Maalim Seif: Tunataka kiti cha Zanzibar UN kirudishwe

Sure, ili isije ikawa kama ishu ya mipaka ya Tanganyika na Malawi. Mkataba wa wakoloni wa 1890 na ule wa 1982 wa umoja wa mataifa vinatukoroga. Tuwekane wazi kabla hatujasambaana.
 
ROU, sorry I doubt this was said!.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Seif Sharif Hamad amesisitiza umuhimu wa Zanzibar kurudishiwa kiti chake katika Umoja wa Mataifa (UN) kama ilivyokuwa kabla ya Muungano.

Ili kufanikisha hilo, Hamad ametaka Wazanzibari kujitokeza kwa wingi katika awamu ya pili ya kutoa maoni ya Katiba, huku akisisitiza Zanzibar kuwa na kiti hicho UN kama ilivyokuwa baada ya Mapinduzi ya mwaka 1964.

Akizungumza jana na wananchi na wafuasi wa CUF Pemba, Hamad alisema Tanzania itapata Katiba mpya Aprili mwaka 2014 ambapo kwa upande wa Zanzibar mchakato huo unahusu wananchi moja kwa moja katika suala la Muungano na marekebisho yake. Alisema wakati umefika kwa Wazanzibari kukirudisha kiti hicho kilichokuwapo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 1964, "Mchakato wa marekebisho ya Katiba kwa upande wa Zanzibar unahusu moja kwa moja Muungano...wakati umefika Wazanzibari warudishe kiti chao UN," alisema Hamad.

Hata hivyo, ili nchi iwe na kiti UN, ni lazima iwe Dola huru au Dola kamili na hivyo haiwezi kujitambulisha kuwa ndani ya Dola nyingine, kwa maana kwamba Zanzibar haiwezi kuwa Dola huru na kuwa sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kuvunja Muungano.

Kwa ukweli huo, Zanzibar haiwezi kuwa na kiti UN bila kuvunja Muungano. Vyama vya siasa Hamad alitaka wananchi na viongozi wa vyama vya siasa kuachana na misimamo wa vyama vya siasa na kuweka mbele alichoita ni maslahi ya Taifa katika suala la kuona Zanzibar inakuwa Dola kamili inayojitegemea, "Katiba ya nchi ni mali ya wananchi na si chama cha siasa, lakini najua kila chama kina Katiba yake, lakini katika suala la marekebisho ya Katiba ni bora wananchi wakaweka maslahi ya Taifa mbele," alisema Hamad.

Msimamo wa CUF, haujaeleza wazi kuwa Muungano uvunjwe bali umeweka wazi kuwa ubadilishwe uwe wa serikali tatu wakati msimamo wa CCM ukidumisha Muungano wa serikali mbili.

Hamad katika ‘kampeni' hiyo, alitaka wananchi wa Pemba kujitayarisha kutoa maoni ya marekebisho ya Katiba awamu ya pili bila ya wasiwasi wala woga na hakuna mtu atakayewawajibisha katika hilo.

Suala la Sensa ya Watu na Makazi

Mapema Hamad alitaka wananchi wajitokeze kwa wingi wakati wa Sensa ya Watu na Makazi Agosti 26 kwa lengo la kuliwezesha Taifa kupata takwimu sahihi zitakazosaidia kuleta maendeleo.

Alisema takwimu za nchi zinahitaji kukusanywa vizuri katika maeneo mbali mbali ambapo Serikali itajua mahitaji ya wananchi ikiwamo maendeleo ya sekta ya afya, elimu na uchumi kwa jumla, "Wananchi jitokezeni kwa wingi katika Sensa ya Watu na Makazi kwa ajili ya kuiwezesha Serikali kutoa huduma zake muhimu za elimu, afya na maendeleo ya uchumi na kujikwamua na matatizo ya umasikini," alisema.

via HabariLeo
 
Maalim ni mroho wa madaraka tu. Hii sera ndio ingeiingiza CUF madarakani kwa uharaka. Nini anachoshindwa kuvunja huo muungano wao na kujitenga kutafuta ukombozi ilhal asilimia kubwa ya waZNZ wanataka iwe hivyo? Jibu ni kuwa Seif ni muoga kuachia kiti alichonacho sasa ndio maana ikawa rahisi kuchakachuliwa na kupewa ukaimu.
 
