Maandamano makubwa nchi nzima

Ningekuona wa maana kama tungeanzia kwenye kupanda kwa gharama za umeme kitu ambacho kinamgusa kila Mtanzania hili la Kiinua mgongo kinavyoonekana bado ni tetesi na serikali inaweza kukana maana hadi sasa hakuna aliyetuwekea uthibitisho hapa jamvini juu ya ongezeko hili la Mafao ya wabunge.
Tuanze kuonyesha kupinga hilo ongezeko hata kama ni tetesi ili isitokee kweli.
 
Wanaoafiki waseme.....,,,,,,
Wasioafiki waseme..........,,.
Walio wengi walaaniwe
 
Kweli nchi watu kujua nafasi yao katika kukosoa serikali bado sana. Na hii inaonyesha ni jinsi gani viongozi wataendelea kujinufaisha pasipo kukemewa. Maana hoja yoyote ya namna hii michango huwa ni inayotoka ni ya watu waliokata tamaa na kuamua bora liende
 
Jamani kama kuna wakati wa kuonyesha uzalendo kama watanzania ndio sasa,tuungane wote kupinga upuuzi huu wa wabunge kulipwa milioni 160,hilo ni ongezeko la zaidi ya asilimia 200,kutoka milioni 43 walizokuwa wakilipwa mwanzo kama mafao ya kustaafu ubunge baada ya miaka mitano.CHADEMA,CUF,NCCR,TLP na vyama vingine vya upinzani tuungane TUFANYE MAANDAMANO NCHI NZIMA kupinga unyonyaji huu.Vinginevyo nitawaona wote wanafiki,wachumia tumbo.

Mbatia keshabariki hilo kwa kusema ni jambo jema maana wanafanya kazi ngumu sana, hivyo wanastahiki kulipwa hivyo.
 
Wewe ndugu ni mpuuzi Kwelikweli,mafao hayo yameandaliwa na kupitishwa na CHADEMA??!!,sishangai kusikia ulishawahi kuugua kichaa!! Mwezi mchanga ushaandama kwani kesho ni tarehe 1 February!!
acha umburula weweee, unategemea lema kwa hilo la kupunguza mafao ya wabunge muelewane?
 
Wewe dada yangu Chris Lukosi,

Mbona Mbowe ana mkwanja wa kufwa mtu. Pia Lema nae siku hizi mabo safi tu.. Tuliza boli dada. Shemeji vp mzima?

Hahahahaha,

Hapo Mbowe na Lema lazima wakufukuze uanachama kwa kosa la kutaka kupunguza mapato ya wakuu
 
Kwa mara ya kwanza Chadema wanaoyaona maandamo machungu.

Angalizo pro-Chadema yeyote atakayeshiriki haya maandamao atafukuzwa na atavuliwa uanachama na atakuwa msaliti.

Mimi Ritz tashiriki haya maandamano.

Ni kama natengeneza picha wamesimama Lisu, Slaa, Mnyika, Mbowe, Mdee na magwanda yao ukaanza kutaja sababu lukuki za kuandamana huku wao wakitakiwa kuitikia ndioooooooooooo....

Tuandamane kususia vikao vya bunge..ndioooooooo...tuandamane kuwafukuza wasaliti...ndiooooooooo...tuandamane blah blah..blah.....wallah ukufikia hapo kwenye mafao jamaa watabaki wanatoa macho tu.
 
cris lukosi nadhani huna akili timamu,nimefuatilia posts na replies zako nikagundua ni mpuuzi tena mjinga mno.haiwezekani thread inazungumzia uzalendo wewe unaleta uchama hapa!acha upu.mbav wewe ni mtu mzima unajifanya ccm wakati hiyo ccm wapo zaidi yako lakini wanasena ukweli inapobidi wewe kikaragosi tu!hebu nibie ktk post hii cdm inakujaje?kila jambo wewe cdm haitusaidii kenge wewe,leo watu wanalia si wa cdm waka ccm au cuf wote wanalalamikia 160m kwa wabunge wewe umekalia mbowe;slaa,shit!huna mchango go to toilet ----in man.
Umemaliza kutukana?
 
wanasiasa hawawezi kuwasaidia wananchi ktk hili, isipokuwa wananchi wakiamua wenyewe, lkn kama wananchi wataendelea kuwashangilia wanasiasa kila wanapoawaona kwa sababu ya rushwa ya ubwabwa, tshirt, na kanga, basi maandamano hayo hakuna, na posho hii itaizinishwa, na watalipwa. Mabadiliko ya kweli, narudia tena, hayataletwa na wanasiasa bali na wananchi watakapoamua kufanya hivyo.

wakati utafika.
 
Sidhani kama watanzania wana mwamko wa vitu kama hivi..... milioni 117*300(wabunge)=bn 35/- hivi hizi zingeingizwa kwenye elimu tu ? miaka 5 tungekuwa wapi? wadanganyika wamelala wakiamka watakuta mashimo ya madini na bahari tupu....
 
11,200,000 @ month (salary)
35,200,000 a year (attending parliamentary sessions.
20,800,000 care allowance.
That's equal to 190,400,000 per year kwa kila mbunge na wapo 375. God help us 190m can build a hospital
 
Maandamano hayo yatapaswa kuwa ya watz wa hali ya chini. Asiwepo mbunge yeyote katika maandamano kwa sbb wabunge wooote lao moja tu.
 
Ndio ujue siasa ni upuuzi tu hapa kwetu, hakuna cha cdm wala ccm wote ni walewale. Hakuna mbunge anaepinga hili halafu wanasimama katika majukwaa wakituambia eti wanataka kutukomboa na umasikini, kama kweli kuna wazalendo na wanaolinda maslahi yetu watanzania tulio masikini basi chama ambacho kinajiamini kipo kwa ajili ya watanzania kipinge.

Bahati mbaya mpaka sasa hivi sijasikia mbunge yoyote awe wa upinzani ama wa ccm akipinga yeye kulipwa kiasi hicho kikubwa, wote kimyaaaa, jamani watanzania tuamke hakuna na HAKUNA chama kinachojali.
 
Back
Top Bottom