Maamuzi magumu...!

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,753
7,845
juggler.jpg
...nimeulizwa swali ambalo natarajiwa nitoe ushauri ambao utamjengea "huyu" dada maisha yake au utambomolea kabisa matumaini kidogo aliyokuwa nayo!
ni hivi....;

maishani mwake amewashi kuwa kwenye mapenzi serious (namaanisha long term, sio chini ya miaka mitatu) na wanaume wawili, ila;

- alisitisha mahusiano na mwanaume wake wa kwanza sababu ya "abuses," physical na psychological...
- alisitisha mahusiano na mwanaume wake wa pili sababu ya "abuses," physical na psychological
- hivi sasa, yupo kwenye mahusiano yasiyozidi mwaka mmoja na partner mpya.. ambaye yupo ok,...sio angel wala devil...

tatizo alilonalo...wale spouses wa mwanzo kila mmoja kwa nafasi yake, wanafanya jitihada usiku na mchana kumshawishi huyu mdada awafikirie upya, kwani pamoja na kwamba hawaku move on kuoa wanawake wengine...pia waliamini time is a healer...ipo siku mwanadada atajichungua upya na kugundua naye alichangia kutokezea breakups hizo...

kwa ushauri wenu, mdada huyu anapaswa kui handle vipi situation hii?...
natamani kumwambia ajaribu wa tatu, lakini mapenzi ni sumu, hayaonjwi!
kwani namuogopea asijejipa matumaini sana kwa huyu watatu
halafu matokeo yake huko mbele ya safari abakie akiilaani bahati yake...

mind you, tafsiri ya abuses huenda inatofautiana baina ya mtu na mtu, au jamii na jamii....
mwenyewe ananisisitiza -" better the devil you know,...!"-

...halahala jamani, mbu mie nasubiriwa na jibu langu jumatatu asubuhi...khaaa!?
 
Mkuu...kumshauri kuhusiana na hili ni pata potea kwani huwezi jua yatakayotokea kesho na keshokutwa.
Ushauri wako unaweza mletea shida mbeleni na akakulaumu wewe kwa yatakayompata.
Nadhani itakuwa vyema kama utamweleza pros n cons za lolote atakaloamua then yeye ndio achague pa kuenda.
Kumbuka....mshauri mbaya ni adui.
 
Heri kufanya uamuzi wa kuendelea mbele kuliko kurudiana na moja x wake,kurudiana na x ni kosa la jinai kwenye mapenzi.
i dnt advyz ha ku-go back 2 any of da x....lyf goz on...

...what if?....maana kwa maelezo yake nilivyomuelewa, namuona kana kwamba kuna udhaifu wake anaoujutia
ambao (japo hakutaka kunifafanulia) anaamini angeujua na kuusahihisha hapo awali, labda wasingefikia huko...
mind you,...anawafahamu vizuri sana hao walitangulia kuliko aliyenaye sasa...

mapenzi ambayo sio serious kivile kama hao waliotangulia.
 
kwa ushauri wenu, mdada huyu anapaswa kui handle vipi situation hii?...
natamani kumwambia ajaribu wa tatu, lakini mapenzi ni sumu, hayaonjwi!
kwani namuogopea asijejipa matumaini sana kwa huyu watatu
halafu matokeo yake huko mbele ya safari abakie akiilaani bahati yake...

mind you, tafsiri ya abuses huenda inatofautiana baina ya mtu na mtu, au jamii na jamii....
mwenyewe ananisisitiza -" better the devil you know,...!"-

...halahala jamani, mbu mie nasubiriwa na jibu langu jumatatu asubuhi...khaaa!?

Sasa Mbu ushauri gani tena anataka wakati hapo kwenye RED ni kama ameshaamua kwamba anaowajua na matatizo yao ni chaguo bora zaidi. Kwahiyo hapo ni kiasi tu cha yeye kuchagua kati ya A na B.

Kama angekua hajaamua kwamba ''Zimwi alijualo halitamla likammaliza'' ushauri wangu ungekua kutokuangalia nyuma unless ANA UHAKIKA kwamba huyo anaetaka kumrudia amebadilika kitu ambacho hakiwezekani!!! Binafsi naona kwamba ni rahisi zaidi kuwa na matumaini na huyoo mpya kwasababu hajaonyesha matatizo so far....kwahiyo kuna uwezekano mkubwa akawa one of the good guys.Tofauti na hao ambao tayari anajua ni wanyanyasaji na hana uhakika kama wameacha/badilika.

Either way yeyote atakaemchagua kuna uwezekano wa kuja kujuta hapo baadae...sasa aamue kama majuto yapi yatakayomla zaidi....Kurudi alipojua kabisa uwezekano wa kuumizwa ni mkubwa au kujaribu bahati sehemu iliyokua na matumaini.
 