Huyo mzee vipi? Kwani kiti cha zanzibar hadi akadai UN, akachonge kiti hata huko Zenji au hawana mafundi seremala?
 
ROU, sorry I doubt this was said!.

Huo ndio msimamo wa Maalim Seif siku zote. Pia anataka sarafu ya Zanzibar irudi na amekuwa anasema hayo mambo kwa miaka sasa. Hiyo ndiyo CUF ya Maalim Seif.
 
Sura yake inaeleweka vizuri tu ni ya "kinyonga". Ni mtu mnafiki mwenye uwezo wa kufanya chochote ili kupata Uongozi. Aogopwe kama 'Ukoma"

Sioni Maalim kakosea nini mpaka kuitwa kinyonga, ukoma, n.k. kasema yaliyo moyoni mwake na siyo yaliyo moyoni kwako! "Kila mtoto na koja lake" ya nini kumkejeli? TUVUMILIANE
 
Makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar akihutubia wafuasi wa CUF visiwani Zanzibar kasema anapendekeza na kutaka pia kiti cha Zanzibar Katika umoja wa mataifa UN kirudishwe.

Kwa usemi huu ni dhahiri Zanzibar inataka kuwa dola huru na muungano kwisha habari yake.

Yote sawa tu. Mbona dola kama "the Otman Empire", "The Roman Empire", "the soviet Union" nazo zilivunjika? Hiyo ndiyo historia na hiyo ndiyo "human development", siyo jambo la kushangaza wala kuogofya.
 
Na Mwinyi Sadallah | 14th August 2012

eu.jpg

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kuna haja kwa Zanzibar kurejeshewa kiti chake katika Umoja wa Mataifa (UN).

Alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na viongozi wa wilaya na majimbo wa Chama cha Wananchi (CUF) katika ukumbi wa Benjamin Mkapa, kisiwani Pemba jana.

Alisema Zanzibar kabla ya Muungano ilikuwa nchi huru iliyokuwa na kiti chake UN na kuelezea haja ya kuwepo kwa mamlaka kamili ya Zanzibar ili iweze kurejesha kiti chake kwenye umoja huo.

Maalim Seif alisema hoja kubwa ambayo Wazanzibari wanatakiwa kujadili katika mchakato wa maoni ya Katiba mpya ni muundo na mfumo wa Muungano.

"Zanzibar tunayo Katiba yetu ya mwaka 1984 ambayo imejitosheleza kwa mambo yetu ya Zanzibar, lakini suala kubwa kwenye mabadiliko hayo kwetu sisi litakuwa ni la Muungano na hili haliwezi kuepukwa," alisema Maalim Seif.

Maalim Seif aliwataka wananchi kuangalia maslahi ya nchi yao kwanza katika mchakato wa kukusanya maoni ya mabadiliko ya katiba na kuacha tabia ya kutetea misimamo ya vyama badala ya maslahi ya nchi na wananchi wake.

"Katiba ya nchi ni mali ya wananchi siyo ya chama chochote, lakini najua kila chama kina katiba yake na hiyo ndiyo itabakia kuwa katiba na mwongozo wa chama husika, kwa hivyo ndugu zangu naomba tulifahamu hili na tuangalie maslahi ya nchi yetu kwanza," alisema Maalim na kupigiwa makofi na wanachama.

