Lukuvi asimamia ujenzi wa barabara usiku

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Na Pamela Chilongola, Mwananchi

UONGOZI wa Mkoa wa Dar es Salaam juzi ulitengeneza barabara ya Kagera hadi Madoto iliyoko maeneo ya Mburahati usiku, kwa ajili ya ziara ya rais Jakaya Kikwete jana.

Rais Kikwete jana alitumia barabara hiyo kutembelea kisima cha maji cha jumuiya ya watumiaji Maji, (Mrosso) kilichopo maeneo ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mburahati Wilaya ya Kinondoni.

Barabara hiyo, ilitengenezwa juzi usiku baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam William Lukuvi kuitembelea saa 10:00 jioni na kubaini kuwa isingefaa kutumika katika ziara hiyo ya mkuu wa nchi.

Baadhi ya wananchi walioshuhudia ujenzi huo walilieleza Mwananchi kuwa muda mfupi baada ya Lukuvi kupita eneo hilo, yalionekana malori yaliyokuwa yakimwaga vifusi vya mchanga kufukia mashimo kwenye barabara hiyo.

"Ujenzi huo, ulianza saa 12:00 jioni hivi na uliendelea hadi usiku.

"Ilipofika saa 3:00 usiku lilionekana tingatinga likichimba barabara na kusawazisha kifusi hicho jambo ambalo lilifanya wakazi wote wa eneo hilo wabaini kwamba kulikuwa na ugeni mkubwa wa kitaifa katika eneo hilo," alisema mkazi wa eneo hilo, Said Omary

Mwandishi wa habari hii jana aliikuta barabara hiyo ambayo siku zote ilionekana kuwa na mashimo, jana usiku ilikuwa ikisawazishwa kwa kuwekwa vifusi.

Hatua hiyo ya uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam umepokelewa kwa hisia tofauti baada ya baadhi ya watu kuiponda na wengine kusema imelenga kujikomba kwa rais Kikwete.
 
Kwa nini kila siku asiwe anahamasisha hivyo? Woga au kujipendekeza kwa kupindukia?
 
Wachina wanapofanya kazi usiku na mchana, wanapoamua kunywa maji moto wakati wa kazi badala ya kujichana tunawaona watu wa ajabu. Kumbe Watanzania wanaweza kufanya kazi usiku!!! Tunaomba Lukuvi aendeleze zoezi hilo la kutengeneza barabara usiku ili barabara hapa mjini ziweze kupitika. Kama ameweza kusimamia barabara hiyo bila shaka uwezo wa kusimamia na zingine pia anao. Lukuvi Mwalimu Nyerere alisema: "it can be done, play your part" effectively!!
 
Wachina wanapofanya kazi usiku na mchana, wanapoamua kunywa maji moto wakati wa kazi badala ya kujichana tunawaona watu wa ajabu. Kumbe Watanzania wanaweza kufanya kazi usiku!!! Tunaomba Lukuvi aendeleze zoezi hilo la kutengeneza barabara usiku ili barabara hapa mjini ziweze kupitika. Kama ameweza kusimamia barabara hiyo bila shaka uwezo wa kusimamia na zingine pia anao. Lukuvi Mwalimu Nyerere alisema: "it can be done, play your part" effectively!!

Ni sifa za bure tu unazompa. amefanya kazi hiyo usiku kwa sababu bosi wake anapita kesho yake. Lukuvi hana habari na kero za watu wa dar kuhuisu barababra!
 
Hivi bado mpaka leo hii tabia tunaiendeleza??? Yaani barabara hazitengenezwi hadi mkubwa apite??????
Ushauri kwa bwana RC
Dsm City wameoza na wamefikia ukomo wa ubunifu.Hivyo ingekuwa busara ukawaamrisha hawa mabwana kufanya yafuatayo:-
1.Barabara zote za katikati ya jiji zingekuwa zinafanyiwa ukarabati usiku;
2.Uzoaji wa takataka ungefanyika usiku maana hakuna msongamano barabarani hivyo quick turn-round ya magari taka itawezesha tani nyingi
zaidi kuzolewa;
3. Usafi wa barabara pia ufanyike usiku.
Miaka ya nyuma walikuwa wanafanya hivyo lakini nadhani wamesahau.
Vilevile tabia ya kudanganya viongozi kwa ukarabati wa dharura uachwe kwani ni bora aone hali halisi halafu aangalie namna inavyoweza kufanyika kwenye bajeti.
 
mzee wa ismani kachemsha.hiyo tabia ya mwaka 47bado anaendelea nayo leo pamoja na hayo gari ikachomoka tairi,mtaona kila rangi
 
Ni sifa za bure tu unazompa. amefanya kazi hiyo usiku kwa sababu bosi wake anapita kesho yake. Lukuvi hana habari na kero za watu wa dar kuhuisu barababra!

