Maajabu ya Mungu: Mtoto alelewa na Nyani miaka 5!

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Wana JF, hii habari ipo kwenye Majira la leo; Hakika Mungu ni Mkuu
Mtoto wa binadamu alelewa na nyani miaka 5 porini

Na Gladness Mboma

WATANZANIA wameombwa kujitokeza kumsaidia kielimu mtoto Bahati Baraka Rose (11) ambaye anadaiwa kulelewa na nyani baada ya kutupwa porini akiwa mchanga wilayani Bukombe, Shinyanga.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kimanga, Tabata, Bw. Pastory Kyombya, alisema mtoto huyo kwa sasa analelewa na Bibi Rose Mbwambo wa Kimanga.

Alisema Bibi Mbwambo alikabidhiwa mtoto huyo na Serikali wilayani Bukombe baada ya kufuata taratibu zote za kiserikali.

Alisema Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukombe, Bw. Richard Nhende, ndiye aliyemkabidhi Bibi Mbwambo mtoto huyo ili amlee baada ya kumwomba.

Bw. Kyombya alisema mtoto huyo anaomba kupelekwa shule kama anavyoshuhudia wenzake wakienda shule na kuwaomba wasamaria wema wajitokeze kumsaidia ili aanze shule mwakani.

Naye Bibi Mbwambo alisema alimchukua mtoto huyo Agosti mwaka huu akiwa kwenye biashara zake Bukombe.

"Nilikuwa nimepanga kwenye nyumba ya kulala wageni ya Neema, nikiwa na wenzangu, mama mmoja (hakumtaja jina) ambaye alikuwa akitupikia chakula alitujia na kutueleza matatizo aliyonayo mtoto Baraka.

"Nilimwonea huruma sana Baraka, baada ya mama huyo kutuelezea historia yake nzima na kwamba hana ndugu na maisha yake ni ya kutangatanga na kututaka tumsaidie," alisema.

Alisema yeye binafsi aliingiwa na huruma ndipo alipofuata taratibu zote za kumchukua mtoto huyo na kuja naye Dar es Salaam kumlea.

Bibi Mbwambo alisema atamtunza mtoto huyo kama anavyotunza watoto wake ila aliomba wasamaria wema kujitokeza kumsaidia ili aanze masomo mwakani ikiwezekana shule ya bweni.

Alisema mtoto huyo alilelewa na nyani miaka kadhaa porini kabla ya kuchukuliwa tena na binadamu baada ya nyani huyo mlezi kuuawa kwa risasi.

Bibi Mbwambo alisema inadaiwa mtoto huyo aliokotwa na nyani akiwa kwenye mfuko wa 'rambo' akiwa mchanga na kumlea kwa miaka mitano.

"Askari wa wanyamapori wa Ushirombo, Bukombe, ndio waliofanikisha kupatikana kwa mtoto huyo baada ya siku moja kumwona nyani akimnyonyesha.

"Hata hivyo, inadaiwa askari hao walipata shida kumchukua mtoto huyo baada ya nyani mlezi kukimbia naye mara zote kila alipokuwa akiwaona, hivyo kuchukua muda mrefu kumpata," alisema.

Alisema mtoto huyo aliendelea kulelewa na nyani huyo hadi alipofikisha umri wa miaka mitano na baadaye askari hao kumvamia tena ili kumnyang'anya mtoto huyo na kusababisha vurugu kubwa kati yao na nyani mlezi.

Bibi Mbwambo alisema katika vurugu hizo, askari walimfyatulia risasi nyani huyo na kumuua huku risasi moja ikimpata mtoto huyo kwenye kidole cha mguu wa kushoto.

Alisema askari hao walimchukua mtoto huyo na kumpeleka katika hospitali ya Bukombe ambako aliendelea kulelewa hospitalini hapo.

Bibi Mbwambo alisema watu mbalimbali walikuwa wakimchukua mtoto huyo na kumlea na walioshindwa walikuwa wakimrudisha hospitalini hapo, lakini msamaria mwema alimchukua, lakini mtoto huyo alimtoroka na kuingia mitaani na kuishi maisha ya shida.

Alisema Baraka alikwishazoea kuishi maisha ya porini, akiparamia miti na kusababisha wasamaria wema waliokuwa wakimlea kulazimika kumfunga minyororo ili asitoroke.

Source: Majira 20 Nov.2008
 
Nimejaribu kutafuta vipande muhimu kwenye hii habari ili niridhike kwamba tukio hili kweli limetokea. Habari yaweza kuwa ya kweli, hata hivyo imeandikwa ki-udaku mno. Mfano, imetajwa hospitali ya Bukombe; gazeti limeshindwa hata kupiga simu kwenye hiyo hospitali tupate kauli yao japo kwa ufupi? Uandishi wa namna hii ovyo kabisa. Website zenye mipicha-picha nazo ovyo. Mwanakijiji.com inaonyesha njia.


