M/kiti wa UVCCM K/njaro aliyehamia CHADEMA, arudi CCM

Status
Not open for further replies.
Kwa hiyo alifuata pesa? Namsikitia sana, naisikitikia CCM pia kulea viongozi wenye uchu wa fedha kiasi hiki (wanaohongeka kirahi)!

Mtalia mpaka basi! Propaganda zenu zinaonyesha mnapumulia ICU, yaani mmeshiwa kabisa!

Ccm sasa hivi ni sawa na lori la mkaa
 
M/KITI WA UVCCM KILIMANJARO ALIYEHAMIA CHADEMA, ARUDI CCM - KUONGEA NA WAANDISHI LEOPARD HOTEL, MOSHI.


Aliyekuwa Mwenyekiti wa jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kilimanjaro ndugu Fredrick Mushi ambaye wiki moja iliyopita alijiunga na CHADEMA akitokea CCM na kupokelewa na wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, ameandika barua kwa Katibu Mkuu wa UVCCM ndg Sixtus Mapunda akiomba kurudishwa kwenye nafasi yake hiyo ya awali.


Katika barua yake, Ndugu Mushi ameueleza uongozi wa juu wa UVCCM kuwa alijiunga na CHADEMA baada ya kuhadaika alipofuatwa na Viongoxi wa juu wa CCM waliokuwa wakimuunga mkono LOWASA pamoja na Mzee Ndesamburo na kumuambia kuwa wahame pamoja nae na kwamba atapatiwa milioni 20.

Na alipokamilisha zoezi la kuita waandishi wa habari na kujitangaza kuhama amekuwa akipigwa danadana kuhusu malipo yake na kwamba mpaka sasa hajapatiwa kiasi hicho cha fedha.

Mushi ambaye alikuwa ni miongoni mwa Vijana wanaomuunga mkono LOWASSA tangu akiwa CCM amesema amejaribu kumtafuta Mzee Lowassa mara kadhaa lakini bila mafanikio. Kwani simu zake kwa sasa zinapokelewa na wasaidizi na wanamjibu Mzee yuko busy.

Mushi ameomba kurudishwa katika nafasi yake kama Mwenyekiti wa Vijana UVCCM Mkoa wa Kilimanjaro na ameahidi kwa namna ile ile ya kuzungumza na waandishi wa habari, ataita tena waandishi wa habari kesho saa nne asubuhi, Leopard Hotel, Moshi mjini na kuongeza kuwa atazunguka kwenye majukwaa katika Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha kuelezea uongo na ulaghai wa CHADEMA wakitumia fedha kuwahonga na kuwadanganya Vijana.
 
We mtoa post kibaraka wa ccm acha propaganda za kijinga hakuna kitu kama hicho na mimi ni shahidi kwa hilo maana toka juzi tuko nae kwenye maandalizi ya kampeni, na pia yeye mwenyewe amepost leo kukanusha hizo propaganda za kumchafua.
 
Kumbe akihongwa anahama na kilichomrejesha ni kuzikosa je akipewa leo ataandika barua ya kuendelea kuwa chadema?

Maajabu
 
Kama unasema Watu wanahamia CHADEMA kwa kuhongwa kwa nini yeye hajahongwa? Bila shaka uzi wako huu ndio utakuwa mwisho wa tuhuma za uwongo kwamba CHADEMA inanunua watu kwa fedha. Utunzi wako unaonyesha amehamia chadema akidhani atapewa fedha sasa amekuta anatoka sifuri kitu ambacho ni CREDIT kwa CHADEMA!.Bila shaka ujumbe wako umefika vizuri kwamba "kama huna moyo wa uzalendo wa kutetea taifa na Watanzania wanyonge, na unataka kufanya kitu chochote tu maadamu unapewa rushwa , USIENDE CHADEMA". Chadema ni kwa wasafi wa moyo na si wasaka rushwa. Rushwa mwisho wake ni ccm ambako hata viongozi wa mikoa wanaweza kuhamia chama kingine cha siasa maadamu tu wapewe rushwa. Kama una viongozi ngazi ya mkoa ambao hawana hata uzalendo , badala yake wanahama chama eti kwa kuwa wameahidiwa rushwa, bado hicho ni chama cha siasa cha kuwakomboa Watanzania? Ila kweli kufa ni kubaya. Ninaona ccm inavyotapatapa wakati inakata roho. Inajivua nguo na kujiacha uchi wa mnyama. Aibu iliyoje?
 