"Mimi najua wapo wanaotaka serikali moja, wengine mbili, tatu, nne, na muungano wa mkataba, lakini wengine wanataka waachiwe wapumue…Yote hayo ni maoni na kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake bila ya kulazimishwa, kwa hivyo wakati wenu ukifika nendeni mkatoe maoni hayo kwa uwazi," alisema Maalim Seif.

"Wakati wenu ukifika nendeni mkatoe maoni yenu kwa uwazi bila ya hofu hiyo ni haki yenu ya kikatiba," aliongeza.

Alisema serikali ya Tanzania tayari imepanga ifikapo Aprili 2014, Tanzania iwe na katiba mpya ambayo inatokana na matakwa ya wananchi wake wa pande mbili za Muungano huo.

Ingawa Maalim Seif hakufafanua kauli yake ya Zanzibar kuwa na kiti chake katika UN, lakini anamaanisha kwamba Zanzibar inapaswa kuwa na mamlaka yake kamili.

Kwa maana hiyo ikiwa Zanzibar itarejeshewa kiti chake katika UN hapatakuwepo na Muungano tena kwa kuwa itakuwa ni nchi kamili ambayo inatambuliwa na UN na jumuiya ya kimataifa kwa ujumla.

Tangu Tume ya kukusanya maoni ya Katiba mpya kuanza kazi hiyo, kumeibuka kikundi kinachofanya kampeni misikitini (Uamsho) kutaka Zanzibar kujitenga katika Muungano huku wengine wakitetea kuwepo kwa Muungano wa mkataba.

Vile vile, baadhi ya Wazanzibari wakiwemo mawaziri na makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamesema kuwa kuna haja ya kuwa na Muungano wa mkataba kwa lengo la kumaliza kero zinazolalamikiwa.

Baadhi ya makada wa CCM waliotaka Muungano wa mkataba ni Waziri asiye na Wizara Maalum, Mansour Yusuf Himid na mmoja wa waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, Ali Nassoro Moyo.

Hata hivyo, baadhi ya makada wamewashambulia na kuwatisha wanachama wa chama hicho wanaotoa maoni tofauti na sera ya CCM ambayo ni muundo na mfumo wa serikali mbili.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, wiki iliyopita wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Jimbo lake la Kitope, alisema wanaopingana na sera ya CCM kuhusu muungano warejeshe kadi zao za uanachama badala ya kusubiri kufukuzwa.

Naye Mbunge wa Uzini (CCM), Dk. Mohammed Seif Khatib, Alhamisi iliyopita akizungumza na waaandishi wa habari mjini Dodoma akiwa na wabunge zaidi ya 30 kutoka Zanzibar alieleza kushangazwa na wanachama wanaotoa maoni ya kuvunja Muungano.

Khatib ambaye ni Mwenyekiti wa wabunge wa CCM Zanzibar, alisema chama hicho kinapaswa kuwachukulia hatua kwa maelezo kuwa walipata nyadhifa zao kwa kutumia ilani ya CCM inayoeleza wazi kuwa sera yake ni ya Muungano wa serikali mbili.

CHANZO: NIPASHE
 
Sioni Maalim kakosea nini mpaka kuitwa kinyonga, ukoma, n.k. kasema yaliyo moyoni mwake na siyo yaliyo moyoni kwako! "Kila mtoto na koja lake" ya nini kumkejeli? TUVUMILIANE

Mkuu Iseesa,
Kama Maalimu alikuwa na nia ya ZNZ kuwa na Kiti UN (Kwa maana ya kuvunja Muungano) hakuwa na sababu za kumchongea Mzee Jumbe kwa Nyerere wakati ule. Huo ndio Ukinyonga wake na watu huenda mbele zaidi na kusema ni uroho wa madaraka.
 