Tukio kama hili limewahi kutokea Urusi. Mtoto alitunzwa na mbwa kwa miaka kadhaa.
Video footage ya huyo mtoto ilionyeshwa kwenye luninga. Japo mtoto aliweza kutoa sauti kama ya bubu, hakuwa anaweza kuongea.




.
 
Waweza kufikiri ni tukio la hivi karibuni (inaelekea mwandishi alitaka watu waamini hivyo).
Kama mtoto aliokotwa akiwa na miaka 5 na sasa ana miaka 11, basi ni tukio la miaka 6 iliyopita.
Halafu hapa wanasema mtoto anaomba msaada....nina mashaka kama huyu mtoto ana uwezo wa kuomba kupelekwa shule ya bweni! Nadhani anayeomba msaada hapa ni mlezi wa mtoto huyo (kwa niaba ya mtoto mwenyewe?).
Hata hivyo ni tukio la kipekee mtoto kulelewa na nyani kwa miaka 5 (kwamba aliweza kumudu maisha magumu ya porini kwa kipindi chote). Labda ni 'George of the jungle' ya kweli.
 
Nina maswali mengi sana ya kuuliza hapa;

1. Mtoto alitupwa kwenye rambo baada ya kuzaliwa ......Hizi taarifa walipata wapi, nani alishuhudia huyo mtoto akiwa kwenye rambo? mi matarajio yangu ni nyani huyo aliye mwokota ndiye alimkuta kwa mara ya kwanza akiwa ndani ya rambo.....! vinginevyo kuna utata hapa! Mtu wa kwanza kumuona mtoto huyu ni askari wa Ushisombo, na walimwona nyani anamnyonyesha...sidhani kama alikuwa kaviringishwa rambo!

2. Kuhusu umri wa mtoto wakati anapokonywa toka kwa ''Mama mlezi'' nyani, ilikuwa ni miaka mitano (sio kadirio)....je hapo napo walijuaje kwamba nyani yule alikaa na mtoto kwa miaka mitano na huo ndio umri wake? au haya ni makisio tu?

3. Kwa nini askari wale wakaamua kumfyatulia nyani risasi kama njia pekee ya kumnyang'anya mtoto? mimi na amini wale ni wataalam wa wanyama pori, hivyo kulikuwa na njia mbadala ya kumpata mtoto bila hata kumuua ''Mama mlezi'' wa mtoto!

Kama ni kweli, hili limetokea, nyani ameonyesha upendo wa hali ya juu kuliko binadamau, kwasbabu nyani alikuwa na uwezo na nafasi nzuri sana ya kumdhuru mtoto yule, lakini akachagua kumlinda kwa nguvu zote na ndio maana alikuwa ananyima kuwaachia mtoto, kwa sababu binadamu alisha mkana kwa kumtupa kwenye pori lao ambayo ni makazi yao ya kudumu! Hapa kutakuwa na namna tu sio bure, askari hawa watakuwa na lao jambo!

3. Hivi haiwezekani binadamu akamvamia nyani na kumwingilia hivyo huyo mtoto akawa na baba binadamu na mama nyani? na sema hivi kwa sababu tumeshasikia mwanamke kalazimishwa kuingiliwa na mbwa (tena hii habari ilitoka huko huko Shinyanga -migodini), tumeshasikia wanaume kuwaingilia mbuzi (hapa mimi nina ushahidi tosha kijijini kwetu kuna kijana alishikwa red handed akimwingilia mbuzi). Ila tu hapa mimi si mtaalam wa baolojia naomba wenyewe mcomment kama hili haiwezekazi pia!

Huo ndio mtazamo wangu!
 
Kama wenzangu,nimeshindwa kujizuia kupata maswali ya hapa na pale.
Huyu nyani alikuwa species gani?Just trying to figure out the whole nyani running away,carrying a 4-year-old human child scenario.Isije ikawa tunadeal with Queen Kongs hapa.

Halafu,ili kuweza kunyonyesha,ina maana nyani alikuwa na mtoto of her own.Je?Alimtelekeza mtoto wake and took on the sapiens au ali-double click?Au mtoto wake pia alikuwa ameuwawa kwa risasi?

"Hata hivyo, inadaiwa askari hao walipata shida kumchukua mtoto huyo baada ya nyani mlezi kukimbia naye mara zote kila alipokuwa akiwaona, hivyo kuchukua muda mrefu kumpata," alisema.

Like 5 years?And,they knew the baby was human,right?
Oooh!I see,Queen Kong also had weapons of mass destruction,ndio maana ilikuwa vurugu kumpata mtoto hata baada ya hiyo miaka mitano.I can live with that.