Mkuu...kumshauri kuhusiana na hili ni pata potea kwani huwezi jua yatakayotokea kesho na keshokutwa.
Ushauri wako unaweza mletea shida mbeleni na akakulaumu wewe kwa yatakayompata.
Nadhani itakuwa vyema kama utamweleza pros n cons za lolote atakaloamua then yeye ndio achague pa kuenda.
Kumbuka....mshauri mbaya ni adui.

....swadakta bro,

hebu nibainishie basi hizo pros & cons kwenye sakata kama hili nami nijifunze kidogo.
kumbuka, maelezo yangu hapo juu ndio kikomo cha uelewa wangu
juu ya sakata hili pia...
 
...what if?....maana kwa maelezo yake nilivyomuelewa, namuona kana kwamba kuna udhaifu wake anaoujutia
ambao (japo hakutaka kunifafanulia) anaamini angeujua na kuusahihisha hapo awali, labda wasingefikia huko...
mind you,...anawafahamu vizuri sana hao walitangulia kuliko aliyenaye sasa...

mapenzi ambayo sio serious kivile kama hao waliotangulia.

dah hapo pagumu mana kuna watu ambao kwenye mapenzi wanaudhaifu wao binafsi,anaweza akaachwa au kuachana na mtu but baadaye yupo radhi kurudiana,cha msingi we mwambie tu aungalie moyo wake upo upande ganu na wewe usitie neno asije akakulaumu baadaye.
 
Sasa Mbu ushauri gani tena anataka wakati hapo kwenye RED ni kama ameshaamua kwamba anaowajua na matatizo yao ni chaguo bora zaidi. Kwahiyo hapo ni kiasi tu cha yeye kuchagua kati ya A na B.

Kama angekua hajaamua kwamba ''Zimwi alijualo halitamla likammaliza'' ushauri wangu ungekua kutokuangalia nyuma unless ANA UHAKIKA kwamba huyo anaetaka kumrudia amebadilika kitu ambacho hakiwezekani!!! Binafsi naona kwamba ni rahisi zaidi kuwa na matumaini na huyoo mpya kwasababu hajaonyesha matatizo so far....kwahiyo kuna uwezekano mkubwa akawa one of the good guys.Tofauti na hao ambao tayari anajua ni wanyanyasaji na hana uhakika kama wameacha/badilika.

Either way yeyote atakaemchagua kuna uwezekano wa kuja kujuta hapo baadae...sasa aamue kama majuto yapi yatakayomla zaidi....Kurudi alipojua kabisa uwezekano wa kuumizwa ni mkubwa au kujaribu bahati sehemu iliyokua na matumaini.

...umeichambua vizuri Lizzy,....

unajua, hata kwangu mimi huo msemo wa "better the devil you know, ...." wakati anasisitiza abuses kwenye past relationship, ndio zilizonifelisha mtihani huu mbu mie...

kwa mtazamo wangu, kuna weakness yake/zake ambazo anajikubalisha kwa "zimwi limjualo..." ambaye angalau wanaweza kukaa chini na kuya address matatizo yao, kuliko hizo "excess baggages" kuhama nazo kwa huyu ambaye bado hajaji commit naye 100%...au?
 
dah hapo pagumu mana kuna watu ambao kwenye mapenzi wanaudhaifu wao binafsi,anaweza akaachwa au kuachana na mtu but baadaye yupo radhi kurudiana,cha msingi we mwambie tu aungalie moyo wake upo upande ganu na wewe usitie neno asije akakulaumu baadaye.

....umeona ee? wewe umenifahamu vizuri...
amenitega, nimetegeka kujidai ati jumatatu nitampelekea jibu la maisha yake, khaaa!

Hili sredi nashindwa kulichangia kwakuwa Mbu kafanya makusudi akalitoa Jumamosi wakati anajua ntakuwa nimeshautwika mtungi.

I'll be back........On Monday!!

...hehehe!....aisee una ahadi na muumba jumatatu utakuwa hapa?
kaji "detoxify" kidogo uje uweke thumni yako hapa,....jumatatu natakiwa nikakabidhi homework yangu bana!
...mwenyewe hajui kujitia kwangu ushauri mwingi, kumbe nachukua maushauri yenu wana jamiiforum!
 
Hili sredi nashindwa kulichangia kwakuwa Mbu kafanya makusudi akalitoa Jumamosi wakati anajua ntakuwa nimeshautwika mtungi.

I'll be back........On Monday!!
teh teh teh heri unyamaze tu wajukuu wasije wakasema babu leo hana busara.
 
....swadakta bro,

hebu nibainishie basi hizo pros & cons kwenye sakata kama hili nami nijifunze kidogo.
kumbuka, maelezo yangu hapo juu ndio kikomo cha uelewa wangu
juu ya sakata hili pia...