Nenda mwana kwenda! Sintopungukiwa na chochote kama zanzibar ikienda, tena nawatakia mafanikio ili mjitegemee muendelee muwe dubai ndogo, which means badala ya kwenda dubai wafanyabiashara wa bara watakuwa wanakuja kununua mizigo kwenu its fine! Lakini mkifanikiwa! Pia sielewi hawa ndugu zenu waliojaa huku kwetu mtatuachia au la! Na la zaidi kuna climate change huko mbeleni hivyo visiwa vitamezwa na bahari sijui mtajipanga vipi maana mtakuwa wakimbizi msiokuwa na nchi LOL....
 
Asalam alykum Hii ni habari njema kwa sisi Zanzibar lkn tu huyu maalim naona kidogo kachelewa kutaka hichi kiti chetu ukweli usio na shaka ni kwamba Zanzibar hatutaki muungano na tanganyika na kama tanganyika wanasema kuhusu wazanzibari au kama wanavyowaita wenyewao wapemba kwamba wanaishi hapo hilo si tatizo kwani tunaishi kila pahala bila hata ya kuungana kwa mfano Wazanzibari wanaishi Kenya, Uganda , Mozambique ,Malawi na kadhalika bila ya kuungana kwa hivyo kuishi isiwe issue tunataka tupumuwe .
 
Kwanini huyu Maalim Seif Shariff Hamad anazunguka MBUYU, ooh Zanzibar iombe kitu chake UN, Ooooh Zanzibar iwe dola kamili ..... !

Kama Mwanaume rijali kweli aukumbatie MBUYU, aseme in BLACK and WHITE Wazanzibari WAVUNJE MUUNGANO NA TANGANYIKA, period.

Hiyo janja ya kuzunguka MBUYU haimusaidii yeye wala Wapemba wenzake.
 
Dah muungano ukivunjika Watanganyika tutapumua, umeme wetu unaopotea Zanzibar itabidi ukatumike Songea, Singida na kwingine, Wazanzibar watupishe kwe vyuo vyetu ili wamasai, wamang'ati nao wasome. Na pia tupige marufuku wavivu kuja bara.
 
Huu muungano ni TIME BOMB! Una mtikisiko mkubwa sana lakini wanauchukulia poa tu! Lazima ijulikane msimamo ni upi na ikiwezekana tupige tu kura ya maoni, kama ni serikali 3, 2 au 1 manake unafiki sasa utafikia mwisho tu!
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kuna haja kwa Zanzibar kurejeshewa kiti chake katika Umoja wa Mataifa (UN).

Alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na viongozi wa wilaya na majimbo wa Chama cha Wananchi (CUF) katika ukumbi wa Benjamin Mkapa, kisiwani Pemba jana.

Alisema Zanzibar kabla ya Muungano ilikuwa nchi huru iliyokuwa na kiti chake UN na kuelezea haja ya kuwepo kwa mamlaka kamili ya Zanzibar ili iweze kurejesha kiti chake kwenye umoja huo.

Maalim Seif alisema hoja kubwa ambayo Wazanzibari wanatakiwa kujadili katika mchakato wa maoni ya Katiba mpya ni muundo na mfumo wa Muungano.

“Zanzibar tunayo Katiba yetu ya mwaka 1984 ambayo imejitosheleza kwa mambo yetu ya Zanzibar, lakini suala kubwa kwenye mabadiliko hayo kwetu sisi litakuwa ni la Muungano na hili haliwezi kuepukwa,” alisema Maalim Seif.

Maalim Seif aliwataka wananchi kuangalia maslahi ya nchi yao kwanza katika mchakato wa kukusanya maoni ya mabadiliko ya katiba na kuacha tabia ya kutetea misimamo ya vyama badala ya maslahi ya nchi na wananchi wake.

“Katiba ya nchi ni mali ya wananchi siyo ya chama chochote, lakini najua kila chama kina katiba yake na hiyo ndiyo itabakia kuwa katiba na mwongozo wa chama husika, kwa hivyo ndugu zangu naomba tulifahamu hili na tuangalie maslahi ya nchi yetu kwanza,” alisema Maalim na kupigiwa makofi na wanachama.

