eliakeem
JF-Expert Member
- May 29, 2009
- 15,654
- 13,797
Mwalimu wangu proffessor Shazia Reuben Mnyuku aliwahi kunifundisha kuwa hakuna technolojia isiyokuwa na matatizo. (There is no rechnology with zero risk). Hivyo mi nadhani tusiangalie mapungufu bali tuchukue yaliyo ya faida na siyo mapungufu. Mapungufu tuyazingatie katika kuchukua tahadhari lakini yaliyo mema tuyaenzi. Japo kuwa Mwalimu alikuwa na mapungufu mengi, hapana shaka kazi aliyoifanyia hii nchi ni kubwa sana kulinganisha na haya mapungufu. Ndiyo maana nasema japo hatunaye bado yungali anaishi mioyoni mwa watanganyika na watanzania kwa ujumla. Nyerere ni alama ya Tanganyika na Tanzania.
Umeongea kwa moyo mnyoofu....... maana hukatai kuwa alikuwa na mapungufu..... halafu pia hukatai kuwa alikuwa na mazuri...... wewe ni mwenye hekima....halafu unatoa hitimisho kuwa mabaya tuyaache tugange na mazuri tu.... sasa kuna ndugu zetu wengine wanasema tugange na mabaya ambayo kimsingi hayana hata chembe ya msaada...