SINA MPANGO WA KURUDI CCM..

Ndugu, toka jana kumekuwa na taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa 'nimeandika barua kwa katibu mkuu wa UVCCM Taifa kuomba nirudi CCM na niendelee kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kilimanjaro'..

Napenda kutumia fursa hii kukanusha vikali habari hizo, kwani zimejaa ulaghai na zimetungwa ili kunigombanisha na wana Chadema wenzangu...

Kwanza toka nijiuzulu, siajawahi kufanya mawasiliano yoyote na Katibu Mkuu wa UVCCM na wala kiongozi yeyote wa CCM, na ndio maana aliyesambaza huo uzushi ameshindwa kuonyesha hiyo barua anayoda nikiandika..

Toka niondoke CCM viongozi wanaweweseka kwani wanajua uwezo wangu, wanajua najua mbinu mbali mbali za kuwamaliza kisiasa..

Hivyo nawaomba wana watanzania, wana Chadema na UKAWA kwa ujumla puuzeni hizo taarifa kwani zimelenga kunichafua jina langu na kuniondolea uaminifu mbele ya makamanda wenzangu..

Niseme tu, sikuondoka CCM kwa kushawishiwa, sikuondoka CCM kwa kuhongwa hata senti moja. Niliondoka CCM kwa utashi wangu, na CCM ni chama kilichopoteza DIRA na kupoteza uhalali wa kuendelea kuwa chama.tawala hapa nchini..

Niwapeni pole sana marafiki zangu, ndugu zangu na wana Chadema wenzangu kwa usumbufu mlioupata kwa sababu ya uzushi Huo..

Mungu Ibariki Tanzania..
Mungu Ibariki Chadema.

By Frederick Mushi..
Mwana wa CHADEMA..


Kakanusha... Mtahaha sana nyie mafisiEmu
 
Kama anasema Watu wanahamia CHADEMA kwa kuhongwa kwa nini yeye hajahongwa? Bila shaka ushuhuda wake huu, ndio utakuwa mwisho wa tuhuma za uwongo kwamba CHADEMA inanunua watu kwa fedha. Amehamia chadema akidhani atapewa fedha sasa amekuta anatoka sifuri kitu ambacho ni CREDIT kwa CHADEMA!.Bila shaka ujumbe wake utafika vizuri kwamba "kama huna moyo wa uzalendo wa kutetea taifa na Watanzania wanyonge, na unataka kufanya kitu chochote tu maadamu unapewa rushwa , USIENDE CHADEMA". Chadema ni kwa wasafi wa moyo na si wapenda rushwa kama huyu jamaa mushi". Saizi yake ccm.Sas ccm mtamkubali na kumwamini tena? Ccm mmempa shilingi ngapi ili aje kwenu? Na ni ngapi mmempa za kuwadhalilisha akidhani anadhoofisha ukawa? Mburura kweli.Ila kweli kufa ni kubaya. Ninaona ccm inavyotapatapa wakati inakata roho.

Mkuu, huyu mtu angekuwa na maana kama angesema alihama baada ya kupewa 20m na azionyeshe kwa waandishi wa habari; aidha, ili kuonyesha jinsi anavyochukia hali hiyo, hizo fedha azitoe kwa ajili ya hudma yoyote ya jamii, lakini kama anasema aliahidiwa halafu hajapewa, imekula kwake !!!! Nani wa kumwamini, kwa nini asilete ushahidi wa kimaandishi ili kuthibitisha malalamiko yake.
 
Mwaka huu magamba mtajuta kumfahamu lowasa,maana kwa mara ya kwanza kwa miaka 54 ya uhuru mgombea wa ccm anapigwa chini na wapiga kura.....teeeeeeeh,teeeeh,teeeeeeh

Pesa za fisadi zimekutia upofu huoni wala husikii.
 
Unajua wa Tz wengi tunajua tunachotaka lakini hatujui tunachohitaji sasa Lowasa anataka kuwapa mnachotaka na Dr Magufuli anataka kuwapa mnachohitaji hapo sasa nikazi yautambuzi wa wahitaji kujua nn muhimu tunachotaka au tunachohitaji nadhani tujenge hoja kati ya kutaka
Nauhitaji kipi ni bora karbuni.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom