Maalim Seif atumia magari ya serikali kummaliza Hamad Rashid

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim seif Shariff Hamad ambaye pia ni makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya mapinduzi (inayoongozwa na sera na ilani ya CCM) jana alijkwenda kwenye mkutano wa chama chake huko Manzese Dar, akiwa kwenye msafara wa magari ya serikali kinyume cha matumizo ya magari hayo, limeandika Mwananchi toleo la leo.

Seif aliwasili kwenye mkutano huo akiwa kwenye msafara wa magari zaidi ya sita, yakiwemo ya serikali likiwamo alilokuwa amepanda.

Msafara wake uliongozwa na pikipiki na magari ya msafara wa viongozi wa Jeshi la polisi…….

Habari zaidi katika Mwananchi.

MY TAKE:

Inaonekana Maalim Seif anatumia hela za walipa kodi (ambazo siyo zile za ruzuku CUF inapata) kujikweza kisiasa na kuwafinya mahasimu wake katika chama chake.

Mwenzake aliyemnyonga hapo hadharani, yaani HR, hana uwezo huo – jee hii kweli ni HAKI SAWA KWA WOTE?

Maalim Seif ni mnafiki aliyepitiliza. Anafuja mali za umma ilhali alipokuwa upinzani alikuwa akiwananga ccm kwa matumizi mabovu ya mali za umma. Hii inaonesha alikuwa hajapata nafasi vinginevyo ni njaa tu ilikuwa inamsumbua sasa kapata kaamua kuwa kama wao ccm!
 
you have raised a very pertinent and valid issue: separation of govt and party functions in so far as utilization public resources is concerned - tatizo lililopo ni kwamba kiongozi anajifanya kukomaa sana akiwa nje ya system... akishaingia ndani, you can't see the difference with everybody else; ama kweli 'if you can't fight them, join them'
 
kweli njaa ni hatari sana, hata slaa alikubali kutokugombea ubunge baada ya kuhakikishiwa kuwa yale masarufu yote ya bungeni atayapata kwa kipindi chote cha miaka mitano. hapa kwa kiasi fulani ndipo ninapokubaliana na kauli ya pengo alipoenda kumzika kadinali mwenzake wa kanda ya ziwa pale alipowambia wale wanaomsakama mkapa kwa ufisadi alioufanya akiwa ikulu kuwa wanapiga kelele kwa sababu tu na wao hawajapata nafasi.
 
Maalim Seif ni mnafiki aliyepitiliza. Anafuja mali za umma ilhali alipokuwa upinzani alikuwa akiwananga ccm kwa matumizi mabovu ya mali za umma. Hii inaonesha alikuwa hajapata nafasi vinginevyo ni njaa tu ilikuwa inamsumbua sasa kapata kaamua kuwa kama wao ccm!

Ungekuwa wewe mkuu ungepanda taxi? Acheni hizo jamani, tushughulike na matatizo ya msingi yanayoikabili nchi yetu.

Hoja kama hii haiwezi kutuondoa hapa tulipo na kutupeleka mbele kimaendeleo, mfano waziri mkuu Mh. Pinda alilikataa shangingi jipya kwa madai ni la gharama san. Mkamshangilia sana mkidai ni mzalendo huku wakati huo huo ofisi yake inaendelea kununua mashangingi ya aina hiyo hiyo kwa ajiri ya makatibu wakuu, mawaziri, manaibu wao na wakuu wa mikoa (wakati yale ya zamani wanauziwa kwa bei bwerere)!

Sasa hapo saving iko wapi kama sio kutaka umaarufu wa kisiasa tu?
 
kweli njaa ni hatari sana, hata slaa alikubali kutokugombea ubunge baada ya kuhakikishiwa kuwa yale masarufu yote ya bungeni atayapata kwa kipindi chote cha miaka mitano. hapa kwa kiasi fulani ndipo ninapokubaliana na kauli ya pengo alipoenda kumzika kadinali mwenzake wa kanda ya ziwa pale alipowambia wale wanaomsakama mkapa kwa ufisadi alioufanya akiwa ikulu kuwa wanapiga kelele kwa sababu tu na wao hawajapata nafasi.

ccm at work!
 
Ungekuwa wewe mkuu ungepanda taxi? Acheni hizo jamani, tushughulike na matatizo ya msingi yanayoikabili nchi yetu.

Hoja kama hii haiwezi kutuondoa hapa tulipo na kutupeleka mbele kimaendeleo, mfano waziri mkuu Mh. Pinda alilikataa shangingi jipya kwa madai ni la gharama san. Mkamshangilia sana mkidai ni mzalendo huku wakati huo huo ofisi yake inaendelea kununua mashangingi ya aina hiyo hiyo kwa ajiri ya makatibu wakuu, mawaziri, manaibu wao na wakuu wa mikoa (wakati yale ya zamani wanauziwa kwa bei bwerere)!

Sasa hapo saving iko wapi kama sio kutaka umaarufu wa kisiasa tu?

ccm at work!
 
Jamani mwache atumie kwakuwa kuwa kwenye shughuli za chama chake hakumwondolei hadhi ya umakamu.
 
Jamani naomba Kujuzwa: Hivi hawa Hamad's is Blood brothers?? Sasa hizi vita za kumalizana zinatoka wapi?
Kosa la Hamad mbaye alikuwa kiongozi wa Kambia ya upinzani ni kukubali cheap money/bakshishi za CCM
 
Ngeleja yupo kanda ya ziwa kunadi sera za ccm, anatumia gar la serikali, pinda akiwa mpanda ki chama anatumia magar ya serikali na huku akiongozana na viongozi wa serikaki, rais akiwa na shughuli za chama anatumia magari ya serikali, seif naye humohumo. Tatizo si seif wa jk, wala si ngeleja n.k. Tatizo ni katiba hailezi au wenye mamlaka hawafuatilii. Ukienda bar usiku unakuta STK, STJ, SU zimepaki nje. Shule zikifungwa/kufunguliwa utakuma magari ya serikali yamepaki nje kusuburia kuchukua watoto wa vigogo/kuwaleta watoto wa wakubwa.
 
magari hayo ni halali yake, kwani ndiyo mfumo alioukuta na kuukubali. tujadili kilicho mtuma pale ninini? je ameongea haki sawa kwa wote had HR? maana huyu mzee hata ccm wamemshinda kuvumiliana wanapotofautiana. kama ccm wangekuwa wanatimuana hovyo mnafiki sitta angekuwa wa kwanza. japo najua wanaogopa kusambaratika. ila sasa CUF bado msiba tu. kwa kheri CUF!!!!!!!
 
Back
Top Bottom