Lowassa si target ya 'Gamba la CCM' atarudi mlango wa nyuma, bali target ni Rostam Aziz - Al-nuur

Turudi kwenye hoja. rostam ni fisadi wachangiaji wengi wamechukizwa na waislam(sio wote) kumtetea fisadi. upande wa pili kikwete anadaiwa ni fisadi papa maaskofu wana mrecommend kuwa ni chaguo la mungu. Swali, iweje waislam(sio wote) kumtetea fisadi waonekane hawakusoma, hawana ufaham, wakati huo huo maaskofu(wakristo - sio wote) kumtetea / kumrecommend fisadi ionekane wako smart wamesoma. WAKE UP SOMETHING IS WRONG HERE.
 
Kwanini Annur wasianzishe Chama? Chama hicho kitakuwa na upendo na Wakristo? Au tutapata ya Al-Shaahab?

Jamani tuweni makini na utulivu wetu... Tupende kuishi kwa Amani na Upendo kuliko kuwaza nani ni mtawala
 
Nimeshtuka kuona ktk gazeti moja linajulikana kama Sauti ya waislam likiandika kwamba Gamba la CCM linalotaka kuvuliwa kwa mapacha 3 lengo kuu ni kumuondosha kabisa Rostam azizi ktk CCM na sio Lowassa.

Eti imeandika wote hao watafukuzwa lkn Lowasa atarudishwa kwa mlango wa nyuma kwa shindikizo la makanisa. Limejenga hoja yao kutokana na kauli ya Kardinal Pengo kusema kanisa halitajitenga na wathumiwa ufisadi alioitoa siku za pasaka. Gazeti hilo limejenga hoja hiyo ikimaanisha ni kutaka kumuokoa Lowassa.

Limesema Gamba la EL linatokana na kuwa karibu na muislam Rostam Azizi.

Hivi kweli Rostama amewasaidia nini waislam hadi kufikia kutetewa? au tayari fedha zake zinapenya kila sehemu? kwani niliwahi kusoma ktk gazeti moja kwamba RA akijinadi kwamba wanawe wote amewakabidhi makanisani kwa malezi ili wapate malezi mazuri na sio misikitini.

Lkn kwa kuwa limeandikwa na gazeti lilosajiliwa Hoja hii inaweza ikawa na chembe ya Ukweli SI YA KUPUUZWA

UPDATED.

tayari rostam hayupo. lowasa kimya. ccm kimya. jee hoja ya gazeti hilo inatimia?

Badala ya kulalama humu naomba kukujuza kuwa na wewe una haki kamili kuandika ukweli kama unaona mwandishi amekosea na kupeleka kwa gazeti hilohilo nao pasi na shaka watakujibu.

Kinachoangaliwa hapo ni mpangilio wa hoja zako katika kuzipangua zile hoja ambazo mwandishi alizitumia.

Tumia nafasi hiyo na sio kutuletea umbeya hapa. Kwani ni nyie mnaoleta majungu ndani ya JF na kufanya JF kiwe kama kijiwe cha umbeya na uzandiki na usengenyaji.
 
badala ya kulalama humu naomba kukujuza kuwa na wewe una haki kamili kuandika ukweli kama unaona mwandishi amekosea na kupeleka kwa gazeti hilohilo nao pasi na shaka watakujibu.

Kinachoangaliwa hapo ni mpangilio wa hoja zako katika kuzipangua zile hoja ambazo mwandishi alizitumia.

Tumia nafasi hiyo na sio kutuletea umbeya hapa. Kwani ni nyie mnaoleta majungu ndani ya jf na kufanya jf kiwe kama kijiwe cha umbeya na uzandiki na usengenyaji.

yupo wapi el. Mbona swala la gamba limeisha?
 
pumbavu kbs mambo ya kiimani sio ya kuyachukulia kirahs namna hvyo,tufanye research kwanza kabla ya kuzungumza aagh!
 
Mzee wa hoja, nakuunga mkono ktk hii hoja yako pamoja na michango yako mingine. Mimi pia ni mmoja wa watanzania tunaofuatilia kwa karibu sana matamko mbalimbali yanayotolewa katika nyakati na vyombo mbalimbali vinavyomilikiwa na hawa islamic fundamentalists. Wanapiga kelele sana kuhusiana na dudu walilolibuni wao wenyewe na kuliita mfumo kristo. Najaribu sana kutafuta hicho kitu kinachozungumzwa, mwisho wake nakutana na propaganda tu za waislam wenye misimamo mikali kutafuta namna ya kupenyeza uanaharakati wao hatari katika maeneo yenye stability za kijamii kama Tanzania.

