vitatu CUF hatapewa hata kimoja ili ionekane ni chama cha Pemba tu
 
Hapo timu ya kampeni imeprove another failure.......haya,tunaendeleaa
 
Huyu JK si walisema amefungua baada ya kuanguka pale Jangwani!?
Sasa alitaka kufuturu nini huko Mbeya?

Njia ya Mwongo ni fupi bajameni. Wengine wakisema kifafa wasirushiwe mawe.
 
Mimi nilishawahi kusema kuwa hili suala la udini wanaloshabikia mashabiki wa CCM wakiwemo viongozi wakuu siku moja litawatokea puani. Kuzungumzia mambo ya dini ya Slaa na hata ndoa yake ni kosa kubwa sana CCM inafanya bila kujijua, Slaa ana dini yake kwa hiyo kumsema vibaya Slaa au dini yake ni sawa na kuwasema wafuasi wa dini yake.

Na nikaendelea kusema tunajua Slaa ni mkatoliki na wakatoliki si haba katika nchi yetu, na kuwasanifu wakatoliki ni kuwasanifu wakristo wote kwa vile huwezi kutenganisha ukatoliki na ukristo. Vile vile tujue si waislamu wote wanaofurahia kitendo anachofanyiwa Slaa. Naweza kusema mahesabu yanayofanywa na timu ya kampeni ya CCM si mazuri na matokeo yake tumeanza kuyaona.

Na ieleweke pia kuwa kwa wakatoliki heshima ya upadri au uaskofu huwa haifutiki viongozi na wafuasi huendelea na heshima ile ile hata kama kaondoka upadri/uaskofu kinachobadilika ni kutolewa vazi la kufanya huduma ya kiuaskofu lakini heshima inabaki pale pale, nafikiri hiki ni kitu kingine ambacho viongozi wa CCM hawakioni wanafikiri ukiacha uaskofu basi umeshagombana na kanisa.
 
Labda hamuwajui hao wanaojiita Maaskofu; Mbeya inaongoza kwa kuwa na Maaskofu wengi na wengi wao ni walaji tu. Hawana ubavu wa kukataa mwaliko wa JK.

Hawa watakuwa wachache ambao wanamchukia JK au wako upande wa Dr. Slaa na wanajaribu kutumia dini kuonyesha JK hakubaliki Mbeya. Hawa ni watu wa mungu, kwanini waogope kutaja majina yao? Mwandishi hataji jina lake na hao Maaskofu wake nao hawataji majina yao. Angalau Wakatoliki bado wana miiko kwenye dini zao, lakini hizi dini zingine ambazo zimejaa Mbeya yaani ni balaa tupu.

Habari zingine zinalengo la kuwadanganya Watanzania badala ya kutoa habari. Wakati huu wa uchaguzi tutasikia mengi sana.
 
Kumbe na wewe hauelewi, huo uzi hauzungumzii ndoa ya Dr. Slaa, unazungumzia wizi wa wake za watu wa Dr. Slaa.
Bado una-display POOR comprehension..naposema 'ndoa' namaanisha mambo binafsi ya Dr. Slaa..mi ni kidume na sharubu siezi kukaa kitako kuongelea uanaume wa mtu mwingine..awe Dr. Slaa au 'Dr.Mkwere', hiyo nawaachienei nyie.
 
Maaskofu wasusia mwaliko wa JK

Saturday, 04 September 2010 21:33
*Ni kushirikiana naye kula futari

"Tunakilaani vikali kitendo hiki tumejiuliza kwa nini tualikwe kwa futuru sisi ambao hatuko kwenye mfungo? Tena tumechukizwa sana na mgombea, kufanyiwa zindiko uwanjani na machifu wakati amefunga," ilieleza sehemu ya waraka wa maaskofu hao kwa Mwananchi Jumapili.

Akiwa katika Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya wazee wa kimila (machifu) wa Usafwa mkoani humo walimvisha Kikwete mgolole, kumpa kiti cha kichifu pamoja na mkuki kama ishara ya kumkubali na kuahidi kuwa wananchi wote wa Mbeya watampigia kura Kikwete.

Dr Kinana inakuwaje hapa? Mnasahau kuunganisha na kulinganisha mambo? Mila, imani na kampeni zinagongana hapa!
 
Back
Top Bottom