Ipo hivi mkuu...watakiwa kumuelezea kuwa yanaweza tokea haya.

Kwa haraka haraka...

kwanini arudiane na mmoja wao.

1.anawajua vyema so atakuwa amepata namna ya kudeal now.
2.watakuwa wamejifunza mapungufu yao hivyo kwasasa watakuwa wamebadilika.
3.wamekutana na wanawake wengi baada yake lakini wamegundua yeye ndio anafaa kuwa mama watoto.
4.Watakuwa wamepevuka zaidi hivyo kujua majukumu yao kwenye mahusiano hivyo ajiandae kula bata.
5.Jamaa alienae sasa hivi haeleweki expire date yake ni lini....
6.Zimwi likujualo halikuli likakwisha....
7.

Kwanini asirudiane nao.
1.wanamtesa kihisia na kimwili...tabia hii si njema na bado hata kwenye ndoa hawajaingia.
Twagemea makucha halisi ya mtu huwa yanaonekana akiingia ndoani...wameanza toa kichapo mapema hii...akiolewa je.
2.wameachika kwa wanawake wengine kwa tabia hii...so wanarudi kwake kwani hakuna mwanamke awezae vumilia kuumizwa.
3.Wanadai wamebadilika na si rahisi kutambua kama kweli kwani twajua jasiri haachi asili.
4.Tayari ana mahusiano na mtu mwingine...ajali hisia zake.
5....
6...

Huu sio ushauri ila ni mwongozo wa nini chaweza kutokea akichagua kwenda njia yoyote....atapoenda popote...matokeo yake anayajua na itakuwa ni uamuzi wake na sio wako.
Ngoja niwahi mpirani...
 
Mbu

Kuna kitu kimoja ambacho nataka kukigusia ambacho sijui yeye kinamhusu au la. Lakini wanawake wengi waliokuwa kwenye abusive relationship huwaelezi kitu kwa wanaume hao. Yaani wanakuwa kama wameshikiwa akili. Na huo mvuto wanaouhisi kwa hao wanaume walio wa abuse hawawezi hata kuu control, ni kama vile wanataka ku prove kitu kwao.
 
Kwenye mapenzi kukumbushana mabaya ya nyuma ni kosa kubwa sana wapenzi wanalifanya. Wakirudiana there is big chance wakalifanya hili kosa. Isitoshe risk nyingine ya kurudiana ni magonjwa(naomba mnielewe hapa).

But kikubwa zaid ini yeye mwenyewe yupi anadhani anamfeel zaidi na anaweza kufanya maamuzi.
 
Kabla sijalewa zaidi....
Mheshimiwa Moskwito labda uniweke sawa kidogo.

Ni yupi kati ya hao wawili ambaye anatamani kurudiana naye? Kwa sababu kama ni wote, namshauri abaki na huyu wa sasa!!

Naomba unambie kabla sijalewa zaidi nikaharibu mazima.
 
Ipo hivi mkuu...watakiwa kumuelezea kuwa yanaweza tokea haya.

Kwa haraka haraka...

kwanini arudiane na mmoja wao.

1.anawajua vyema so atakuwa amepata namna ya kudeal now.
2.watakuwa wamejifunza mapungufu yao hivyo kwasasa watakuwa wamebadilika.
3.wamekutana na wanawake wengi baada yake lakini wamegundua yeye ndio anafaa kuwa mama watoto.
4.Watakuwa wamepevuka zaidi hivyo kujua majukumu yao kwenye mahusiano hivyo ajiandae kula bata.
5.Jamaa alienae sasa hivi haeleweki expire date yake ni lini....
6.Zimwi likujualo halikuli likakwisha....
7.

Kwanini asirudiane nao.
1.wanamtesa kihisia na kimwili...tabia hii si njema na bado hata kwenye ndoa hawajaingia.
Twagemea makucha halisi ya mtu huwa yanaonekana akiingia ndoani...wameanza toa kichapo mapema hii...akiolewa je.
2.wameachika kwa wanawake wengine kwa tabia hii...so wanarudi kwake kwani hakuna mwanamke awezae vumilia kuumizwa.
3.Wanadai wamebadilika na si rahisi kutambua kama kweli kwani twajua jasiri haachi asili.
4.Tayari ana mahusiano na mtu mwingine...ajali hisia zake.
5....
6...

Huu sio ushauri ila ni mwongozo wa nini chaweza kutokea akichagua kwenda njia yoyote....atapoenda popote...matokeo yake anayajua na itakuwa ni uamuzi wake na sio wako.
Ngoja niwahi mpirani...

...hehehe!....

aise umeiweka vyema sana...nitai print kisha nitatafuta mkalimani aniwekee kwa 'kidhungu,' maana mdada mwenyewe "...know what i mean" nyiiiingi!
 
Back
Top Bottom