Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,701
- 41,446
Maandamano yaliyofanyika kwenye majiji yalikuwa ya kumtahadharisha Rais asisaini uchafu uliopo mezani pake kuwa sheria, lakini kumkumbusha pia kuwa huko mtaani watu wanateseka kwa maisha magumu licha ya bidii kubwa wanaoyoifanya kupambania maisha yao. Mateso ya maisha magumu wanayoyapata ni kutokana na sera mbovu za uchumi za CCM, usimamizi mbaya wa taasisi mbalimbali, kodi na tozo kamua damu zilizowekwa na CCM, ufisadi wa viongozi wa serikali ya CCM, na urasimu wa hovyo kwenye shughuli mbalimbali za kibiashara na kiuchumi.
Ili kuondokana na madhira mbalimbali ambayo yametengenezwa na viongozi na watendaji wa CCM, ni lazima kuwepo na mifumo inayoruhusu watu wazuri, wenye uwezo, waadilifu na wenye uchungu na maisha ya wananchi kuweza kuwaongoza wananchi. Hilo nalo limekuwa ni gumu kutokana na sheria mbaya za kishetani zilizowekwa na hawa viongozi wa CCM, ambao kila mara hutengeneza mazingira rahisi ya kuiba kura, kupora uchaguzi na kuwatangaza wagombea wa uchaguzi ambao hawajachaguliwa na mwananchi yeyote kuwa wawakilishi wao, kupitoa sheria takataka za uchaguzi.
Ndiyo maana leo tuna Bunge batili. Ni bunge batili kwa sababu linaundwa na watu waovu waliopora mamlaka ya wananchi kuwachagua watu waowataka. Tuna Waziri Mkuu asiye na kura hata moja ya mwananchi yeyote. Na tuna mawaziri na wabunge rundo ambao hawajachaguliwa na yeyote. Licha ya mahakama kutangaza kuwa watu hao ni batili kuwepo bungemi, lakini bila aibu, wameendelea kubakia Bungeni, na kulifanya Bunge kuwa nyumba ya waovu.
Tahadhari imefikishwa kwa Rais kwa njia ya maandamano kuwa takataka aliyowekewa mezani na Bunge batili, kutaka aisaini kuwa sheria ya uchaguzi, asithubutu kufanya hivyo.
Wito ni kuwa maandamano yashuke ngazi ya mikoa, hatimaye wilaya, mpaka hapo itakapotamkwa kuwa hiyo takataka imeondolewa, na maoni ya wananchi ndiyo yatatengeneza sheria ya uchaguzi.
LAKINI ikitokea Rais akasaini hiyo takataka iliyopitishwa na Bunge batili kuwa sheria, basi maandamano yawe ya nchi nzima, na yasiyo na kikomo, mpaka matakwa ya umma kuhusiana na sheria ya uchaguzi, yatakapopewa uzito unaostahili. Wananchi tusikubali kamwe kupuuzwa wala kudharauliwa, tena na watu ambao ni wawakilishi batili.