M/kiti wa CCM Shinyanga, Khamis Mgeja na John Guninita wajivua uanachama CCM na kujiunga CHADEMA

Na Dr. JP Magufuli asipopewa msaada wa kisaikolojia ikiwa ni pamoja na ulinzi madhubuti hachelewi kuhamia UKAWA...!!
 
Afadhali wanaondoka aisee. vijana tukijenge chama kwa misingi iliowekwa.magamba ndo yanavuka sasa yanaenda eti kuvaa gwanda kumbe ufisadi uleule.
 
Wimbi la wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kuhama chama chao na kwenda UKAWA hasa kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kunaweza kupelekea mgogoro wa kisiasa baina ya wanachama wa zamani waliokikuza na kukilea chma dhidi ya wanachama wageni ambao miongoni mwao walikuwa wapiganaji msitari wa mbele kuing'ong'a na kuizodoa CHADEMA. Hili pia linaweza likachochewa na kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA aliyoitoa hivi karibuni kuwa mwanachama mpya wa siku moja ana haki sawa na mwanachama wa zamani kama yeye Freeman Mbowe. Hivi Wabunge wote wale 150 wanaopanga kukihama CCM wakihamia CHADEMA wanachama asili wa chadema nafasi yao itakuwaje?
Hayawahusu, haya mapenzi ya dharura yametoka wapi? wanafiki wakubwa NAMUTAISOMA NAMBA MAKA HUU NDANI YA NJI II....
 
1.MGANA MSINDAI MKOA WA SINGIDA pia huyu ndie alikuwa mwenyekiti wa wenyeviti wa CCM TANZANIA 2.OLE NANGOLE MKOA WA ARUSHA 3.HAMISI MGEJA MKOA WA SHINYANGA,kwa wenyeviti wa wilaya wengine watuwekee
 
bado tunawasubili kinana na mangula mwaka huu ccm itabakiwa na mwenyekiti na familia yake pamoja na watoto wake wa mkopo nape na makonda
 
Wimbi la wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kuhama chama chao na kwenda UKAWA hasa kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kunaweza kupelekea mgogoro wa kisiasa baina ya wanachama wa zamani waliokikuza na kukilea chma dhidi ya wanachama wageni ambao miongoni mwao walikuwa wapiganaji msitari wa mbele kuing'ong'a na kuizodoa CHADEMA. Hili pia linaweza likachochewa na kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA aliyoitoa hivi karibuni kuwa mwanachama mpya wa siku moja ana haki sawa na mwanachama wa zamani kama yeye Freeman Mbowe. Hivi Wabunge wote wale 150 wanaopanga kukihama CCM wakihamia CHADEMA wanachama asili wa chadema nafasi yao itakuwaje?

Kwani CHADEMA ikisambaratika si ndio ahueni kwenu au? Mbona mnaingiwa woga sasa? mi nlitegemea mngekaa kimya ili hayo yatokee msherehekee..!
 
Alafu kuna watu eti wanapinga ujio wa Lowassa ndani ya CHADEMA/UKAWA

Safi sana Mbowe na Kamati Kuu mliona mbali kwa maslahi ya ukombozi wa Taifa hili.

Adui yetu mkuu ni CCM na mfumo wake na Lowassa ni silaha tosha iwe ni silaha ya "mass destruction" au vinginevyo tunachohitaji hapa ni ushindi tu.

Wee waache! Wanafikri haya mafuriko ni ya kawaida? Kama babu hajui kusoma alama za nyakati atuache kabisaaaa!!! CCM inaenda kufa naye anataka aturudishe nyuma! Big up Mbowe hata kama uliwaburuza wao walitakaje?
 
Back
Top Bottom