Maandamano kuunga mkono serikali yetu juu ya EAC

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,887
3,412
Tunajiandaa kufanya maandamamno nchi nzima kwa mara ya kwanza kuunga mkono uamuzi wa serikali ya Tanzania kuamua kuilinda ardhi yetu kwa vizazi vijavyo tunafanya hivyo ili wale wanaofikiri kikwete yuko peke yake kwenye hili wapate picha halisi.

Sisi watanzania bado tunafikiria kama kujiunga na huo umoja wa mafisi au la!
tunaomba tupewe nafasi.

Kikwete mtoto wa Bagamoyo kwa mara ya kwanza tumeona unaipenda nchi yako.
 
Tunajiandaa kufanya maandamamno nchi nzima kwa mara ya kwanza kuunga mkono uamuzi wa serikali ya Tanzania kuamua kuilinda ardhi yetu kwa vizazi vijavyo
tunafanya hivyo ili wale wanaofikiri kikwete yuko peke yake kwenye hili wapate picha halisi
sisi watanzania bado tunafikiria kama kujiunga na huo umoja wa mafisi au la!
tunaomba tupewe nafasi!
Kikwete mtoto wa Bagamoyo kwa mara ya kwanza tumeona unaipenda nchi yako!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
nakuunga mkono ms..kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 6
 
MAANDAMANO YAANZIE KERO ZA NDANI KWANZA NDIPO AL-SHABAAB WASIPOTUSTUKIA NDIPO TUENDELEE NA HAYO YA NJE YA MIPAKA YETU

Tuanze kwanza kuandamania serikali kututungia katiba wakati wananchi wenye jukumu hilo kikatiba tupo.

Na kama Al-Shabaab watakua hawajastukia maandamano yetu hayo basi ndipo tupange maandamano mengine ya kupinga posho ya wabunge na ugumu wa maisha shingoni mwetu ndipo tuje tukavuke mipaka kwenda kuandamania vya nje ya nchi.

Zaidi ya hapo, unafiki STOP!!!!

Tunajiandaa kufanya maandamamno nchi nzima kwa mara ya kwanza kuunga mkono uamuzi wa serikali ya Tanzania kuamua kuilinda ardhi yetu kwa vizazi vijavyo
tunafanya hivyo ili wale wanaofikiri kikwete yuko peke yake kwenye hili wapate picha halisi
sisi watanzania bado tunafikiria kama kujiunga na huo umoja wa mafisi au la!
tunaomba tupewe nafasi!
Kikwete mtoto wa Bagamoyo kwa mara ya kwanza tumeona unaipenda nchi yako!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Tunajiandaa kufanya maandamamno nchi nzima kwa mara ya kwanza kuunga mkono uamuzi wa serikali ya Tanzania kuamua kuilinda ardhi yetu kwa vizazi vijavyo
tunafanya hivyo ili wale wanaofikiri kikwete yuko peke yake kwenye hili wapate picha halisi
sisi watanzania bado tunafikiria kama kujiunga na huo umoja wa mafisi au la!
tunaomba tupewe nafasi!
Kikwete mtoto wa Bagamoyo kwa mara ya kwanza tumeona unaipenda nchi yako!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Ninyi ni watu wa ajabu sana. Mnafanya maandamano kuunga mkono serikali uamuzi wa kulinda ardhi yenu wakati serikali hiyo hiyo inagawa ardhi kwa mashirika makubwa ya kilimo cha biashara kutoka nchi za nje kwa visingizio vya uwekezaji? Kama huu si wendawazimu sijui ni nini tena.
 
Hivi wale waliopewa ardhi karibia Hekta 300,000 kwa miaka 99 ijayo ni Watanzania? Si bora kuwapa ardhi wakenya, waganda na warundi watakafanya makao yao kuwa Tanzania, kuliko wakorea na wamarekani watakaokuja kuchuma na kuhamishia mazao yao huko makwao?

Hivi mnadhani haya madhahabu na ma-almasi yaliyokwisha kuchimbwa huku nchini, kama huo mtaji ulikuwa unawekezwa Tanzania, huenda 30-50% ya watanzania wasiona kazi leo wangekuwa na chakufanya?
 
Sita hakupewa Nishani, sababu mojawapo huenda ni hiyo ya kukataa ardhi kutokuwa sehemu ya EAC maana kama hili lingeonekana ni uzalendo uliotukuka basi tungeandama kupinga 6 kutopewa nishani! Najua Makinda alipewa Nishani, Je ni kwa lipi kama si kutetea na kupitisha hoja za kifisadi na ukandamizaji?
 
Tunajiandaa kufanya maandamamno nchi nzima kwa mara ya kwanza kuunga mkono uamuzi wa serikali ya Tanzania kuamua kuilinda ardhi yetu kwa vizazi vijavyo
tunafanya hivyo ili wale wanaofikiri kikwete yuko peke yake kwenye hili wapate picha halisi
sisi watanzania bado tunafikiria kama kujiunga na huo umoja wa mafisi au la!
tunaomba tupewe nafasi!
Kikwete mtoto wa Bagamoyo kwa mara ya kwanza tumeona unaipenda nchi yako!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Aridhi ya Loliondo waliko fukuzwa Wamasai na kumilikishwa Waarubu tena kwa miaka mia moja itarudishwa lini?????????? Wamasai walilipwa fidia, kama hakuna kitu hapo ni usanii mtupu ni zero kubwa!!!!!!!!!!!!

hoja nzuri lakini umeiharibu kwenye conclusion. Hapo sababu ni ipi hasa?? Kuupongeza uamuzi wa serikali au kuwazodoa wapinzani wa JK? By the way, tangu mwanzo wa hii issue ardhi ndani ya EAC hakukuwa na mtanzania aliyekubaliana nayo so hakukuwa na mtanzania anayetaka serikali ikubaliane na EAC au kama yupo weka evidence hapa. Pia, tambua msimamo huo wa serikali umekuwa influenced na wananchi ambapo WOTE tulisimama kidete kupinga so unatushangaza kwa mbwembwe zako hizo!! Na haya ndio matatizo ya serikali inapopungukiwa cha kupongezwa matokea yake hata issue zilizo obvious inaleta mbwembwe.

Najua maandamano kama haya Kova na Al-Shabab yake ya kusadikika hawana shida nayo so yatapata kibali na askari wa kuyasindikiza
 
Naona watu kwa upofu au kutokujua kwa makusudi wanachanganya land lease na land owenership. EAC ilikua mambo ya land yaende kwenye ownership ya land, na nchi zote wanachama wangetakiwa kurekebisha sheria zao kuendana na hili. Sheria za Tanzania bado ni land lease. Hizo hectares walizopewa wawekezaji, pale inapobidi, bado Rais(watanzania) ndiye mmiliki wa Ardhi yote ya nchi hii. Rais anaweza kunulify hizo title deeds zao siku yeyote atapoona hazina maslahi kwa nchi. RUBADA walishafanya hivyo kwa wawekezaji kadhaa.

Hata kama tuna chuki naye kwa mambo mengine mengi kwa hili la ARDHI ndani ya EAC, JK is RIGHT, na kama ikibidi HATULIHITAJI hilo shirikisho kama condition yao ni Ownership ya ARDHI yetu.

Hayo Maandamano lini na wapi???
 
hilo siko tayari kwani ni wajibu wao kufanya hivyo. Wanatakiwa pia warudishe Ardhi yote waliyoigawa kwa wageni kwa kisingizio cha uwekezaji.
 
Wenzangu hamjaona hatari sana iliyofanyika? Yaani wabunge kama sikosei wa 5, wametoa uamuzi mkubwa kama huo. Kwa nini maswala makubwa kama hayo yasijadiliwe bungeni? Au ndo kama kawaida siri???Maana je kama hao wangepata cha juu kama kawaida ya CCM kupokea cha juu si ingekula kwetu? Au hao wabunge hawakupewa cha juu ndo maana hawakutia sahii Maana maamuzi ya kutotia sahii yalikuja jioni sana kutokana na vyanzo vya habari
 
Mkuu nakuunga mkono suala hili kujadiliwa bungeni. Ila ningefurahi zaidi kama lingeletwa kwa wananchi wenyewe kuamua kama wanataka huo muungano au hawautaki na hasa likujumuisha suala la ARDHI yao ya RUTUBA. Hata Umoja wa Ulaya(E.U) kulikua na referendum za kuchagua kuingia au kupinga E.U kwa nchi zote wanachama.

J.K wakikulazimisha marais wenzako waambie unataka kura ya maoni ya wananchi kuhusu kujiunga EAC.
 
Back
Top Bottom