Tanzania ni nchi yenye amani ambayo imejengwa katika misingi ya kuheshimiana, kupendana na kuaminiana, bila kusahau kusaidiana bila kujali itikadi za kidini, kikabila, usehemu atokeako mtu wala jinsia yake au ulemavu alionao; na kwa sasa bila kujali itikadi yake ya kisiasa. Suala kubwa linaloanza kuonekana kuwatenga watanzania, na ambalo linaanza kujengwa na watu hatari kama hawa ni dini ya mtu. Watu wenye busara ktk nchi hii, akiwemo Baba wa Taifa Mwl. J.K. Nyerere wameiona hatari hii kwa muda mrefu na kulikemea katika muda wote wa uhai wao lakini watu wenye ubinafsi wameendelea kulichochochea kwa lengo la kujinufaisha na matengano wanayoyahubiri.

Mchakato wa katiba nao sasa umeingiliwa kama sehemu ya kupenyeza huu uchochezi wao. Ni ukweli usiopingika kuwa, wao kama watanzania, pia wana nafasi ya kutoa maoni yao ya aina ya katiba inayotakiwa hapa nchini kwa sasa, lakini kibaya ni kuwa kinachowasukuma kuzungumzia suala hili ni kulinda maslahi ya dini yao bila kujali kuwa nchi hii ina waumini wa dini nyingine pia! Wanadai mahakama ya kadhi, wanadai kuondosha 'mfumo kristo', sijui waweke mfumo 'ujahidina vile', wanadai nchi ijiunge na OIC, kwa ufupi wanataka nchi iwe ya kiislam na kufuata misingi ya kiislam. Sasa suala la kijiuliza, je hizo harakati zao za kubaguzi zitafanikiwa kweli au wanataka waendelee kulalamika kuwa nchi inatawaliwa kikristo?

Napendekeza kuwa hawa watu wapuuzwe katika madai yao ya hatari hatari haya. Nakubali kuwa baadhi ya madai yao ni ya kimsingi, mfano, kupata mapumziko siku yao ya kuabudu, ingawa inatakiwa sasa suala hilo liangaliwe upya, si kwa dini yao, bali dini zote ili siku za kazi zisiathilike kwa kuwa na siku nyingi zaidi za mapumziko! Suala jingine ninaloliunga mkono ni kupinga huu mswada wa katiba uliobana namna ya kupata na kushughulikia maoni ya wananchi kuhusiana na katiba mpya, ingawa sikubaliani na yale yanayoombwa yanayoegemea kwenye dini yao tu bila kujali kuwa kuna dini nyingine hapa nchini. Kitendo cha kutaka mahakama ya kadhi kwenye katiba yetu kitapelekea hawa jamaa kutaka pia katiba itambue ulinzi wa majini ya shehe yahaya pia!

mh hata CDM wanatumia Propaganda. jee na wao msimamo mkali?
 
"Hivi kweli Rostama amewasaidia nini waislam hadi kufikia kutetewa? au tayari fedha zake zinapenya kila sehemu? kwani niliwahi kusoma ktk gazeti moja kwamba RA akijinadi kwamba wanawe wote amewakabidhi makanisani kwa malezi ili wapate malezi mazuri na sio misikitini. "Implication ya kauli yako ni kuwa "kweli Lowassa kalisaidia kanisa kwa hiyo tumtetee"
 
Hata kama kilchoandikwa na hili gazeti ni kweli. Kumfukuza Rostam ni kazi inayofanywa na Kikwete ambaye ni muislam mwenzake.
 
nani kasema Rostam muislamu? labda hawamjui? baadhi ya waislamu sijui hawafikirii hata sielewi, yaani kati ya waislamu na Rsotam nae ni muislamu? mmh haya
 
jamani dini ni Mbili tu, umaskini na udosi(utajiri), sasa wewe endelea kupiga kelele kuhusu dini kisha mwishoni tutajua kama maisha yako yote utayaendesha kwa fedha za Lowassa, Chenge na wenzake au kwa fedha za JK, Rostam na wenzake. nawasilisha!
 