Sisemi kwamba hadithi ni ya uongo.I just need help making sense out of it.
 
Kwa ujumla hii habari inamaswali mengi kuliko majibu. mimi ni swali moja tu ambalo linanisumbua, kwa namna ninavyo fahamu ni kuwa mtoto mwenye miaka mitano atakuwa na uzito unaokaribia kilogramu 25, sasa huyu nyani anuwezo wa kubeba mtoto au kitu cha kilogramu 25? hapa mimi inanifanya nisiamini hizi habari.
 
Mimi kilichonisikitisha ni kuuwawa kwa yule Nyani! Km Next Level alivyosema...kweli hao watu wa wanyamapori hawakuwa na njia nyingine? Ipo picha ya mtoto na Mlezi wake wa sasa katika moja ya magazeti ya leo
 
Mimi kilichonisikitisha ni kuuwawa kwa yule Nyani! Km Next Level alivyosema...kweli hao watu wa wanyamapori hawakuwa na njia nyingine? Ipo picha ya mtoto na Mlezi wake wa sasa katika moja ya magazeti ya leo


Mkuu unaweza kuiscan ukaiweka hapa, tuione picha hiyo inafananaje.....wengine tupo bush!
 
Picha hiyo natumaini inaonekana japo si clear sana
 

Attachments

  • Bahati baraka.pdf
    773.4 KB · Views: 502
Ubarikiwe mkuu Liz snr ....nimeipata unono kabisa na ubarikiwe!

Mbona huyo mtoto kama kafanana vile na Rose Mbwambo mama yake mlezi? au ni macho yangu?
...Ni kweli wanafanana au ndio amebuni njia ya kupata msaada wa kusomeshewa mtoto wake akaamua kutunga story ili apate huruma ya watu... Bongo noma!!
 
Japo hii habari imefinyangwafinyangwa ki fiction zaidi, ila kitendo cha askari wa wanyama pori kumuua yule nyani ni kosa la mauji na wanastahili kujibu tuhuma hizo katika hizohizo habari za kifiction. Mi nafikiri kama ingekuwa ya kweli kuna watu wengi sana wanafanya research ya nyani na sokwe kwa nini wasipige picha za video? kwa muda wote walipokuwa wanamfuatilia.

Anyway hapa hakuna wa kujibu maswali mengi niliyo nayo kuhusu hii "fiction story" na hata mwandishi wa gazeti hili hana majibu.
 
Japo hii habari imefinyangwafinyangwa ki fiction zaidi, ila kitendo cha askari wa wanyama pori kumuua yule nyani ni kosa la mauji na wanastahili kujibu tuhuma hizo katika hizohizo habari za kifiction. Mi nafikiri kama ingekuwa ya kweli kuna watu wengi sana wanafanya research ya nyani na sokwe kwa nini wasipige picha za video? kwa muda wote walipokuwa wanamfuatilia.

Anyway hapa hakuna wa kujibu maswali mengi niliyo nayo kuhusu hii "fiction story" na hata mwandishi wa gazeti hili hana majibu.

Huyu Rose Mbwambo anatakiwa abanwe vizuri, huyo ndo anajua ukweli kama ni fiction au laaa!

Halafu huyu mama jamani inasemekana ni mfanya biashara, sasa ni mfanyabiashara gani anashindwa kumlipia mtoto huyu Elimu ya Msingi hata ya Secondary? Na kwa nini alienda kumbeba huko kwao Ushirombo?

Haya mambo yananitatiza kwelikweli!
 
mmh, mbona wanafanana sana jamani? na pia mfanyabiashara kweli ashindwe kumsomesha? isije ikawa ni mradi,nisamehe lkn si iiamini sana hii hadithi.labda watufafanulie zaidi.
 
A monkey in Dhenkanal protects and takes care of a twenty-four day old human baby when his mother is engaged in household chores. The monkey comes to the house in the morning and spends the whole day taking care of the baby and at times even sleeps in the house with the little one. This incidence has become the talk of the town and the locals are also surprised, though pleasantly protects and takes care of a twenty-four day old human baby when his mother is engaged in household chores. The monkey comes to the house in the morning and spends the whole day taking care of the baby and at times even sleeps in the house with the little one. This incidence has become the talk of the town and the locals are also surprised, though pleasantly

monkey_babysitter
 
  • Thanks
Reactions: amu
Hawa waandishi wengine wanatazama makatuni ya tarzan na kuunga unga habari,sio mbaya ni katika kutufurahisha,ila mtoto wa miaka mitani kwa kimo ni sawa na nyani mwenyewe. au walikusudia miezi mitano.
 
The Wolf Boy from India...mnamjua huyu naye?


2008-11-20-genc_kurt2.jpg


2008-11-20-pruthmain_487811a.jpg



2008-11-20-wolfboy2.jpg

 
Back
Top Bottom