“Mimi najua wapo wanaotaka serikali moja, wengine mbili, tatu, nne, na muungano wa mkataba, lakini wengine wanataka waachiwe wapumue…Yote hayo ni maoni na kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake bila ya kulazimishwa, kwa hivyo wakati wenu ukifika nendeni mkatoe maoni hayo kwa uwazi,” alisema Maalim Seif.

“Wakati wenu ukifika nendeni mkatoe maoni yenu kwa uwazi bila ya hofu hiyo ni haki yenu ya kikatiba,” aliongeza.

Alisema serikali ya Tanzania tayari imepanga ifikapo Aprili 2014, Tanzania iwe na katiba mpya ambayo inatokana na matakwa ya wananchi wake wa pande mbili za Muungano huo.

Ingawa Maalim Seif hakufafanua kauli yake ya Zanzibar kuwa na kiti chake katika UN, lakini anamaanisha kwamba Zanzibar inapaswa kuwa na mamlaka yake kamili.

Kwa maana hiyo ikiwa Zanzibar itarejeshewa kiti chake katika UN hapatakuwepo na Muungano tena kwa kuwa itakuwa ni nchi kamili ambayo inatambuliwa na UN na jumuiya ya kimataifa kwa ujumla.

Tangu Tume ya kukusanya maoni ya Katiba mpya kuanza kazi hiyo, kumeibuka kikundi kinachofanya kampeni misikitini (Uamsho) kutaka Zanzibar kujitenga katika Muungano huku wengine wakitetea kuwepo kwa Muungano wa mkataba.

Vile vile, baadhi ya Wazanzibari wakiwemo mawaziri na makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamesema kuwa kuna haja ya kuwa na Muungano wa mkataba kwa lengo la kumaliza kero zinazolalamikiwa.

Baadhi ya makada wa CCM waliotaka Muungano wa mkataba ni Waziri asiye na Wizara Maalum, Mansour Yusuf Himid na mmoja wa waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, Ali Nassoro Moyo.

Hata hivyo, baadhi ya makada wamewashambulia na kuwatisha wanachama wa chama hicho wanaotoa maoni tofauti na sera ya CCM ambayo ni muundo na mfumo wa serikali mbili.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, wiki iliyopita wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Jimbo lake la Kitope, alisema wanaopingana na sera ya CCM kuhusu muungano warejeshe kadi zao za uanachama badala ya kusubiri kufukuzwa.

Naye Mbunge wa Uzini (CCM), Dk. Mohammed Seif Khatib, Alhamisi iliyopita akizungumza na waaandishi wa habari mjini Dodoma akiwa na wabunge zaidi ya 30 kutoka Zanzibar alieleza kushangazwa na wanachama wanaotoa maoni ya kuvunja Muungano.

Khatib ambaye ni Mwenyekiti wa wabunge wa CCM Zanzibar, alisema chama hicho kinapaswa kuwachukulia hatua kwa maelezo kuwa walipata nyadhifa zao kwa kutumia ilani ya CCM inayoeleza wazi kuwa sera yake ni ya Muungano wa serikali mbili.
 
Sura kamili ya Maalim inajidhiri. Safi sana Maalimu Seif kwa kueleza kilicho moyoni.
Kwa mantiki hiyo Maalimu anasema kuwa hoja ya serikali 3 au mkataba haina maana tena.
Afadhali Maalimu amesema wazi tofauti na alivyokuwa anajificha nyuma ya pazia.

Muungano sasa umefikia hatima yake, na tunashukuru kuachana kwa usalama.

LET ZNZ GO!

Nadhani hii imekuwa sera ya CUF siku zote, kwa hiyo alichokisema Maalim si kitu kipya. Kwangu mimi ni haki yao kufanya hivyo na nawasisitizia wapiganie kwa nguvu zote.
 
Back
Top Bottom