Lowassa: Wanaotakiwa kuwajibika wawajibike

MASIKITIKO

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
959
428
Waziri mkuu aliyejiuzuru EL amesema"viongozi wanaotakiwa kuwajibika kwa kujiuzuru Serikalini wafanye hivyo kama alivyofanya yeye" SOURCE TBC1 habari 20:00
 
Waziri mkuu aliyejiuzu EL amesema"viongozi wanaotakiwa kuwajibika kwa kujiuzuru Serikalini wafanye hivyo kama alivyofanya yeye" SOURCE TBC1 habari 20:00

Amwambie swahiba wake aliyekuwa Magogoni kupiga deal za rasilimali za nchi
 
Ila jamani mwalim aliwakataeni na ndo kifo kilipomkuta.tubuni na kumrudia mungu mwalim hatawaacha japo mlhmtanguliza nyie mtakuwa kuni
 
Hii santuri ya Lowassa karibu itachuja sasa. Hata kama ana mengi ya kusema, siyo kila siku yeye tu.
 
Huyu jamaa ana matatizo makubwa sana...Ni bahati mbaya sana kwamba hajui hili.....

Kama kweli anataka kuwa Rais wa nchi hii 2015, basi keshatibua kila kitu kwa sababu tayari anakaribia kumaliza missiles zake zote!!
 
Hii santuri ya Lowassa karibu itachuja sasa. Hata kama ana mengi ya kusema, siyo kila siku yeye tu.[/QUOTE

Mkuu,ni kweli kayasema hayo,tena aliulizwa swali na Kisu ndo akasema "wawajibike"kama alivofanya yeye. C suala la kuendeleza "santuri"
 
Bado kidogo tutayasikia mengi zaidi. Ila itafika mahali hatutajua ni nani wa kumwamini. Ila inabidi ringi za ndondi zijengwe mpyaaa! na gloves ziagizwe marekani. chichim oyee!
 
Huyu jamaa ana matatizo makubwa sana...Ni bahati mbaya sana kwamba hajui hili.....

Kama kweli anataka kuwa Rais wa nchi hii 2015, basi keshatibua kila kitu kwa sababu tayari anakaribia kumaliza missiles zake zote!!

Mkuu DC,

Lowassa inawezekana anaweza kuwa anajua anachokifanya, kinachoendelea ni kuvurugana ili wote tukose. Unakumbuka sakata ya u-Spika mwaka jana jinsi Mzee wa Viji-cent alivyoomba kuwa Spika na kuitisha press conference na kumshushia makombora Anko Sam Six?

Kwa hiyo kinachoendelea ni kuropoka kwa kwenda mbele na kuvurugana. Sikutegemea kuona gazeti la Mtanzania likimwaga siri za nyaraka za chama. Mgogoro ulio ndani ya Chama ni mkubwa, siyo kama jinsi wanavyotudanganya kwamba hali siyo mbaya sana si ajabu wanajuta hata kwanini walikuja na hiyo idea ya "Operation Vua Gamba". RA alipotoka, hakutoka kwa nia njema, alitoka kwa shingo upande na sasa ameamua kuwarudi na within secretariat kuna watu wa mafisadi na ndio wanao-feed hizo info za nyaraka.

Kama wapinzani wanaweza kucheza kete zao vizuri, wanaweza kujikuta wanavuna kutokana na hizi vurugu.
 
Lowassa bana...nitoke vipi??

Mambo ya kitoto kweli..

Kwa ccm atatulia tu..au akimbie mapema ..urais hapati huyu..
 
Keil, siri za chama hazitoki kwa kuwa tu mafisadi wana watu wao ndani. Ni pamoja na kuwa Mukama na Nape can not just stop talking about it.

Hawa wawili mtu ukipata muda kidogo tu wa kuongea nao faragha, na kuonyesha chuki fulani dhidi ya Lowassa au RA siyo lazima iwe na Chenge, basi wanabwabwaja kama mwali wa Kaole aliyelishwa kungu. Siri ziko nje nje Lumumba na Magogoni.

DC, sidhani kama ENL amegusa hata stoo ya kwanza ya missile zake. Ukiona hadi watu wa ENL wanaombea Mwakyembe apone na arudi mzima, basi ujue kuna kitu Mwakyembe anakijua ambacho kitamfaidisha ENL mwishoni. Time will tell.

Mimi kinachonikera kuhusu ENL ni mengi, ila kubwa mojawapo ni kwa nini yeye tu anadhani ana haki ya kusema kila siku? Kwa nini isiwe RA au Chenge? Kwa nini isiwe Sita?
 
Now the plot gets more interesting, by the time we will be nearing 2015 tutakuwa tumejua mengi sana!
 
Back
Top Bottom