Aliogopa nini? Kufukuzwa kazi na JK? No way! hana ubavu wa kufukuza mafisaadi wanaotuuibia na kuendeleza umasikini hapa nchini, itakuwa RC mmoja kwa sababu ya ubovu wa barabara?
 
Lukuvi kawakilisha sura halisi ya utendaji kazi wa viongozi wetu hawafanyi kazi kwa kujituma hadi kuwe na msukumo nyuma yake, alikuwa wapi siku zote, kwa akili yake Lukuvi alidhani kwa kufanyakazi hadi usiku wa manane ataonekana mchapakazi kumbe on the other side of the coin kaonyesha uvivu wa kutowajibika siku za kawaida, laiti kama tungekuwa na rais mwelewa angehoji kitendo hicho na si kusubiri aletewe taarifa na wasaidizi wake ambao mara nyingi hudanganya.

Hata enzi za Nyerere kulikuwa na udanganyifu wa aina hii, barabara zilikuwa zinafukiwa mashimo wakati wa ziara zake lakini siku moja alishitukia ujanja wao, alialikwa na bwana shamba mmoja kwenda kujionea jinsi bustani ya kijiji ilivyostawi kumbe wameng'oa miche toka shamba jingine na kuipandikiza bila hata mizizi, alichofanya Nyerere ni kuchelewa kwenda kwa makusudi ilipofika jioni ndipo akaomba akaonyeshwe bustani na kukuta miche yote imesinyaa.
 
Yani tabia za zamaaaaaaaniiii. Kweli hii mtu std 7.
Anyways ndio mana yupo alipo na elimu yake.
 
Sisi waafrika!! ndio maana watu wanasema tuna IQ ndogo kwa sababu ya watu kama akina Lukuvi.
 
Ni sifa za bure tu unazompa. amefanya kazi hiyo usiku kwa sababu bosi wake anapita kesho yake. Lukuvi hana habari na kero za watu wa dar kuhuisu barababra!

Hey hey!! Hujanisoma sawasawa naona. Sijamsifu Lukuvi ninachosema ni kwamba alipaswa kuifanya kazi hiyo iwe endelevu sio wakati wa ujio ama matembezi ya Rais pekee. Aige mfano wa Wachina wanaofanya kazi usiku na mchana bila kuchoka na kunywa maji moto badala ya chai na zege la chapati na maharage ama chai na mkate wa siagi na mayai na kuku anazokula Lukuvi!
 
Hii ni RAI kwa kila mtanzania na huu ni ujumbe kwa JK,Kwa kila mtanzania huu ni wakati wa kuepukana na wanasiasa wanaoliangamiza taifa kama CCM,Nawaomba wananchi msichague chama hiki.Mfano wa kwanza wakati wa Mkutano wa WEF miti na maua vilipandwa usiku au siku mbili kabla na miti hiyo ilikuwa na umri mkubwa na ali hassan mwinyi ulifanyika usafi wa kufa mtu huku machinga na masai wote wakufukuziliwa mbali kupisha mkutano huo.Mfano wa pili ni hili la barabara kujengwa usiku kucha ili kuhakikisha rais hajui machungu ya barabara mbovu za mburahati na bonyokwa na sehemu nyingine nyingi.Kwa mara ya kwanza nakupongeza kibonde kwa kumwambia ukweli rais kuwa alikuwa anadanganywa ile barabara imewekwa kifusi usiku wa kuamkia siku ya ziara.Hizi siasa za ndio mzee sasa inatakiwa watanzania tuepukane nazo na kufumbuka macho nakuhakikisha kuwa tunafanya uchaguzi na kuuondoa mfumo wa utumwa na utwana uklioletwa na JK pamoja na genge la mafisadi.
 
kwani yeye Rais mwenyewe halijui hilo?? kwamba hizo bara bara ni mbovu na hazipitiki, na kwamba zinatengenezwa ili 'yeye' asipate tabu anaopita huko vichochoroni kwetu???

wote lao moja tu!!
 
Kama Ningalikuwa mimi ndio Rais huyu jamaa leo asingerudi Ofisini. Huu upuuzi wa kufukia mashimo ndio watu wanauita Ujenzi wa Barabara. Upuuzi mtupu na hata wanaoshabikia ni wapuuzi big time
 
Maoni yenu nitayafikisha na yatafanyiwa kazi,ahsanteni sana

Asante sana. Ila mwambie hivi wananchi wa mburahati wanauliza alikuwa wapi siku zote kuja kututembelea? ameona uchaguzi umekaribia ndio anatukumbuka?
 
Back
Top Bottom