Lugha za Matusi.

Wanadamu kwa tabia tunapenda kusikia kwa masikio yetu 'yasiyotamkwa', yaani yale ambayo jamii inayakataza na kuyakemea. Sasa ili mtu apate hamu/bashasha ya kujifunza lugha ngeni, matusi ndo ya kwanza kumfundisha kwani hayo yatamvuta na kumchangamsha mpaka awe na hamu ya kujifunza mambo ya maana na ya siriaz. Kumbe matusi ni ndoano ya kukuvuta kuingia katika lugha mpya na utamaduni wa wenye lugha; vitu ambavyo ni vizito vyenye kuhitaji muda, umakini na toiling. Matusi mtu hahitaji nguvu nyingi kufunza, na ndiyo maana yanatangulizwa ili kukuandaa kwa kazi inayofuata ambayo ni sarufi ya lugha.
 
Kwa nini mtu ukitaka kujifunza lugha mpya unaanza kwanza kufundishwa matusi.
Hapo ni sawa na kupewa tahadhari kwamba katika jamii hiyo hayo ni matusi........... Maana usije ukamtamkia mtu na akakufanyia kitu mbaya. Na hivyo utakuwa makini katika matamshi yako
 
Nikilikuwa najifunza lugha fulani, nikaambiwa nikiwakuta wazee niwaambie mwisenye, ndio salamu yao, ehh bwana ehh kumbe bonge la tusi.
Uzuri ni kwamba mzee mmoja nilikuwa nimefikia kwake, na aliyekuwa ananifundisha hiyo lugha ni mwanawe mkubwa.
Adhabu yangu akaibeba yeye.
 
Sipati picha Mzee wa Kikurya umwite shoga mbele ya mke wake na watoto, halafu ujitete kuwa hujui lugha.
Nyambafuuuu
 
miaka ya tisini nilitaka kujifunza kijaluo, nikakosea mwalimu wangu akawa mdada, maneno aliyoniambia kuwa ndiyo goodmorning...ilikuwa balaa almanusura nikatwe shingo.
 
Back
Top Bottom