Mzee wa hoja, nakuunga mkono ktk hii hoja yako pamoja na michango yako mingine. Mimi pia ni mmoja wa watanzania tunaofuatilia kwa karibu sana matamko mbalimbali yanayotolewa katika nyakati na vyombo mbalimbali vinavyomilikiwa na hawa islamic fundamentalists. Wanapiga kelele sana kuhusiana na dudu walilolibuni wao wenyewe na kuliita mfumo kristo. Najaribu sana kutafuta hicho kitu kinachozungumzwa, mwisho wake nakutana na propaganda tu za waislam wenye misimamo mikali kutafuta namna ya kupenyeza uanaharakati wao hatari katika maeneo yenye stability za kijamii kama Tanzania.

Tanzania ni nchi yenye amani ambayo imejengwa katika misingi ya kuheshimiana, kupendana na kuaminiana, bila kusahau kusaidiana bila kujali itikadi za kidini, kikabila, usehemu atokeako mtu wala jinsia yake au ulemavu alionao; na kwa sasa bila kujali itikadi yake ya kisiasa. Suala kubwa linaloanza kuonekana kuwatenga watanzania, na ambalo linaanza kujengwa na watu hatari kama hawa ni dini ya mtu. Watu wenye busara ktk nchi hii, akiwemo Baba wa Taifa Mwl. J.K. Nyerere wameiona hatari hii kwa muda mrefu na kulikemea katika muda wote wa uhai wao lakini watu wenye ubinafsi wameendelea kulichochochea kwa lengo la kujinufaisha na matengano wanayoyahubiri.

Mchakato wa katiba nao sasa umeingiliwa kama sehemu ya kupenyeza huu uchochezi wao. Ni ukweli usiopingika kuwa, wao kama watanzania, pia wana nafasi ya kutoa maoni yao ya aina ya katiba inayotakiwa hapa nchini kwa sasa, lakini kibaya ni kuwa kinachowasukuma kuzungumzia suala hili ni kulinda maslahi ya dini yao bila kujali kuwa nchi hii ina waumini wa dini nyingine pia! Wanadai mahakama ya kadhi, wanadai kuondosha 'mfumo kristo', sijui waweke mfumo 'ujahidina vile', wanadai nchi ijiunge na OIC, kwa ufupi wanataka nchi iwe ya kiislam na kufuata misingi ya kiislam. Sasa suala la kijiuliza, je hizo harakati zao za kubaguzi zitafanikiwa kweli au wanataka waendelee kulalamika kuwa nchi inatawaliwa kikristo?

Napendekeza kuwa hawa watu wapuuzwe katika madai yao ya hatari hatari haya. Nakubali kuwa baadhi ya madai yao ni ya kimsingi, mfano, kupata mapumziko siku yao ya kuabudu, ingawa inatakiwa sasa suala hilo liangaliwe upya, si kwa dini yao, bali dini zote ili siku za kazi zisiathilike kwa kuwa na siku nyingi zaidi za mapumziko! Suala jingine ninaloliunga mkono ni kupinga huu mswada wa katiba uliobana namna ya kupata na kushughulikia maoni ya wananchi kuhusiana na katiba mpya, ingawa sikubaliani na yale yanayoombwa yanayoegemea kwenye dini yao tu bila kujali kuwa kuna dini nyingine hapa nchini. Kitendo cha kutaka mahakama ya kadhi kwenye katiba yetu kitapelekea hawa jamaa kutaka pia katiba itambue ulinzi wa majini ya shehe yahaya pia!
umeandika utumbo mwingi ila kwenye red highlight ni beyond utumbo.
 
QUOTE=MzeeWaHoja;1910525]kwani ccm hao?[/QUOTE]

Matatizo ya kupenda spoonfeeding haya, yaani wewe mpaka uone imeadikwa CCM ndo akili yako iweze kuchakachua (kujua). Nani washereheshaji wa udini nchini, ni mwenyekiti wa chama kipi ni mpiga kampeini mzuri wa uimarishwaji wa udini Tanzania. Ni kundi lipi hasa kivitendo na kinadharia limezidumisha fikra na kampeini hizi za udini kwa maslahi ya kisiasa? Yaani wewe, zama hizi, miaka hii na kwa maisha ya sasa akili yako haina tembo kadi, karagabao!
 
Back
Top Bottom