Feedback
JF-Expert Member
- Mar 14, 2011
- 7,988
- 4,507
Propaganda zinazosambazwa na vijana wa chama cha Mapinduzi CCM na baadhi ya viongozi wake zinakiongezea chama maadui bila sababu za msingi.
Imekuwa ni kawaida kwa vijana wa chama cha Mapinduzi kumuona kila mtu adui yeyote anayekosoa viongozi wake, chama au serikali, binafsi naona kama "ujinga mpya" umeingia ndani ya CCM ya sasa.
Hapo mwanzo vyama vya upinzani vilionekana kama adui wao mkuu, lakini siku za karibuni chama kimetengeneza maadui wengi kuliko marafiki zake. Yaani kwa sasa CCM na serikali yake hawamjui adui yao ni nani na rafiki yao ni nani, yeyote anayetoa mawazo mbadala kwao ni adui.
Mtu akisema kuwafukuza Acacia bila kurekebisha sheria za madini ni kazi bure anaitwa kibaraka wa mabepari. Akitokea mwingine akasema kuwanyima mikopo wanafunzi waliosoma shule binafsi ni ubaguzi, anatukanwa eti hataki watoto wa maskini wapate mikopo au anataka kukwamisha juhudi za rais Magufuli.
Leo hii makanisa yameongezwa kwenye orodha ya maadui wa CCM, akitokea Askofu akashauri jambo lisilowapendeza basi atashambuliwa na pengine kuchunguzwa uraia wake. Mchungaji Kakobe alisumbuliwa na TRA kwa kushauri viongozi 'watubu' akiwemo rais pengine kwa nia njema tu. Leo hii kanisa la KKKT limekuwa adui wa CCM kwa ukuitaka serikali ikomeshe uhalifu, Baraza la maaskofu katoliki (TEC) nalo liko kwenye orodha ya maadui wa CCM.
Wazazi na vijana wao wanaodai haki ya kupata mkopo wa elimu ya juu ni maadui wa CCM wamewekewa kigezo cha leseni ya biashara. Vyombo vya habari na Bloggers wote wanaodai uhuru wa vyombo vyao wamekuwa maadui wa CCM na serikali yake, leo kusajili blog lazima ulipe mamilioni ya pesa.
Mashekhe wa Uamsho tayari wao ni maadui wa CCM, Taasisi za Kiraia kama LHRC, TLS ni maadui wa CCM, Mtandao wa wanafunzi wa chuo vikuu TSNP nao ni maadui wa chama na serikali yake kwa vile tu wanadai haki yao.
Katika orodha ya maadui, CCM pia imewaunganisha hadi mataifa ya magharibi, Marekani na nchi za Umoja wa Ulaya EU wanaonekana ni maadui wa chama na serikali kwa hisia tu kuwa nchi hizo zinashirikiana na baadhi ya watu kuihujumu serikali ya Magufuli.
Kitu ambacho CCM hawakijui labda kwa ignorance ni kwamba kwa kadri wanavyotengeneza maadui wengi ndivyo wanavyopunguza marafiki, makundi haya (maadui zao) yakiungana pamoja dhidi ya serikali sijui kama CCM itaweza kuhimili nguvu yake.